Nguruvi3,
Naona umepanic ghafla nakukumbusha tu weka maneno ya akiba maandiko yako dhidi ya Zitto siyo msahafu.
Ni ushauri mzuri sana maana kama ilivyo leo kwa Lowassa yawezekana kesho na keshokutwa ikawa kwa Zitto, akiba ya maneno kwenye siasa hizi za kitanzania zisizosimama kwenye misingi ni muhimu sana.
Mpaka sasa it is clear kwamba Lowassa anaiendesha Chadema kwa remote control. Hatujui alianza lini kuiendesha kwa remote. Sasa hivi ndio tunaona hadharani lakini inawezekena alishaanza miaka mingi tu.
Katika sakata hili anayesikitisha zaidi ni Dr. Slaa. Yeye ndio anakatwa ili aingizwe Lowassa. Yaani Slaa atalazimika kukiri mbele ya umma wa watanzania kuwa Lowassa anafaa zaidi kuongoza nchi kuliko yeye. Hii ni karma inayompata Slaa.
Katika uchaguzi kila mgombea ana nafasi fulani ya kushinda. Iwapo watanshinda, basi watapata fursa ya kujipaka rangi mbalimbali za kupendeza na kuonekana mashujaa, ila ikitokea wakashindwa basi Chadema itakuwa na wakati mgumu unaotokana na interna power struggle. Hii ni kwa sababu watu anaokuja nao Lowassa wako makundi mawili , kundi la kwanza ni matajiri wanaotaka uhakika wa deal zao na kundi la pili ni wanasiasa opportunists wanaotaka vyeo. Wakipata serikali kutakuwa na vyeo vingi vya kugawana. Iwapo watashindwa uchaguzi itabidi wagawane vyeo vya ndani ya chama tu. Hapo ndipo itakuwa kimbembe. Matokeo ya kimbembe hicho sio lazima yawe mabaya, lakini ni mtikisiko unaoweza kurudisha nyuma sana upinzani nchini.
Umegusia mambo muhimu sana, kama kuna watu wanadhani wataweza kumcontrol Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania(kwa katiba iliyopo) tena Rais mwenyewe ni Edward Ngoyai Lowassa basi watakuwa wanajidanganya sana,kinyume chake wabunge wengi wa Chadema watajenga ufuasi kwa Lowassa binafsi(Lowassa ana historia nzuri sana kwenye hili, iwe kwa vyeo au kwa favour zingine) na pia ataweza kushirikiana na wabunge wa vyama vyote ikiwepo CCM(anajua vizuri kuishi nao), hatimaye mwishowe badala ya Chadema kumsimamia ni Lowassa ndiye atakayeisimamia Chadema na kuipeleka atakavyo, tuna mifano mingi Afrika juu ya siasa za chama na urais, na wakati wote Urais uwa unashinda, Bingu wa Mutharika na Joyce Banda wa Malawi ni mifano mzuri.
Otherwise nampongeza sana Dr Slaa kwa kukubalia kuachia nafasi ya urais bila shida, sio watu wengi wanaweza kufanya hili kwenye siasa za Afrika, japo legacy yake juu ya ufisadi itaathiriwa sasa kwa kuanza kumpigia kampeni aliyemuita fisadi awe Rais lakini kwenye suala la kutokuwa na "uchu wa madaraka" atajijengea heshima kubwa.Hili litakumbukwa ata miaka mingi ijayo na kwa kweli anastahili pongezi.