Edward Lowassa hatoruhisiwa kugombea Urais!

Informer

JF-Expert Member
Jul 29, 2006
1,586
6,639
Ujumbe huu wa Theo Mutahaba (kumbuka alifanya hivi nyakati za Zitto) uliosambazwa kwa wanahabari:
Ndugu Mbowe,

Mmeangaika kwa kipindi kirefu kukijenga Chadema, lakini umekiuza. Umekibomoa chama na kuingia kwenye mitego ya CCM ambayo mmekwepa kwa muda mrefu.

Kutokana na dharura iliyopo, napenda niwataarifu kwamba, Tumeshirikiana kwa kipindi kirefu, tangu 2010, na lengo kubwa limekuwa ni kulisaidia chama chenu kikue. Tumeweka maisha yetu hatarini kwa ajili yenu ili ukombozi upatikane. Kwa kifupi wengi ndani ya TISS wamechukizwa na uamuzi huu, siyo wa kumkaribisha Lowassa, bali wa kumpa nafasi kwenye Urais, na bila shaka wataungana na Magufuli. Zitto alipowekwa, tuliwaambia na ushahidi, na mkakinusuru CHADEMA. Kila mara tunawapa nyaraka na ushahidi mwingi. Kwa nini mmetupuuza?

Chadema mmeonekana kama wasaliti na watu wanaotafuta madaraka kama lowassa. Hasa Mbowe, bila kuangalia maslahi ya umma.Dr. Slaa aliogopwa zaidi na watawala

Hivi sasa chama tawala kina fanya mikakati mizito kumzuia Lowassa kugombea. Kabla ya Dodoma, kuna wanasheria na Makachero toka TISS waliwekwa kukusanya ushahidi kutoka ndani na je ya nchi, dhidi ya Lowassa, Rostam, Karamagi na Chenge. Na kwa taarifa yenu Apson anafanya kazi ya TISS siyo ya Lowassa. Chama inashirikiana na Serikali za Uingereza na Marekani kuonyesha uchafu wa Lowassa. Zaidi ya yote, wana ushahidi mwingi sana wa kimaandishi, sauti na video kumuonyesha Lowassa akigawa Rushwa na kufanya kampeni kabla ya muda muhafaka.Kwa kifupi, ushaidi tuliouona, Lowassa atazuiliwa na mahakama.

Kikao cha Jana usiku ambayo Rais Kikwete alishiriki kupitia Skype imedhamiria kutumia vyombe vya dola na vya habari kumuanika Lowassa na uchafu wake. Kwa maana hiyo Lowassa haendi kokote. Mkimisimamisha mmekwisha. Wasiwasi wa CCM ilikuwa ni Dr. Slaa na siyo Lowassa. Lowassa ana fedha nyingi sana nje ya nchi hadi na biashara haramu. Account zote zimeshapatika. Rostam anafanya kazi nzito, na hawa wote wanakuja kuunganishwa na Chadema pamoja na Mbowe.

Kadhalika kuna watu wengi sana kutoka CCM ambao wanakuja kuisambaratisha chama Chenu. CCM walijua wazi kabisa kwamba Dr. Slaa asingekubali uchafu wa Lowassa na angejiuzulu Lowassa akikaribishwa na kundi lake la Mafisadi. Hi imeshatokea, kwa maana kwamba CCM wana taarifa za Dr. Slaa kujiuzulu ingawa hawana uhakika. Kazi kwenu ila mkipuuza huu ushauri hamna chenu.
 
kama tukimkataa Lowasa kwa sababu ni mchafu basi hata akitubu Mungu hatamkubali,hakuna njia nyingine ya kuondoa hawa majambazi madarakani tusipomkubali Lowasa,nawahakikishia ccm itashinda uchaguzi mkuu kama kawaida na itatawala tena miaka kumi na Magufuli atafanya kazi na walewale maana hawana jipya,Lowasa atatusaidia kuiondoa ccm halafu tugeukiane baada ya ccm kuzikwa,hapo ndiyo tutaona njia
 
hii nchi ni ya wananchi kama wananchi wanamkubali hzo takataka zote ulizoandika hazna maana

masi dada yawezekana kuna kitu flan usichokijua kuhusu TISS na mtu kuingia ikulu..
Lowasa tunajua mnamkubali lakn hawezi kuingia ikulu kwanamna yoyote ile
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: DSN
Sasa mkuu kwani mumzuie lowasa agombanie,,,hiyo itaionesha kwamba wanamuogopa Lowasa.Na kwa taarifa yako jana hiko kikao unachosema kilikuwa bluff tu,,,mikakati mikubwa ni kutisha media na kumtumia Mtikila ilikwama,,,,,,yaani leo hadi bossi wangu kasema utaratibu umebadilika yaani hakuna morning briefing tena ndani ya boti letu....nadhani kikubwa kibaya ambacho kinahangaikiwa ni kuidentify na kuisolate all the inflitrators within...na mabossi wanalaumiwa maana wao walianticipate akitoka atatoka na sympathizers wake within kumbe ile ilikuwa chaka ambayo ilifeediwa na El inflitrators.But anyhow lowasa sio kivile ni kwamba hofu ipo kwenye spillover effect ya majimboni.
 
Hamjui chadomo ni chama la mafisadi na watu wenye uchu wa pesaa?wameona wamchukue lowasa ili wamuibie vizuri kwa kumpamba na kumpa kiti cha ugombea urais...kweli wajinga wataliwa sana but CCM nyie mamburura mtangoja sanaaaa.....
 
masi dada yawezekana kuna kitu flan usichokijua kuhusu TISS na mtu kuingia ikulu..
Lowasa tunajua mnamkubali lakn hawezi kuingia ikulu kwanamna yoyote ile
wanaanchi ndo wenye nchi
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom