Edward Lowassa special thread

Edward Lowassa special thread

TAARIFA KWA 4U MOVEMENT DODOMA.

Habari, Wana 4u movement mliopo Dodoma na Watanzania wote wenye mapenzi mema na Edward Lowassa tunawaasa kutovaa T-shirt zozote za 4u movement au zenye jina la Edward Lowassa katika kipindi chote cha mikutano ya Chama.

Najua na kutambua hadi jana tarehe 07/07/2015 zaidi ya wana 4u movement 3600+ plus wamewasili Dodoma lakini wingi wetu usiwe sehemu ya kuwa chanzo cha vurugu ya Aina yeyote.

Tuna Taarifa za kuaminika kuna watu wenye mpango wa kutumia T-shirt zetu za 4u movement kufanya vurugu ndani ya Mji wa Dodoma kwa makusudi ili kuiondelea sifa ya utulivu na umakini wa Movement yetu. Yeyote atakae husika kufanya fujo au vurugu zozote kwa Makusudi huku akitumia jina letu tutakuwa msatari wa Mbele kumshughulikia.

Tunawaasa na kuwaomba wana 4umvt na Watanzania wote kuwa watulivu na wavumilivu na kuwapa nafasi Wajumbe wote wa vikao vya Maamuzi kwa kutii na kufuata kanuni za chama kufanya maamuzi kwa Utulivu maana ule wakati mabadiliko uliotabiriwa na Baba wa Taifa kuwa ukifika Basi mabadiliko tutayapata ndani ya CCM na tukikosa tutayapata nje ya ccm lakini ipo nafasi kubwa sana ya kuyapata Mabadiliko haya ndani ya CCM chini ya Balozi wetu wa 4u movement Mh Edward Lowassa.

Ahsanteni

Hemedy Ally
Mratibu Taifa (National Coordinator)
@4u movement
# UTUMISHI
# UWAJIBIKAJI
# UMOJA
# UZALENDO

Wewe ni mpuuzi,mjinga,mpumbavu ambaye sijawaji kumwona duniani.mipango mpange nyinyi na tena lowasa wenu ameshasema hatishwi na chama sasa unataka kupofusha watu na mikakati yenu.tunajua mipango yenu ya uhaini ndani ya chama maana mmejiapiza lazima muwe nyinyi kana kwamba wengine wote wapuuzi tu ila mzee wenu.mabadiliko aliyosema nyerere ni wezi kutoenda ikulu na so vinginevyo.
 
Mkuu upo sahihi kwa tuhuma hizo ni ngumu kupita hasa hilo la kuanza kampeni kabla naona kama litamuondoa kiulaini
 
Kama kuna ukweli wowote kwenye habari...Hakuna shida yeyote maana atakuwa ana saidia ,kutoka MWANZA KWENDA DAR,ingikuwa kutoka MWANZA kwenda DODOMA,Au Dar KWENDA DODOMA ningekuwa na wasiwasi wa kisiasa....

HEBU TUTAJIE HAYO MAGARI YA LOWASSA YANA ITWAJE,,nipo mwanza ila sijawahi kuona LOWASSA COACH,aU LOWASSA EXPRESS,naenda DAR ijumaa nitapata unafuu,,nisaidie ni save 25,000..

Nduguyangu me mwenyewe nipo huku nyansaka bora tulijue tuangushie aisee
 
hata kuchukua form hakuwa na sifa basi walimsubili kibla wachinjie mbali,
 
kumbe wewe mpumbavu baada ya kutuandikia mambo ya manA unatuletea mipasho ya kwenye kanga wacha kukimeza utakikalia hicho
 
Huu uzi ni maalum kwa ajili ya kuwatisha watanzania waliopo dodoma na kuwatisha ccm na kamati kuu kuwa iwapo watamkata Lowassa basi atahamia ACT na ndio na ndio maana hiyo slogan ya UZALENDO umeiweka hapo. Nawashauri muhame mapema na kutisha watu ili waamue kwa shinikizo.
FISADI anapaswa kuwa JELA na sio jukwaani akigombea urais.
 
Lowassa ndo mtia nia wa kwanza jina lake kukatwa..! Mtajibeba mwaka huu
 
Pamoja na nguvu kubwa ya mazingaombwe aliyokua nayo ya kucheza na media pamoja na fedha chafu hizi ndo sababu maalum hawezi kupita hata mchujo wa kwanza wa NEC(5 bora).

1. Ana tuhuma nzito za ufisadi wa richmond uliosababisha kujiuzulu na kutikisika kwa serikali 2008.Tuhuma hizi hakuweza kusafishwa mahakamani(walimbeba ) jambo linalopelekea tuhuma kusimama palepale kisheria.

2. Operation VUA GAMBA, target ya hii kauli mbiu ilikua ni lowassa,Mara baada ya kujeruhiwa bungeni 2008 chama chake kiliona ufisadi ni tatizo kikaanzisha operation ambayo ilipanga kumwangamiza kabisa kisiasa ndugu Ngoyayi alikwepaje tumuulize NAPE ,hapa maana yake chama chake chama chake HAKIMTAKI.

3. Amekiuka sheria ya fgarama za uchaguzi ya mwaka 2011 kifungu Namba 14(1_2)mma kifungu namba 20(1-4) sambamba na kifungu namba 24 cha sheria hiyo ambayo inakataza mgombea yoyote wa nafasi ya urais,ubunge au udiwani .Ikumbukwe hadi sasa Lowassa ametumia zaidi ya billioni 50 kwa ajili ya kuwahonga waandishi wahabari,wenyeviti wa CCM wa mikoa,wabunge,waandesha bodaboda,maaskofu,mashekhe na hivi juzi ametumia zaidi ya shilingi billion 35.5 kuwahonga REDET.

4. Lowassa amezungukwa na wapambe ambao wana criminal records za kifisadi baadhi ni Rostam,Andrew chenge,Nazir Karamagi,Anna Tibaijuka,Kingunge etc.

5. Ugonjwa wake ,mzee ana mgogoro wa Afya si vizuri kuweka details zote hapa lakini hata nyie wenyewe mmeshajionea ameanguka mara kadhaa katika safari tu za kutafuta wazamini kutkana na power ya media manipulation hamkutangaziwa.

6. Alianza kampeni kabla ya wakati ,hamna asiyetambua yeye na wenzake walianza kampeni mapema hadi ikasababishia adhabu ,hata hivyo kipindo cha adhabu alikua bado anaendelea na kampeni hii tafsiri yake ni UTOVU WA NIDHAMU .

Ni hayo tu


We unameza kisu...

Mi nameza kichwa cha treni kabisaa kamwe hapiti.
 
Mtoa mada usimeze kisu kunywa maji ya betri ya gari chagua yale makali yatafaa zaidi.
 
subilini taarifa ya kukatwa hili awapeleke msituni maana inaonekana ameishaanda jeshi lake hayo matisherti mtavalia huko tuone
Misitu yenyewe lowassa na mafisi wenzake wameifyeka kuuza mbao nje ya nchi..nafikiri watatumia kale kamsitu ka wahuni na vibaka wenzao hapo selander bridge
 
Back
Top Bottom