Edward Lowassa hatoruhisiwa kugombea Urais!

Edward Lowassa hatoruhisiwa kugombea Urais!

Swala ni kwamba ccm wanamwogopa lowassa kuliko slaa, itafahamika mwaka huu
 
Hahaha tou cant be serious.Lowassa ataingia ikulu kwa gharama yoyote. Nyie TISS njaa sana.
 
Mmmm.. yani TISS mmekuwa mkikusanya taarifa za hao uliowataja tangu lini? Tangu miaka nane iliyopita? Kwa maana hiyo sasa hivi ndo zimekamilika? Umesahau mmoja wa uliowataja ndo chief editor wa katiba pendekezwa? Kweli wewe ni wale tiss wanaoweka vitambulisho vyao juu ya meza bar....mfa maji haachi kutapatapa.
 
Mkuu mbona tuna taarifa kabla yako? Hata sisi tulikuwa kwenye hicho kikao chadema IMO ndani ya ccm ila ccm haimo ndani ya chadema
 
ndugu mbowe,

mmeangaika kwa kipindi kirefu kukijenga chadema, lakini umekiuza. Umekibomoa chama na kuingia kwenye mitego ya ccm ambayo mmekwepa kwa muda mrefu.

Kutokana na dharura iliyopo, napenda niwataarifu kwamba, tumeshirikiana kwa kipindi kirefu, tangu 2010, na lengo kubwa limekuwa ni kulisaidia chama chenu kikue. Tumeweka maisha yetu hatarini kwa ajili yenu ili ukombozi upatikane. Kwa kifupi wengi ndani ya tiss wamechukizwa na uamuzi huu, siyo wa kumkaribisha lowassa, bali wa kumpa nafasi kwenye urais, na bila shaka wataungana na magufuli. Zitto alipowekwa, tuliwaambia na ushahidi, na mkakinusuru chadema. Kila mara tunawapa nyaraka na ushahidi mwingi. Kwa nini mmetupuuza?

Chadema mmeonekana kama wasaliti na watu wanaotafuta madaraka kama lowassa. Hasa mbowe, bila kuangalia maslahi ya umma.dr. Slaa aliogopwa zaidi na watawala

hivi sasa chama tawala kina fanya mikakati mizito kumzuia lowassa kugombea. Kabla ya dodoma, kuna wanasheria na makachero toka tiss waliwekwa kukusanya ushahidi kutoka ndani na je ya nchi, dhidi ya lowassa, rostam, karamagi na chenge. Na kwa taarifa yenu apson anafanya kazi ya tiss siyo ya lowassa. Chama inashirikiana na serikali za uingereza na marekani kuonyesha uchafu wa lowassa. Zaidi ya yote, wana ushahidi mwingi sana wa kimaandishi, sauti na video kumuonyesha lowassa akigawa rushwa na kufanya kampeni kabla ya muda muhafaka.kwa kifupi, ushaidi tuliouona, lowassa atazuiliwa na mahakama.

Kikao cha jana usiku ambayo rais kikwete alishiriki kupitia skype imedhamiria kutumia vyombe vya dola na vya habari kumuanika lowassa na uchafu wake. Kwa maana hiyo lowassa haendi kokote. Mkimisimamisha mmekwisha. Wasiwasi wa ccm ilikuwa ni dr. Slaa na siyo lowassa. Lowassa ana fedha nyingi sana nje ya nchi hadi na biashara haramu. Account zote zimeshapatika. Rostam anafanya kazi nzito, na hawa wote wanakuja kuunganishwa na chadema pamoja na mbowe.

Kadhalika kuna watu wengi sana kutoka ccm ambao wanakuja kuisambaratisha chama chenu. Ccm walijua wazi kabisa kwamba dr. Slaa asingekubali uchafu wa lowassa na angejiuzulu lowassa akikaribishwa na kundi lake la mafisadi. Hi imeshatokea, kwa maana kwamba ccm wana taarifa za dr. Slaa kujiuzulu ingawa hawana uhakika. Kazi kwenu ila mkipuuza huu ushauri hamna chenu.

wewe mzimu nini??????
Can someone find me a proper area to dispose off this bullshit????
 
