DV Lottery (green card) 2012 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

DV Lottery (green card) 2012

Discussion in 'International Forum' started by YoungCorporate, May 1, 2011.

 1. YoungCorporate

  YoungCorporate JF-Expert Member

  #1
  May 1, 2011
  Joined: Apr 30, 2010
  Messages: 388
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  habari za leo wanajamii, mashabiki wa man u poleni kwa kipigo toka imarati...

  Kwa wadau wanaofuatilia dv lottery 2012 matokeo yameshatoka leo May1, nilitaka kuuliza kuna yeyote humu amepenya jamani?? Au kuna ambaye amewahi kupata dv lottery (nazungimzia ile yenyewe inayotolewa na state department sio phishy agents) hii anisaidie maujanja pamoja na docs za kuwa nazo ikiwa umechaguliwa??
   
 2. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #2
  May 1, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,774
  Likes Received: 83,114
  Trophy Points: 280
  Sidhani kama kuna ujanja wowote ni bahati ya mtu tu. Na nawafahamu baadhi ya Wabongo waliobahatika kuchaguliwa katika bahati nasibu hii. Ila ni vizuri kukamilisha taratibu zote mapema badala ya kusubiri mpaka dakika za mwisho ambapo inakuwa ni kazi ngumu mno kutuma maombi. Unaweza ukapoteza masaa chungu nzima katika jitihada za kutuma maombi yako bila mafanikio yoyote.
   
 3. YoungCorporate

  YoungCorporate JF-Expert Member

  #3
  May 1, 2011
  Joined: Apr 30, 2010
  Messages: 388
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  mkuu nashukuru labda nifanunue kidogo, ile stage ya kutuma maombi online ilishapita sasa nimechaguliwa kwa ajili ya kwenda kufanyiwa interview na masuala mengine sasa ndio nilitaka kujua kama kuna mzoefu aliepata miaka ya karibuni anipe details, ni kipi hasa wanahitaji?
   
 4. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #4
  May 2, 2011
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,122
  Likes Received: 617
  Trophy Points: 280
  Hongera kwa kuchaguliwa, fuata maelekezo waliyokupa hauhijati cha ziada hawana mambo ya kiswahili hao.
   
 5. Buggy

  Buggy JF-Expert Member

  #5
  May 2, 2011
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 239
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Duuuu...siamini. Nimepata dv lottery!!!!!!
   
 6. YoungCorporate

  YoungCorporate JF-Expert Member

  #6
  May 2, 2011
  Joined: Apr 30, 2010
  Messages: 388
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  mkuu hongera pia kwa kuchaguliwa....its time to take tough decisions
   
 7. K

  Kahinda JF-Expert Member

  #7
  May 2, 2011
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 849
  Likes Received: 133
  Trophy Points: 60
  Kwanza utapata barua ya kukujulisha kuwa iko miongoni mwa waliochaguliwa kwenye DV loterry hiyo.
  Kisha utatatakiwa kujaza form ambayo state dept watakutumia ili kudhibitisha kwamba unakubali au unaafiki ili hatua nyingine zifuate.
  ukisha wajibu kuwa umekubali kisha watakutumia form za kujieleza wewe na familia yako yote yaani familia yako kama umeoa,wazazi wako wote.
  utaeleza umewahi kuishi wapi miaka 10 iliyopita hiyo ni pamoja na shule,nchi ulizowahi kuishi.
  Watahitaji nakala ya kila cheti ambacho utaelezea kuwa nacho,km.vyeti vya shule, kuzaliwa kama unavyo au affidavits zozote utakazo kuwa nazo.
  Utatakiwa kupima afya yako kwa daktari watakaye kuelekeza wao na huyo akisha kamilisha vipimo atakupa majibu yako na bahasha ambayo iko sealed kwa ajili ya kuwatumia.Itakuchukua muda kias kwamba unaweza ukadhani hiyo kitu haipo watakuwa wanafuatilia taarifa ulizowapa.Endapo kuna kitu wanataka watawasiliana nawewe moja kwa moja.Kama kila kitu ulichowapa kiko kamili watakujulisha siku ya kwenda kwenye enterview na mahali. Kwa wale ambao wako USA unaweza kuadjust stutus yako au kuomba viza ya migrant.
  Gharama ni kubwa kidogo kuliko viza ya kawaida hivyo jiandae kwa hilo.
  Hayo ni maelezo kwa kifupi form zenyewe zinajieleza, na hawana usumbufu wowote.
  kumbuka siku ya enterview kwenda na nakala halisi ya kila document uliyowatumia kwani watahitaji kuziona nakala halisi na watataka nakala hizo tena kwani zile za mwanzo zilikuwa kwa ajili ya state dept na hizo za sasa ni za uhamiaji(consular office).
   
