Ebu tujikumbumbushe, enzi hizo ulikuwa wapi?

Ebu tujikumbumbushe, enzi hizo ulikuwa wapi?

Shulea ya Msingi Sabasaba... Nakumbuka siku moja tulilala chini wanafunzi wote kisha kila mwalimu anapita anatuchapa fimbo moja moja, afu walimu wwenye walikwua zaidi ya 20. acha kabisa!

C.C. platozoom
 
Last edited by a moderator:
Ha ha ha ha, ukipata ngh'oroto na makamirwa niletee.

Na yale matunda ya sanyenge.

Butimba Mazoez Pr...tulikuwa tunawah namba saa 11 asubui..tunaweka mawe na mlinzi af tunapanda milimani kwenda kutafuta sungwi na upuru wa kuuza....tumeanza ujasilia kitambo..wacha tujiajili tu dah
 
Shulea ya Msingi Sabasaba... Nakumbuka siku moja tulilala chini wanafunzi wote kisha kila mwalimu anapita anatuchapa fimbo moja moja, afu walimu wwenye walikwua zaidi ya 20. acha kabisa!

C.C. platozoom

Lakini wewe kwenu ilikuwa karibu kabisa na shule, kwa nini ulikuwa unachelewa?
 
Kuna mwalimu alikuwa anaitwa mwalimu Malita, basi mimi nikatumwa ofisini nikasema nimetumwa kwa mwl Lita (eti nimeweka umoja maana Malita ni mengi), hapo ndo nimeanza kujua jua kiswahili, sikumbuki nilichapwa fimbo ngapi lakini saa izi naona kama nilionewa.
 
Dah kitambo sana!
Nakumbuka nilikuwa nikichelewa najichagulia namba. Mwalimu akianza "hili darasa waliowahi ni 12", mimi najichagulia, labda 4. Akianza namba moja pita mbele, mbili,..., akifika 4 najitokeza. Siku ya kwanza ubishi ukatokea, jamaa akashindwa kujitetea kuwa namba 4 ni yake akala mboko. Siku nyingine nikakutana na mwalimu mtata. Alivyoona tupo wawili tuna namba moja. Akatuambia tumnong'oneze nani alikuwa ana namba inayofuata..., Loh, siisahau siku hii!!!
 
Dada yako huyo!!

cc Kongosho

Hapo ndo huwa nnapochoka JF.....bas kwa heshima na taadhima ninaomba radhi kwa Dada Kongosho....Alaf jamani tukumbushane salamu tulizokuwa tunafundishwa na walimu wetu esp walimu wa English aka Kiingleza...Pale Bukoba mjini shule ya Rumuli Primary School kwa wale nshomile walitufundisha hivi...Monitor anaanza kwa kusema...Who are we? Sie tunajibu....We are young pioneer, our moto is discpline and success, also we need good leadership...Good Morning Teacher..........sasa vuta picha kwa watoto wa uswazi tulivyokuwa tunatamka iyo mambo...ni Janga...cc Kongosho
 
Duh! mmepitia mengi kumbe!

Sisi watoto wa waalimu tulikuwa tunapewa favour kubwa sana kuchelewa chelewa shule!

Mi nimesoma shule 4 mpaka kuja kuhitimu shule ya msingi mwaka 2005..

Nimeanzia Borenga primary... villa hukoo

Nikahamishiwa Kwata Primary.. Tanga

Nikahamishiwa Mwenge Primary.. Dodoma vijijini

Baadae nikaja malizia Nyanza Primary School, Mwanza City class of 2005!...(Nyanza C kwa Celina Lemunge!)

Nakumbuka siku moja mwalimu alinichapa fimbo za mgongo mfululizo eti kisa sijamwagilizia kabustani..! dah! nilimwangalia kwa hasira sana kidogo nimbebe na mimba yake! lol..

Please kama kuna classmates wangu humu tusakane!

cc Slave.
 
Last edited by a moderator:
Aga Khan Primary School Kigoma, enzi hizo nawakumbuka akina Mwamvita Makamba na ndugu zake eti sasa Mwamvita eti yuko Vodacom makao makuu South Africa kweli, yule mdada niliemfundisha hesabu na siku zingine ananiomba daftari langu anakili ili apate vema kweli,haya ngoja na mimi nipambane niwe mwanasiasa ili watoto wangu nao wapate vyeo vya bure.Mbaya zaidi hata hanikumbuki kama niliwahi kumpatia madaftari yangu aangalizie
 
Dah...Mtumishi umeongea kwa uchungu hadi :A S cry:...ila na wewe si ungepiga chata kabisa....angekukumbuka
 
Nakumbuka nilinunuliwa buti matata Sana na mzee wangu yaani ngozi mtupu nikiwa Std two teh teh teh Enzi hizo darasa zima wanapekua isipokuwa watoto wa walimu.Basi bhana ile siku sitaisahau,yaani darasa zima walini-mind wakaanza kunichana live et nimevaa viatu vya wakoma.

Kufika break ya saa nne nilikuwa sinahamu ikabidi nivirudishe nyumbani na toka siku hiyo sikuvivaa tena ikawa visingizio mwanzo mwisho.
 
Dah...Mtumishi umeongea kwa uchungu hadi :A S cry:...ila na wewe si ungepiga chata kabisa....angekukumbuka

Hahaha ndugu yangu mimi nilikuli kwenye familia ya kitumishi sasa nikawa kama zoba(nilikuwa ukinitajia mwanamke sijui kufanya matusi nakupeleka moja kwa moja kwa mwalimu hahahaha) ingawa namshukuru Mungu uzoba wangu umenisaidia kufika hapa nilipo, hata kama siyo mbali ila ntafika tu maana sikati tamaa hata kidogo.Ntafika kwa nguvu zangu mwenyewe na kwa uweza wa Mungu
 
Hahahhahah...hapo umeongea mtumishi...ila umenikumbusha enzi za kusemewa kisa umetaka kufanya matusi na mtoto wa watu.....hasa hasa kwenye kombolela....nakumbuka kulikuwa na jamaa kazi yao ni kuvizia...wakiwafuma tu utaskia eti kama mnataka nisiende kusema basi na mimi nataka....dah...utoto una vimbwanga vyake.....Kama ulicheza kombolela tupia hapa
 
Kumbukumbu p/s, si unajua mambo ya kuwahi namba. Njia ya kufika shule kutoka home lazima upite kiwanja cha biafra, watu walikuwa wanasema uwanjani kuna majini ile asubuhi asubuhi na kweli tukipita tunaona nazi zimevunjwa na lugha iliyoandikwa ni kiarabu na shillingi shillingi. Msela wangu mmoja alikuwa anaokota nazi anaila na shillingi anazichukua tunaenda kuzitumia kwenye mihogo na kachori.

Safi sana ..... na huyo msela wako lazima alikua anatumia kitimoto walau mara moja kwa wiki!
 
Butimba Mazoez Pr...tulikuwa tunawah namba saa 11 asubui..tunaweka mawe na mlinzi af tunapanda milimani kwenda kutafuta sungwi na upuru wa kuuza....tumeanza ujasilia kitambo..wacha tujiajili tu dah

Kaka upuru ndio nini, matunda fulani au?
 
Enzi za Magubike Primary School kunamwalimu mmoja alikuwa anaitwa Kayuki mmama alikuwa anachapa kichizi.
 
Mtejeta pr school - Mpwapwa, Nzovwe pr school - Mbeya, Mlabani pr school - Ifakara!
 
Back
Top Bottom