Kuwa TISS ni sawa na mahindi ya kuchoma barabarani?acha uzezeta TISS sio mazezeta wa kujianika hivyo.
 
Mbona intelligentia ya Rwanda iliondoka yote na Kagame anaendelea kupeta hadi leo hii? Hivi kwa nini watu tuogope TISS kana kwamba wao ni miungu? Mliundwa mkawekwa kulinda maslahi ya nchi mkaamua kulinda maslahi yenu kwa hivyo ushauri wenu ni sawa na ZERO kwa sasa.....msiendelee kuudhi watanzania waliopigika acha bla bla hapa. Akishinda ataunda TISS nyingine, akishindwa atakayeshinda ataamua kuendelea na ninyi au kuunda aina nyingine ya intelligentia inayofaa maana hii imeshindwa kazi kama sisi tunakuwa wa kwanza katika matumizi mabaya tu ya pesa...mlikuwa wapi hadi mkapendekeza mafisadi papa kuwa wakuu wa vyombo vikuu vya nchi yetu na kama siyo ninyi wenyewe.....aheri ungekaa kimya

WaTZ wengi wajinga sana hasa wale wanaofaidika na mfumo uliopo. Akili ya kufikiria hawana
 
Awagoli mara ngapi? Mbona kawafunga na mkono jeuri yake luwasa chadema wali mtowa ukuu sasa kaenda kulipa kisasi mliseme mie fisadi sasa nani fisadi?lakini dr slaa kaelewa mapema akajuwa hap ni kifooo
 
kama tukimkataa Lowasa kwa sababu ni mchafu basi hata akitubu Mungu hatamkubali,hakuna njia nyingine ya kuondoa hawa majambazi madarakani tusipomkubali Lowasa,nawahakikishia ccm itashinda uchaguzi mkuu kama kawaida na itatawala tena miaka kumi na Magufuli atafanya kazi na walewale maana hawana jipya,Lowasa atatusaidia kuiondoa ccm halafu tugeukiane baada ya ccm kuzikwa,hapo ndiyo tutaona njia

na isitoshe km ni uchafu ni kipi kichafu zaidi lowassa ama ccm.basi km idhu ni hiyo aliyemchafu xaidi ndo akatqliwe ie ccm
 
na isitoshe km ni uchafu ni kipi kichafu zaidi lowassa ama ccm.basi km idhu ni hiyo aliyemchafu xaidi ndo akatqliwe ie ccm

CCM siyo sufuria ni chama na chama ni watu akiwemo Lowasa. Kama CCM ni chafu nae Lowasa ni mchafu bila shaka na hawezi takata kwa kuhamia CHADEMA. Tatizo watanzania ni wepesi wa kuyumbishwa sana na mara nyingi hushabikia vitu bila tahadhari na kujiuliza mambo maswali magumu. Poleni sana. Huu ushabiki mliufanya 2005 mnataka kuurudia tena then mje mlalamike kina Rostam wakianza kupiga bingo kwenye GAS? Mmesahau hata kina Karamagi waliojigawia bandari yetu kwa miaka 25 wako nyuma ya huyu? Habu fikirieni kwanza.
 
CCM siyo sufuria ni chama na chama ni watu akiwemo Lowasa. Kama CCM ni chafu nae Lowasa ni mchafu bila shaka na hawezi takata kwa kuhamia CHADEMA. Tatizo watanzania ni wepesi wa kuyumbishwa sana na mara nyingi hushabikia vitu bila tahadhari na kujiuliza mambo maswali magumu. Poleni sana. Huu ushabiki mliufanya 2005 mnataka kuurudia tena then mje mlalamike kina Rostam wakianza kupiga bingo kwenye GAS? Mmesahau hata kina Karamagi waliojigawia bandari yetu kwa miaka 25 wako nyuma ya huyu? Habu fikirieni kwanza.

haya umemaliza kuongea nenda choo uta wazeeee afu ukalale mtoto mzuri eee
 
Hata Kenya ilikuwa hivyo kwa rais Uhuru Kenyata. Punguza pressure au umetumwa na magamba wenzio?
 
Back
Top Bottom