Duru za siasa: Uchaguzi Mkuu USA

What an about turn! Kweli leo tumeshuhudia democracy at work kwa kuwapa nafasi wenye duku duku mioyoni kuzitoa kwa uhuru ili mwisho wa yote umoja upatikane. Convention ya DNC ilipoanza ni wachache walikuwa na tumaini kwamba mambo yangeisha salama lakini hapana, busara badala ya ubabe ikapewa nafasi. Naam, Busara badala ya ubabe! Kwa mbali nakumbuka ya Dodoma mwaka jana. Je kuna chochote Wtanzania tunajifunza hapa?

Kwa sasa Paul Simon anaimba wimbo wa Bridge over troubled water. Wenzetu wako mbali.
 
Sarah Silverman amezungumza kauli itakayoweza kuleta sintofahamu

Kama comedian amesema, wanaosema Bernie of burst are ridiculous

Kulikuwa na kushangilia kwa hali ya juu kwa Clinton team, huku miong'ono ikiendelea kwa Bernie supporter

Sijui itapokelewaje ingawa inasemwa ni power of 'comedy'
 
Eva Longoria

-Anatoka Texas, na historia inasema Texas ilikuwa Mexico

-Trump akituita criminal na rapist ni matusi, in fact baba alikuwa Veteran

-Naamini mgombea anayetuamini wote Hillary

-Hillary amesimam health, envorn n.k. na ni most qualified candidate

*Huyu ni star wa desperate wives

Anamkaribisha seneta Cory Booker wa New Jersy
 
Cory Booker

Ansema

-240 miaka iliyopita mababu zetu walisimama hapa kutangaza tutakuwa huru, leo tupo hapa kuthbitisha uhuru na kuhakikishia tunaendelea kwa ubora wa utamaduni wetu

-Anaongela historia na patriotism

-Anaongelea Trump anavyoligawa Taifa, akisema kutukana PWO kama McCain ni kuwatukana mashuja na huyo si kamanda in chief

-Anasema wamexico wanaleta crime, anamzungumzia jaji aliyekuwa na ugomvi

-Anazungumzia Trump na wanawake, na kusema anatukana wanawake katika hali asiyoweza kutukana watoto wake

-Trump anasema ataendesha nchi kama anavyoendesha biashara zake

-Alikuwa tajiri aki declare bankruptcy akisema pesa alizochukua kwa shughuli hizo ilikuwa deal, huku akiacha watu wengi katika matatizo

-Amerika tunasimama kwa Bully, na nyakati za crisis hatuachi value zetu

-Anazungumzia vale za Clinton kuhusu disability na weledi wake wa kisheria kusaidia watu wanaohitaji msaada wa kisheria

Amepigania watu na tunamjua
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Cory Booker anaongea katika inspiration ya hali ya juu sana

Anaongea kwa kasi, mpangilio na mantiki

Amemaliza lakini anaongea sana , kwa mantiki inspiration na hamasa

Amemaliza
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Chery

Huyu ni victim wa Trump University

-Alikuwa embarrassed na jinis alivyotapeliwa na Trump University

-Trump ametapeli, watu 5000 wakiwemo Polisi, wajane n.k.

-Anauliza utapeli wa Trump ni mwanaume gani anaweza kuufanya

-Msidanganyike kwa Tapeli Waamerika

Amemaliza.

Video ya kumu introduce Michelle Obama
 
  • Thanks
Reactions: BAK
MICHELLE OBAMA

Anasema

- Ni ngumu kuamini ni miaka 8 tangu nilipokuwa hapa kueleza kwanini mume wangu awe Rais

-Niliwambia juu ya mabinti zetu na kwa muda wote wamekuwa ni wasichana wakubwa,

-Tulivyowaeleza mabinti juu ya chuki na kwamba siyo spirit ya nchi hii

-Motivation yao ilikuwa 'wakienda low, tunakwenda high'

