Edward Lowassa akosoa uongozi wa Rais Magufuli

Edward Lowassa akosoa uongozi wa Rais Magufuli

...eti maanayake nini..? hata Obama anakosolewa ijekuwa Magufuli...?? alichosema Lowassa matumizi lazima yaidhinishwe na bunge na sio kupanga na kujitekelezea mwenyewe. kesho akisema anataka bilioni mbili zikakarabati nyumba yake pia usijekuhoji...
Watanzania wengi tu kama nyumbu! Warahisi kusifia bila kudadisi yaani sisi hadi tuje kuwa na akili ya kujiuliza maswali kabla ya kusifia ni karne moja ijayo! Ngoja siku atasema fungu fulani likajenge hekalu chato ndio tutajua kuwa tulikuwa tunasifia ujinga
 
Kwa MTU anayejali utawala wa sheria unaozingatia separation of powers kufuta kitu kilichoidhinishwa na bunge ni dharau kwa chombo hicho!!!!
Kwa MTU anayejali utawala wa sheria unaozingatia separation of powers kufuta kitu kilichoidhinishwa na bunge ni dharau kwa chombo hicho!!!!


Wewe na fisadi Lowasa wote ni vilaza, haujui kama raisi Kikatiba ndiyo mwenye uwezo wa kuamua siku gani iwe sikukuu na nipi isiwe? Kwa taarifa yako tu wacha kubadilisha matumzi ya fedha bali Raisi wa JMTZ ana uwezo wa kuzifuta kabisa hizo siku na zisiwepo na hii ni Kikatiba kabisa!
 
Watanzania Warahisi kusifia bila kudadisi yaani sisi hadi tuje kuwa na akili ya kujiuliza maswali kabla ya kusifia ni karne moja ijayo! Ngoja siku atasema fungu fulani likajenge hekalu chato ndio tutajua kuwa tulikuwa tunasifia ujinga
Ni wewe usiyepima maoni ya Lowasa....yule ni mwizi tu na alitumia hizi hafla kuuza fulana na anasa...ndio maana kwa sasa hata CHADEMA wanatumbuwa ruzuku hoteli za kitalii..! Hana sifa hata za kugombea serikali ya kijiji.
 
Fungulia uzi swala la Sioi lakini kwa hili yeye Lowassa katoa sababu kwamba pesa za serikali ziidhinishwe na bunge ! Na isiwe taasisi ya urais
Hana credibility ya kuzungumzia maamuzi ya raisi ambayo yameleta tija kwenye miundombinu....alisema Dr.Slaa Kinyesi kimehamia chumbani harufu lazima...yule angekuwa Raisi tungeanguka kabisa...hana uwezo...kwa sasa ngoja atumbuwe ruzuku ya chadema ambayo siku hizi mikutano inafanyika hoteli za nyota 5!
 
Huyu huyu Lowassa si ndiye aliyebuni njia tatu kutoka Morocco kwenda Mwenge, mbona hazungumzii ajali mbaya zilizosababishwa na uamuzi wake?. Huyu huyu Lowassa si ndiye aliyetaka kutuletea mvua za mazingaombwe kutoka Thailand?. Kukosoa ni kazi nyepesi sana wala haihitaji nguvu za ziada, kubuni kipya chenye faida kwa jamii ndipo mtihani ulipo.
 
Kwa MTU anayejali utawala wa sheria unaozingatia separation of powers kufuta kitu kilichoidhinishwa na bunge ni dharau kwa chombo hicho!!!!
Hiyo ni kweli. Ni kuona una mawazo sahihi kuliko wao,ni kuona kuwa hawakufanya maamuzi sahihi, ni kuona kuwa hawaoni matatizo yakuyapa vipaumbele.
 
Fungulia uzi swala la Sioi lakini kwa hili yeye Lowassa katoa sababu kwamba pesa za serikali ziidhinishwe na bunge ! Na isiwe taasisi ya urais
Hana kitu....bure kabisa...,anazidi kuififisha CHADEMA...kalagabaho...amkaaa!
 
mapendekezo yake yapo wapi?

upinzani kazi yao ni kukosoa Tu!

Lowassa anapinga bilioni 2 za sherehe za Muungano kujenga barabara, badala yake alitaka watu wakaserebuke na kuzitumbua hizo fedha.

Hayo ndiyo maneno ya mtu aliyetaka kuleta mabadiliko TZ!
- Amlalamikia Rais Magufuli kugawa fedha kwa shughuli mbalimbali wakati chombo chenye mamlaka kugawa fedha kipo ambacho ni bunge.(Pesa za uhuru na Pesa za Muungano)
- Asikitishwa na uachishwaji wa kazi kwa wafanyakazi, asema hali ngumu ya uendeshaji wa mashirika hayo ndio usababisha utendaji hafifu
- Asononeshwa na hali ngumu ya maisha mtaani.
- Asikitishwa na ushukaji wa huduma ya Bandari kushuka kwa asilimia 50 na kusababisha vijana wengi kusota mtaani.
- Kitendo cha wahisani kujitoa kuisaidia nchi asema n i pigo kubwa kwetu kwa mustakabali wa uchumi wa nchi
- Asema si kweli kwamba uongozi wa Rais mstaafu Kikwetu kila mtu alikuwa mla rushwa, ni kweli mfumo ule ulikuwa mbovu na wa kifisadi.
 
Banafsi naona Lowasa amesisimukwa Kwa muda.
 
Ujue Lowasa mimi huwa namuona kama hajitambui vile sijui nani kamroga anaongea pumba tupu yani hajui hata pesa ipi inatakiwa kuidhinishwa na bunge na pesa gani ipo kwenye mamlaka ya Rais,mtu mzima hovyo kabisa.
 
Back
Top Bottom