Hawa jamaa ni matapeli hasa, mimi kuna mtu ninamfahamu alitaka mkopo wa Tsh 3m for two weeks, walimzunguusha 1 week, wakati walimwambia atapata mkopo ndani ya 3 days.
1. alitakiwa kujaza form ya Shs 20,000 non-refundable, kabla ya kuuona mkataba, na form yenyewe ilikuwa inaulizia jina, mtaa yaani vitu personal tu.
2. Next day wakamwambia inabidi achangie stationary Shs 100,000 (non-refundable)akatafuta akawapa
3. Aliporudisha form kwa ajili ya makubaliano ya mkopo, masharti yalikuwa aweke kadi ya gari, Alipopeleka kadi wakamwambia gari yako inabidi iwe imekatiwa comprehensive insurance na kumtaka atoe Shs 300,000 wamkatie, akawapa na hawakumpa hiyo insurance
4. Alipoonana na mkurugenzi anayejukana kama Hamis Faraji kwa ajili ya kusign mkataba akaambiwa interest rate ni 30% kwa mwezi, akawaambia kama inawezekana kupunguziwa kwa kuwa yeye alitaka kwa wiki 2 wakakataa. Hivyo akaona kama ni hivyo basi bora aache kwani wiki ilikuwa imeisha, wakamwambia hawatamrefund pesa yoyote aliyotumia kama ataacha process ( yaani ni Tshs 420,000), ikabidi akubali kuendelea na mchakato, Lakini siku ya kwenda kuchukua hiyo pesa wakamwambia tena katika account aache Ths 150,000 hivyo akapata mkopo wa 2,850,000 badala ya 3M,
After 1 week aliporudisha wakamwambia arudishe 3,900,000 out of (420,000 +150,000) hapo sasa akawajia juu na kuwapa Tshs 3,600,000 only
Ukiangalia ni kwamba kwa mkopo wa Tshs 2,850,000 within 1 week walipata extra 1,320,000 ambayo ni sawa 46% of interest in 1 week. Sasa kama huu si wizi na utapeli ni nini?
My Take
Watu kama hawa easy finance wanadidimiza wananchi na kuiba jasho la wananchi masikini huku vyombo vya kuregulate na ku-oversight financial sector vikiwa havina habari. Huu ni wizi uliohalalishwa ambao ni sawa na ufisadi. Unatarajia mjalisiamali atajikwamua na maisha katika mazingira kama haya.