Ukisikia mwenzio amelizwa usiharakishe kufanya conclusion ukisema huyu ni mzembe tu, ukaacha kuangalia upande wa mhusika wa pili.
Nataka kusema kwamba, tutakuwa tunafanya makosa kudhani kwamba kwa kuwa organisation fulani inafanya biashara kwenye ardhi yetu basi moja kwa moja hawa jamaa ni
legit na wanafuata ethics za biashara wanayodai kuiendesha. Kinachoshtua na ambacho sikutegemea, mawaziri na wakuu wengine serikalini wanahongwa (imetokea Asia). Biashara nyingine zinatumia mwanya kushamiri kwenye nchi zinazozubaa kurekebisha sheria zake.
Miaka kadhaa nyuma nilisoma magazeti yakitahadharisha kuhusu
Loan sharks. Wakati huo waliokuwa wakilizwa walikuwa ni waganda.
Kuna thread humu inawahusu Easy Finance.
Ni uzalendo kuelimisha umma. Haya mambo ya utandawizi siku hizi, ni vyema tukasaidiana tuwagutukie
criminals waliovaa suti. Internet imeturahisishia kazi kufuatilia yanayotokea nchi nyingine, kujua kipi ni cha kutilia mashaka. Umeshawahi kusikia kuhusu illegal
MLM?
Wameshaliza watu nchi nyingi tu na wamekuwepo Tanzania hata kabla ya 2005; ila baadae kidogo ndio watu watagutuka. Miezi minne iliyopita wamekuwa kwenye kashkash mbali mbali na
Interpol. Na sasa wanafanya purukushani huko Asia hususani India.
Watu wataanza kulalama kwamba navuruga business za watu, kwa hiyo sitawataja hapa, hata hivyo sio muhimu sana kwani zaidi ya asilima 30 ya wakazi wa jijini wanaifahamu biashara hii.
Illegal pyramid or Ponzi schemes.
Microfinance: BoT to crack down on loan shark creditors
.