El Baradei Atinga Tahrir Square Misri Na Upinzani Wote Nyuma Yake

'Nina furaha isiyo kifani kusimama hapa mbele yenu. Natambua kwamba kila Mmisiri kweli ni nafsi maalum sana katika ukombozi wa nchi hii. Toka sasa uhuru wa kujitawala baada ya zaidi ya miaka 30 nchini mwetu juu yetu ...,@ El Baradai anaendelea na hutuba Tahriri Square.
Nakumbuka huyu jamaa Mubarak alimuwekea ngumu sana sasa upepo wa mabadiliko umetokea sijui kama Mubarak atasalimika
 
Kambuni kubwa kubwa za maswahiba wa Rais Mubarak ama yamechomwa hadi majivu au mali zote kuopolewa na wananchi.
 
Huyu mheshimiwa Hosni Mubarak amekuwa kibaraka wa Marekani na nchi za magharibi kwa miaka yote thelathini alokuwa madarakani.

Pesa ya msaada kwa nchi ya Misri haiwezi kuhesabika ni mabilioni ya fwedha. Matokeo yake Mubarak na watu wake wamejilimbikizia mali ndani na nje ya nchi hiyo wakiwasahau wananchi na hasa kizazi kipya ambacho hakina matumani ya maisha bora.

Mwanae Mubarak aitwae Gamal ambae ndie alikuwa akitarajiwa kumrithi baba yake kiti cha enzi cha uraisi hivi sasa yupo London ambapo aliingia jumatano iliopita. Ana nyumba kubwa na nzuri tu pale Knightsbridge na aliishi Uingerea kwa muda mrefu tu akiweka fwedha kwenye akiba benki.

Tatizo kubwa ambalo litakuwa likitatulika kidogokidogo ni kwamba watu wa aina ya Hosni Mubarak wanaishi kwenye dunia yao na hawako kwenye kuona hali halisi.

Lakini kwa kuwa wananchi wa Tunisia walianza basi kila sehemu yenye watu wenye akili timamu watafuata mapinduzi haya yanayofanywa na wananchi wenyewe na sio jeshi wala mtu fulani peke yake.
\
Kila mtu ameona na sidhani kama kuna haja ya kutumia jeshi kupindua mtu ila nguvu ya umma ina nguvu ya ajabu kweli kama tulivyoona kwa Tunisia and now Misri ni changamoto kwa nchi nyingine kwenye bara hili zenye utawala wa udikteta na pia ambazo zilikuwa na uchaguzi uliochakachuliwa
 
rumour has it Mubarak has left the country na inawezekana yuko UK vile vile matajiri kadhaa na kiongozi wa ndp wameenda dubai.
Wamisri wakimtimua Mubarak na kumweka El Baradei nitawaona watu wa ajabu sana. But again inaonekana watu wote wenye uwezo wa kutawala either ni wazee, wako associated na mubarak na chama chake au wanatoka wings za muslim brotherhood.
Inaonekana wakati wa matatizo ya wa-Misri huyu jamaa hakuwepo ila baada ya nguvu ya umma kuwa ya ajabu ndio anajitokeza sasa hapo watu ndio wanaanza kuuliza where was he all this time???
 
Nakumbuka huyu jamaa Mubarak alimuwekea ngumu sana sasa upepo wa mabadiliko umetokea sijui kama Mubarak atasalimika
Mubarak, kama kweli bado yupo Misri, asemekana kutoa amri nyingine yenye mema zaidi kwa kumuagiza waziri mkuu afanye hima kuhakikisha serikali imeingiza fedha kila kona ya uchumi wa Misri kusaidia kupunguza bei za bidhaa na huduma mbali mbali ili wananchi wapate kufurahia unafuu wa maisha.

Ajabu ni kwamba waandamanaji wao wanasema hakuna cha zaidi na Mubaraka badala ya kuondoka kwake ndipo watarudi majumbani mwao kuacha maandamano.
 
