EGMA (kampuni ya Kitilya na Mboya) vs Stanbic bank

EGMA (kampuni ya Kitilya na Mboya) vs Stanbic bank

Hivi sheria zinasemaje. Inakuwaje bosi wa TRA anakuwa mkurugenzi wa kampuni binafsi inayofanya udalali wa kifedha.Mgogoro wa kimaslahi lazima utaibuka tu.
 
Mpaka majipu yanaisha huyu mgonjwa atakuwa ameshakufa.
 
Ombeni sefue katumbua jipu zito ITV jamani

Kumbe ile kampuni iliyotupiga ikishirikiana na Stanbic bank wahusika ni Harry Kitilya aliyekuwa kamishina mkuu wa TRA na Mboya. Sasa ukitaka kujua dunia haramu +na yule miss utaelewa sasa na yeye aliingizwaje!!

Mh. Magufuli, kurudishiwa hela haisaidii tunataka walioohongwa wafungwe waende ndani.

SFO wametaja waliohusika ni mzee wetu H. Kitilya na Mboya. Kuweka nchi iwe na adabu wapelekwe mahakamani na kesi isikae mizezi 3.

Na kama wao wana ama walitumika kama middleman wasema top nani.

Taarifa ya SFO inasema wazi kuwa Harry Kitilya alikuwa kwenye timu maalum ya serikali ya Tanzania iliyokuwa inahusika kutafuta huo mkopo na wakati huo huo alikuwa ni 'wakala' wa Stanbic bank! Huu ni uhuni na utani uliopitiliza! Kamishna wa Internal Revenue (appointed by the President) anajigeuza kuwa agent wa Bank tena wakati anaongoza mazungumzo kati ya serikali na hiyo Bank? Sasa kwenye meza ya mazungumzo alikuwa anawakilisha upande gani? Serikali au wakala?

Lakini kuna kitu kingine hapa, Shose Sinare kama sikosei ni mtoto wa Dr Hawa Sinare. Huyo mama ni mjuzi wa 'double agent system'. Rex Attorneys ambako ndiko aliko huyo mama walifanya hivyo hivyo kwenye mgogoro wa Dowans na Tanesco, walikuwa wanawakilisha pande zote! Yote tisa, kumi, Dr Hawa Sinare aliteuliwa kuwa mwenyekiti wa bodi ya Kahawa wakati huo akiwa anasimamia (kama wanasheria) uuzwaji wa mali za KNCU!. Na siku chache kabla ya uchaguzi akatangaza kujiondoa CCM na kumuunga Lowassa mkono. Sasa binti yake ndio hivyo yuko kwenye saga ya Stanbic. Shida.
 
OMG! Nakumbuka issue ya KNCU ....sasa ndio muelewe kwanini hadi wazee kama Warioba, Butiku n.k walisimama kuhakikisha EL hapiti .....tungegawa nchi mdomoni wa watu hatari mno .....
 
Kitila ni mwizi na anajulikana toka zamani. Tra alifukuzwa kimia kimia bila yeye kujua
 
Lipumba sasa apewe u GAVANA WA BANK KUU, maana hii siyo nafasi ya CHAMA au Ukada na katiba haimfungi Rais kumteua Lipumba kuwa Gavana wa BOT, anaweza tusaidia haa wengine wezi tu mpaka kero
 
Lile jina la aliyekuwa Miss linafanana na yule mama aliyehama ccm kwenda cdm wakati wa dakika za mwisho...je wana uhusiano wowote?
 
Uyo uyo kwenye uzi wake wa nan anastaili kuwa waziri wa fedha,jamaa kamsifia sana Kitilya,kumbe mpiga dil tu

Ni nani nchi hii msafi?? Hata huyo Magu mbona nae kaiba, ile Hotel kwani kajenga kwa pesa zake??
The Boss alikuwa anaongelea ujuzi na uzoefu wa Kitilya na angeisaidia vipi nchi kukuza Uchumi wetu..