-Uchaguzi ni kuonyesha tunavyo shape maisha ya watoto wetu

-Mtu mwenye qualification pekee kati ya wagombea ni Clinton

-Alposhindwa na Obama hakuwa na hasira au chuki

-Hillary hakukata tamaa , alijua kuna kazi kubwa kuliko masilahi yake binafsi

-Ninacho admire kwa Hillary, hawi distracted na wala hakimbii chochote

-Nataka mtu anayejua kazi ya Urais

-Ukiwa na nuclear code na military, unahitaji kuwa well informed na steady

-Nataka Rais mwenye public record, mtu anayepigania watu

-Nataka Rais atakayefundisha kila mtu kila mmoja ni muhimu, wote ni wamoja, na crisis ikitokea hatugeukiana, tunasililizana kwasababu tuna nguvu kwa pamoja.

-Katika uchaguzi huu nipo naye
 
Michelle

- Hillary anajua thamani za Taifa

-Anajua Polisi ofisa wanaotaka kuwapa watoto Amani

-Anajua watu waliokuwa Orlando wakitoa damu kwa majeruhi

-Ninaamka kila asubhi katika nyumba iliyojengwa na watumwa. Hiyo ndiyo ndoto ya Amerika.

-Kwasababu ya Hillary, watoto wetu wa kike sasa wana gurantee kuwa wanaweza kuwa Rais wa Amerika

-Asiwepo anayewaambia we need to make America great again, tayari ni great

- Hatuwezi kukaa nyuma na kusema kila kitu kipo sawa

-Kati ya sasa na November tunapaswa kufanya tuliyofanya miaka 8 iliyopita

-Tutoe upendo, tugonge milango ili Hillary awe Rais

Amemaliza

Hotruba ilikuwa nzuri sana
 
ELIZABETH WARREN

Anasema

- Thank you Bernie, amewashukuru Michelle na Cory Booke

-Tunachaguo, upande mmoja mtu aliyerithi pesa na kuendelea kutapeli, anayejijali. Kwa upande mwingine, mwanamke tough, asiyekataa tamaa na mwanamke asiyekata tamaa

-Tupo hapa, chaguo letu ni Hillary, nipo na Hillary

***kuna kelele background****

Eliza anaendelea

- Amerika ni nchi ya opportunity

-Ninaheshima kwa US, naogopa sifa ya US inapotea kwa watu wanaofanya kazi wakiwa na ujira mdogo, nyumba, huduma za watoto, wanafunzi na mikopo, watu wana madeni na familia zinaogopa kuanguka, hii si sawa

-US si masikini, stock market zinakwenda juu, CEO wanatengeneza pesa, lakini mafao hayafikii

-System is rigged!!!!

-Washington wanatumikia mashirika, wall street, lakini jaribu kuwatumikia watu, utapata moto. Dem wamechukua vita hiyo

-Dem inasimama kwa consumer, tumepigana na tume improve maisha ya mamilioni, ahsante Obama
 
Warren Elizabeth

-Kuna tofauti kwa watu wanao keep system rigged kama GOP na watu wanaopigania watu kama Dem

-GOP wamekataa tax cut, tuition n.k. Kwa GOP waliosema no, Nov waamerika watawafikia

-Trump alikuwa wapi bila kuwasadia watu. Maisha yake ni ku take advantage of rigged system

-Trump anasema alikuwa excited na recession kwasababu alijua itamsaidia katika real estate

-Successful business man aliye file bankruptcy 6 times

-Ni mtu gani huyu anayetumaini watu wapoteze nyumba na maisha kwa faida yake. Ni mtu gani huyu anayetapeli wanafuzi? Nitawaambia, ni mtu asiyetakiwa kuwa Rais wa Marekani

-Trump anajua watu wa Amerika wana hasira akiona kutoka Trump tower. Juzi ameonge kwa saa nzima, licha ya kuzungumzia upuuzi wa wall ambao hautajengwa, je, ulisikia idea yoyote?

