Katika mambo magumu mwaka wa mwisho ni uchaguzi wa project title kisha unajiaandaa vizuri kuitetea inakataliwa mchana kweupe.
Kitu kingine ni prototype implementation vijana wanapata tabu sana, mtu yupo final year ndio anaona kwa mara ya kwanza resitor, inductor, sijui capacitors kwa macho, miaka yote minne ni ma theory tu, halafu lecturers wanavojua kukaza utadhani waliwajengea msingi tangu 1st year.
Binafsi naona hizi project hazina tija kwasababu wengi hawafanyi wenyewe wanafanyiwa na hili ni tatizo la vyuo sio wanafunzi.
Ebwanaee ukipata idea nitafute kama ratiba yangu itaruhusu nipate pesa hapa naona kuna fursa[emoji16]