EGMA (kampuni ya Kitilya na Mboya) vs Stanbic bank

EGMA (kampuni ya Kitilya na Mboya) vs Stanbic bank

Naamini kabisa pesa nyingi kama hii mpaka bank itoe kuna idhini ya bank kuu BOT, nafikiri ndani ya BOT kuna uozo wa hali ya juu, hii Stanbic hata mwaka mmoja haujapita imetoka kupiga dili la Escrow, je hawa na bank ya mkombozi wako juu ya sheria za bank kuu?
Gavana mkuu ana nini mpaka sasa anatazamwa tu?
Pale BOT ajira nyingi za watoto wa vigogo wasio na ujuzi kabisa,
 
Wizi huu umefanywa na Kamishna Mkuu wa Zamani TRA Kitilya ka ushirikiano na Mkurugenzi Mtendaji wa Zamani wa Stanbic Bank ambae pia alikuwa Mratibu wa Kampeni wa Ndugu Lowassa anaitwa Bashiru Awale alietimuliwa hivi karibuni hapa nchini walizidisha deni kwa dolla million sitta sawa na 15 Billion tsh. Iligundulika baada ya Maofisa wa BOT kuhisi huo mchezo
 
Kipindi cha BBC outsource alihojiwa yule mpelelezi wa rushwa kubwa SFO akadai Tanzania viongozi wetu wanashiriki rushwa wakishirikiana na Stanbic bank na akadai watatoa taharifa nyingine ya Rushwa waliopata viongozi wetu maana wanatoa mpaka wawe na uhakika hawabahatishi..nilichoshangaa ni kwamba wao wanasema kuna uwizi sana hapa na wao wanazo taharifa watatoa mpaka wawe na vithibiti kamili kwa nini serikali yetu isiwatume watu kadhaa kujua huo wizi kuriko kusubiri miaka kadhaa watoe katika link zao..
 
Naamini kabisa pesa nyingi kama hii mpaka bank itoe kuna idhini ya bank kuu BOT, nafikiri ndani ya BOT kuna uozo wa hali ya juu, hii Stanbic hata mwaka mmoja haujapita imetoka kupiga dili la Escrow, je hawa na bank ya mkombozi wako juu ya sheria za bank kuu?
Gavana mkuu ana nini mpaka sasa anatazamwa tu?
Pale BOT ajira nyingi za watoto wa vigogo wasio na ujuzi kabisa,

Wizi huu umeanza kabla ya Escrow ilikuwa 2013
 
Huyo sefue inabidi ajipime kama bado anafaa katika huu mfumo magufuli au la.anawalinda bot kwa kumun'gunya maneno.
 
Wizi huu umefanywa na Kamishna Mkuu wa Zamani TRA Kitilya ka ushirikiano na Mkurugenzi Mtendaji wa Zamani wa Stanbic Bank ambae pia alikuwa Mratibu wa Kampeni wa Ndugu Lowassa anaitwa Bashiru Awale alietimuliwa hivi karibuni hapa nchini walizidisha deni kwa dolla million sitta sawa na 15 Billion tsh. Iligundulika baada ya Maofisa wa BOT kuhisi huo mchezo

Mkuu BOT hawajui kitu maana hawa jamaa kabla hawajaanza uchunguzi wanahojiwa kwa kitu wanachotaka kufanya katika kipindi bbc kama si outsorce ni hardtalk harafu inaweza pita hata mwaka wanakuja na mrejesho wa kazi yao sasa wanadai kuna Rushwa kubwa ingine ni vile umeme ndio tatizo kama unawafatilia utajua mengi kuriko hao BOT unaowasema maana wanasubiri kama sisi tu kupata taharifa za uwizi wa fedha..
 
Kuna mini katika utendaji wa taasisi zetu kushindwa kuweka wazi madudu ya wizi hadi tungoje nchi za nje hasa uingereza wayaibue. BOT, STANBIC wachunguzwe ushiriki wao katika wizi na kuchukuliwa hatua. Sasa kazi tu.
 
Mkuu BOT hawajui kitu maana hawa jamaa kabla hawajaanza uchunguzi wanahojiwa kwa kitu wanachotaka kufanya katika kipindi bbc kama si outsorce ni hardtalk harafu inaweza pita hata mwaka wanakuja na mrejesho wa kazi yao sasa wanadai kuna Rushwa kubwa ingine ni vile umeme ndio tatizo kama unawafatilia utajua mengi kuriko hao BOT unaowasema maana wanasubiri kama sisi tu kupata taharifa za uwizi wa fedha..

Maafisa wa BOT ndio waliohisi huu mchezo baada ya kufanya reconciliation kati ya deni lililo ripotiwa na Stanbic Tz na Stanbic UK wakaona tofauti kufuatilia hiyo tofauti wakakuta ni Agent fee ambayi haikuwa kwny mkataba na ilipitia kweny kampuni ya Kitilya ndipo ikaomba Msaada wa SFO
 
Du! ama kweli Tanzania ni zaidi ya tuijuavyo. Wazungu walihangaika na chenji ya RADA hadi ikapatikana. Kilichofanyika kutokana na hiyo chenji hakionekani hadi leo na wahusika wanaendelea kula bata mtaani na wengine hadi leo ati ni WATUNGA SHERIA WA NCHI YETU.

Leo Wazungu hao hao wamehangaika kufunua uozo uliokithiri kwenye mkopo, wametutajia hadi wahusika japo naamini kunma wengine zaidi ya hao waliotajwa, badala ya kukamata hao waliotajwa na kuanza kushughulika nao Serikali inadiriki kusema ati inaendesha uchunguzi. Kama walipiga mchana kweupe na mkajifanya hamuoni, leo hii Serikali hiyo inataka kuchunguza nini.

Naamini hiyo kashfa hata HAZINA kwa maana ya Waziri na waandamizi wengine wanahusika na walijua hilo mapema sana kwani mikataba ya kukopa inapitiwa na kuidhinishwa na HAZINA
 
Jpm tumbua majipu ya wapiga dili wa ccm,hili linagusa wizara ya fedha,fyeka wote,filisi wote,peleka mahakaman.Kwenye hili Mwigulu,Saada na jk wamo.Cjui rais wa awamu kaz yake ilikuwa nini hasa?
 
AISEE OMBENI SEFUE KATUMBUA JIPU ZITO ITV JAMANI

KUMBE ILE KAMPUNI ILIOTUPIGA IKISHIRIKIANA NA STANBIC BANK WAHUSIKA.N HENRY KITILYA XTRA ....NA MBOYA ...SASA UKITAKA KUJUA DUNIA HARAMU +NA YULE.MISS UTAELEWA SASA NA YEYE ALIiNGIZWAJE

MH MAGUFULI KURUDISHIWA HELA AISAIDII TUNAKA WALIOOHONGWA WAFUNGWE WAENDE NDANI..SFO WAMETAJA WALIOHUSIKA N MZEE WETU H KITILYA NA JAMAA MMOJA SOMEBODY MBOYA..KUWEKA NCHI IWE NA ADABUWAPELEKWE MAHAKAMANI NA KESI iSIKAE MIZEZI 3..

NAKAMA WAO WANA AMA WALITUMIKA KAMA MIDDLEMAN WASEMA TOP NANI..
ni EGMA, sio EFGM. na ni Harry, sio Henry
 
Maafisa wa BOT ndio waliohisi huu mchezo baada ya kufanya reconciliation kati ya deni lililo ripotiwa na Stanbic Tz na Stanbic UK wakaona tofauti kufuatilia hiyo tofauti wakakuta ni Agent fee ambayi haikuwa kwny mkataba na ilipitia kweny kampuni ya Kitilya ndipo ikaomba Msaada wa SFO

Mkuu nachosema SFO wanachunguza hata msipoomba msaada nakukumbusha kesi ya Rada na sasa ivi wamesema wanachunguza uwizi mwingine ambao umefanywa kwa kupitia Stanbic na yule Mpelelezi alisema wao kazi yao ni Kuchunguza Grand Corruption na si lazima waombwe wakihisi tuu..kama BOT wanajua waseme saa izi kilichopo mbele maana wale SFO washaanza uchunguzi kwa kesi ingine au wewe ambae unajua nijulishe Mkuu..
 
Dah inasikitisha kuona uingereza inatusaidia kuibua madudu yetu, hivi hao mabalozi wanakazi gani huko abroad, nikweli hawajui maofisa wetu wanapokuja huko wanafanya madudu gani, ofisi zao huwa wapo waambata kibao mpaka maofisa usalama, ila nasikia wanalipwa mishahara duni, (but where is loyalty) hata hvyo nyie maofisa waandamizi, nyie wasomi wetu kwenye positions muhimu ni mbwembwe tu, majivuno, suti, magari na nyumba zakifahari, lakini ni aibu tu. Huwa mnajidai tu lakini hamna lolote. Yani mmeitia aibu nchi na raia wake. Hamna hata aibu, nasasa mnaumbuka.

Hivi unafikiri Uingereza wamejua tu bila kupenyezewa vitu na maofisa Wa hapa ? Au unafikiri SFO hakuna maofisa Wa Tz haya mambo tuyaacheni kama yalivyo
 
Sefue ametumia lugha laini mno! Anasema kama kuna watu walihongwa! Kah!!! Waingereza wamesema wazi kuwa zile pesa zilitumika kuwahonga maafisa wa serikali Tanzania!
Sefue anataka kuweka credit kwa benki kuu Tanzania kitu ambacho Nina mashaka nacho, benki nao in watuhumiwa katika hili! Ningewaelewa kama wangekuwa wa kwanza kukamata hawa wezi na kuwafikisha kwenye vyombo vya dola bila kusubiri hisani ya waingereza kutukamatia!
Kama waingereza wasingefuatilia sidhani kama hii pesa ingerudi! Inaonekana kabisa hapa kuna ubia wa uovu kati ya benki kuu na stanbic bank! Haiwezekani hii benki ikawa inatoa Fedha cash kwa mabilioni katika muda mfupi bila kuwa na hofu na benki kuu kama hawana ubia! Wakati wa sakata la escrow ni hawa hawa waliruhusu pesa zichukuliwe kwenye viroba kwa mabilioni na mpaka Leo "wamegoma" kutoa orodha ya wahusika na wanaendelea na biashara kama kawaida pamoja na bunge kupiga makelele! Namwomba Magufuli awatembelee kwa kushtukiza na awaombe hiyo orodha ya escrow tuone kama naye watamgomea! Hilo jipu linamsubiri Magufuli maana watanzania wanalijua japo nasikia inasemekana limekaa pabaya!! Tukubali tuna matatizo makubwa ya uadilifu benki kuu, wanakubali kutumiwa na mafisadi!
Stanbic Tanzania In Financial Scandal Scandal - Bing News
 
Back
Top Bottom