EFD: Wafanyabiashara Kariakoo wagoma!

EFD: Wafanyabiashara Kariakoo wagoma!

Operation tuko pamoja daima
Wafanyabiashara wa kariakoo na Tanzania tumeamua kutonunua mashine za EFD kutokana na usumbufu wake , na kwa vile serikali imekataa kuweka mfumo mzuri wa ulipaji kodi, Tar 10 tumeazimia kufunga biashara zetu ili serikali isikie kilio cha watu wake. Mashine hizi zina ufisadi mkubwa kuliko wa Richmond. Tuma kwa watu 100 pamoja na mikoani.jioni njema ndg
 
Hizi mashine zishagoma ccm msilazimishe nasikia na njombe wamegoma pia hii ni hatari
 
Hili ndo tatizo la mipango ya serikali ya kukurupuka.....hapo lengo kwa walioshinikiza hizo mashine halikuwa kusaidia TRA ipate mapato bali wao dili lao lilikuwa kuuza hizo mashine na mpaka sasa wamepiga hela ya maana......AU MMESAHAU YALE MAMBO YA SPEED GAVERNOR? WATZ TUNASAHAU HARAKA SANA NA HII YOTE BCOZ OF NJAA KALI....HII NCHI SHAMBA LA BIBI.
 
Serikali imechemka sana, vile wao wanahela wanajisahau hivi uta mlazimisha mtu anunue hicho kifaa kwa 700,000 wakati hujampa mtaji? Bei yake halali haifiki hata laki 2!!!! Kuhusu sehemu inayo ingiza pesa sana serikali ni bandarini sio kariakoo kama ulivyosema.Nakutakia siku njema
 
Kimsingi lazima watu walipe kodi kwa ajili ya maendeleo ya nchii.ukichangia kwa kulipa kodi wewe kama mlipakodi utaweza kuwawajibisha hao wanaotumia vibaya fedha za walipa kodi ili ukikwepa kulipa kodi utashindwa kuwawajibisha hao wanaokula kodi yako tunaanze kulipa kwanza kodi then tuendelee kuwawajibisha wanaotumia kodi vibaya.
we unajua kodi tunayolipa inakwenda wapi? Au na wewe ni walewale? Watu wanazunguka dunia nzima kuomba omba tu huku wanajiongezea kiinua mgongo bungeni alafu vijijini hamna kitu. We unashabikia uzuzu?
 
Mwigulu yuko wapi? Niliona Mbeya na Songea wakimuita Jembe wafanyaBiashara.
Sasa ni wakati wake kufika KKo ili athibitishe Ujembe wake.
 
Tunataka barabara nzuri, tunataka hospitali zenye huduma nzuri, tunataka huduma nzuri za maji bila kusahau tunataka Elimu bora na ya bure.HII INAWEZEKANA TU KAMA TUTALIPA KODI MBONA WAFANYAKAZI WANALIPA KODI BILA TATIZO.LIPA KODI KWA MANUFAA YA NCHI YAKO
mdau unadhan wafanyakaz ndo tunapenda kulipa kod??lebda wewe,hakuna binadam anayependa kulipa kodi,sema hivi wafanyakaz kwakua tunakatwa moja kwa moja,ila kama ingekua tunalipwa then tunapeleka kod mahali tulipoelekezwa,aaa wapi tusingelipa
 
hii ndio hasara ya serikali kutokuwa sikivu. Waache wafanyabiashara wajinunulie mashine sehemu nyingine, ninyi ni kuwafuatilis sawa sawa kuhakikisha kwamba hawakwepi kodi.
 
Tatizo si mashine, tatizo ni bei ya hizo mashine na ubora wa hizo mashine, mimi nimenunuwa moja mpaka leo wameshindwa kuiunga kwenye kompyuta yangu, wananambia nibadili software kutoka windows 8 kurudi nyuma kwenye windows 2007.

Sasa huo kama si ujinga ni nini?

Na hakuna pakulalamika nimeshakwenda mpaka TRA wananambia mfate wakala, wakala anataka nibadili software au ninunuwe kompyuta yenye software ya kizamani na ibaki kwa kazi hiyo hiyo tu, wakati mimi nnatumia excel na quick-books mpya kwa rekodi zangu za mahesabu.

Hizi EFD ni mzigo tu, ikiwa mimi ambae nna uzoefu wa hii teknolojia ya kompyuta zinanipa taabu seuse mfanya biashara wa Kariakoo ambae hajawahi kutumia hata kompyuta toka kuzaliwa inakuwaje?

Teknolojia za elektroniki zinatakiwa ziondoe matatizo na zirahisishe kazi na zisidishe matatizo.

Waje na kitu mbadala.
 
Bora turudi enzi za duka la kaya kuliko kuwasikiliza hawa watu.wanyang'anywe leseni wote.
 
mwanza hamna mgomo
maduka yapo wazi kabisa hapa ila kulikuwa na tetesi za mgomo
 
Tatizo sio hizo Mashine, tatizo ni %18 kwa kila bidhaa itakakayozwa.!
 
Tatizo si mashine, tatizo ni bei ya hizo mashine na bora wa hizo mashine, mimi nimenunuwa moja moaka leo wameshindwa kuiunga kwenye kompyuta yangu, wananambia nibadili software kutoka windows 8 kurudi nyuma kwenye windows 2007.

Sasa huo kama si ujinga ni nini?

Na hakuna pakulalamika nimeshakwenda mpaka TRA wananambia mfate wakala wakala anataka nibadili software au ninunuwe kompyuta yenye sogtare ya kizamani na ibaki kwa kazi hiyo hiyo tu, wakati mimi nnatumia excel na quickbooks mpya kwa rekodi zangu za mahesabu.

Hizi EFD ni mzigo tu, ikiwa mimi ambae nna uzoefu wa hii teknolojia ya kompyuta zinanipa taabu seuse mfanya biashara wa Kariakoo ambae hajawahi kutuia hata komyuta toka kuzaliwa inakuwaje?

Teknolojia za elektroniki zinatakiwa ziondoe matatizo na zirahisishe kazi na zisidishe matatizo.

Waje na kitu mbadala.

Wewe upo mjini unapata shida hiyo walio wilayani inakuwaje?
 
Kuwapokonya leseni sio suluhisho, hao TRA ndio wanaharibu katika hizo mashine. Suala ni kukaa na kusikiliza madai yao.

Hata wakipokonya tutarudi kwenye uchinga au hata kwenda nchi jirani.ushauri wa bure kwa serikali ifungue viwanda kuliko kutegemea viwanda watu pekee yake ,
 
Back
Top Bottom