Mkuu JokaKuu zingekuwa enzi za Kambarage jamaa huyo asingetia mguu tena Arusha/Tanzania, kwa mawazo yao wanachukulia JK kuwa mpole na muhungwana kama ni dalili za kuwaogopa vile, which's totally false. Admin ya Rwanda na wapambe/wateule wao wana mambo ya chini chini sana - raia wengi Tanzania walionya kuhusu kuruhusu Rwanda kujiunga na jumuhia, lakini Mseveni ndio akawapigia debe PK (Rwanda) 4 a reason, kubwa ikiwa ni kumsogeza karibu comrade-in-arm i.e like mind mwezake waendeleze ndoto zao za SIRI - yaani mikakati yao ya siku nyingi tangu wakiwa kwenye vita vya misituni (Luwero Triangle huko Uganda), haya tunayo yashuhudia kwenye Jumuhia siku za hivi karibuni si ya bahati mbaya, yanakuwa instigated na hao wawili. Mh.Kenyatta kutokana na Umri wake kuwa mdogo ukilinganisha na wakina M7 na PK ndio maaana wanamuingiza kwenye mkenge taratibu taratibu bila ya yeye kulitambua hilo, wakisha mlainisha na kumsoma vizuri watangehuzia kibao - jamaa hawa wako highly unpredictable, oh yes M7 na PK waliwahi kugehukana huko DRC wakapigana vita kwa muda, kama wanafikia hatua ya kugehukana wao kwa wao, itakuwa mtu baki? Zingekuwa enzi za mzee Kibaki wasingeweza kutamba kama wanavyo tamba hivi sasa, wanaendelea kuvunja kanuni za jumuhia with impunity hawajali ma azimio yaliyo wahai kufikiwa kwenye jumuhia, wao wanaleta mapendekezo mbadala ya ajabu ajabu mfano fast tracking Political .... hii ina umuhimu gani kwa hivi sasa? Mawazo yao yote yako kwenye kutaka kutawala Africa Mashariki na kuleta vurugu walizo zoea, hawana jema lolote kwenye jumuhia yetu- Majivuno tu. Hivi Seziraba anataka kutueleza nini anaposema Tanzania tunataka kuchuma tusichopanda!! Rwanda imewahi kupanda kitu gani cha maana katika ustawi wa EA zaidi ya kufanya member countries kutoelewane, juzi juzi tu alimwachia mwenzake Njoroge aiseme Tanzania kuhusu wahamiaji haramu kutoka Rwanda as if Raia wa nchi nyingine hawakuwa affected na zoezi hilo! Always wako self centered na kijifanya wana majibu ya kila tatizo ndani ya Jumuhia. Tuwe wakweli hapa tangu Seziraba akabidhiwe cheo hicho kuna mambo mengi yamefanyika under his watch ni as if amakuja na mikakati ya aina fulani chukulia mifano ifuatayo: Rwanda kushurtisha baadhi ya members wasusie vikao ili walazimishe vikao viwe vina rotate kwenye miji ya members countries,kitu ambacho hakikuwahi kupendekezwa siku za nyuma, kuingia Rwanda tu ndio kelele zikahanza hawataki vikao vifyanike Arusha muda wote, si hilo tu waliwahi kuja na a wild idea eti makao makuu yahamie Nairobi!! Hivi Rwanda ina bifu gani na Nchi yetu iliyo wahi kuwahifadhi Maelfu ya Wanyarwanda ikatumia resources zake kuwasomesha baadhi yao mpaka wakahitimu vyuo vikuu, watu hawa hawana shukrani.