-Trump hana plan, job, senior wau wanafuni

-Anatumia hofu kuwatisha , anajenga hofu na chuki, kati ya makundi ya jamii

-Divide and concur ni njia mbovu
 
ELIZA WARREN
Tukigeukiana hatutaweza kushinda changamoto

- Hii ni juu ya share values zetu kwa wagombea

-tunaamini yoyote ana haki sawa na hakuna ubaguzi, na tupo naye

-Tunaamini hakuna anayefanya kazi halafu aishi katika umasikini

-Tunaamini kila mtoto anastahili fursa na tupo naye

-tuaamini seniorwanapaswa kustaafu kwa heshima, Hillary atatenda

-Tunaamini makampuni ya mafuta yajue sayansi inasema kweli, tupo naye

-Tunaamini ujira sawa kwa wanawake , Hillary atapigania hilo

-Tunaamini sharia sawa, na mabenki yakivunja sharia yatupiie mbali

-Tunaamini kusiwepo na bad deal

Anashukuru, na amemaliza
 
BERNIE SANDERS

-Anashangilia na ukumbi mzima bila kujali ni upande gani

-Ninayo heshima kuwepo hapa usiku huu kwa kufuata nyayo za Elizabeth Warren na kumshukuru Michelle Obama , ametufanya tujivunie

-Tuwashukuru waliojitolea katika kampeni

-Tuwashukuru watu milioni 2 waliochangia kampeni yetu

-Kila mtu anajua average contribution was 27

-Niwashukuru watu milioni 13 waliopiga kura kwa political revolution

-Waliotupatia wajumbe takribani elfu na ushee

-Wajumbe, ahsante kwa kuwa hapa na kazi mliofanya

-Nategemea kura zenu wakati wa roll call kesho usiku

-Shukrani maalumu kwa watu wa Vermont, walioniunga mkono kama mayor, congressman na Seneta pamoja na familia yangu

-Naeelewa watu wapo disaapointment na matokeo ya mwisho, na ni haki kusema hakuna aliyehuzunika kuliko mimi

-Jivunie mafanikio tuliyoyapa
 
SANDERS

-Kwa pamoja tumeanza Amerika Rev na Rev inaendelea

-Uchaguzi unakuja na kwenda, lakini jitihada za watu kutengeneza serikali ya watu na si 1% yenye social, equal and env mapambano hayo yanaendelea

-Ni wazi kwa kiasi niachoweza kuwa. Huu si uchaguzi si wa wagombea, si wa kampeni strategy, fund raising au things media imetumia muda kujadili

-Uchaguzi ni juu na lazima uwe juu ya watu wa Amerika na future tunayoitengeneza kwa watoto na vizazi

-Ni uchaguzi wa kumaliza miaka 40 ya umasikini, ni juu ya kuelewa kama hatubadili uchumi, vijana wetu wanaokuja watakuwa na maisha mabovu

-Ni uchaguzi wa usawa na kuondoa umangimeza

-Si kiroho, wala kimaadili kwamba top 10 % inamilizi Zaidi ya 90%
Au 10% imepata 85% ya income

-Ni uchaguzi wa kukumbuka tulikuwa wapi miaka 7.5 baada ya miaka 8 ya GOP kuharibu uchumi

-GOP wanataka tusahau kuwa kwa ulafi wa wall street uchumi ulikuwa mbovu kuliko wakati mwingine

-Watu watu milioni walipoteza kazi kwa mwezi na uchumi ulikuwa una collapse, ninawashukuru kwa uongozi wa Obama kutuondoa hapo

-Tumefanya maendeleo lakini Zaidi tunahitaji mabadiliko. Ni uchaguzi unataka mtu anayejua mambo, siyo hofu, name calling, tunahitaji uongozi utakaosaidia kuondoa umasikini, kuleta watu pamoja na kutufanya wamoja na si kutukana Latino na Mexcion, muslims, Amerika Afrika, na Sikh kutugawa

-Based on her idea, busara zinasema Hillary Clinton atakuwa Rais wa US

Watua wanshangilia*********

-Chaguo kuhusu single mom aliyeniambia Nevada, anaogopa future ya binti wake. Ni uchaguzi juu ya watu kutoishi katika umasikini

-Mama huyo anatambua lazima tuongeze minimu wage

-
 
SANDERS

-Trump hana wazo la kuongeza pesa

-Trump anaamini huuge tax break kwa milionea

-Uchaguzi ni juu ya kuwajali raia wa US

-Mamilionea wanataka kutumia mamilioni kunua uchaguzi. Hillary ata nominate judge anayejali watu.

