"E Motherland" ndani ya JamiiForums ni kwa kusudio maalumu. Ni vyema niwashirikishe

E Motherland

Member
Oct 1, 2023
20
10
U hali gani msomaji? Pole na majukumu ya hapa na pale ya shughuli zote za ujenzi wa taifa

E Motherland ni ID mpya inayomilikiwa na mimi mwandishi (Jina kapuni) ikiwa chini ya uangalizi mzima wa uongozi wa JamiiForums. Lengo la kuanzisha ID hii ni kukupasha habari za burudani zinazowahusu wasanii hasa wa muziki na michezo ya runinga ikiwemo ucheshi. ID hii itajihusisha zaidi na kazi za kisanaa kutoka kwa wasanii chipukizi ambao wanafanya vyema katika tasnia hizi

Hivyo ID hii itakuwa maalumu kwa ajili ya burudani (exclusives) wala haitojihisisha na siasa kwa ujumla. Karibuni tuutumie muda wetu wa ziada kuburudisha akili zetu kutokana na mchoko wa hapa na pale tuupatao katika mihangaiko yetu ya hapa na pale

Naombeni kukaribishwa humu jukwaani. Pia naomba kuitambulisha ID hii na kuiwasilisha kwenu wana JamiiForums kwa ujumla

Karibuni kwa maoni na ushauri
 
Anza kuandika jukwaa la celebrities tuone.
Sina uzoefu mkubwa wa uandishi ama uwasilishaji taarifa. Lakini nimejaaliwa kipawa cha kufikisha taarifa mbele ya hadhira na watu wakaipenda

Hivyo mtaniwia radhi katika uwasilishaji mbovu nitakaokuwa nao

Ahsante
 
Sina uzoefu mkubwa wa uandishi ama uwasilishaji taarifa. Lakini nimejaaliwa kipawa cha kufikisha taarifa mbele ya hadhira na watu wakaipenda

Hivyo mtaniwia radhi katika uwasilishaji mbovu nitakaokuwa nao

Ahsante
Ujumbe sahihi hufikishwa kwa lugha sahihi,kama hujui kuandika kajifundishe kwanza,JF ipo tu utaikuta.
 
Back
Top Bottom