Inategemea na maeneo na ukanda pia,pasaka hufunika katika maeneo yaliyo na wakristu wengi,huwezi kwenda kusherekea sikuku ya pasaka zanzibar mana karibia robo tatu ya watu watakuwa katika mfungo wa ramadhan
Hata sikuku ya idi pia ina maeneo yake kwan si kila sehemu kuna waislam wa kutosha kuweza kuifanya iwe vibe.Nimekaa maeneo ya Zanzibar kwa mda wa miaka zaidi ya minne ,sikuu zote zimenikuta huko.
Sikuku ya pasaka ukiwa Zanzibar shamla zake hutaziona labda uende kanisani wakati wa usiku au asubui ya pasaka ,kisha ukale pilau lako then uende viwanja huko utapata vibe.kwenye bar vibe lipo na sijui kama wanywaji wana sikuku maalum mana huwa wapo tu.
Miaka ya nyuma mimi kama mkristu kwenye familia yetu tulikuwa hatusherekei kabisa sikukuu zisizo za kikristu.
Yani unaweza kukuta ni siku ya idi lakini tunaenda shamba kulima na hakuna mshituko au mwamko wowote ,miaka ya 90s huko hasa maeneo ya mikoani na sehemu zilizo na wakristu.
lakini sikuku kama pasaka,x-mas na mwaka mpya watu walikuwa hawalali,ilikuwa ni kukesha hadi asubui,
Miaka imeenda baadae mchanganyiko wa watu ukaongezeka,hapa muislam hapa mkristu,lakini sikukuu zilikuwa na vibe la hatari ,watu waliburudika wakubwa kwa wadogo,pilau lilipikwa kila kona ya mji,watu walinunua nguo mpya na zawadi za kutosha.Pilau ilisikika katika pande zote nne za dunia
Nyumba zilikuwa zinafungwa ,watu wote wanatoka nyumban kwenda viwanja,hiyo siku mtu asiye toka nyumban atatoka.wasio pika pilau kwao watapika ,wasio kula nyama watakula
Miaka ya 1990 hadi 2005 kulikuwa na vibe sana kwenye sikukuu ,uchumi ulikuwa sio haba ,wenye kulima walivuna,wafanyakazi mishahara kidogo lakini ilikizi mana tozo zilikuwa sio za kuumizana kama leo hii,bei ya vyakula ilikuwa chini,bei ya bia

ilikuwa chini ,sodo bei poa .
Kiukweli uchumi haukuwa wa kutesana sana,mana hata asiye kuwa na pesa chakula alikuwa nacho,hivyo uhakika wa kupika ubwabwa maharage ulikuwepo
Siku zimeenda mara mikesha ikazuiliwa

,watu kuwepo mtaani mwisho saa sita,marufuku kuwasha mioto wala kulipua fataki hadi kibali maalumu.
Marufuku kupiga mziki hadi kibali maalumu.
Mtaani kusherekea sikukuu mwisho saa sita ,ukikutana na wazee usiku zaidi ya saa sita lazima wakunyanyase tu,ikawa kukimbizana na polisi licha ya kutambua wazi kuwa watu wanasherekea sikukuu

lakin walikomaa tu na saa sita yao eti watu walale na wakati ndo mwanzo vibe linapamba moto.
Maisha yakaenda,uchumi ukawa una dolala kwa mtu mmoja mmoja

tozo zikapamba moto,mvua hazinyeshi,mtu analima lakini havuni,mfanya kazi ndo angalau ,lakini vitu bei ipo juu,ukishika hela inapotea utazani kuna chuma ulete
Ikafika mahali hata polisi hawasumbuki na kufukuza mtu mtaani,ikifika saa tatu unajirudiaha tu nyumbani mwenyewe,mana hela huna utaenda wapi sasa! Na ukafanye nini!
Watu wakawa wanaenda makanisani usiku wakitoka huko wanaelekea kulala tu,hakuna vibe la mkesha tena,upepo wa kiuchumi haupo poa,kila mmoja mnyonge yani hakuna mwamko wa kisherekea kabisa .
Kesho yake watu wanapika kilo mbili za pilau wanakula wanamaliza ,hata hela ya soda wengine walikosa je ya kwenda viwanja itapatikana?

Watu wakawa wapole,siku ya sikukuu , saa tutu tu za usiku mitaani panakuwa peupeee ,watu hakuna kila mmoja yupo makwao kulala.Disco zinapogwa ila watu ni wakuhesabu na ni wale wanao jiweza kidogo tu.
Ikafika mahali mwenye pesa yake ndo mwenye sikukuu kama huna pesa wewe huna sikukuu ,watu wakazoea mwishowe sikuu imekuwa ya kawaida na watu wanaichukulia poa tu
Yani ni bora uzima ,bora tumefika,bora tumeuona mwaka ,mengine majaaliwa.

Sikukuu ina vibe

,sikukuu ni furaha ,sikukuu ni amani ya dunia sikukuu ndo uzima wa mwanadamu ,sikukuu ndo kila kitu katika maisha ya duniani ,mana tupo kwa furaha ,siku zetu ni chache za kuishi na uwepo wetu haujirudii .
Tufarahini inapobidi na tufahi kwa amani ,hata kama huna kitu we furahi tu ila sikukuu zilikuwa na vibe sana zamani kuliko sasa.