 8. YoungCorporate

  YoungCorporate JF-Expert Member

  #8
  May 2, 2011
  Joined: Apr 30, 2010
  Messages: 388
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  mkuu shukrani sana kwa maelezo yaliyonyooka, hiyo barua ya kuniarifu nimeshinda nimeipata na wameandika niiretain, sasa sijui hizo form zinatumwa kwa posta au online? Na pia unakadiria itachukua muda gani toka kupata barua ya kuchaguliwa na kuitwa kwenye interview? Na pia wastani wa gharama ni kiasi gani mm nipo tanzania. Na je kwa uzoefu wako ni visa category gani ambayo ni nzuri kwa mm ambaye natarajia kwenda kuongeza nondo na kupiga boksi la uhalali? Natanguliza shukrani
   
 9. K

  Kahinda JF-Expert Member

  #9
  May 2, 2011
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 849
  Likes Received: 133
  Trophy Points: 60
  Naomba nikupe tahadhali hivi karibuni nilikuwa bongo na mtu mmoja akapata email ya kitapeli ikimujulisha kuwa amewin green card, sasa angalia kuna matapeli. Forms hizo zitatumwa kwako kutoka state dept zina (bar code).

  Kumbuka hakuna malipo yoyote ambayo utatakiwa kuyafanya mpaka siku ya kuitwa ubalozini kwakuwa uko Tanzania.
  Na hiyo itakuwa baada ya kukamilisha hatua zote hizo ambazo si chini ya miezi 6(napo sema miezi sita mara nyingi ni zaidi ya hiyo miezi) kwa maana taarifa zako zote na historia yako maafisa wa FBI na makachelo wengine wa kimarekani watazifanyia kazi wakisha kuclear kwamba siyo jambazi au huna matatizo yoyote ya kiafya n.k ndipo watakapo kujulisha tarehe na saa ya interview hapo ubalozini.

  Siku ya interview huna maelezo mengi wanachotaka ni kukuona physically maana kumbuka muda wote utakuwa umekuwa unawasiliana nao kwa makaratasi na picha tu,hivyo wanachofanya siku hiyo nikukagua document's ulizowatumia na original copies ulizo nazo.Hivyo mpaka kufikia hatua hiyo huwa kuna miezi kadha. Jitahidi kuwa mkweli maana hawa jamaa watafika mpaka kijijini kwako(Kufanya Vetting).

  Huchagui aina ya visa/viza kwani hiyo greencard or DV lottery Visa inajieleza, ni visa inayokupa status ya kuwa mkazi wa marekani(permanent residence),ambapo unakuwa na haki zote za raia wa Marekani isipokuwa kupiga kura kwenye uchaguzi wa ngazi za kitaifa(federal).

  Hivyo na sisitiza kama una barua hiyo na huna uhakika nayo nenda Ubalozi wa marekani uthibitishe kwani kuna utapeli umeenea hasa kwa kuzingatia kuwa watu wengi ni wageni kwenye swala hili, usimtumie mtu malipo yoyote malipo yanalipwa siku ya interview ambayo haifanyiwi mahala popote zaidi ya ubalozini.
   
 10. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #10
  May 2, 2011
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Nilipata email kama two weeks ago ikinitaarifu kuwa nimebahatika kuwa chosen, na nilipie USD 800 per person. Actually nikawapigia watu wa kitengo cha diversity visa US Embassy ku-confirm nao wakaniambia it is absolutely scammer. Ningependa kutoa tahadhari kuwa usijiingize kwenye kulipia kwa postal orders au online. Ni vizuri ukalipie ubalozini kwani uwezekano wa kuibiwa ni mkubwa sana. This is from my personal experience not from someone else.
   
 11. Original Pastor

  Original Pastor JF-Expert Member

  #11
  May 2, 2011
  Joined: Nov 14, 2007
  Messages: 1,256
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Wakuu Heshima mbele kuuliza si ujinga , Ila ujinga wakati wa kwenda . Je na mimi naweza kujiunga online nikajaza Greencard ili na mimi nichaguliwe??? Au Mkuu unafanyaje hapo???
   
