Son of Gamba
JF-Expert Member
- Oct 26, 2012
- 4,718
- 6,979
Afadhali mumeanza kuliona hilo mapema, sisi tukisema tunaambiwa eti vibaraka wa CCM. Jamani ukweli uko wazi kabisa, Lowassa hamna kitu pale, jamaa liko tu kama zezeta vile, eti ndio liwe Rais? Hapana aisee, hatuwezi kuwa na rais kama huyu hata kidogo.Heshima kwenu wana JF.
Nimefatilia kwa karibu sana sana hotuba ya Mhe. Mgombea u Rais kupitia UKAWA aliyoitoa hapa LAPF kwenye kongamano la wanawake BAWACHA na kubaini jambo moja kubwa sana.
Kauli mbiu ya kongamano ni "LOWASA NA HATMA ZA CHANGAMOTO ZA WANAWAKE TANZANIA"
Nimesikitika kuwa nilitegemea kwenye hotuba Yake ataweza kuelezea mikakati ya ukombozi huo wa mwanamke. Nasikitika kuwa sikuona mahali popote akiongelea changamoto hizo na jinsi ya kuzitatua.
Ameishia kuimba Wimbo wa Mhe. Magufuli "Alinselema Hadija, mchaka mchaka chinja" na kuzungumza mambo ya MAHABA!!!!!!!!
Nasikitika kusema mimi kama mwanamke nimeondoka na kiu yanguuuu!!!!!!!!!! Ngoja nimsubiri mzee original wa Alinselema. I hope atatuondolea kiu hii!!!!!! Tunataka kuona SERA za ukweli za kumkomboa mwanamke, sio MAIGIZO.
Naomba kuwasilisha.
Queen Esther