\
Kila mtu ameona na sidhani kama kuna haja ya kutumia jeshi kupindua mtu ila nguvu ya umma ina nguvu ya ajabu kweli kama tulivyoona kwa Tunisia and now Misri ni changamoto kwa nchi nyingine kwenye bara hili zenye utawala wa udikteta na pia ambazo zilikuwa na uchaguzi uliochakachuliwa
The Finest, hii avatar lini tena mtu wangu au macho yangu tu mzee???
 
rumour has it Mubarak has left the country na inawezekana yuko UK vile vile matajiri kadhaa na kiongozi wa ndp wameenda dubai.
Wamisri wakimtimua Mubarak na kumweka El Baradei nitawaona watu wa ajabu sana. But again inaonekana watu wote wenye uwezo wa kutawala either ni wazee, wako associated na mubarak na chama chake au wanatoka wings za muslim brotherhood.
Hili unalolisema yawezekana kabisa maana kwa mazingira ambayo utangazaji wa Baraza jipya la Mawaziri kutoweka jana mara baada ya Elbaradei kuhutubia pale Tahrir Aquare na kwa namna ambavyo lugha anayotumia Elbaradei inavyooana mahala na ule ujumbe wa pili wa White House tayari inaonyesha Misri kuanza mwezi Februari na TRANSITIONAL GOVERNMENT si kipindi kirefu.

Behind the scenes Diplomacy inaendelea kwa spidi kali ajabu mpaka sasa.
 
rumour has it Mubarak has left the country na inawezekana yuko UK vile vile matajiri kadhaa na kiongozi wa ndp wameenda dubai.
Wamisri wakimtimua Mubarak na kumweka El Baradei nitawaona watu wa ajabu sana. But again inaonekana watu wote wenye uwezo wa kutawala either ni wazee, wako associated na mubarak na chama chake au wanatoka wings za muslim brotherhood.

Hizi romours umezipata wapi mkuu?
 
Leo ni siku ya Saba (Jumatatu) ya maandamano ya kumtoa Mubarak katika madaraka,kuna utulivu wa uvunjwaji wa sheria kama uizi (looting),na utupaji mawe hovyo mitaani,pia kumekuwa na milio michache ya risasi si kama ilivyokuwa siku za nyuma.Maandamano makubwa yanaelekea tena Tahir Square kutoka katika kila pande za mji wa Cairo.Ndege za Jeshi zimekuwa zinaruka chini chini karibu maeneo yote ya mjini haswa Tahir Square ambako baadhi ya waandamaji wamelala hapo.Habari kutoka Al-Jazeera zinasema Rais Hosni Mubarak bado yupo Cairo na Jana Jumapili akifuatana na VP mteule Omar Suleiman alitembelea kambi za Jeshi zilizopo karibu na Mji wa Cairo.Mke wa Rais Suzzane Mubarak pamoja na Mtoto mkubwa wa Rais Gamal Mubarak wamekimbilia London.Kuna taarifa kuwa Rais anaandaa utaratibu wa kukimbilia uhamishoni Riyadh (Saudi Arabia) au Tel Aviv (Israel)...Jumapili mchana jumla ya ndege binafsi 17 zimeondoka Cairo kuelekea UAE na inasemekana zilikuwa zimechukua familia za matajiri kutoka Cairo.Miongoni mwa walioondoka ktk msafara huo yupo Mohammed Al Amoudi ambaye yupo katika forbes billionnaire wa 2010.

Serikali ya Marekani imefunga Ubalozi wake mjini Cairo na Balozi wa Marekani Nchini Misri Mama Margaret Scobey amewataarifu raia wote wa Marekani wanaotaka kuondoka Misri wawasiliane na Ubalozi huo na kuanzia Leo (Jumatatu) mchana kuna ndege zitakazowasafirisha watu kuelekea Washington na New York,inasemekana kuna Jumla ya Waamerika 50,000 Nchini Misri.Waziri wa Ulinzi wa US,Robert Gates amekuwa kwenye simu na Mkuu wa Majeshi wa Misri na Israel kwa karibu masaa manne siku ya Jumapili,kwa vyovyote itakavyokuwa,ni wazi kwamba Rais Mubarak ataachia madaraka na kutaundwa serikali ya mpito kuelekea Uchaguzi.Maamuzi yoyote yatakayombakisha Rais Mubarak madarakani yatazidi kuleta maafa.Jumla ya watu 120 wamekufa katika miji ya Cairo,Alexandria na Suez.

Wamisri wanaoishi katika Nchi za Marekani,Canada,Uingereza na Ujerumani wamekuwa wanazishikiza Nchi hizo wamuombe Rais Mubarak aachie uongozi ili apishe uchaguzi huru na wa haki.

