Edward Lowassa atoweka ghafla kwenye media nchini

Edward Lowassa atoweka ghafla kwenye media nchini

Kampeni zimeshaisha, ulitaka aseme nini kila siku,?
Baada ya kampeni watu wanapumzika kabla ya kuanza hatua inayofuata.
Mapambano bado yanaendelea ya kumkomboa mtanzania kutoka kwa mkoloni ccm.
Lowasa yuko mioyoni kwa watanzania walio wengi, ndio maana pamoja na kupewa mapumziko ya kuapishwa kwa mnayemuita raisi, nchi iko kimya kama kuna msiba.
 
Media zinafuata what is news by that time ni ujinga kufuata story ambayo haiuzi ndo maana hata Magufuli itafikia wakati amezoeleka linakuja jipya cjui escrow mpyaa ama nene
 
...thread za kitoto kama hizi ndio zinapendwa sana na magamba.!
 
Kaingia wapi huyo mamvi

Anamalizia Kukata GOGO. Vuta Subira Soon Akishamaliza Kuombewa Tatizo Lake Hilo Kubwa Na Tata Lililomuanzia Mkoani Geita Na TB Joshua Baada Ya Mchungaji FEKI Yule Wa Kawe Tanganyika Packers Kushindwa Utamwona Tu Mkuu.
 
kama we mwenyewe unamkumbuka hadi kumuanzishia post basi ujue wapo ambo hawahitaji hata kukumbushwa kuhusu lowassa
 
Anamalizia Kukata GOGO. Vuta Subira Soon Akishamaliza Kuombewa Tatizo Lake Hilo Kubwa Na Tata Lililomuanzia Mkoani Geita Na TB Joshua Baada Ya Mchungaji FEKI Yule Wa Kawe Tanganyika Packers Kushindwa Utamwona Tu Mkuu.
Ila katika vitu vimemnyika raha mzee wa mamvi ni kitendo cha kukata gogo hadharani kule Chato. Wana Chato hawatakuja kumsahau. Aliharibu hali ya hewa kwa masaa kadhaa.
 
Hivi Lizaboni ulitaka umuone wap na kampeni zimeisha??? Akiendelea kuonekana mnaongea...kakaa kimya mnasema...yaan ukitaka post yako isomwe humu andika tu lowassa hata kama ni title bila maelezo watu watakucomment....Lowassa ni hatariiiiiii!!!! Laisi wetu wa tano..kama mwenyew anavyojiita 'laisi' hatauza hvyo....magazeti lazima yatafute habari mpya...Lowassa kawainulia uchumi sana sshv hata mkakati limenunuliwa lol!!!! Lizabon aendelea tu kujiuza huku jf lowassa humkuti hata kidog...
 
Nitakuwa mchoyo wa fadhira kama nisipo mshukuru Lowassa kwa kuniwezesha kipesa pia. Wengi mlikuwa mnapoteza muda kumshangilia ila hela yake tumeila sisi. Tangu kutangaza nia Arusha hadi kutafuta wadhamini ndani ya CCM. Mzee Lowassa sitakusahau, kwa kuchoma pesa wewe ni noma sana.

Utaendelea kuwa mtumwa. Tofautisha kati ya anaefanya kazi au kibarua ili apate pesa na mtu ambae pesa inanfanyia kazi.
 
Mkuu, kumbe ndo maana kuna wakati ulitusaliti kwa muda. Ulimpamba Lowasa kwa muda wa wiki moja tu then ukamgeuka. Aisee wewe ni noma kabisa

Nahisi LAKI si pesa atakua ameamua kubadili ID kabisa.
 
Last edited by a moderator:
Wadau, amani iwe kwenu.

Ilikuwa ni jambo lililozoeleka kila unapotune radio ama kuangalia TV au kuperuzi gazeti na hata kuangalia mitandao ya kijamii kusikia ama kuona jina la Lowasa likitawala kwenye media hizo. Hali hiyo iliwaaminisha baadhi ya Watanzania kuwa hakuna mtu muhimu Tanzania kama Edward Lowasa. Tena wengine wanadiriki kusema kuwa eti Magufuli anakalia kiti ambacho si chake.

Cha kushangaza zaidi, tangu tarehe 1 Novemba, jina la Lowasa limepotea ghafla kwenye media nchini. Hii imekuja siku mbili tu baada ya Dr Magufuli kukabidhiwa cheti cha ushindi wa nafasi ya Urais, hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam.

Kwa sasa ni jambo la kushangaza kuona hata zile media ambazo kila uchwao walikuwa wanatuaminisha kuwa Lowasa ndiye mkuu katika taifa hili wameacha kutangaza habari zake. Mathalan, ITV na Channel Ten, TV zilizokuwa zinatumiwa na Lowasa kama mdomo wake hawajaonesha taarifa yoyote ya Lowasa tangu juzi. Hii ni kusema kuwa TV hizi zimebadili gia angani na sasa wanatumia muda mwingi kutoa habari za Magufuli.

Bye Bye Lowasa.

Mkuu , hivi kina mussa allan wameishia wapi? Ama ndo ngalawa imezama?
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom