Edward Lowassa akosoa uongozi wa Rais Magufuli

Edward Lowassa akosoa uongozi wa Rais Magufuli

Magu mpeni miaka miwili tu atakuwa kama wenzake tu maana baada hapo uchaguzi utakuwa umekaribia hivyo lazima aende ki CCM maana yeye ndo atakuwa ni Rais na wakati huo huo ni Mwenyekiti wa chama.
kwa taarifa yako magu hana njaa ya uongozi
 
LOWASSA NI "JEMBE", huyu jamaa tungempa nchi, sasa hivi mtaani hali ni ngumu sana. "NAJUTA" kumpa kura Magufuli, naisoma namba sasa hivi.
Safi sana rais wetu wa mioyo mzee lowassa kwa kuona hayo, 2020 "una" kura yangu!
 
Wewe na fisadi Lowasa wote ni vilaza, haujui kama raisi Kikatiba ndiyo mwenye uwezo wa kuamua siku gani iwe sikukuu na nipi isiwe? Kwa taarifa yako tu wacha kubadilisha matumzi ya fedha bali Raisi wa JMTZ ana uwezo wa kuzifuta kabisa hizo siku na zisiwepo na hii ni Kikatiba kabisa!
EL sio kilaza,kwani hizi sherehe impact yake ni nini,au tuzungumzie namna ya kuadhimisha
 
Ile ada elekezi ya shule binafsi iliishia wapi?

Mipango
Mipango
Mipango

Ni lazima tuwe na mfumo unaoamini katika:

Uhuru wa mtu kutoa maoni yake.
Kutambua kuwa cheo ni dhamana sio haki ya mtu mmoja. Ukichaguliwa kuwa kiongozi sio kwamba wewe ni mungu wa kuamua kila jambo bila kukosolewa.

Utu, kwa sasa watanzania hatuna utu kabisa ,hata ukiangalia michango ya kimawazo inayotolewa humu ndani imejaa ubinafsi ,dharau,ukabila ,udini,ushabiki,chuki na wivu. Hata wale wanaoshabikia kutumbuliwa majipu ni wazi kuwa ni watu wenye hasira na chuki za muda mrefu zilizojengwa na CCM na viongozi wake kwa Muda mrefu na wakawa wanasifiana bila kukosoana. Watu wanatamani majipu yauawe na sio kufikishwa mahakamani yote ni chuki ndani ya mioyo ya watanzania.

Uadilifu, hakuna uadilifu ukianza na ngazi ya familia. Kwenye ndoa hakuna uadilifu,wazazi sio waadilifu kwa watoto n.k. Ukifika kwenye taasisi za dini pia hakuna uadilifu .
Ni vyema Magufuli akakubali kuunda taifa lenye sheria zinazomfanya kila mtu kuwa muadilifu na mzalendo. Kwa sasa bado kuna harufu ya kujitafutia himaya ya kisultani kutokana na kuungwa mkono na kundi kubwa ambalo kwa muda mrefu pia limekua likitawala hii nchi na matatizo ndio hao hao waliosababisha.
Niliwahi kusema kuwa Magufuli atangaze mali zake na pesa alizo nazo kwenye akaunti. Baada ya hapo ufanyike usajili wa mali zote kubwa zilizopo kwenye nchi hii. Kuna watu watakutwa na nyumba 1000 huku wakiwa ni watumishi wa umma wanaoheshimika na kutukuzwa kwenye jamii. Waadilifu watajulikana. Wanaojifanya kushinda kwenye mitandao wakiwatukana wengine na kumsifu magufuli huenda wakawa ni majipu yanayotaka kumpotezea malengo. Tuliona nguvu kubwa iliyokuwa inatumika kumremba na kumsifu JK kila kukicha na safari zake kuziita zenye tija kwa taifa leo hii hao hao wamehamia kwa Magufuli na kuanza kumponda JK. Hii ni aina ya unafiki na woga wa kusema ukweli. Kama safari za JK zilikua na tija kwa taifa zitabakia milele kuwa na tija. Kama zilikua hazina tija basi zitakua hivyo milele sio mpaka aje Magufuli ndio ziambiwe kuwa hazina au zina tija.
Unafiki ni kitu kibaya sana. Nadhani hata mh.Magufili ameanza kugundua unafiki wa watu wanaotaka kupewa vyeo kwa kusifu kila kitu hata kibaya. Umeya wa jiji ni mfano kuna makada wa CC M walishaanza kulazimisha ushindi kwa kudhani kuwa watasifiwa na kuonekana mbele ya Rais lakini alipobaini ule uhuni akajitoa kwenye mitego miovu.
Panapobidi Rais akosolewe hata kama ni mtu wa kabila lake na dini yake.Tumkosoe tu. Tukijenga mambo ya kulindana kikabila na kidini baadae akija Raisi Mpemba tena msabato atadharaulika hata kama atakua muadilifu kwa kiwango gani kisa anatokana na kundi dogo kwenye jamii. Atakosa kundi kubwa la kumpamba na kumsifu kwa kila jambo kuliko hata Mungu.
Mvua itanyesha atasifiwa rais badala ya Mwenyezi Mungu. Magonjwa yataibuka atalaaniwa rais badala ya shetani n.k. Uadilifu unajengwa kwa kukosolewa na kukubali kukosolewa.
Nyerere alishindwa vibaya kwa sababu watu hawakutaka kumkosoa na kuonyesha nini wao wanaona kinafaa. Kwa kujiamulia kila jambo na kupigiwa makofi nchi ilizidi kuwa Maskini tofauti na malengo ya kudai uhuru.
Bunge liendelee kuaminika na kuwa mshauri mkuu wa serikali na kuielekeza serikali na sio serikali kulielekeza bunge.

Haki, ni lazima haki isimaniwe kwa nguvu zote. Tumeona baadhi ya taasisi zikikumbwa ba kashfa watu wanasimamishwa kazi lakini nyingine tunasoma kwenye Magazeti makashfa ya mabilioni lakini watu wanahamishwa na kupewa idara nyingine nyeti zaidi. Hii sio sawa. Kila mtu abebe mzigo wake mwenyewe mbele ya sheria.

Usawa, wote tunahitaji kupata sehemu ya keki ya taifa hili kwa usawa. Kukosekana kwa usawa ndiko kumepelekea kukosekana kwa uzalendo miongoni mwa watanzania.
Kuna vijiji tuliona kule kilwa kwenda Liwale wanakaa siku tatu njiani kutokana na barabara mbovu sana lakini hawajakumbukwa kwa haraka kama wale wa Mwanza kuelekea air port na wale wa Moroko Kuelekea Mwenge kule dsm.
"WISELY MAN WISELY THINKING" YOU HOT
 
Watu wamekalia kusifu unapowaambia juu ya utawala wa kisheria unawachanganya. NA sasa wameshapendekeza asiwe na ukomo wa madaraka kama kina Kagame na M7
Hiki kivuli cha utawala wa sheria ndo kitawaweka benchi zaidi ya mdhaniavyo, lowassa naona na ukongwe wake wote anapotea kiakili na pia kisiasa! Hizo pesa zilishaidhinishwa na bunge, magufuli badala ya kuzipeleka kwenye kuserebuka, kazipeleka kupanua barabara mwanza, sasa hapo tatizo liko wapi?
Uzuri ni kwamba wananchi wanapendezwa na haya maamuzi magumu ya Magufuli yaliyo ndani ya misingi ya sheria.
 
Hakika historia itawahukumu.
Amesema Magufuli atavuma kwa kipindi kifupi kwani hana vision.
Ana vision ya kutaka kusifiwa, hâta mawaziri wake wanamuiga Kama lukuvi hawafanyi kazi bila camera, wakuu Wa mikoa Kama makonda kila siku anataka kusikika
 
kutokana na ufinyu wa akili yako unaona kapunguza gharama poleni sana maana najua mko wengi auko peke yako wenye mawazo mgando
Hujaelewa nini hapo?
Nimesema kama shule imekupiga chenga huwezi ona hilo punguzo. Na wewe ni wazi hujaelewa hapo!
Tatizo uko uwanjani unacheza mpira wa miguu ila UNAKABIA macho, utapigwa goli nyingi tu!
Tumia kichwa kufikiri pia sio kufugia hizo nywele nyeupe tu kama avatar yako.
 
- Amlalamikia Rais Magufuli kugawa fedha kwa shughuli mbalimbali wakati chombo chenye mamlaka kugawa fedha kipo ambacho ni bunge.(Pesa za uhuru na Pesa za Muungano)

- Asikitishwa na uachishwaji wa kazi kwa wafanyakazi, asema hali ngumu ya uendeshaji wa mashirika hayo ndio usababisha utendaji hafifu.

- Asononeshwa na hali ngumu ya maisha mtaani.

- Asikitishwa na ushukaji wa huduma ya Bandari kushuka kwa asilimia 50 na kusababisha vijana wengi kusota mtaani.

- Kitendo cha wahisani kujitoa kuisaidia nchi asema n i pigo kubwa kwetu kwa mustakabali wa uchumi wa nchi.

- Asema si kweli kwamba uongozi wa Rais mstaafu Kikwete kila mtu alikuwa mla rushwa, ni kweli mfumo ule ulikuwa mbovu na wa kifisadi.


