Hot27
JF-Expert Member
- Oct 31, 2020
- 308
- 422
Habari za wakati huu member wote wa JF. Bila kupoteza muda niende moja kwa moja kwenye mada ama swali kwa wenye ujuzi na wanaopenda kufahamu.
Jambo liko hivi, Leo wakati nimeenda duka la hatua chache toka ninapoishi nimekutana na jambo lililonishangaza kidogo.
Nilipofika dukani nikamkuta mzee, nadhani ni mstaafu ameamua afungue duka maranyingi nawakutaga watoto wake. Baada ya kumpatia hela kiasi cha shilingi 2000 na kuchukua mahitaji yangu ambapo hela iliyobaki ilikua Tsh 300. Sasa wakati ananipatia ile hela iliyobaki vidole vikagusana nikahisi shoti kama ya umeme iliyonishtua.
Baada ya ile shoti nikahisi ni zile chuma za dirishani ikabidi niziachie haraka hali ambayo yule mzee aliigundua.
Kwa maelezo yake aliniambia kuwa anawiki sasa yuko kwenye hali hio, maranyingi ni yeye ambae anahisi hio hali na si anaegusana nae ila leo amekutana na mtu ambae ameona pia hio hali ambae ni mimi.
Naomba kuuliza hiki kitu kinawezekana?! Nini chanzo chake na je, inatibika?! Ni kivipi anaweza kuitibu hio hali?!
Natanguliza shukrani zangu za dhati kwenu.