Hivi hata wewe kila unakogeuka unaona wenzako wanaiba tu, hivi na wewe utaacha kufanya hivyo?? Si tunasemaga Samaki mmoja akioza au?? Hakukuwa na msafi yeyote kwenye serikali ya JK
 
Last edited by a moderator:

Acha kuhalalisha wizi mkuu,Mwizi nyumbani kwake jela mkuu na cyo kupewa wizara ya fedha
 
Kwanza nampongeza Kitilya kufungua consultancy baada ya kustaafu na sio kwenda kulima au kufuga ngombe na kuku!, ili at such senior position, ukistaafu unaendelea kufanya kazi za brain power!.

Iwapo alikuwa silent partner tangu yuko TRA, hapo ndipo kwenye conflict of interest ashitakiwe tuu kwa kufanya biashaa akiwa mtumishi wa umma ila kesi ya kwanza iwe ile ya wamiliki wa kampuni ya AnBen maana walifanya biashara wakiwa ikulu!, tena hapa kinga ya kutokushtakiwa haihusiki, kwa sababu ile kinga inahusu majukumu yake tuu ya kiais akiwa ikulu, kufanya biashaa ikulu sii miongoni mwa majukumu ya mpangaji wetu tuliyempangisha kwenye ile nyumba!.

Lakini kuna kitu kingine hapa, Shose Sinare kama sikosei ni mtoto wa Dr Hawa Sinare. Huyo mama ni mjuzi wa 'double agent system'. Rex Attorneys ambako ndiko aliko huyo mama walifanya hivyo hivyo kwenye mgogoro wa Dowans na Tanesco, walikuwa wanawakilisha pande zote! Yote tisa, kumi, Dr Hawa Sinare aliteuliwa kuwa mwenyekiti wa bodi ya Kahawa wakati huo akiwa anasimamia (kama wanasheria) uuzwaji wa mali za KNCU!. Na siku chache kabla ya uchaguzi akatangaza kujiondoa CCM na kumuunga Lowassa mkono. Sasa binti yake ndio hivyo yuko kwenye saga ya Stanbic. Shida.
Shose ni Senare, binti wa Melckzedec Senare (RIP), mtangulizi wa Kitilya pale TRA!. Dr. Hawa ndio Sinare, mwanasheria nguli, na mwalimu wa kujitolea wa sheria UDSM!.

Pasco
 
Ningeomba THE BOSS aje alisemehe ili maana anamkubal sana uyo KITILYA

Ndo maana nilitoa list
ili wachunguzwe alie clean apewe

lakini nikuambie kitu
kuna bad boys wa finance na economics kama football tu

kuna Maradona na Suarez na Baloteli pia..
ni wazuri wakituliza vichwa kuisaidia timu
ingawa pia na bad boys...wakipata upenyo ndo kama hivyo....

ukweli unabaki pale pale hivi ni vichwa vikitumika vizuri nchi inasogea
tazama TRA walikuwa wanakusanya ngapi kwa mwezi kabla ya kitilya
au kabla ya Bade.....
 
so nilichosoma na hakisomeki ni kuwa,mtoto wa mgimwa karudi Tanzania,ghafla kapata kazi bank.Then anaingia kwenye high level meetings na wakubwa wake then anaanda mikutano.

okay, anaacha kazi tena anarudi London. 😄😄

sad story mzee mgimwa anakufa south africa kwa kuugua ghafla .😅😅
hii nchi ngumu sana aise
 
Dah inasikitisha kuona uingereza inatusaidia kuibua madudu yetu, hivi hao mabalozi wanakazi gani huko abroad, nikweli hawajui maofisa wetu wanapokuja huko wanafanya madudu gani, ofisi zao huwa wapo waambata kibao mpaka maofisa usalama, ila nasikia wanalipwa mishahara duni, (but where is loyalty) hata hvyo nyie maofisa waandamizi, nyie wasomi wetu kwenye positions muhimu ni mbwembwe tu, majivuno, suti, magari na nyumba zakifahari, lakini ni aibu tu. Huwa mnajidai tu lakini hamna lolote. Yani mmeitia aibu nchi na raia wake. Hamna hata aibu, nasasa mnaumbuka.

Hawa SFO wanapiga kazi sana sababu wako kibiashara zaidi. Hela wanayotakiwa kulipwa na Stanbic kwa kushinda kesi ya sakata hili ni ndefu kuliko hata tuliyopigwa siye, achilia mbali na faini.
 