Kumekuwa na maandamano katika nchi za Jordan,Yemen na wanafunzi wa Nchini Sudan wameandamana kuunga mkono maandamano ya Misri.Vuguvugu hili la maandamano lilianzia Tunisia ambako mhitimu wa chuo kikuu alijichoma moto baada ya kubugudhiwa na askari wa mji alipokuwa anauza mboga mboga bila kuwa na kibali.Wimbi hilo limepita pia Algeria ambako bei ya mkate imepanda sana.Nchini Libya kumetolewa onyo kali kuhusu namna yoyote ya mkusanyiko wa watu,matumizi ya simu,na intaneti yamekuwa yakisikitishwa kila wakati katika Nchi hiyo iliyopo karibu na Misri na Tunisia.
 
Mbarak appoints new minister for interior security. He is still hanging on
 
rumour has it Mubarak has left the country na inawezekana yuko UK vile vile matajiri kadhaa na kiongozi wa ndp wameenda dubai.
Wamisri wakimtimua Mubarak na kumweka El Baradei nitawaona watu wa ajabu sana. But again inaonekana watu wote wenye uwezo wa kutawala either ni wazee, wako associated na mubarak na chama chake au wanatoka wings za muslim brotherhood.

Hosni Mubarak bado yupo na ataendelea kuwepo nchini Misri kwa muda ila mwanae Gamal amekimbilia UK ambako ana nyumba na pia anamiliki pasi ya kusafiria ya UK.

Watu wengine ambao ni mashuhuri au "prominent" wamekimbilia nchi za jirani kama Saudi Arabia na Oman na wengine wenye fwedha lukuki wapo Ulaya au Marekani.

Hio ndio hali halisi mkuu.
 
Dakika chahe zilizopita Bunge la Uingereza limetoa TAMKO la kumtaka Rais Mubarak aachie njia zote kuu za mawasiliano ikiwemo internet, kwa haraka.
 
Kwa mujibu wa Egyptian State TV, kuna maandamano nchi nzima nchini Misri na idadi ya watu mijini Cairo na Alexandria ni zaidi ya mara tatu ya idadi ile ya watu tuliowahi kuona katika siku za mwanzo wa maandamano nchini humo.

Mubarak bado aendelea kushinikizwa na wananchi wake ajiuzulu.
 
Egyptian State TV? Walikuwa na vipindi vya mapishi nashangaa wametangaza saa ngapi. Kesho ndio kuna the biggest rally kuadhimisha wiki moja tokea protest ianze. They expect more than million people will be on the street
 
Vikundi vya Upinzani nchi Misri sasa wapanga MAANDAMANO YA WATU ZAIDI YA MILIONI MOJA kuvamia ikulu ya Rais Mubarak hapo kesho siku ya Jumanne kumtoa kwa nguvu ikulu.

Sasa naona maandamano kuchukua sura mpya kabisaa si ku ya kesho.

Viongozi hao waelezea kwamba hii ni hatua yao katika kutambua kwa namna ya pekee kutimia wiki moja tangu MAANDAMANO NCHINI MISRI ZIIANZE kwa fikra zao wenyewe wananchi wa kawaida.
 
Kuna mwandamanaji moja anasema kwenye mahojiano, "hii ni siku yangu ya tatu mfululizo Tahir (Independence) Square, na nimejiandaa kubakia hapa hata peke yangu katika siku zote za maisha yangu nikiandamana kupinga uwepo wa Mubarak madarakani."

Huyo bwana akaongeza akidai kwamba "isitoshe, nitakua na furaha zaidi nikiuaua hapa hapa Tahir Square kwani ikitokea hivyo nitakua nimetimiza wajibu wangu kutaka uhuru zaidi."
 
Siku ya leo pale Tahir Square kumetapika kabisa waandamanaji; haijabainika wazi kama ndio itakua ni sehemu ya maandalizi ya ONE MILLION MAN MATCH kwenda kumuondoa Mubarak kwa nguvu Ikulu hapo kesho.
 
Friday, January 28, 2011 is being broadcast by Al Jazeera na now as
THE DAY THAT EGYPTIANS LOST THEIR FEAR
to take head-on against the tyrant rule of Mubarak rule.
 
Al Jazera wametangaza kwamba Israel inahofia kwamba kilichotokea Iran (extremists kukamata madaraka) yaweza kabisa ikatokea Misri wakati wowote.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom