Duru za siasa: Chama cha ACT-Wazalendo Mpini wa CCM kumaliza upinzani(?)

Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
13,752
2,000
Dr Kitila Mkumbo anakula ‘matapishi yake’
ACT kuvuruga juhudi za katiba ya Wananchi
CCM yapumua, ujio wa ACTkupunguza nguvu za upinzani

Wanajamvi,
Siku za karibuni chama kipya cha ACT(Alliance for Change and Transparency) kimepata usajili wa kudumu. ACT inaungana na mlolongo wa vyama vya upinzani vingine vikiwa vya ‘briefcase’

Katika mfululizo wa mabandiko yajayo, tutaangalia chimbuko, mikakati na athari za ACT katika siasa za nchi yetu. Tutakuwa na sehemu V ili kueleza kwa undani hayo tuliyoyasema.

Sehemu I
ACT kinaundwa na kundi la wanachama wa Chadema ‘waliofukuzwa’ kutokana na kile kilichojulikana kama Waraka wa siri. Fuatilia uzi huu. https://www.jamiiforums.com/great-t...pecial-mgogoro-kambi-ya-upinzani-chadema.html

ACT inaundwa na watu wasiojulikana kisiasa, hakuna siri tena, ACT ina mikono ya wanachama wa CDM waliofukuzwa. Ushahidi wa hilo unapatikana kwa kauli ya Dr Kitila Mkumbo akijitambulisha kama mwanachama wake.

Yaliyojiri A
Mtakumbuka Kitila alianza harakati kwa makala gazetini akitaka uwepo wa chama mbadala cha kisiasa nje ya CCM na Chadema. Makala zililenga kuundaa umma hasa wanachama wa Chadema kupokea ujio wa ACT. Kuandika makala za matukio mbali mbali ni sehemu ya uandishi wa Kitila, kwa hili tunasema ni makusudi na wala si makala za kuhabarisha kama ilivyoonekana.

Yaliyojiri B
Wiki iliyopita ACT kimepata usajili wa kudumu. Wiki moja baadaye Kitila akasikika katika vyombo vya habari akijitambulisha rasmi kama mwanachama, na kwenda mbali kwa kusema anamshawishi Zitto Kabwe ajiunge na agombee uenyekiti.

Yaliyojiri C
Katika bunge la katiba mh Zitto alizungumzia suala la muungano.
Huko nyuma aliwahi kuzungumzia serikali 3 katika makala ambayo kumbu kumbu zetu inayo.
Kinyume na msimamo wa awali Zitto alisimama kati na kati bila kuweka msimamo wake wa wazi kuhusu suala hilo.

Yaliyojiri D
Ukawa walitoka bungeni na Zitto akiwa mmoja wapo. Katika mikutano yao kule Zanzibar mh Zitto hakuhudhuria na wala hajasikika akizungumza popote pale.

Yaliyojiri F
Baada ya usajili wa kudumu ACT kupitia mwenyekiti wake wameeleza uwepo wa jopo la wataalamu watakaoandaa katiba ya ACT. Kwa maana hiyo uongozi uliopo ni wa mpito na huenda kukakawa na uchaguzi wa mpito pia

Huu ni mtiririko kwa ufupi kuhusu chanzo na ujio wa ACT chama kinachopigiwa upatu wa kuendeshwa kitaalamu.

Hebu tuangalie sehemu ya pili tukipitia hoja za hapo juu na kuzifafanua,
Inaendelea..........
 

Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
13,752
2,000
Sehemu ya II

Hakuna kosa lolote la raia kujiunga na kikundi cha kisiasa halali na wala hakuna kosa lolote la watu kuwa na mikakati ya kisiasa, ndivyo inavyofanyika duniani.

Ujio wa ACT una maswali mengi ya kujiuliza na kama kweli lengo lake ni sahihi au uundwaji wake ni kwasababu za msingi.

Dr Kitila na waraka wake walisema Zitto Kabwe hakuhusika na uandishi wa waraka.
Katika mahojiano ya wiki hii Kitila amekiri kuwa na ‘mitazamo sawa ya kisiasa ' na Zitto.
Kwa hili tu kuna sababu za kuamini Zitto alishiriki katika uandikaji wa waraka uliowaletea matatizo

Kitila katika waraka alidai kutokuwepo kwa demokrasia ndani ya Chadema ikiwa ni pamoja na ukanda.Alinanga viongozi wa Chadema kama wenye akili ndogo.
Katika mahojiano ya wiki iliyopita Kitila kasema atamshawishi Zitto ajiunge na ACT na agombee uenyekiti.

Kitendo hicho ni cha kula ‘matapishi yake'.
Kitila alikuwa na haki ya kumwambia Zitto ajiunge na ACT kama mwanachama.

Kitendo cha kumtaka awe mwenyekiti ni kwenda kinyume cha demokrasia.
Mwenyekiti anaomba na kuchaguliwa, alichokifanya Kitila ni kutumia influence yake kuwashawishi wanachama kuwa Zitto anafaa kuwa mwenyekiti hata kabla hajasoma wala kujua sera za chama

Je, kuna tofauti gani na kile alichokuwa anakilaani akiwa Chadema?
Je huku si kumeza matapishi yake.

KUHUSU ZITTO NA KAULI ZA KITILA
Zitto alikimbilia mahakamani ili kudai haki yake anayoona amedhulumiwa na Chadema.
Ukweli ni kuwa alichokitaka ni kuwa mjumbe wa bunge la katiba.

Alifahamu kama uchaguzi ungerudiwa Kigoma angeshinda kwa kishindo.
Wasi wasi wake ulikuwa muda ambao usingemruhusu ajiunge na bunge la katiba.

Uwepo wa ZZK mahakamani si kwa ajili ya demokrasia, bali masilahi yake na washirika wake kama inavyoanza kudhihiri sasa hivi.

Ikumbukwe katika waraka, Kitila alimtaja ZZK kama mhusika mkuu ambaye alikuwa anaandliwa kuwa mwenyekiti kama ambavyo anamwandaa sasa kuwa mwenyekiti wa ACT

Hili la kumtaka awe mwenyekiti hata kabla ya katiba kuetengenezwa au ZZK kujua malengo ya chama linasema ukweli kuwa ile nia ya waraka ilikuwa kumweka ZZK katika ueneyekiti wa Chadema kwa hali yoyote kama ambavyo Kitila sasa anajribu kufanya.

KWANINI TUNASEMA ZZK ANA MASILAHI BINAFSI NA AKINA KITILA

Katika ‘yaliyojiri A' hapo juu, lengo la Kitila lilikuwa kuwaambia wanachama wa Chadema wenye uaminifu na ZZK kuwa kuna chama kipya ambacho kinaazishwa na wana waraka akiwemo ZZK.

Haiwezekani Kitila aliyeandika nyaraka na kusimamia mambo mengi ya Chadema aamke usiku mmoja na kuyakana aliyoyasimamia na kuyaandika eti kwa kutaka chama mbadala zaidi ya CCM na Chadema.

Hii maana yake ni kuwa Kitila aliweza kuamka siku moja na kugundua kuwa kile alichokuwa anasimamia ni upotofu na sasa kuna mbadala mwingine mbioni ambao ni ACT.

Hapa kuna kukosa uaminifu wa kisiasa, ingawa hakuna mwanasiasa mwaminifu.
Yatosha kusema, je akili ndogo aliyoikimbia Chadema amefanikiwa kuifanya iwe kubwa, au ameIkuza kwa ukubwa wake?


Inaendelea..

‘yaliyojiri B' ufafanuzi
 

Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
13,752
2,000
Sehemu III


Yaliyojiri B hapo juu.
Kitila ambaye ni mtu mwenye ushawishi ndani ya ACT amekwenda mbali na kusema Zitto agombee uenyekiti. Hili lina maana moja kubwa.

