Edward Lowassa atoweka ghafla kwenye media nchini

Edward Lowassa atoweka ghafla kwenye media nchini

Jamaa alichukua mpaka nafasi ya Mungu, akasujudiwa, akaogopwa! eti ukisema anaumwa..unakufa!

lile pepo la upagazi lililowapata wale washabiki lishindwe na limeishashindwa
 
Media zinafanya biashara hivyo zinaenda na mahitaji ya walaji. Kila jambo na majira yake.
 
Mtoa mada unaharaka sana subiri Ukawa Wanajielewa hawaendi kwa nguvu za upepo kimya kirefu kina mshindo trip hii Lowasa atafanya siasa za maana nyie jipangeni mashambulizi yanakuja
 
Mtoa mada unaharaka sana subiri Ukawa Wanajielewa hawaendi kwa nguvu za upepovkimya kirefu kina mshindo trip hii lowasa atafanya siasa za maana nyie jipangeni mashambulizi yanakuja
 
Kampeni zimeshaisha, ulitaka aseme nini kila siku,?
Baada ya kampeni watu wanapumzika kabla ya kuanza hatua inayofuata.
Mapambano bado yanaendelea ya kumkomboa mtanzania kutoka kwa mkoloni ccm.
Lowasa yuko mioyoni kwa watanzania walio wengi, ndio maana pamoja na kupewa mapumziko ya kuapishwa kwa mnayemuita raisi, nchi iko kimya kama kuna msiba.

Ndimu hizo za kuondoa kichefuchefu ndo zimekujaa.
 
Wadau, amani iwe kwenu.

Ilikuwa ni jambo lililozoeleka kila unapotune radio ama kuangalia TV au kuperuzi gazeti na hata kuangalia mitandao ya kijamii kusikia ama kuona jina la Lowasa likitawala kwenye media hizo. Hali hiyo iliwaaminisha baadhi ya Watanzania kuwa hakuna mtu muhimu Tanzania kama Edward Lowasa. Tena wengine wanadiriki kusema kuwa eti Magufuli anakalia kiti ambacho si chake.

Cha kushangaza zaidi, tangu tarehe 1 Novemba, jina la Lowasa limepotea ghafla kwenye media nchini. Hii imekuja siku mbili tu baada ya Dr Magufuli kukabidhiwa cheti cha ushindi wa nafasi ya Urais, hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam.

Kwa sasa ni jambo la kushangaza kuona hata zile media ambazo kila uchwao walikuwa wanatuaminisha kuwa Lowasa ndiye mkuu katika taifa hili wameacha kutangaza habari zake. Mathalan, ITV na Channel Ten, TV zilizokuwa zinatumiwa na Lowasa kama mdomo wake hawajaonesha taarifa yoyote ya Lowasa tangu juzi. Hii ni kusema kuwa TV hizi zimebadili gia angani na sasa wanatumia muda mwingi kutoa habari za Magufuli.

Bye Bye Lowasa.

Ninachokifahamu kwa EL ni kwamba pesa ya ufisadi iliukuwa inamsumbua akapatikana mjanja mmoja kwa jina Mbowe akamwambia ikulu ni yako mzee kiroho paaaaaaaaaaaaaaa ETI unasemaje Mbowe IKULU ni yako mzee CCM watakutambua cha msingi kata fungu hapa Dr. Slaa namtimua hawezi kubishana na mimi mzee akasema unataka bil ngapi Mbowe nipe 20 tu nakuuzia chadema mzee akasema chukua 15 zinakutosha na kampeni ufanye wewe mbowe akasema hapana pamoja na kuwa afya yako siyo nzuri tutasafiri wote na tupige kampeni wote na madaktari tutawaleta kwa ajili yako kwa hakika mwaka huu ni wako vijana wanasema ni wewe tu EL akaamini kazi ikanza kwa mafuriko na gharika kuja kwenye uchaguzi mweleka chali.

Mbowe unajua mzee hapa ungeniongeza zile tano tungewalipa mawakala vizuri EL nipishe huko ila ili kuondoa aibu ya kushindwa tukatae matokeo tuseme CCM wameiba kura na tena tufanye maandamano ya bila ukomo nchi nzima watu hawataangalia kushindwa kwetu bali akili na mawazo yoote yatakuwa kwenye maandamano, kuomba kibali cha maandamano wakakutana na Polisi wanaojua kazi zao marufuku nchi nzima kuandamana sasa media wataandika nini tena hapoooooooooooooooooooo???????? Hakuna namna inabidi apumzike tu mzee EL PESA WAMEKULA WAJANJA NA IKULU HAIPATIKANI KWA PESA BALI KWA NEEMA YA MUNGU. NAFUTIKA, HATA MIMI NILITAKA SANA KUWA DAKTARI LAKINI NILIKWAMA KAMA EL KWA KUWA NEEMA HIYO SIKUJALIWA KUIPATA.
 
Halafu JF siku hizi haina kitufe cha like. Sijui kimeenda wapi
Kitufe cha like ndio kilikuwa kinatumiwa na wale jamaa wa milimani city kupeleka trafic kubwa kwenye server ilikohostiwa JF kama njia ya kuhack kwenye kupitia layer 7 baada ya kupigwa pin layer 4 ndio maana ilipotea halafu unajifanya hujui mlichokuwa mnafanya cc Invisible Max melo
 
Last edited by a moderator:
Ni wenye upeo na IQ kubwa tu ndo wanajua Alichowafanya Lowasa , Kutoka viti 74 vya upinzani ndani ya Bunge 2005 - 10 hadi zaidi ya viti 120 vikiwemo Viti Maalumu, Angalia Baadhi Miji Mikubwa mliyoitamani ikiwemo Dar es salaam (Nape kakiri ) Bakora za Lowasa zimewacharaza.
Mbegu ya mabadiliko Aliyoipanda Lowasa Ndani ya Mioyo ya watanzania wengi wakiwemo Vijana subirini Mavuno yake mtayaona miaka mitano ijayo, kwani ahadi alizoahidi Mh;Pombe Elimu Bure , Tanzania itakayojaa viwanda , Meli mbili kubwa ,Maji kutoka ziwa victoria Hazitekelezeki
Kumbe Sera ya mabadiliko haikuwa ya chadema ilikuwa ya lowasa hivyo ameondoka nayo.
Pia ahadi za ukawa kweli zimetekelezeka kwa kukata gogo chato
 
Kweli waafrika tuna matatizo ya akili, akiandikwa sana mnauliza why? asipoandikwa maneno kibao! Nafikiri Tanzania bado sana na kweli tuendelee kuisoma namba wote. Rejea Donald Trump kuhusu waafrika
 
Ni mpumbavu tu mwenye kushabikia yanayotokea leo kwenye Taifa hili.

Hakuna cha kujivunia katika Taifa hili zaidi ya ujinga. Ujinga wetu ndiyo gharama yetu.

unapoona mzawa wa Taifa hili anaishi kama mtumwa na mgeni kwenye nchi yake uelewa hakuna uhuru bali utumwa.

Ajabu ni pale unapoona mtumwa huyu anapofurahia hali yake ya kitumwa. Vitoja hivi vipo tu Tanzania.

Ndiyo maana imefika hata mahali watawala wao wanawaita wananchi wao malofa nao wanafurahi kuwa hivyo.
 
Naona watu wana tekenya, anyway wahenga walisema ukiona kobe kainama.........! I belive drama is still going on!
 
Wadau, amani iwe kwenu.

Ilikuwa ni jambo lililozoeleka kila unapotune radio ama kuangalia TV au kuperuzi gazeti na hata kuangalia mitandao ya kijamii kusikia ama kuona jina la Lowasa likitawala kwenye media hizo. Hali hiyo iliwaaminisha baadhi ya Watanzania kuwa hakuna mtu muhimu Tanzania kama Edward Lowasa. Tena wengine wanadiriki kusema kuwa eti Magufuli anakalia kiti ambacho si chake.

Cha kushangaza zaidi, tangu tarehe 1 Novemba, jina la Lowasa limepotea ghafla kwenye media nchini. Hii imekuja siku mbili tu baada ya Dr Magufuli kukabidhiwa cheti cha ushindi wa nafasi ya Urais, hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam.

Kwa sasa ni jambo la kushangaza kuona hata zile media ambazo kila uchwao walikuwa wanatuaminisha kuwa Lowasa ndiye mkuu katika taifa hili wameacha kutangaza habari zake. Mathalan, ITV na Channel Ten, TV zilizokuwa zinatumiwa na Lowasa kama mdomo wake hawajaonesha taarifa yoyote ya Lowasa tangu juzi. Hii ni kusema kuwa TV hizi zimebadili gia angani na sasa wanatumia muda mwingi kutoa habari za Magufuli.

Bye Bye Lowasa.
Mkuu si unajua tena moto wa mabua,namnukuu JK
 
Back
Top Bottom