Ile ada elekezi ya shule binafsi iliishia wapi?
Mipango
Mipango
Mipango
Ni lazima tuwe na mfumo unaoamini katika:
Uhuru wa mtu kutoa maoni yake.
Kutambua kuwa cheo ni dhamana sio haki ya mtu mmoja. Ukichaguliwa kuwa kiongozi sio kwamba wewe ni mungu wa kuamua kila jambo bila kukosolewa.
Utu, kwa sasa watanzania hatuna utu kabisa ,hata ukiangalia michango ya kimawazo inayotolewa humu ndani imejaa ubinafsi ,dharau,ukabila ,udini,ushabiki,chuki na wivu. Hata wale wanaoshabikia kutumbuliwa majipu ni wazi kuwa ni watu wenye hasira na chuki za muda mrefu zilizojengwa na CCM na viongozi wake kwa Muda mrefu na wakawa wanasifiana bila kukosoana. Watu wanatamani majipu yauawe na sio kufikishwa mahakamani yote ni chuki ndani ya mioyo ya watanzania.
Uadilifu, hakuna uadilifu ukianza na ngazi ya familia. Kwenye ndoa hakuna uadilifu,wazazi sio waadilifu kwa watoto n.k. Ukifika kwenye taasisi za dini pia hakuna uadilifu .
Ni vyema Magufuli akakubali kuunda taifa lenye sheria zinazomfanya kila mtu kuwa muadilifu na mzalendo. Kwa sasa bado kuna harufu ya kujitafutia himaya ya kisultani kutokana na kuungwa mkono na kundi kubwa ambalo kwa muda mrefu pia limekua likitawala hii nchi na matatizo ndio hao hao waliosababisha.
Niliwahi kusema kuwa Magufuli atangaze mali zake na pesa alizo nazo kwenye akaunti. Baada ya hapo ufanyike usajili wa mali zote kubwa zilizopo kwenye nchi hii. Kuna watu watakutwa na nyumba 1000 huku wakiwa ni watumishi wa umma wanaoheshimika na kutukuzwa kwenye jamii. Waadilifu watajulikana. Wanaojifanya kushinda kwenye mitandao wakiwatukana wengine na kumsifu magufuli huenda wakawa ni majipu yanayotaka kumpotezea malengo. Tuliona nguvu kubwa iliyokuwa inatumika kumremba na kumsifu JK kila kukicha na safari zake kuziita zenye tija kwa taifa leo hii hao hao wamehamia kwa Magufuli na kuanza kumponda JK. Hii ni aina ya unafiki na woga wa kusema ukweli. Kama safari za JK zilikua na tija kwa taifa zitabakia milele kuwa na tija. Kama zilikua hazina tija basi zitakua hivyo milele sio mpaka aje Magufuli ndio ziambiwe kuwa hazina au zina tija.
Unafiki ni kitu kibaya sana. Nadhani hata mh.Magufili ameanza kugundua unafiki wa watu wanaotaka kupewa vyeo kwa kusifu kila kitu hata kibaya. Umeya wa jiji ni mfano kuna makada wa CC M walishaanza kulazimisha ushindi kwa kudhani kuwa watasifiwa na kuonekana mbele ya Rais lakini alipobaini ule uhuni akajitoa kwenye mitego miovu.
Panapobidi Rais akosolewe hata kama ni mtu wa kabila lake na dini yake.Tumkosoe tu. Tukijenga mambo ya kulindana kikabila na kidini baadae akija Raisi Mpemba tena msabato atadharaulika hata kama atakua muadilifu kwa kiwango gani kisa anatokana na kundi dogo kwenye jamii. Atakosa kundi kubwa la kumpamba na kumsifu kwa kila jambo kuliko hata Mungu.
Mvua itanyesha atasifiwa rais badala ya Mwenyezi Mungu. Magonjwa yataibuka atalaaniwa rais badala ya shetani n.k. Uadilifu unajengwa kwa kukosolewa na kukubali kukosolewa.
Nyerere alishindwa vibaya kwa sababu watu hawakutaka kumkosoa na kuonyesha nini wao wanaona kinafaa. Kwa kujiamulia kila jambo na kupigiwa makofi nchi ilizidi kuwa Maskini tofauti na malengo ya kudai uhuru.
Bunge liendelee kuaminika na kuwa mshauri mkuu wa serikali na kuielekeza serikali na sio serikali kulielekeza bunge.
Haki, ni lazima haki isimaniwe kwa nguvu zote. Tumeona baadhi ya taasisi zikikumbwa ba kashfa watu wanasimamishwa kazi lakini nyingine tunasoma kwenye Magazeti makashfa ya mabilioni lakini watu wanahamishwa na kupewa idara nyingine nyeti zaidi. Hii sio sawa. Kila mtu abebe mzigo wake mwenyewe mbele ya sheria.
Usawa, wote tunahitaji kupata sehemu ya keki ya taifa hili kwa usawa. Kukosekana kwa usawa ndiko kumepelekea kukosekana kwa uzalendo miongoni mwa watanzania.
Kuna vijiji tuliona kule kilwa kwenda Liwale wanakaa siku tatu njiani kutokana na barabara mbovu sana lakini hawajakumbukwa kwa haraka kama wale wa Mwanza kuelekea air port na wale wa Moroko Kuelekea Mwenge kule dsm.