Edward Lowassa Atembelea Maonyesho ya Nane Nane Morogoro

Edward Lowassa Atembelea Maonyesho ya Nane Nane Morogoro

Daaah , Lowasa ni shidaaaa.
Huyu mtu ni mwanasiasa mkali sana.
Anajua kucheza na siasa kwa wakati. Siamini kuwa kuna mtu wa kupunguza nguvu ya Lowasa kisiasa. Anajua kupangilia mambo yake.
Na bahati nzuri baada ya kuaondoka CCM anaishi kwa raha na amani na afya yake imeimarika sana. Kuna watu walifikiri kuwa Lowasa ni mroho wa madaraka lakini kuimarika kwa afya yake kunaonyesha kuwa alichokuwa anakipigania ni watanzania wawe na maisha bora na elimu bora ndio maana walipomnyima nafasi ya kuwatumikia akatulia bila wasi wasi.
Sijui CCM walimfanyaje mana afya yake iliyumba sana akiwa kule pamoja na kwamba kule alikua na marafiki wanafiki. Waliokua wanamchekea kwa nje ila kwa ndani walikua wanamwangamiza kimya kimya kwa maneno ya chini chini.

Bado Lowasa ana nafasi kubwa ya kutimiza ndoto zake. Ajipange tu na kumwomba Mungu asiye na Chama wala kabila.
 
IMG-20160808-WA0045.jpg
IMG-20160808-WA0043.jpg
 
Leo tarehe 7/8/2016, Aliyekuwa waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania *Mh. Edward Ngoyai Lowassa* (Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CHADEMA) alitembelea maonesho ya nanenane mkoani Morogoro; Kuangalia, Kusikiliza na kushauriana na Wakulima mbalimbali juu ya changamoto za kilimo.

Mheshimiwa Edward Lowassa atakua huko kwa siku mbilimbili kwa ajili ya shughuli hiyo.
Kumbe ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu siyo Mjumbe wa Kamati Kuu? Vipi kamanda nyomi ilikuwepo ya kutosha?
 
Umekiri kuwa huna style nyingine! Maana yake lowassa ni mwisho wa reli kwa uvaaji??? Unamzungumziaje Yule wa koti la draft??
Hahahah hamna Lowasa ana mapigo fulani ya kicowboy ndio nikasema hayo ni mapigo yangu ,yaani huwezi sijui kunivalisha Jordans badala ya Travolta au Stacy Adams ,mkuu mmoja akaniambia nimemuiga kumbe na yeye hayo ni mapigo yake ndio nikakiri wacha tu nikuige siwezi badilisha style .......huyo wa koti la draft kwa kweli utanisamehe mapigo yake hata nishikiwe bunduki siwezi
 
Asante Yesu...nafurahi kuona umeachia uponyaji kwa baba huyu...ona anavyong'a a sasa na afya nzurii... Nakuomba sawa sawa unavyosamehe dhambi zangu na kuniponya...Mlinde baba huyu na uachilie uponyaji wa kweli... nafuta roho zote za mauti kwa damu ya Yesu...hakuna mshale utakaorushwa ukafanikiwa juu yake pasipo wewe Mungu kuruhusu....kwa kuwa sote tumetenda dhambi na kupungukiwa na utukufu wako. Kwa njia ya Msamaha wa dhambi pale Goligota nahakika umetuweka huru...Amen
 
Hizo hela si atugawie huku munduli walau tufanyie BIASHARA
 
Back
Top Bottom