EGMA (kampuni ya Kitilya na Mboya) vs Stanbic bank

EGMA (kampuni ya Kitilya na Mboya) vs Stanbic bank

Sefue ametumia lugha laini mno! Anasema kama kuna watu walihongwa! Kah!!! Waingereza wamesema wazi kuwa zile pesa zilitumika kuwahonga maafisa wa serikali Tanzania!

Sefue anataka kuweka credit kwa benki kuu Tanzania kitu ambacho Nina mashaka nacho, benki nao in watuhumiwa katika hili! Ningewaelewa kama wangekuwa wa kwanza kukamata hawa wezi na kuwafikisha kwenye vyombo vya dola bila kusubiri hisani ya waingereza kutukamatia!

Kama waingereza wasingefuatilia sidhani kama hii pesa ingerudi! Inaonekana kabisa hapa kuna ubia wa uovu kati ya benki kuu na stanbic bank! Haiwezekani hii benki ikawa inatoa Fedha cash kwa mabilioni katika muda mfupi bila kuwa na hofu na benki kuu kama hawana ubia! Wakati wa sakata la escrow ni hawa hawa waliruhusu pesa zichukuliwe kwenye viroba kwa mabilioni na mpaka Leo "wamegoma" kutoa orodha ya wahusika na wanaendelea na biashara kama kawaida pamoja na bunge kupiga makelele!

Namwomba Magufuli awatembelee kwa kushtukiza na awaombe hiyo orodha ya escrow tuone kama naye watamgomea! Hilo jipu linamsubiri Magufuli maana watanzania wanalijua japo nasikia inasemekana limekaa pabaya!! Tukubali tuna matatizo makubwa ya uadilifu benki kuu, wanakubali kutumiwa na mafisadi!

Benki kuu na Wizara ya fedha ndio chanzo kikuu cha ufisadi nchini. Bila kuwadhibiti hao tunacheza pata potea
 
Hili jipu huenda likahitaji upasuaji mkubwa na tiba ya ndani endelevu- linaonekana kuwa limezaa vijipu vidogo vidogo. Ingawa kichwa cheke ni EJIMA ( hivi bosi wake yule mweupe mrefu bado hajakamatwa ?), jipu kubwa linawezekana kuwa katikati ya Stambiki, hazina, BIOTI na ofisi ya mwanasheria mkuu wa sirikali. Vijipu vidogo yawezekana vimetanda hadi wizara ya fedha, Magogoni, na kwingineko. Sumu yake (mgao wa Usd 6 M) huenda ilienea sana. Lakini huyu jamaa mrefu , mwembamba na mweupe( za mwizi arobaini) lazima atatwambia.

Jenerali wa Takukuri aliwahi kulalamika( kwa hisani ya wikileaks) kwamba hakukuwa na political will ya kupambana na ufisadi. Sasa hakuna cha kusingizia -Twende kazi kabla sukari hazijapanda !
 
huo marehemu mboya mkewe ndo yule anayeishi makongo juu?
 
Naamini kabisa pesa nyingi kama hii mpaka bank itoe kuna idhini ya bank kuu BOT, nafikiri ndani ya BOT kuna uozo wa hali ya juu, hii Stanbic hata mwaka mmoja haujapita imetoka kupiga dili la Escrow, je hawa na bank ya mkombozi wako juu ya sheria za bank kuu?
Gavana mkuu ana nini mpaka sasa anatazamwa tu?
Pale BOT ajira nyingi za watoto wa vigogo wasio na ujuzi kabisa,

Wizi huu umefanywa na Kamishna Mkuu wa Zamani TRA Kitilya ka ushirikiano na Mkurugenzi Mtendaji wa Zamani wa Stanbic Bank ambae pia alikuwa Mratibu wa Kampeni wa Ndugu Lowassa anaitwa Bashiru Awale alietimuliwa hivi karibuni hapa nchini walizidisha deni kwa dolla million sitta sawa na 15 Billion tsh. Iligundulika baada ya Maofisa wa BOT kuhisi huo mchezo

Kuna mini katika utendaji wa taasisi zetu kushindwa kuweka wazi madudu ya wizi hadi tungoje nchi za nje hasa uingereza wayaibue. BOT, STANBIC wachunguzwe ushiriki wao katika wizi na kuchukuliwa hatua. Sasa kazi tu.

Du! ama kweli Tanzania ni zaidi ya tuijuavyo. Wazungu walihangaika na chenji ya RADA hadi ikapatikana. Kilichofanyika kutokana na hiyo chenji hakionekani hadi leo na wahusika wanaendelea kula bata mtaani na wengine hadi leo ati ni WATUNGA SHERIA WA NCHI YETU.

Leo Wazungu hao hao wamehangaika kufunua uozo uliokithiri kwenye mkopo, wametutajia hadi wahusika japo naamini kunma wengine zaidi ya hao waliotajwa, badala ya kukamata hao waliotajwa na kuanza kushughulika nao Serikali inadiriki kusema ati inaendesha uchunguzi. Kama walipiga mchana kweupe na mkajifanya hamuoni, leo hii Serikali hiyo inataka kuchunguza nini.

