El Baradei Atinga Tahrir Square Misri Na Upinzani Wote Nyuma Yake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

El Baradei Atinga Tahrir Square Misri Na Upinzani Wote Nyuma Yake

Discussion in 'International Forum' started by Uwezo Tunao, Jan 30, 2011.

 1. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #1
  Jan 30, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  [​IMG]

  Dr Mohamed El Baradei ajichanganya na waandamanaji mitaani kuwahutubia na kuwatia wazimu mkali kwa kitendo cha kuonekana tu hata kabla ya tamka neno.

  Yule kiongozi mstaafu wa Tume ya Umoja wa Mataifa kuthibiti mabaya Nguvu za Nuklia Duniani, Dr Mohamed El Baradei, aongoza njia katikati ya umati mkubwa ajabu kwenda kuwahutubia Wa-Misri wanaoandamana wenye hasira nyingi kutaka serikali ya Hosni Mubarak ijiuzulu.

  Kulikua na mlipuko mkubwa sana wa kelele za furaha zikisikika kila mahali tangu habari kuenea kwamba El Baradei yuko njiani anakuja kuwahutubia.


  Hiyo hali iliendelea muda mrefu hata kabla kiongozi huyo hajawasili mahali hapo huku akisaidiwa na walinzi vijana wadogo wa kujitolea wakimzingira kila upande.


  Haikuwa kazi rahisi hata kidogo hata kusema sentensi akamaliza mara baada ya waandamanaji kumtia machoni pale uwanja wa Tahriri Square.


  El Baradei, kwa kufungua tu kinywa chake kwa sentensi ya kwanza tu huku akiwapungia waandamanaji kila upande, alitoa maneno machache kwa lugha ya Kiarabu na karibu kila mwandamanaji mahali hapo kuonekana wazi kulewa na furaha, shangwe na nderemo kwa takriban muda wa dakika 15 na yakatafsiriwa na Al Jazera kwa Kiingereza kama vile:


  "Wameiba uhuru wetu, tumelitambua hilo na tayari tupo kwenye safari ya kujikomboa. Hakuna wa kuturudisha nyuma - Mubarak na serikali yake zima wajiuzulu mara moja," El Baradei adondosha huo 'mzinga' dhili ya Mubarak dakika chache zilizopita.
   
 2. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #2
  Jan 30, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Tahrir Square Related Videos
  [​IMG]
  [​IMG]
  [​IMG]
  [​IMG]
  [​IMG]
  [​IMG]
  [​IMG]
  [​IMG]


  Taarifa zimebaini watu waliokamatwa na jeshi jana usiku wakiiba sehemu mbalimbali katika mitaa ya Cairo sasa watambulika, kwa mshangao wa wengi, kuwa wengi wao wametokea kuwa ni maafisa usalama wenye vitambulisho vya Interior Ministry (Wizara ya Mambo ya Ndani) lakini kwa nguo za kiraia.

  Al Jazera yatangaza punde tu.
   
 3. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #3
  Jan 30, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
 4. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #4
  Jan 30, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  [​IMG]


  Thousands of Egyptians gather in Cairo's Tahrir Square heeding a call by the opposition for a 'march of a million' to mark a week of protests. Photographer: Khaled Desouki/AFP/Getty Images

  ___________

  'Nguvu ya Umma' nchni Misri yawafungulia maelf wa wafungwa kila kona ya nchi tangu jana usiku. Miongoni mwao ni wafungwa 34 hatari wa kikundi cha Muslim Brotherhood.
   
 5. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #5
  Jan 30, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  joto la mabadiliko limekuwa kali!
   
 6. Tangawizi

  Tangawizi JF-Expert Member

  #6
  Jan 30, 2011
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 2,835
  Likes Received: 927
  Trophy Points: 280
  Mwenzako akinyolewa......
   
 7. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #7
  Jan 30, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Kaka kama uliona ule umati uliojaa Tahrir Square tangu juzi kwa sasa ni karibia mara mbili yake.

  El Baradai achukuliwa na umati mkubwa sana wa waandamanaji toka nyumbani kwake ambako awali aliwejuiliwa na Mubarak kutotoka nje. Wananchi waongoza barabara zote ya miguu na kiongozi huyu kuja kuwahutubia.

  Jamani, kwa 'Nguvu ya Umma' sina hamu!!!

  [​IMG]
   
 8. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #8
  Jan 30, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Hapa haambiwi tena mtu akaangalie kitu gani wananchi wanaweza wakafanya katika nchi pindi tu wakiamua.
   
 9. H

  Hegelyakoni Member

  #9
  Jan 30, 2011
  Joined: Oct 7, 2010
  Messages: 31
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kwa hapa kwetu sioni dalili kama kikwete anaweza kumaliza miaka mitano salama sijui labda?
   
 10. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #10
  Jan 30, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Brotherhood, wametoa tamko la kumuunga mkono Mohamed Mustafa ElBaradei ambaye aliwahi kuwa Director General of the International Atomic Energy Agency.
   
 11. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #11
  Jan 30, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  'Nina furaha isiyo kifani kusimama hapa mbele yenu. Natambua kwamba kila Mmisiri kweli ni nafsi maalum sana katika ukombozi wa nchi hii. Toka sasa uhuru wa kujitawala baada ya zaidi ya miaka 30 nchini mwetu juu yetu ...,@ El Baradai anaendelea na hutuba Tahriri Square.
   
 12. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #12
  Jan 30, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  30 January 2011 Last updated at 08:53 ET Egypt protests: Anti-Mubarak protesters dominate Cairo

  [​IMG] Please turn on JavaScript. Media requires JavaScript to play.