Supreme court italinda wanawake kuchagua uzazi, LBGT, Immigrants na Env

-Fikiria Trump ata elect supr justice wa aina gani

-Trump ataacha watoto wakishindwa kwend vyuo na kubakia na madeni

-Mimi na Clinton tumekubaliana ku revolutionalize mambo

-83% watakwenda Univ, tukipunguza deni kwa watoto

-Uchaguzi ni juu ya climate change na kuifanya dunia iwe mahali pa kuishi

-Hilary anasikiliza wanasayansi kuzuia tabia nchi kama kuongezeka kwa bahari

-Trump amekataa syansi, anaamini climate change ni hoax

-Hillary anajua kazi ya Rais ni kuhofia next generation

-Kampeni ni kwenda kwenye universal health care

-Clintion anaamini katika universal health care

-Anataka kuona watu wana access kwa huduma za afya

-Trump position katika health care ni same old GOP policy
 
SANDERS

-US inalipa high price ya dawa, Clinton anajua medicare inapaswa kuchukua hatua za kuhakikisha hali inarekbishwa

-Immigration, kuhakikisha comprehensive reform

-Hllary anajua hilo, na uchaguzi ni kuwaleta watu na si kuwatenga

-Trump anatukana kundi moja hadi jingine, Clinton anafahamu tunakuwa na nguvu tukiwa wamoja

-Tunakuwa wamoja, wanaume na wanawake tunapokuwa pamoja

- Kutokubaliana na Hillary ndiyo maana ya demokrasia

-Katika convention tumekuja pamoja kuliko yaliyotugawa
 
SANDERS

-Kazi yetu nikuhakikisha platform inatekelezwa na controlled senate Congress na nitafanya kila linalowezekana kuhakikisha hilo linatokea

-Hillary amepigania healthcare na nime serve naye katika senate na najua anvyopigania haki za watoto na wanawake

Hillary atakuwa Rais mzuri, ahsanteni sana nyote

Amemaliza
 
NI HII 'DEMOKRASIA' YA DEMOCRAT YA MAREKANI TUHIMIZWAYO KUIFUATA?
;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;
Bernie Sanders' campaign manager says Democrats should stop calling for Hillary Clinton to be jailed. The Vermont senator's supporters have gone ballistic over leaked DNC emails which show an anti-Sanders bias and pro-Clinton collusion among officials. (RT)
------------------------------
Among the emails included in the release by hackers Friday were plots by DNC staffers to plant questions about Sanders' Jewish faith ahead of the Kentucky and West Virginia primary contests.(CNN).
-----
Rep. Adam Schiff, who is the top Democrat on the House intelligence committee, went much further, claiming that Trump was Russia's preferred candidate because of his warm words about Putin and the doubts he has cast on the utility of NATO.
"I wouldn't put anything past the Kremlin," Schiff said, calling Trump "a dream candidate for Moscow" and describing the Russians as "very afraid of Hillary Clinton."
"The Russians have the motive, they have the means certainly," Schiff told CNN's Wolf Blitzer, adding that they had interfered in the political affairs and elections of other countries(CNN)
-------------------------------------------
Debbie Wasserman Schultz's move follows a leak of emails appearing to suggest that party insiders tried to thwart the campaign by Hillary Clinton's rival. Bernie Sanders had pressed for Ms Wasserman Schultz to quit on the eve of the convention.(BBC)
-----------------------------------

Sources :
Stop calling to 'lock up' Clinton, Sanders campaign manager tells Bernie's supporters
US election: Email row claims Debbie Wasserman Schultz - BBC News
WikiLeaks - Search the DNC email database
Sanders: 'Awful' DNC emails should cost party chair her job - CNNPolitics.com
Vladimir Putin: Who wins if he meddles in 2016 race? - CNNPolitics.com
===================================================
MY TAKE

