Salaam wakuu.
Kuna wimbo mmoja unaimbwa sana juu ya elimu bure katika utawala wa awamu ya tano wa Magufuli. Kama ni kweli elimu hiyo inatolewa bure, basi kuna watumishi wanamuhujumu. Shule ya Sekondari Maendeleo, iliyopo Kata ya Wazo wilaya ya Kinondoni inawatoza wazazi na kuwazuia wanafunzi ambao wazazi wao hawajalipa kuingia darasani.
Walimu wanatumia kigezo cha kutaka matokeo mazuri ya mitihani ya kidato cha pili na nne kwa kuwachangisha fedha hizo kwa kisingizio ya mitihani ya majaribio.
Pia wazazi wametakiwa kutoa shilingi elfu kumi kila mmoja ili shule inunue printa. Sasa cha kujiuliza, kama elimu bure imekuwa mzigo kwa Serikali, kwa nini haisemi hadharani watu tujue? Na hii ni shule iliyopo Dar, sijui zile za pembezoni hali ikoje, hii elimu bure ni kiinimacho na kutaka sifa kwa hii Serikali?