EFD: Wafanyabiashara Kariakoo wagoma!

EFD: Wafanyabiashara Kariakoo wagoma!

Anyways..mashine zinaweza kua ni tatizo kwamba bei yake iko juu..ila tukiangalia kinachowapa hasira wafanyabiashara wengi ni ile 18% ya VAT ambayo inasababisha bei ya bidhaa zao kuwa juu na wengi wanahofia kupoteza wateja na pia wengi wao sio wakweli mana walikua wanapeleka hesabu za uongo TRA ili walipe kodi kidogo, sasa mashine zinakuja kuweka ukweli waz na watu hawako tayari kupoteza pato lao!
sio kila mashine ina kata 18%
14m hadi 3999999 mashine inakata 0%
40m hadi ..................................18%

watu wanahofu mashine ikirekodi imerekodi haifutichi karne na karne
kwa hiyo ujanja hamna
 
Mgomo huu si kuhusu mashine tu. Vile vile tunalalamikia kutopewa nafasi ktk Bunge la katiba mpya ( Wafanyabiashara hatuna wakilishi wakati hata wakulima,wavuvi,wafugaji. n.k wamewakilishwa).
 
Jk anahusikaje hapo?
Waache ujinga kulipa kodi ni lazima tatizo wameshazoea kukwepa kodi.

Kwanini asihusike wakati yeye ndo analea ujinga ndani ya serikali yake,
 
Mpaka uchaguzi mkuu ufike tutajikuta hata tukiongea au tukipumua tunatozwa kodi za kifisadi ili chama cha baba kipate pesa za kushinda.Bora punda afe mzigo wa baba ufike.

Wajinga ndio tuliwao
 
Tunataka barabara nzuri, tunataka hospitali zenye huduma nzuri, tunataka huduma nzuri za maji bila kusahau tunataka Elimu bora na ya bure.HII INAWEZEKANA TU KAMA TUTALIPA KODI MBONA WAFANYAKAZI WANALIPA KODI BILA TATIZO.LIPA KODI KWA MANUFAA YA NCHI YAKO

Je vyote hivyo vimepatikana tangia awali ambapo kodi zililipwa pamoja na rasilimali kibao tulizoko nazo? Kama havikupatikanika angali uongozi serikalini ni ule ule?
 
Dada FaizaFoxy nimekupenda Bureee! ukitulia tu ukauweka uchama na unazi pembeni,unaandika kisomi sana, japo najua sometimes huwa unacoment upuuzi just for funy na kuchemsha akili za watu. So suluhisho ni nini mama juu hili jambo ,unafikiri nini TRA wafanye, maana kulipa kuodi ni lazima na ni muhimu kwa maendeleo ya nchi

Hata mie leo kwa kweli amenifurahisha ametoa wazo la uhakika.Hebu jitahidi uwe hivyo kila siku
 
Last edited by a moderator:
Suluhisho ni sahali sana, wafanye kama walivyofanya Singapore. Hakuna asiyelipa kodi na hesabu zote computerized, waende wakaone wenzao wamefanya nini.

Unajuwa Singapore hata vi faini vya mtu sijuwi kala chwingam njiani, katema mate, wanalipia madukani.

Hivi hii mijitu huwa haioni au basi hujifanya ni mapunguani tu, michaga imejazana huko TRA inafanya nini? zaidi ya kuiba tu? Inaonesha ikipewa safari za nje kazi yao ni kulewa tu na hawaoni wala hawajui wanaenda kufanya nini.

acha ukabila ndugu yangu
 
Tatizo si mashine, tatizo ni bei ya hizo mashine na ubora wa hizo mashine, mimi nimenunuwa moja mpaka leo wameshindwa kuiunga kwenye kompyuta yangu, wananambia nibadili software kutoka windows 8 kurudi nyuma kwenye windows 2007.

Sasa huo kama si ujinga ni nini?

Na hakuna pakulalamika nimeshakwenda mpaka TRA wananambia mfate wakala, wakala anataka nibadili software au ninunuwe kompyuta yenye software ya kizamani na ibaki kwa kazi hiyo hiyo tu, wakati mimi nnatumia excel na quick-books mpya kwa rekodi zangu za mahesabu.

Hizi EFD ni mzigo tu, ikiwa mimi ambae nna uzoefu wa hii teknolojia ya kompyuta zinanipa taabu seuse mfanya biashara wa Kariakoo ambae hajawahi kutumia hata kompyuta toka kuzaliwa inakuwaje?

Teknolojia za elektroniki zinatakiwa ziondoe matatizo na zirahisishe kazi na zisidishe matatizo.

Waje na kitu mbadala.

Umeandika kwa kuchapia sana angekosea Dr. W. Slaa hapa kila tusi la zamani ungetukana.
 
Last edited by a moderator:
Hawataki kulipa kodi? Wao si maajenti tu wa kukusanya kodi? Hapa serikali inabidi ikae kimya, wakipitisha siku tatu iwanyanganye leseni zao za biashara kuonyesha kuwa 'the system works..'


Sio rahisi kufanya kama unavyofikiri ,tena kwa kuongozwa na akili ndogo.
 