Kwanza nakushukuru sana Mkuu Nguruvi3 na wachangiaji wengine kwa kuendelea kuimarisha jukwaa hili kwa juhudi na maarifa. Pili nakushukuru (Nguruvi3) sana kwa kusaidia kwa kiasi kikubwa kuumulika uchaguzi wa Marekani. Kupitia hapa tumeweza kugundua uendeshaji wa uchaguzi wa kidemokrasia ambao tumekuwa tukishauriwa kuufuata hasa katika vyama vyetu vya siasa hapa nchini na hata katika uendeshaji wa serikali. Kwa kila hatua kuanzia kampeni mpaka sasa kwenye kutangaza wagombea wa vyama nilikuwa na furahia kuona namna demokrasia safi inavyofanya kazi hapo Marekani.

Lakini kugundulika kwa upendeleo katika kupata mgombea wa 'democrat', chama kinachojinasibu kwa demokrasia iliyotukuka na kupitia serikali kinayoongoza kinahimiza nchi nyingine za ulimwengu kuifuata, kimenihuzunisha kweli.
Tujifunze wapi sasa demokrasia ya kweli? Sielewi viongozi wetu wa kisiasa walioalikwa kwenye mikutano ya vyama hivyo kama watadhubutu kutueleza ukweli juu ya hili la 'unafiki' wa demokrasia ya kimarekani? Ukweli hili ni doa kwa wahubiri wa demokrasia ya kimarekani.

Jambo la kushangaza pia ni namna wamarekani (CNN) wanavyojaribu kugeuza mapungufu ya demokrasia yao kwa kuihusisha Kremlin. Wameshindwa kuwalaani na hata kushauri wafukuzwe kwenye chama hao walioshiriki kubadilisha matakwa ya wamarekani wengi kwa sababu wanazozijua wao. Pia hata FBI imejikita kutafuta wale waliowezesha kutoa mapungufu haya ya demokrasia badala ya kuwashughulikia wakandamiza demokrasia. Ni ajabu sana hii, kwa nchi (Marekani) tunayohubiriwa inajali haki, utawala bora, na mengine kama hayo katika uendeshaji wake. Wahusika wa kuhujumu matakwa ya wamarekani wanatakiwa kuadhibiwa zaidi ili kuhalalisha ubora wa demokrasia ya Marekani inayoenezwa ulimwengu.

Kama ndiyo hivi hiyo tume yao ya uchaguzi itakwaje, haki itatendeka?

Ya kwangu ni hayo. Tuendelee kueleweshana juu ya Uchaguzi huu wa wamarekani hadi November,2016 na baada ya hapo.
 
NI HII 'DEMOKRASIA' YA DEMOCRAT YA MAREKANI TUHIMIZWAYO KUIFUATA?
MY TAKE

Kwanza nakushukuru sana Mkuu Nguruvi3 na wachangiaji wengine kwa kuendelea kuimarisha jukwaa hili kwa juhudi na maarifa. Pili nakushukuru (Nguruvi3) sana kwa kusaidia kwa kiasi kikubwa kuumulika uchaguzi wa Marekani. Kupitia hapa tumeweza kugundua uendeshaji wa uchaguzi wa kidemokrasia ambao tumekuwa tukishauriwa kuufuata hasa katika vyama vyetu vya siasa hapa nchini na hata katika uendeshaji wa serikali. Kwa kila hatua kuanzia kampeni mpaka sasa kwenye kutangaza wagombea wa vyama nilikuwa na furahia kuona namna demokrasia safi inavyofanya kazi hapo Marekani.

Lakini kugundulika kwa upendeleo katika kupata mgombea wa 'democrat', chama kinachojinasibu kwa demokrasia iliyotukuka na kupitia serikali kinayoongoza kinahimiza nchi nyingine za ulimwengu kuifuata, kimenihuzunisha kweli.
Tujifunze wapi sasa demokrasia ya kweli? Sielewi viongozi wetu wa kisiasa walioalikwa kwenye mikutano ya vyama hivyo kama watadhubutu kutueleza ukweli juu ya hili la 'unafiki' wa demokrasia ya kimarekani? Ukweli hili ni doa kwa wahubiri wa demokrasia ya kimarekani.

