Mag3
Platinum Member
- May 31, 2008
- 13,063
- 22,755
Ni kweli DNC imeanza kwa vituko. Pamoja na kuachia ngazi kwa aliyekuwa mwenyekiti, Debbie Wasserman Schultz, mambo bado si shwari ndani ya DNC na leo kaonja joto la jiwe kwa wanaoaminiwa ni wafuasi wa Bernie Sanders. Hao wafuasi ambao wanaonekana kutokubali tamko la Sanders la kumuunga mkono Clinton, wameshikilia kwamba kama matakwa yao hayatimizwi hawako tayari kubadili msimamo wao. Kwenye Breakfast Club wamemzomea Debbie hadi ikabidi akatishe hotuba yake.KUJUIZULU KWA Ms.WASSERMAN
Democrats wamefanya damage control mapema kwa kumshinikiza Ms Wasserman ajiuzulu. Licha ya kujiuzulu,ameonekana ukumbini akiendelea na maandalizi ya mwisho
Habari hii haimgusi Bi Clinton moja kwa moja kama mhusika.
Inamgusa kupitia maandalizi ya mkutano,kampeni na distractions zinazoambata nalo
Bado details za nini kimetokea zinasubiriwa, lakini ni mpango mahususi kuamkia siku muhimu kwa Democrats
Nani anahusika, linabaki swali, tunaona siasa zikiwa na timing! 'mchezo mezani'
Madhara kama tulivyoeleza bandiko la hapo juu yapo katika maeneo haya
1. Kupoteza Focus: Habari iliyotanda imefunika mkutano mkuu kwa siku nzima.
Na haineokani kama itapotea siku za karibu.
Hii inaweza kuwa kibwagizo na pengine kati kati ya mkutano yakatokea makubwa
Kesho anaongea Michelle Obama na Benie Sanders miongoni mwa wengi.
Ilitarajiwa wa set tome ya mkutano, kinyume chake emails zimechukua nafasi.
Hili ni pigo kubwa kwa kampeni ya Clinton
2. Trump apata silaha: Kama anavyomwita crooked Clinton na sasa hili linahusu Democrats, Trump atasema Sanders hakutendewa wema a system ipo rigged.
Hili atalifanya kila siku na athari zake ni kama namba 1 hapo juu
Lengo ni kuwavuta wafuasi wa Sanders ambao bado wana uchungu na chaguzi
3. Vidonda kuvuja damu: Sanders amesha mui endorse Clinton,tofauti na Cruz aliyesababisha timbwili bila endorsement.
Hata hivyo Sanders alisema Bi Wasserman anampendelea Clinton katika hatua za awali
Hoja ya Sanders ililenga kumshinikiza Wasserman akubali wazo la kuwa na chaguzi kwa taratibu anazotaka. Kwamba, kwenye closed elections, zifanywe open.
Hii ni kwasababu aliamini kushinda katika open na si closed. wasserman alikataa
Hoja ya pili,'super delegates' wasihesabiwe kabla ya mkutano mkuu,nalo lilikataliwa
Hoja ya wasserman ilikuwa kuwa, kubadili kanuni mchezo ukiendelea halikuwa jambo la haki. Kwamba, Sanders alifahamu taratibu, akazikubali na ku sign
Sasa, hili la emails Sanders anasema. 'alishasema hatendewi haki'
Na kwavile zime leak, hakuna atakayejali ni haki gani hakutendewa bali kuona hakutendewa haki tu.
Wafuasi wake wenye machungu wataamka kwa hasira na litawagawa democrats.
Trump atakapoisukuma hoja hiyo, hasira na vidonda vilivyoanza kupona vitaibuka upya.
Nini kitatokea Sanders atakapoongea kesho haijulikani.
Je, atamwaga mboga kama Cruz? Atafanikiwa kushawishi wafuasi wapuuze suala hili?
Ikizingatiwa wafuasi wa Sanders walikuwa waandamane kudai sera ya dollar 15 kwa saa kama kima cha chini, huenda kesho kukawa na maandamano zaidi
Katika fukuto hilo democrats wapo katika mtafaruku pengine mkubwa kuliko wa Trump. Tusubiri nini kitatokea
Tutawaletea habari za mkutano in 'real time' mambo yakienda kama tunavyotaraji
Tusemezane