  [​IMG]

  Barabara za mji wa Alexandria kwalipuka upya baada ya kupata maneno ya El Baradai kujiunga pamoja na waandamanaji mtaani.
   
 13. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #13
  Jan 30, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Safi X-Paster, tuko pamoja.

  Muslim Brootherhood wasisitiza wapinzani wote nchini Misri wawe wamoja. Watangaza kuwa El Baradai, tangu sasa ni mzungumzaji rasmi wa kambi zima ya upinzani Misri.

  Taabu kweli kweli!!!
   
 14. M

  Mfwatiliaji JF-Expert Member

  #14
  Jan 30, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 1,325
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Naona amewatinga mkwala mzito wamarekani kuwa hata wakim-back up Osni ni lazima ang'oke; kama si leo basi kesho haitaisha kabla hajakimbia
   
 15. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #15
  Jan 30, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Balozi Mbali mbali na mikampuni ya kimataifa imeanza tangu mchana kuondoa wafanya kazi wao walioko nchini Misri.
  Mhe Membe kwa upande wetu ndugu zetu walioko Misri hali ikoje????
   
 16. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #16
  Jan 30, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Washington waanza kuonyesha kuegemea zaidi kwa wananchi waandamanaji wa Misri.

  Raisi Obama asema kitendo cha kubadilishana tu viti kamwe haielekei kwenye matarajio ya Wa-Misri; asisitiza US wanataka kuona mabadiliko makubwa nchini humo ikiwa ni pamoja na Kubadilisha KATIBA ya nchi hiyo.

  Hapo sasa patamu!!
   
 17. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #17
  Jan 30, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Wakati mambo yakiendelea Tahrir Square pale jiji Cairo, taarifa kutoka ikulu ya Mzee Mubabaraki ni kwamba atarajia kutangaza sasa baraza zima baada ya Makamu na Waziri Mkuu hapo jana.
   
 18. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #18
  Jan 30, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Jinsi hali ilivyo katika bara letu zima hivi sasa wala rais moja asije akajitia matumaini kwamba huenda akasaidiwa na marais wengine kwani ni dhahir kwamba MALAIKA WA MABADILIKO KWA FAIDA YA WANYONGE Barani Africa hivi sasa anapita na kupiga hodi karibu katika kila nchi hasa wale wabadhirifu na wadhalimu.

  Ni kipindi cha kila kiongozi kujibebea tu mzigo wake mwenyewe.
   
 19. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #19
  Jan 30, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  ElBaradei joins protesters in central Cairo

  By Marwa Awad and Dina Zayed

  CAIRO | Sun Jan 30, 2011 12:44pm EST

  CAIRO (Reuters) - Egyptian opposition leader Mohamed ElBaradei told thousands of protesters in central Cairo on Sunday that an uprising against Hosni Mubarak's rule "cannot go back."

  ElBaradei, a Nobel peace laureate and retired international diplomat, said earlier he had been given a mandate to make contact with the army and build a new government in Egypt.

  "I bow to the people of Egypt in respect. I ask of you patience, change is coming in the next few days," he said.
  "You have taken back your rights and what we have begun cannot go back," he said as crowds chanted "Down with Mubarak."
  "We have one main demand -- the end of the regime and the beginning of a new stage, a new Egypt."

  Mubarak, clinging on despite unprecedented demands for an end to his 30-year rule, met on Sunday with the military which is seen as holding the key to Egypt's future while in Cairo.

  "Mubarak has to leave today," ElBaradei told CNN before joining up to 10,000 demonstrators who defied a curfew to gather in Tahrir, a rallying point in the center of Cairo.

  Protesters are angry over poverty, corruption and political repression. They held banners saying "Game over Mubarak" and "Please leave, you psycho, Hear the voices of 80 million Egyptians."

  "I don't care who becomes president at this point. I don't necessarily support ElBaradei but the fact is he's showing there is an alternative," said Laila Ali, a 35-year-old mother of two. "Mubarak has to go, preferably today rather than tomorrow."

  Others were skeptical of the bespectacled ElBaradei, who has been criticized by many government opponents in recent months for spending a lot of time outside the country.

  Some protesters argued among themselves over the pros and cons of ElBaradei. A few posters said "ElBaradei no!." But he later left in a car as a crowd of supporters ran after him in a stampede that almost caused him to fall.

  "He is Egyptian like the rest of us. We don't need him down here. But of course anyone that joins is most welcomed," said Mustafa, 24, a pharmacist.

  But asked if he would support ElBaradei for president, he added: "He is a decent man. He understands politics and we will accept any leader as long as they respect our freedom, ensure there is democracy. Anything other than that we will be back on the streets."

  (Additional reporting by Shaimaa Fayed and Sherine El Madany, writing by Andrew Hammond; editing by Maria Golovnina)

  ElBaradei joins protesters in central Cairo | Reuters
   
 20. W

  We can JF-Expert Member

  #20
  Jan 30, 2011
  Joined: Sep 4, 2010
  Messages: 681
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Upepo huu hautazimika Misri. Vumbi la upepo huu, lipo kila nchi barani Africa sasa, kuanzia kuliko upepo, kunakoelekea upepo na mbaka upepo ulikotoka. Hii inamaana kwamba, hata viongozi watakaoteuliwa/kuchaguliwa sasa kuongoza nchi hizo ambako mageuzi yatafanyika, wakifanya mchezo, watu wanawatoa tena. Hii inaonyesha pia kwamba, Mungu ameamua kuwakomboa watu wake kwa namna ya ajabu! Tukipata viongozi waadilifu, rasilimali hata kama zingelikuwa kidogo vipi, zingeligawanywa KWA HAKI.

  Ole wao wadhaniao kuwa kwa kujilimbikizia mali za wanyonge, wataishi milele......
   
Loading...