 12. Mzuzu

  Mzuzu JF-Expert Member

  #12
  May 2, 2011
  Joined: Jul 11, 2007
  Messages: 487
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 45
  Hiyo green card ni visa category na huwezi kubadilisha inaitwa DV visa na ukija wapewa green card inayokupa uwezo wa kufanya hayo yote uliyoyataje legally. Fomu utapata kwa posta kwa adress uliyopatia barua inweza kuja baada ya miezi 4 hivi zipo online pia unaweza kuzicheck uzifahamu but hushauriwi kuzijaza kwa vile wanavytuma wanakuwa wametoa na visa allocation namba. Ukijaza na kurudisa utasubiri tena kama miezi mi 4 mingine then itakuja barua nyingine kukupa visa interview appointment ubalozini hapa ndo utaenda na vyeti vyako original na copy, kwenye fomu hakuna vyeti unavyotuma bado kumbuka hapo watauliza level ya elimu yako na historia na familia dependants unaotegemea kuondoka nao au watakaokufuata kwa kutumia visa yako baadaye.

  Gharama mwaka 2009 ilikuwa $750 kwa kila kichwa sidhani kama imeshuka zaidi itakuwa imepanda tu! Unaruhusiwa kuondoka na familia yako yote yaani mke watoto na dependants wako wote wanaokutegemea walio chini ya 18 yrs ambayo ni single. So jiandae wanapokea $ na madafu pia kwa thamani hiyo siku ya interview. Hamna maswali ya kusumbua ila ni kujustify tu vyeti na familia yako

  Kwa ujumla itakuchukua kama mwaka hivi kumaliza process na kupata Visa ya kuingia US na pia utapewa 6 months uwe umesafiri. Kingine muhimu uwe na contact ya mtu anayekufahamu ambaye atatakiwa kusign affidavit form ya kukupokea na kukuguide usijekuwa public charge and anatakiwa aonyeshe uwezo wa kifedha kukuhudumia kwa miezi michache.
   
 13. Mzuzu

  Mzuzu JF-Expert Member

  #13
  May 2, 2011
  Joined: Jul 11, 2007
  Messages: 487
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 45
  Unaweza kucheza kwa kuweka picha yako American visa standard kwa www.dvlottery.state.gov kuanzia mwezi October hadi Dec kila mwaka wanapokea entries kwa siku 60 tu kila mwaka kwa ajili ya maombi ya mwaka unaofuata
   
 14. YoungCorporate

  YoungCorporate JF-Expert Member

  #14
  May 2, 2011
  Joined: Apr 30, 2010
  Messages: 388
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  mkuu thanks again, hii ninyozungumzia ni dv halisi inayotolewa na state department katika website ya dvlottery.state.gov barua ina bar code na pia namna ya kuipata ni baada ya kujaza info za wakati wa kuapply kama umewahi kushiriki dv nadhani unaelewa. Nimeona kwenye ile barua maelezo zaidi yanapatikana dvselectee.state.gov ambapo pia zile form za kentuck zipo ambapo natakiwa kuzijaza na kuzituma, sasa kuna clause moja kwenye form yataka nijaze mwenyeji wangu US adress yake na simu lakini mm sina mtu wa karibu alie US hapo nafanyeje?

  Kuhusu pesa ni kweli wamesema ni pesa ya viza kawaida nitalipia ubalozini ambapo kwa category ya dv ni kama usd 420 hilo sio tatizo kwangu, pia kwenye form wanahitaji nijaze mji ninanotarajia kwa perm residedc, sijawahi kufika us sina idea, je mkuu unakauzoefu na amerika unipe ideas?

  Mambo mengine ni ya kawaida kama vyeti pasip
   
 15. YoungCorporate

  YoungCorporate JF-Expert Member

  #15
  May 2, 2011
  Joined: Apr 30, 2010
  Messages: 388
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  mkuu mbona naona kama maelekezo yanataka nijaze ile ya online tena wanasuggest mapema iwezekanavyo coz wanataka by sept 30 this yr iwe tayrai nimeitwa kwenye interview?? Au mm sijaelewa?? Hapo kwenye mwenyeji ndio nina tatizo sina mtu ninayemfahamu aliopo US, je nitumie skills gani?? Pia nina elimu ya chuo lakini mpaka sasa sijafuatalia cheti coz nilipata kazi baada ya kumaliza so sikufuatalia tena na ninajua itachukua muda, je naweza kusbmit zile result slips tu then vyeti halisi nikatumia vya 4 na 6, mm natumia category ya education kama eligibility?
   
