Moneytwister
JF-Expert Member
- Jul 22, 2022
- 316
- 1,032
Eid inabamba sana Dar es salaam ila kwa sisi tuliopiga misele uko mikoani x-mas ndo baba lao kuna eid moja ilinikuta mbeya aise utafikir sio sikukuu watu wamepoa vibayaa mnoo
Duh!mfia dini kwenye ubora wako!pole sana mzeeKufananisha sikukuu ambazo ni ibada na sikukuu zisizofahamika mwanzo wake isipokuwa kutoka kwenye ushirikina huweza kukupelekea ukakufuru kabisa,kuwa makini mara nyingine unapouzungumzia uislamu mkuu, hakuna mtu aliyewahi kupata hasara kwa kunyamaza, kama huna cha kuandika unanyamaza tu.
abdulqadirj
Vipi mkoani kwenu? Hakunaga vibe?Idd inabamba Temeke Mbagala , kigamboni , kisemvule huko mkuranga hizi ni Islamic province lazima vibe liwe juu
Kufananisha sikukuu ambazo ni ibada na sikukuu zisizofahamika mwanzo wake isipokuwa kutoka kwenye ushirikina huweza kukupelekea ukakufuru kabisa,kuwa makini mara nyingine unapouzungumzia uislamu mkuu, hakuna mtu aliyewahi kupata hasara kwa kunyamaza, kama huna cha kuandika unanyamaza tu.
abdulqadirj





Kwa hii orodha mkuu, utakuwa unaishia Kijiji I mno tena ndani ndani sana!Niamini mimi..kule sikukuu kwa mpangilio ni hivi
1.Mwaka Mpya
2.Krismass
3 Pasaka
4 Nanenane
Hizi zilizobaki ni kama ziko sawa tu
Muungano, Eid, Nyerere day, Mapinduzi, Sabasaba nk.
Mkuu itakua unaishi idodi au mtera kama ni kule basi sawa maana hata msikiti hakunaNiamini mimi..kule sikukuu kwa mpangilio ni hivi
1.Mwaka Mpya
2.Krismass
3 Pasaka
4 Nanenane
Hizi zilizobaki ni kama ziko sawa tu
Muungano, Eid, Nyerere day, Mapinduzi, Sabasaba nk.
Kariakoo kukiwa na mzunguko mkubwa neema yake inafika hadi KilimanjaroIla sio kilimanjaro
SawaKariakoo kukiwa na mzunguko mkubwa neema yake inafika hadi Kilimanjaro
Hiyo misafara ya kwenda Moshi mwisho wa mwaka inachagizwa na kilichotokea siku 40 zilizopitaMmesahau ile misafara inayoelekea kaskazini kwaajili ya sikukuu za mwisho wa mwaka hii skukuu ya idi sawa ni kubwa ila ukiongelea amsha amsha amsha asee achana kabisa na xmass hao waislamu wenyewe wanasubiri maana kila kona ni nyimbo kuanzia tarehe 15 mpka mwaka unaisha![]()
😂 mkuu naishi Town kabisa Pasiansi hapa.Kwa hii orodha mkuu, utakuwa unaishia Kijiji I mno tena ndani ndani sana!
Nane nane😂😂
SawaHiyo misafara ya kwenda Moshi mwisho wa mwaka inachagizwa na kilichotokea siku 40 zilizopita
Km hujaingiza cha kutosha huwez kuwa kwenye msafara utaishia kupiga simu tu kuwajulia hali
Au labda uwe chawa kwa wenye nazo
Mkuu itakua unaishi idodi au mtera kama ni kule basi sawa maana hata msikiti hakuna
Achana na nane nane, Kuna vijiji sikukuu zao ni siku ya Gulio/Mnada hapo watu watapiga monde, watagegedana na watoto ndo siku ya kuvaa vizuri na kutembeleana wataenda gulioni kununua mahitaji yao na kuinjoi, watu wazima na wazee watakesha Gulioni siku hiyo.Inategemea uko wapi. Kuna kipindi nilikuwa sehemu fulani zaidi ya mwaka.
Huwezi amini NANE NANE ndio sikukuu inayobamba maeneo hayo, kuliko zote hizo zilizotajwa.
Ok ni kweli kanda ya ziwa nane nane Ina nguvu sana😂 mkuu naishi Town kabisa Pasiansi hapa.
Mzee kwa Mwanza umuhimu wa Eid ni kwa wanafunzi tu kufuraia kutoeenda shule, ni kama ilivyo nyerere day au sabasaba.
Ila atkeast nanenane watu huwa wanaifurahia kwa kwenda kwenye maonesho na watoto kucheza michezo mbalimbali kama kushinda soda kwa kurusha ringi.
Uko simiyu kama sikoseiEid ni mwisho kabisa mkuu, huku nilipo hata hawajui kama kuna sikukuu ya eid na vile iko jumamosi ndo kabisaa, watoto hawaendi shule kisa ni weekend.
Yaani hawajui kitu kuhusu uislam, hizi sikukuu ni eneo na eneo. Huku nanenane na sabasaba zinabamba kuliko eid aisee.