Kwamba, ZZK ana kesi mahakamani. Na kwa vile bunge la katiba halionekani kuwa na mwendo mzuri, ZZK anatakiwa ajitokeze ACT kwa shughuli za chama chao.
Njia nyepesi ya kufanya hivyo ni Kitila kuandaa wanachama kuhusu ujio wa ZZK.

Kitakachotokea ni ZZK kulazimisha kushindwa kesi mahakamani ili aonekane hana mahali pa kwenda bali kufuata ushauri wa rafiki yake kujiunga na ACT.

Hivyo kauli ya Kitila ililenga kumtengenezea ZZK mazingira mazuri ya kuondoka Chadema kama ‘victim of circumstance' yaani mhanga wa mazingira ambayo ni ‘uonevu wa Chadema'

Yaliyojiri C

Zitto hakuweka msimamo wake kwa kuhofia kwenda kinyume na msimamo wa chama chake kipya cha ACT. Ndiyo maana katika bunge la katiba alizungumza kati na kati ili maneno yake yasije mrudi siku sera za chama chake zitakapokuwa wazi,sera asizozijua lakini anataka uenyekiti azitetee

Lakini basi, kama ana ugomvi na viongozi wa Chadema, ZZK hakupaswa kuuendeleza nje na kufikia hata kususia mikutano ya UKAWA.

Hii ina maana moja kubwa kuwa siasa za ZZK ni za visasi na inaondoa maana nzima ya yeye kusimama na umma. Je, huu si usaliti wa umma ule ule anaosema anasimamia?
Vipi atoke nje ya UKAWA ikiwa haamini mikakati yake kwasababu tu haelewani na baadhi ya viongozi?

Yaliyojiri F
Endapo ZZK alikerwa na umangi meza ndani ya Chadema, iweje asikanushe kutajwa kwake kuwa mwenyekiti wa ACT hata kabla ya katiba na sera za chama au uongozi wa muda haujasimikwa?
Je, huu si unafiki wa kusema jambo moja vibaya na kulitenda kwa namna nyingine ‘vizuri" ?

Kuna sababu za kuamini kuwa ujio wa ACT utakuwa na madhara makubwa katika siasa za nchi hii.
Ukisoma mtiririko wa matukio hapo juu, utaona Kitila na wenzake wamedhamiria kuua upinzani badala ya kukabiliana na CCM

Mbinu zote za makala na mahojiano zimelenga ''kuhujumu'' narudia '' '' kwa maana ya kuwa Kitila alikuwa anatengeneza mazingira ya kuwasiliana na wanchama wa Chadema ili waondoke na ZZK.

Tayari mazingira ya kuondoka kwa ZZK yameshawekwa sawa na sasa ni wanachama na hata kundi kubwa la viongozi.

Katika siasa hilo halina tatizo ni mkakati wa kisiasa. Kwa mazingiara ya nchi yetu mkakati huo si wa maendeleo bali kurudi nyuma kihatua ingawa rangi zinaonekana kung'aa.

KWANINI NI KURUDI NYUMA

Wanachokifanya akina Kitila ni sawa na kuiba wanachama wa Chadema.
Tunarudia kusema huo ni mkakati wa kisiasa.

CDM ni chama kichanga kisiasa kwa maana hakijawahi kuwa na madaraka ya umma wala kuwa na uwakilishi unaoweza kutishia status quo ya CCM.
Kitila hata afanikiwe katika mbinu zake bado atakuwa na matatizo ya kisiasa.

Inaendelea
 

Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
13,752
2,000
Sehemu ya IV

Matatizo ya kisiasa ya ACT yatakuwa kudumaa.
Watagawana wanchama na Chadema na hata idadi ya wabunge na huo ndio utakuwa mwisho.
Watarudi kweny matatizo yale yale waliyoyakimbia ambayo sasa wanayaona ni bora, kwa mfano kutaja mwenyekiti asiyejua sera za chama.
Kuweka mwenyekiti kwa urafiki, na kuendesha chama kwa hila za udanganyifu na si siasa za kisayansi. Kuna kundi litakalochanganyikiwa na vyama hivi na kujikuta ima likisusia siasa au kuamua kurudi CCM

Wasichokijua akina Kitila ni kuwa ugomvi wao ni faraja kwa CCM.
Na CCM itatumia mbinu za kuwachochea ili iendeleze mbinu zake za kutawala na hasa kutumia mwanya huo kuharibu mchakato wa katiba.

