Naomba nikupe tahadhali hivi karibuni nilikuwa bongo na mtu mmoja akapata email ya kitapeli ikimujulisha kuwa amewin green card, sasa angalia kuna matapeli. Forms hizo zitatumwa kwako kutoka state dept zina (bar code).
Kumbuka hakuna malipo yoyote ambayo utatakiwa kuyafanya mpaka siku ya kuitwa ubalozini kwakuwa uko Tanzania.
Na hiyo itakuwa baada ya kukamilisha hatua zote hizo ambazo si chini ya miezi 6(napo sema miezi sita mara nyingi ni zaidi ya hiyo miezi) kwa maana taarifa zako zote na historia yako maafisa wa FBI na makachelo wengine wa kimarekani watazifanyia kazi wakisha kuclear kwamba siyo jambazi au huna matatizo yoyote ya kiafya n.k ndipo watakapo kujulisha tarehe na saa ya interview hapo ubalozini.
Siku ya interview huna maelezo mengi wanachotaka ni kukuona physically maana kumbuka muda wote utakuwa umekuwa unawasiliana nao kwa makaratasi na picha tu,hivyo wanachofanya siku hiyo nikukagua document's ulizowatumia na original copies ulizo nazo.Hivyo mpaka kufikia hatua hiyo huwa kuna miezi kadha. Jitahidi kuwa mkweli maana hawa jamaa watafika mpaka kijijini kwako(Kufanya Vetting).
Huchagui aina ya visa/viza kwani hiyo greencard or DV lottery Visa inajieleza, ni visa inayokupa status ya kuwa mkazi wa marekani(permanent residence),ambapo unakuwa na haki zote za raia wa Marekani isipokuwa kupiga kura kwenye uchaguzi wa ngazi za kitaifa(federal).
Hivyo na sisitiza kama una barua hiyo na huna uhakika nayo nenda Ubalozi wa marekani uthibitishe kwani kuna utapeli umeenea hasa kwa kuzingatia kuwa watu wengi ni wageni kwenye swala hili, usimtumie mtu malipo yoyote malipo yanalipwa siku ya interview ambayo haifanyiwi mahala popote zaidi ya ubalozini.