eFootball Special Thread

Razorblade imebid niende kufukua mfumo wako wa mara ya kwanza uone utofauti...

AMF sio sawa na SS mkuu
 
Mkuu huu ndo uleule mfumo ambao uliniambia nikiushika nitashinda sana sasa sijui wapi pamebadirika πŸ˜‚.

Selikavu aje aseme hapa kama amenifunga kwa kupita kati, nilienda kwenye mechi kuangalia hilo tobo mnalosema lakini sijaliona.
Nimekuambia twende leo kaka ukaone uzaifuπŸ˜ƒπŸ˜ƒ
 
Nani huyo ningekua mimi chuma ya 8 na πŸƒβ€β™‚οΈ πŸƒβ€β™‚οΈ πŸƒβ€β™‚οΈ
Huyu jamaa yangu shabiki wa liver anaongea mno alafu kitambo tangu 2022 anapost anacheza hili gameπŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒnikamwomba game ya kirafiki akaweka dakika 15🀣🀣🀣na mchezo wangu kwel wa kuvizia dakika 15 nikasema hana. BahatiπŸ˜ƒπŸ˜ƒ mpka nilichoka kufunga nikawa nafika golini napiga mpira kwa kipa wanguπŸ˜ƒπŸ˜ƒ
 
Tamba mkuu wakati wako huu πŸ˜‚

Hujanifunga sababu ya DMF ila huo ni uwezo wako, unacheza friendly nyingi kunizidi kwahiyo kiwango chako hakiwezi kuwa palepale.
Me bado nasisitiza mchezo wa jana kaka sikuwa kwenye ubora maana umefika golin kwangu mara nyingi... Targets yangu siku hizi nikujua kukaba nafasi mpinzani asipite
 
Me bado nasisitiza mchezo wa jana kaka sikuwa kwenye ubora maana umefika golin kwangu mara nyingi... Targets yangu siku hizi nikujua kukaba nafasi mpinzani asipite
Namie nataka kucheza mchezo ambao mtu nikimfunga ajiulize amefungwaje.

Nataka kuhakikisha nacheza mpira rahisi na kuwa mtulivu ndani ya box.
 
Hayo mabadiriko ni sawa na asha na aisha πŸ˜‚

Nilicheza na wewe kwa mfumo ule nikala 6 kwa mfumo uleule pia Selikavu akanifunga mechi 3+.
Second striker sio saww na Attacking midfield...

SS hashuki kufata mipira na moja ya roles zake sio kushuka kusaidia team kukaba yeye anasogea eneo ambalo atapokew mpira chini kdg ya center foward...

AMF anashuka kukaba mkuu anafata mpira chini kabisa huku
 
Nitarudi kukuambia huu mfumo unavyocheza mkuu.
 
Hamna huu mfumo ni mimi ndo sijaushika bado ila unavitu ambavyo nahitaji πŸ˜‚.
Sawaa sikatai kuwa watu wengi wana prefer fowards wengi mbele kuanzia wa nne...

Ila shida kwako ipo kwenye midfield mzee πŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒ
 
Sawaa sikatai kuwa watu wengi wana prefer fowards wengi mbele kuanzia wa nne...

Ila shida kwako ipo kwenye midfield mzee πŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒ
Kwanza tukubali kuwa hakuna mfumo ambao hauna udhaifu ila ni namna gani unaweza punguza huo udhaifu kulingana na mbinu na sifa za wachezaji kwenye maeneo husika.

4-1-3-2 huu mfumo una AMF watatu ambao mmoja anakaa kati na wawili pembeni, nilichobarisha hapo ni kumfanya CAM kuwa SS ambapo bado yupo kwenye nafasi ileile isipokuwa amesogea juu kidogo.

Timu ikiwa haina mpira SS pamoja na hao CF's wanakabia juu na timu ikiwa inashambulia anashuka kupokea mipira kwa mmoja miongoni mwa SMF(R au L) ambae atakuwa ameingia ndani kama namba 10.

Udhaifu wa kwanza hapo upo kwa Mbappe ambaye akienda juu kurudi kuzuia wakati timu inshambuliwa ni mara chache.

Udhaifu wa pili upo upande wa Beckham ambaye speed yake ni ya kawaida kiasi kwamba nikipoteza mpira Trent akiwa juu yeye siyo wakutegemea sana kukulinda.

Udhaifu mwingine kwakuwa nashambulia kwa idadi kubwa maana yake hata mabeki wa kati wanasogea juu kiasi cha kutoa nafasi kwa mpinzani mwenye washambuliaji wenye speed na anaetumia mipira mirefu.

Mstari wowote wa viungo unavunjwa kwa pasi ndefu haijalishi kutakuwa na idadi kubwa kiasi gani ila kama mpinzani ataweza kudondosha mipira nyuma ya viungo wa kati au anaweza kupiga vizuri pasi ndefu hapo kati anaweza pita vizuri tu ila kwa battle ya viungo hapo kati kwangu bado ninao wengi.

Selikavu hataki kukubali kuwa ame improve na badala yake anataka kukaza kuonyesha mfumo wangu kati kuna tobo jambo ambalo hajanithibitishia hata kwa hizo mechi zote alizoshinda, kuwa mkweli mkuu umekutana na Amrabat mara ngapi hapo kati na zote amekupora mipira πŸ˜‚
 
Unakumbuka siku nilikwambia twende uwanjani nikuonyeshe udhaifu wa huu mfumo wako kwenye flanks na nikafanya hivyo sasa na mie nataka uonyeshe udhaifu wa mfumo wangu hapo kati πŸ˜‚
Kaka kama kumbukumbu zangu zipo vizuri mfumo huu tumechezea mchezo wa mwisho achana na ya leo usiku...

Unakumbuka kilichotokeaπŸ˜ƒπŸ˜ƒ
 
πŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒSawaa kaka nisiongee sanaπŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒtukutane leo usiku
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…