Mtego wa Noti
JF-Expert Member
- Nov 27, 2010
- 2,591
- 1,599
acha waanze na sisi tunapasha kuanza hii kazi takatifu ya ukombozi...cheeeeers misri
Kuna kila dalili aelekea Uingereza kule kulee mitaa alikotaka Mhe Lowassa kujiopolea hekalu kupitia vijimilioni vya dola kupitia kwa mwanaye.Sina uhakika kama Uingereza wanaweza kumpokea.
Katiba(wakati ambao walikuwa hawana makamu wa rais) ya misri inasema rais akijiuzulu basi spika wa bunge anashikilia nchi na kuitisha uchaguzi ndani ya siku 60.Mubarak ana urafiki mkuwa sana na serkali ya Israel, na akiondoka basi Kiongozi wa shirikisho la wapinzani Mohamed Mustafa ElBaradei ataongoza serikali ya mpito.
Mubarak hana pa kukimbilia zaidi ya Tel Aviv.
Wamisri nadhani hawataki kiongozi yoyote yule ambaye alikuwa chini ya serikali ya Mubarak, ila uwamuzi wanao wananchi wa Misri wenyewe.Katiba(wakati ambao walikuwa hawana makamu wa rais) ya misri inasema rais akijiuzulu basi spika wa bunge anashikilia nchi na kuitisha uchaguzi ndani ya siku 60.
Kuna kitu kilinishangaza, awali wakati harakati zinaanza Misri askari polisi walikuwa wakitumia mabomu ya machozi kusambaratisha wanamapinduzi.
Maganda ya mabomu hayo yaliandikwa "made in Usa"
Inaamnisha us wanam'finance Mubarak!
Marekani lazima ijikomba kwa wananchi kwa sababu wameshaona kuwa hakuna dalili za jamaa kuendelea kuwepo madarakani.ni hivi, US is giving aid to Egypt amounting to 1.5 bil annually, for millitary & citizens
ila Mubarak, anaishi like king, kawasahau citizens, na cha ajabu he was grooming his own son to be President, imagine, ila tayari US imeegemea kwa wananchi, washamgeuka jamaa
Marekani lazima ijikomba kwa wananchi kwa sababu wameshaona kuwa hakuna dalili za jamaa kuendelea kuwepo madarakani.
Mwenzako akinyolewa......
Haa ha ha haa ha!! Umeamka vibaya leo EMT hebu kazimue kwanza. Umenikumbusha yule kijana litongozi akimchelewesha binti wa watu njiani na ndoo zito lenye maji ndani. Ile ilikua kali mzee!!Za kwako weka waves
Hebu ngoja kwanza, hivi katika miaka yote hiyo ya uongozi wa umri wa baba mwenye mji wake mwenyewe, Hosni Mubarak hakubahatika hata siku moja kuvuna japo hata ka PhD kamoja ka-hesima??Dr Mohamed El Baradei=dr W.Slaa wa tz
Dr Mohamed El Baradei=dr W.Slaa wa tz
Ikiwa ni siku ya sita kwa shinikizo za maandamano mfululizo nchini Misri wananchi kumng'oa Rais Hosni Mubarak, uongozi wa Marekani sasa yabadilisha zaidi msimamo kuwa mkali zaidi kutaka kuona mabadiliko makubwa ya haraka nchini humo.
Hali hii inakuja siku moja tu tangu kiongozi wa vikundi vyote vya upinzani nchini Misri, Mohamed El Baradei, kuhutubia umati mkubwa ajabu wa waandamanaji na kupokelewa uzuri pale Tahrir Square hapo jana jioni.
Kauli za Ikulu ya White House Marekani sasa inasisitiza msimamo wa kuomba jamii nzima ya kimataifa iunge mkono nchini Misri kile walichokiita "JUHUDI ZA KISTAARABU KULETA SERIKALI YA MPITO". Huko nyuma kidogo kauli yao ilikuwa ni kusisitiza tu pande zote mbili "kujizuia na aina zozote za matumizi ya fujo na mabavu".