Jambo la kushangaza pia ni namna wamarekani (CNN) wanavyojaribu kugeuza mapungufu ya demokrasia yao kwa kuihusisha Kremlin. Wameshindwa kuwalaani na hata kushauri wafukuzwe kwenye chama hao walioshiriki kubadilisha matakwa ya wamarekani wengi kwa sababu wanazozijua wao. Pia hata FBI imejikita kutafuta wale waliowezesha kutoa mapungufu haya ya demokrasia badala ya kuwashughulikia wakandamiza demokrasia. Ni ajabu sana hii, kwa nchi (Marekani) tunayohubiriwa inajali haki, utawala bora, na mengine kama hayo katika uendeshaji wake. Wahusika wa kuhujumu matakwa ya wamarekani wanatakiwa kuadhibiwa zaidi ili kuhalalisha ubora wa demokrasia ya Marekani inayoenezwa ulimwengu.

Kama ndiyo hivi hiyo tume yao ya uchaguzi itakwaje, haki itatendeka?

Ya kwangu ni hayo. Tuendelee kueleweshana juu ya Uchaguzi huu wa wamarekani hadi November,2016 na baada ya hapo.
Mkuu ahsante kwa mchango wako. Kuna hoja ningependa kuchangia katika mabandiko mawili yajayo

1. Ni ukweli usiopinga hakuna demokrasia 100% duniani.
Ukamilifu wa Demokrasia ni kwa viwango

Demokrasia haina ufanano. Ni makubaliano ya jamii katika kupanga, kuamua na kuendesha waliyokubaliana. Utimilifu wa demokrasia ni pale makubaliano yanapotekelezwa hata kama si kwa kiwango chote, lakini katika kiwango kinachokubalika

Ni sawa na mtihani,kuna 'bench mark' kwamba aliyefaulu anatakiwa kiwango fulani.

Sasa kama ni 70 , 80 au 90, wote watakuwa wamekidhi haja.

Tofauti na wenzetu, mauza uza yalitokea nchini na hasa Zanzibar yanatutofautisha nao

Uchaguzi wetu ni kwa utaratibu wetu na viwango vyetu.
Hakuna anayepaswa kutuingilia midhali tumekubaliana.

Wanatuingilia pale ambapo hatukubali tulichokubaliana.
Kufutwa kwa uchaguzi Zanzibar ni mfano mzuri.

Wazanzibar walikubaliana kupitia katiba matokeo yabandikwe, na yalibandikwa.
Wakakubaliana mwenye matatizo ayafikishe tume, hakuna aliyefikisha.

ZEC bila sababu ikafuta matokeo bila msingi wa kisheria unaonyesha mamlaka hayo

Kilichofanyika ni kutangaza uchaguzi mwingine ambao kikatiba hauonyeshwi unless awepo anayeweza kutueleza wapi uchaguzi wa marudio wa jumla umetajwa katika sheria gani.

Katika msingi huo, sisi hatukufikia hata ile bench mark tunayosema wenyewe

Hoja kuhusu sisi si kufuata demokrasia yao, bali kutoheshimu makubaliano yetu wenyewe

Wenye nguvu wanatumia kusimamia makubaliano kinyume na makubaliano husika

Demokrasia ni pana,watu wakipinga kwa hoja. Watu wakipewa fursa ya kujieleza na kueleza duku duku zao. vyama vyote vinapopewa fursa sawa.

Ni pana,matokeo yanatangazwa katika kituo na si 'uhariri' kutoka ''central office''

Demokrasia yao haina msimu, watu wanaruhusiwa kufanya siasa kila siku bila kuwaingilia

Ni Demokrasia pana watu wanapokubaliana kutokukubaliana kwa njia za hiari

Demokrasia ni pana pale vyombo vya umma vinapotumika kwa umma na si kundi la watu

Kwa kiwango chochote, wanaweza kutopata 100% lakini wapo kati ya 80 na 100.
Sisi tupo wapi? Tunawezaje kujilinganisha nao?

Hoja ya pili inafuata
 
Back
Top Bottom