Hio Kampuni mbali ya Kitine na Mboya Shareholder mwengine ni Jamaa Mmoja M kenya anaitwa Peter Nyabuti. Huyu Jamaa ana sifika kwa Rushwa katika secta ya Bima. makampuni ya serikali yote yametiwa ndani na Jamaa huyu wa Kenya na Kampuni yake ya ASTRA ndio inayo pewa kazi zote za mashirika ya Umma.
amekua akitoa rushwa kubwa sana huko TPA BOT TPTC TTCL PPF TANESCO , TRA Na kwengine . Ni mkenya lakini cha kushangaza makampuni haya ya Hawataki kabisa kuwatumia wazawa . Kumbe anashirikiana na Kitine kupata hizi tenda.

imekua tabu kwenye secta hii kwa local brokers kuendelea kwa rushwa kubwa ya huyu Nyabuti na kampuni yake. Lakini cha kushangaza zaidi ni sheria ya Bima yenyewe imetengenezwa kuwapa ilaini wageni kufungua Brokers Tanzania.
Mgeni akiwa na 15m basi anatafuta mwenyeji boya na anaruhusiwa kupewa leseni na kamishna ambaye ni mbishi sana katika kulinda soko hili..yeye amekua ndio kikwazo kikubwa kwa local kampuni.

JPM mfumo wa Tenda ubadilishwe na Tunaomba kampuni za nje ya Bima ya Broker ziwekewe masharti magumu kupata leseni ikiwa pamoja na mtaji wa kuweka Bank kuu kwa uchache iwe USD 250,000.
HAIWEZEKANI TUWE WAPUMBAVU WAGENI WAJE TU HALAFU WATOE RUSHWA NA BAADA YA KUPATA WANAANZISHA HIZI KAMPUNI NYENGINE KUIBIA SERIKALI
 
Sefue ametumia lugha laini mno! Anasema kama kuna watu walihongwa! Kah!!! Waingereza wamesema wazi kuwa zile pesa zilitumika kuwahonga maafisa wa serikali Tanzania!

Sefue anataka kuweka credit kwa benki kuu Tanzania kitu ambacho Nina mashaka nacho, benki nao in watuhumiwa katika hili! Ningewaelewa kama wangekuwa wa kwanza kukamata hawa wezi na kuwafikisha kwenye vyombo vya dola bila kusubiri hisani ya waingereza kutukamatia!

Kama waingereza wasingefuatilia sidhani kama hii pesa ingerudi! Inaonekana kabisa hapa kuna ubia wa uovu kati ya benki kuu na stanbic bank! Haiwezekani hii benki ikawa inatoa Fedha cash kwa mabilioni katika muda mfupi bila kuwa na hofu na benki kuu kama hawana ubia! Wakati wa sakata la escrow ni hawa hawa waliruhusu pesa zichukuliwe kwenye viroba kwa mabilioni na mpaka Leo "wamegoma" kutoa orodha ya wahusika na wanaendelea na biashara kama kawaida pamoja na bunge kupiga makelele!

Namwomba Magufuli awatembelee kwa kushtukiza na awaombe hiyo orodha ya escrow tuone kama naye watamgomea! Hilo jipu linamsubiri Magufuli maana watanzania wanalijua japo nasikia inasemekana limekaa pabaya!! Tukubali tuna matatizo makubwa ya uadilifu benki kuu, wanakubali kutumiwa na mafisadi!
Kwa jinsi Sefue anavyoongea je kama Ikulu ilishiriki wakati huo je yeye atapoma maana sasa hivi anajifanya mkali wakati kipindi kile alikuwa mstari wa mbele kutetea uovu wa Ikulu na hakuwa upande wa wananchi.
 
Kuna mmiliki mmoja wa Hiyo kampuni ni marehemu,kila nikiona SFO namkumbuka kamanda Yericko Nyerere alivyotumbua jipu la ? 1.5m
huyo kamanda wako wakipuuzi aje tena aendelee na zile porojo zake kwenye serikali hii ya magufuli aone moto wake. maana alikuwa mzushi aliyepitiliza kwa kutuletea uongo humu.
 
Back
Top Bottom