Tunaendekeza mambo ya kijinga sana nchi hii. Kila kitu siasa tu. Kama wamegoma waachwe hivyo hivyo na kama sheria ingeruhusu wapokonywe leseni zao. Najua kutakuwa na mahangaiko kwa muda fulani lakini hakuna dawa nyingine. Watakaotaka kufanya tena biashara waelewe kwamba bila hizo machine hakuna leseni. Waache biashara tuone kama wataenda kulima. Kwa hili serikali ikomae hadi mwisho. Mbona siku nyingine wanafunga biashara zao kwa hiari yao wenyewe.

Wakiendeleza mgomo, serikali ikaribishe wafanya biashara wengine. Kwanza hao jamaa wa Kariakoo wamejaza misukule ndani ya biashara zao. Ni wacheche wanaofanya biashara bila mambo hayo


Hakuna mgomo kariakoo ,ni wafanyabiashara wameamua kufunga maduka yao.Sijui wewe kama Serikali untaweza kuwalazimisha watu wafungue maduka ,watu wamejiajiri kariakoo hakuna alieajiriwa.Ingekuwa ni rahisi kufanyika hivyo Serikali ingalikuwa imeshachukua hatua hizo mapema sana.
 
Kukwepa kulipa kodi ni kurudisha nyuma maendeleo ya nchi..!!!


Katika taarifa zinazowasilishwa na TRA ndani ya wizara husika T.R.A huwa wanasema wamevuka lengo katika ukusanyaji wa kodi kutoka vyanzo mbali mbali(hapo mashine hamna),kwa nini sasa mashine iwe ni lazima?.Umewahi kujiuliza ni nani alikaa na kuliasisi hili suala la wafanyabiashara watumie mashine?.Je waliwashirikisha wafanyabiashara katika hili au ni kikundi cha watu wachache walikaa na kuamua jambo hili kwa manufaa yao?
 
Hii sredi imenifungua sasa. Nimegundua changamoto zifuatazo:

1. Kuna matatizo ya kiufundi na elimu duni kwa watumiaji -Nadhani hoja ya msingi hapa iwe ni kuboresha na kuimarisha utoaji elimu, maana hakuna teknolojia isiyokuwa na changamoto zake

2. Kuna tatizo la gharama za mashine kwa kuwa TRA imetoa exclusive rights kwa wakala maalum. Pengine dhamira ya hili inaweza kuwa ni nzuri (kudhibiti uchakachuzi) lakini hili linahitaji kuangaliwa upya. Udhibiti wa bei ni jambo la msingi.

3. Inaonekana mashine hizi zinawabana wafanya biashara kutokwepa kodi. Kama tatizo ni kwamba kodi imekuwa kali nadhani ni bora waweke bayana, badala ya kupindisha hoja. Maana kukwepa kodi si jambo la kizalendo hata kidogo!.

Najaribu kutafakari ukubwa wa laki saba (mara moja kwa miaka) kwa hawa wafanyabiashara wa Kariakoo..

Waungwana tulipe kodi tujenge nchi. Hao wanaoibomoa kwa kutafuna kodi zetu dawa yao ipo jikoni!
 
Ukabila ni nini, kwani uongo? nani waliojazana TRA?

Rished Bade ni mchaga..? Mama Masele ni mchaga...? Au kwa sababu mlimuona Kitilya kakaa pale juu mkaona kila mtu ni mchaga..? Kachunguze TRA ujue nafasi nyeti zimeshikwa na watu gani then uje hapa kuongea..
 
Hawataki kulipa kodi? Wao si maajenti tu wa kukusanya kodi? Hapa serikali inabidi ikae kimya, wakipitisha siku tatu iwanyanganye leseni zao za biashara kuonyesha kuwa 'the system works..'

Mfumo wa kulipa kodi sio mzuri, tunaiga bila kuiga namna ya matumizi na kulipa kodi hizo.

Inavyotakiwa bei ya bidhaa na faida ni mali ya mfanyabiashara. Baada ya hapo kuna asilimia kadhaa za kodi zianatakiwa baada ya hiyo gharama ya manunuzi na faida, tax hiyo anayetakiwa alipe ni mnunuzi si mfanyabiashara. Kwa mtindo unaofanywa tax Tanzania mlipaji wa kodi ni mfanyabiashara badala ya mnunuzi, ndio kosa linalifanyika kuiga kuwa na cash registers bila kujua mfumo sahihi wa matumizi ya kodi.

Nchi zinazotumia mfumo huo hasa zilizoendelea bidhaa madukani zimeandika bei yake hiyo ni pamoja na faida ambayo mfanyabiashara ameshaijumlisha kwenye bei ya bidhaa. Hivyo kama soda ni $ 1.00 na ndio bei iliyoonyeshwa, mfumo wa tax pengine ni 9% ya bei hiyo, basi mnunuzi atalipia $1.09. Uwazi huo ndio unaotakiwa, lakini kwa mfumo unaofanywa na watathmini wetu wa kibongo ni mwendo wa kibongobongo ndio unaolalamikiwa kuwaminya mno wafanyabiashara. Biashara ngumu siku hizi hawa kwa hawa wa rejareja.
 
Back
Top Bottom