Naamini hiyo kashfa hata HAZINA kwa maana ya Waziri na waandamizi wengine wanahusika na walijua hilo mapema sana kwani mikataba ya kukopa inapitiwa na kuidhinishwa na HAZINA
wizara mama ina la kujibu hapa. aliyewahi kuwa waziri wa fedha wakati huo akae mkao!

attachment.php



attachment.php
 

Attachments

  • 1.jpg
    1.jpg
    36.9 KB · Views: 1,222
  • 2.jpg
    2.jpg
    64.7 KB · Views: 1,226
Hivi unafikiri Uingereza wamejua tu bila kupenyezewa vitu na maofisa Wa hapa ? Au unafikiri SFO hakuna maofisa Wa Tz haya mambo tuyaacheni kama yalivyo
ukifanya hizo kazi kwa muda mrefu utajua bila ya hat kuambiwa, kuna some crucial indicators ambazo ndizo zitakazoku-lead. matumizi ya fraud software huusika.
 
Hivi Jakaya lilikuwa chaguo la mungu kweli!? Alikuwa wapi yote haya yanatendeka. Naona aibu kurudi CCM baada ya kuihama kwa sababu ya uongozi wa Jakaya. Eti walioiba EPA warudishe wenyewe pesa bank!! Nyoooooo.
 
...mwenzake na Harry Kitilya (former boss wa TRA) alikua anaitwa Dr. Fratern Mboya (ni marehemu sasa) alikua boss wa CMSA na enzi hizo aliwahi kuwa Dean-Faculty of Commerce and Management - UDSM..

Hapo ndipo kifo huniacha hoi. Unaweza ukawa na pesa nyingi kiasi kwamba unaweza pata matibabu yoyote unayoyataka katika hospital zozote duniani lkn mungu akikung'ang'ania lazima tu roho umkabidhi. Tena kwa kuwa alikuwa mwizi atangulie tu maana hamna namna tena.
 
Hii benki nayo nani anaiwekea uzio, ilitoa mifwedha bila kufuata utaratibi wakaiwekea uzio haijafanywa lolote,
 
Naamini kabisa pesa nyingi kama hii mpaka bank itoe kuna idhini ya bank kuu BOT, nafikiri ndani ya BOT kuna uozo wa hali ya juu, hii Stanbic hata mwaka mmoja haujapita imetoka kupiga dili la Escrow, je hawa na bank ya mkombozi wako juu ya sheria za bank kuu?
Gavana mkuu ana nini mpaka sasa anatazamwa tu?
Pale BOT ajira nyingi za watoto wa vigogo wasio na ujuzi kabisa,

Ungeandika; Pale BOT ajira nyingi za watoto wa vigogo wezi na vibaka na wasio na ujuzi wowote ninge like posti yako. (Unategemea nini kama hao mabosi ndio wezi wakubwa na watoto wao wamewekwa hapo BOT?)
 
Huyo mtoto wa waziri aliyeajiriwa ni Mgimwa??? ndiyo maana alikataa postmortem ya baba yake..

Kweli nchi hii haina wazalendo tutafute consultants waje ku run nchi jaman
 
Hivi unafikiri Uingereza wamejua tu bila kupenyezewa vitu na maofisa Wa hapa ? Au unafikiri SFO hakuna maofisa Wa Tz haya mambo tuyaacheni kama yalivyo

Uzuri wa wenzetu, wana institutions zenye majukumu na mamlaka kufatilia effectively ufanyaji wa biashara kwa kuzingatia sheria za nchi zao, iwe ndani ya nchi zao au nje ya nchi. Wafanya biashara wao ni lazima watoe facts zote katika ma-deal yao...including capital invested, contracts, owners, revenues, financial reports zote, bank statements, expenditures zote, na vithibitisho, audit reports, mikataba ya employees, consultants.....Haya yote wanapokaguliwa nilazima yaendane na masharti ya leseni na vibali ulivyopewa. Vikienda kinyume kuna adhabu za kufungiwa, faini n.k. Na ndio maana Tanzania tunajua thamani za mikataba yetu na wachimba mafuta au gesi au madini ni kwa kutafuta data kwenye vyombo nchini zinakotoka hizi kampuni. sio rahisi kupata hizi data hapa kwetu...(uzembe na u-much know).

Kwahiyo nirahisi kwa wenzetu kugundua makosa kama hayo ya EGMA, Mfano mwingine tazama FIFA sasa hivi...wewe ulijuaje South africa walitoa rushwa kupata kombe la dunia! Ni TRA ya USA inayoitwa IRS, kushirikiana na Mabenki waliweza kunasa matumizi ya anasa ya members wa FIFA mgt... akaingizwa mwanasheria and the FBI.....FIFA mgt yoye chali...you see my friend...

Sie tunao Mwanasheria mkuu, Prosecutors, TAKUKURU, BOT, BRELA, TRA, CAG, BRELA, our Embassy offices abroad wanashindwaje mpaka haya yafanywe na waingereza....ndio hayo nimesema maofisa wetu ni mbwembwe tu. Nina mifano mingi mkuu wrong business practices ambazo wenzetu wanazidhibiti....kama vile rushwa zote, uharibifu wa mazingira, haki za binaadam, kutofata sheria za nchi husika, kukwepa kodi, money laundering, ....
 
Kwa wingi wa majipu haya....inabidi MAGUFURI aongeze speed ya kuyatumbua.....sisi tutamsaidia kuyasafisha.......na kuvifunga bandeji vidonda...,,yeye kazi yake iwe ni kiyatumbua tu....
 
Sasa sisi wananchi tuna raha sana vigogo wanavyodondoshwa tunabembea kiulaini
 

Attachments

  • 1449043851193.jpg
    1449043851193.jpg
    30.9 KB · Views: 336
Back
Top Bottom