 16. Mzuzu

  Mzuzu JF-Expert Member

  #16
  May 3, 2011
  Joined: Jul 11, 2007
  Messages: 487
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 45
  Kama wamekutumia mzee we jaza tu haraka kumbuka kuna watu 100,000 waliochaguliwa na watakaopata Visa ni 55,000 tu na anayewahi ndo anayepata. Jaza fomu kwa ukweli kila kitu coz wanafuatilia na ukiitwa ht km una transcript utaonyesha hizo japo itakuchukua mwaka kuitwa. Kumbua hizi ni Viza za 2011/2012 fiscal year so ni lazima interview zianze baada ya mwaka wa fedha kuanza Oct 11. Suala la mwenyeji mzee ndo kuumiza kichwa kwani ndo waTz wengi huwa wanashindwa kumaliza mchakato hapo, na mbaya zaidi ndo wanataka ajaze affidavit na ipitie iwe notarized US

  Ni bora uanze kufikiria mapema coz isije kukusurprise inasumbua sana mkuu!
   
 17. MNDEE

  MNDEE JF-Expert Member

  #17
  May 3, 2011
  Joined: Jul 10, 2009
  Messages: 494
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 0
  Mkuu kwa maelezo ninayosoma hapa inaonekana kuna mabadiliko, back in 2001 ndugu yangu mmoja alishinda dv loteri, mambo yalikuwa rahisi tu.

  Kwa wale walioshinda wasije wakakata tamaa wakidhani kama hawana mtu USA basi watupilie mbali ndoto zao. Kuna gharama ya visa, vipimo, nauli na pesa ya kuanzia maisha, back then yule ndugu yangu zaidi ya address alionyesha bank statement milioni 6.

  Nawashauri wale walioshinda watumie mtandao kucheki miji mbali mbali ya USA, linganisha gharama za maisha, hakikisha ile sehemu unachagua (kitongoji) kuna usafiri wa public yaani mabasi na treni, itasaidia kupata usafiri hadi pale utakapojikwamua ukanunua gari.

  Kwa vile unahitaji mahali pa kufikia cheki hotels/motels/Inns zile za bei ndogo, wasiliana nao, ubagaini bei, watakupa discount nzuri kama ni mteja wa kukaa muda mrefu - muda mrefu could be two weeks, three weeks, a month etc. Hapa utakuwa umeshapata address unayohitaji kujaza kwenye form za visa.

  Tengeneza Resume/cv yako uanze kutafuta kazi - assuming 'umekwenda shule' unaweza uzika bila shida. Fungua profile Linkedin, Moster na kwengine. Wako watu walifanikiwa kupangiwa interview na wengine kupata kazi wakiwa nje ya USA. Infact kama utafanya hii mapema inaweza kukusaidia kuamua uende mji gani. All the best!
   
 18. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #18
  May 3, 2011
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  Msiangaike sana muulizeni |Nyani ngabu yeye alipata kijani kwa kuoa XXXL la North dakota....short cut way....
   
 19. K

  Kahinda JF-Expert Member

  #19
  May 3, 2011
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 849
  Likes Received: 133
  Trophy Points: 60
  Ni kweli mara nyingi wanapenda uwe na mwenyeji wa kukupokea.Kwa sababu wanategemea kuwa mara unapoingia USA utahitaji mahali pa kuishi, na kuna hatua nyinginezo za kufanya kama kupata namba ya Social Security ambayo bila kuwa na namba hiyo ni vigumu kufanya jambo lolote hasa kupata kazi, kufungua account ya banki, kupata leseni ya udereva na mambo mengi. Kwa hiyo katika kipindi hicho unapokiwa kwenye hatua hiyo unahitaji mwenyeji.

  Huyo mwenyeji ukimpata atakuandikia barua ambayo utakwenda nayo ubalozini siku ya interview ni kama mdhamini wako, nasema hivyo kwa kuwa nisha dhamini watu wawili ambao nao walipata green card zao wakiwa huko nyumbani, na nilijitahidi kuwaelezea kila hatua kwani na mimi nilibahatika kupata hiyo card.Labda ni kuambie kuwa ni gharama kidogo lakini utaona matunda yake ndugu yangu, kwa hiyo kazana na usichelewe kwani mko wengi na watachujwa kutoka watu 100,000 waliopewa barua kama yako hadi 55,000 tu.
   
 20. YoungCorporate

  YoungCorporate JF-Expert Member

  #20
  May 4, 2011
  Joined: Apr 30, 2010
  Messages: 388
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  mkuu thanks sana, sasa nataka kutuma hii form je naweza kutumia posta yetu ya kawaida, je on average posta za kawaida hutumia muda gani kufikisha barua U.S, DHL naona ni ghali mno...je nikitumia posta sitapoteza muda sana?
   
Loading...