Bila kutetea, tukumbuke kitabu kimoja kitakatifu kuna mfano ambapo uponyaji ulifanywa siku rasmi ya kuabudu, pia, msamaria mmoja alimsaidia mtu bila kujali kwamba atakuwa najisi kwa kutokwa damu nyingi.

Hebu tufananishe, maamuzi ya haraka ambayo yanafaida, kwa mfanmo kupeleka vitanda vya kutosha hospitali ya taifa, kupunguza tatizo la vitanda kwa mama wazazi; na kuamua barabara sumbufu za muda mrefu kule Mwanza na pale Morocco-Mwenge zitengenezwe na kupunguza kama siyo kupunguza kero kwa wananchi; mtoa mfano kwenye kitabu kitakatifu aluliza, lipi muhimu, kuokoa maisha au kusubiri utaratibu ambapo maisha yanakuwa yamepotea.

Kero za hospitali, mabarabara, na utaratibu mbovu, mfano sheria dhaifu ya manunuzi, vimelalamikiwa kwa muda mwingi sana. Na mara nyingi, kufuata utaratibu, mfano, wa manunuzi ya vifaa tiba, kungechukua muda mrefu, tena na kuumiza wengi. Mheshimiwa anauwezo wa kutangaza hali ya dharura na akafanya maamuzi yenye maslahi mapana, tena kwa afueni na faraja kwa walio wengi. Kama ilivyo kawaida, walio wengi wanafurahia hatua zinazoendelea kuchukuliwa, wachache, ambao kwa namna fulani walifaidika na udhaifu wa taratibu, wanalalama kwani hawaamini kwamba mabadiliko yamefika.

Kwenye aina za leadership, kuna moja inaitwa contingency leadership, ambapo kiongozi anawezajitokeza, na kukidhi haja ya kimazingira ya uongozi. Mh ameibuka kipindi ambapo nchi inahitaji kwa udi na uvumba aina ya uongozi anaoendelea nao.

Waliohaki watulie na maendeleo sasa yanakuja. Kumbukeni, viongozi kipindi kilichopita waliwekeza katika kuaminisha taifa kwamba nchi hii ni masikini na hatuna namna ya kutoka, lakini mkuu amewaonesha kinyume chake. Ni matumaini makubwa yenye sababu za msingi kabisa. TUUNGANE KWA PAMOJA KWENDA MBELE, TUSIRUDI MISRI.
 
Acha kubwabwaja onyesha kifungu cha Katiba Raisi wa JMTZ alichokiuka!
Poa km nabwabwaja ila unadhani kuna rais aliyewahi kushika nchi hii hakufuata katiba?Na km hakuna bac ujue Magufuli ataweza na kufanikiwa ila hofu yng n kwamba wote waliapa km alivyoapa yy na ktk katba ileile
hebu jaribu kuwaza kdogo shekhe kuendesha nchi co kaz kubwa coz kla ktu kpo kimuongozo systematically dont b stupd
 
Lowassa anajaribu kuwarudisha CHADEMA kundini... Anaongea pumba tupu... Yeye kama ataki watu wa Mwanza wajengewe barabara aseme tunajua ana chuki na wasukuma sababu walimwonyesha misimamo yao,,, alitaka hizo hela zikanunulie kofia na kukodisha ngoma hiyo ndio vision au kwake kupunguza msongamano kwenye barabara kwa kuzipanua sio vision?

Hiyo pesa zilishaidhinishwa na bunge alichofanya Magufuli ni kubadili tu matumizi tena kwa mema sio kwa ubaya vision imekosekana wapi hapo.. Fisadi mwizi mkubwa ebu atupishe tujenge nchi yeye alijua kuiba tu.
Unaonekana ni mropokaji, hujataka kujikita kwenye hoja ya msingi. Haya anayoyafanya Magufuli na kusifiwa hivi sasa, ndiyo aliyokuwa anayafanya Buhari kule Nigeria, sasa waulize wanigeria kama wana hamu naye tena. Tuache ushabiki Magufuli anahitaji kutulia na kufanya mambo kwa umakini asipende publicity isiyo na maana.
 
Je wewe ni mtabiri? Ongelea issues zilizopo wakati huu sio unaleta mambo ya kufikirika yasio na maono
Kwan wkt huu kuna issue ipi kubwa sana kuona kwamba nchi inaelekea kuzur kufutwa maadhmsho ya hzo ckukuu au kutengwa hela hzo kwa ajil ya barabara au yy kusafr nje kwa mara ya kwanza kwa kutumia magari?
Je umejarbu kuangalia majirani zako au hata ndg zako wanafaidikaje na utawala huu isije kuwa ww tu ndo unanufaika hujawah kuona baba ana uwezo lkn familia yake inalala njaa?
Nchi haiendeshwi kwa personal interest coz mm rais basi niamue nafanyaje then nkiondoka mwngne akija alete yake tutaendelea kweli tuache ushabk uco na maana nchi haijeng yy bali wananchi cc yatupasa tuwe upande wa pl wa coin yy upande mwngne ili iwe hela na itumiwe na wote
 
Hayo ni mawazo ya Lowasa kwani na yeye anatoa kilichomo moyoni ,lakini tumkumbushe kuwa Rais yuko sahihi kwani pesa ile imeenda kutatua kero za wananchi , kwa upande wa mashirika ya umma yamefikia hapo kwa kuwa viongozi hao waliotimuliwa waliyageuza kuwa mashamba yao ya kuvunia ,kwa mfano yule bosi wa vitambulisho naye lowasa anasema kuwa Rais alikosea kumtimua ,acheni magufuli wetu achape kazi hii ni nyota ya asubuhi tuliyopewa na Mungu
watanzania tumekuwa tukimtafuta Rais kama huyu kwa miaka mingi na sasa neema imetuangukia baada ya Mungu kusikia kilio chetu , kuongea mawazo negative dhidi ya Rais wetu ni kututia kichefuchefu wakati ninyi mlikuwa madarakani kwa muda mrefu tokea nchi inapata uhuru na mkashindwa kufanya lolote lenye tija kwa Taifa letu .God bless Magufuli
 
Poa km nabwabwaja ila unadhani kuna rais aliyewahi kushika nchi hii hakufuata katiba?Na km hakuna bac ujue Magufuli ataweza na kufanikiwa ila hofu yng n kwamba wote waliapa km alivyoapa yy na ktk katba ileile
hebu jaribu kuwaza kdogo shekhe kuendesha nchi co kaz kubwa coz kla ktu kpo kimuongozo systematically dont b stupd


Bado unabwabwaja tu kama kibogoyo, nimekuuliza kifungu gani cha Katiba raisi wa JMTZ amekivunja?
 
Hata alipokosolewa Kikwete mlisema hayahaya. Nyie ndio nyumbu wazee kweli alipokuwa anaambiwa apunguze safari mapovu yalikuwa yanawatoka, leo magufuli kabana safari mnampongeza, hovyoo.ccm tatizo hamuwezi kuukosoa uongozi wenu na ndio maana mnailetea nchi majipu nchi ninanuka usaha sasa.
 
lowasa..jpg
 
...eti maanayake nini..? hata Obama anakosolewa ijekuwa Magufuli...?? alichosema Lowassa matumizi lazima yaidhinishwe na bunge na sio kupanga na kujitekelezea mwenyewe. kesho akisema anataka bilioni mbili zikakarabati nyumba yake pia usijekuhoji...
Yeye hasemei kumkanya kuhusu kumkosoa Mh. Magufuli bali aliyomkosoa hayana tija! Hiyo ndio point yake sasa kama anamkosoa kuwajibisha mafisadi ?!?!!? Any way ni mmojawaposoon mambo yatakuwa hadharami/ bayana! Kwani nae yumo!
 
- Amlalamikia Rais Magufuli kugawa fedha kwa shughuli mbalimbali wakati chombo chenye mamlaka kugawa fedha kipo ambacho ni bunge.(Pesa za uhuru na Pesa za Muungano)

- Asikitishwa na uachishwaji wa kazi kwa wafanyakazi, asema hali ngumu ya uendeshaji wa mashirika hayo ndio usababisha utendaji hafifu.

- Asononeshwa na hali ngumu ya maisha mtaani.

- Asikitishwa na ushukaji wa huduma ya Bandari kushuka kwa asilimia 50 na kusababisha vijana wengi kusota mtaani.

- Kitendo cha wahisani kujitoa kuisaidia nchi asema n i pigo kubwa kwetu kwa mustakabali wa uchumi wa nchi.

- Asema si kweli kwamba uongozi wa Rais mstaafu Kikwete kila mtu alikuwa mla rushwa, ni kweli mfumo ule ulikuwa mbovu na wa kifisadi.
Mtu mnafiki utumjua tu kwa matendo na kauli zake,toka lini Lowasa akawahurumia wananchi,saa hizi tuna barabara swaafi pale Mwenge yote hiyo imewezekana kutokana na ubinifu na ujasiri wa raisi wetu Magufuli,enzi zake hela hiyo iliishia kwenye mvinyo Ngurdoto
 
Back
Top Bottom