Akina Kitila kama chama cha wenye ‘akili' kubwa as opposed na akili ndogo za kule walikotoka na walikotengeneza walipaswa wawavute wanachama kwa sera zao na wala si mbinu za kuiba wafuasi.

Kuwavuta wanachama kwa sera kungesaidia kupata wanachama kutoka kona zote za kisiasa ‘across political spectrum' na hivyo kujenga utahbiti.

Mbinu wanzotumia akina Kitila ni hafifu, dhaifu na zinatia shaka zaidi ya matumaini.
Kama lengo la siasa ni kumfanya ZZK awe mwenyekiti basi nchi hii ina safari ndefu ya kisiasa.

Ni kwa mantiki hiyo, katika siku za usoni kutakuwa na kuhama kwa wanachama kutoka makundi mbali mbali kwenda upande mwingine, hujuma dhidi ya ACT na CDM na kutengeneza ombwe kubwa sana la upinzani nchini.

CCM INAPUMUA

Ugomvi unaofukuta kati ya ACT na Chadema utawapa nafuu sana CCM kwasababu huo ndio utakuwa muda wa kujijenga kisiasa, kusahaulisha maskando kama ya IPTL na kuendelea kuwagwa wapinzani.Hilo litafika hadi kwa UKAWA na huo ndio utakuwa mwisho wa UKAWA

Kwa jicho la haraka ACT hakionekani kuwa kama tishio kisiasa, tatizo lake kitakuwa chama ambacho kitawavuruga zaidi wapinzani na kitatoa nafuu sana kwa CCM.
Ujio wake ambao ni wa hasira za kisiasa hautaidhuru CCM, utadhuru upande wa upinzani.

Jitihada hizo zimeanza kuonekana kwa namna ambavyo ZZK na akina Mwigulu wanahusishwa vema sana katika kashfa zinazoendelea wakitajwa kama mashujaa wa taifa.

Hiyo ni mbinu ya kuondoa jicho kwa Chadema na kuanza kumzungumzia ZZK akipambwa kwa msaada wa CCM.Lengo ni kumaliza nguvu ya upinzani.

Nini kitatokea katika mambo ya kitaifa

Inaendelea sehemu ya V


 

Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
13,752
2,000
Sehemu ya V

KATIBA MPYA KUTOPATIKANA
ILIYOPO ITAFANYIWA MAREKEBISHO KUKIDHI HAJA ZA CUF
UKAWA WATAKUWA WAMEFIKIA TAMATI BILA JUISI YA MAEM
BE

Katika uzi huu
https://www.jamiiforums.com/great-t...ka-historia-ya-juisi-ya-maembe-kujirudia.html

Tumeeleza matukio ya nyuma yaliyopelekea ukawa kushindwa kisiasa na hatimaye kususia bunge la katiba baada ya kuona kila jambo linashindikana.

Ni kwa bahati mbaya UKAWA hawaonekani kutenda yale yalikusudiwa.
Duru ilisema kama wanataka kufanikiwa ni vema waanze mkakati mapema.

Inavyooenkana wamewasubiri CCM na sasa ni mtifuano hata pale walipokuwa na advantage ya kufikia umma mapema.

Na hata sasa inaonekana mkakati wao kisiasa ni hafifu na huenda ikiwa ndio mwanzo wa mwisho kama hawatabadili misimamo na mikakati. Mikakati yao lazima ilenge kukabiliana na CCM wenye pesa.Habari za kuvuja siri za vikao vyao inaonyesha udhaifu mkubwa licha ya ukweli kuwa mikakati yao ni dhaifu kwa kuanzia.

Ujio wa ACT utaleta mtafaruku na kusimamisha jitihada za kupata katiba mpya.
CCM inajua haiwezi kuandika katiba bila ya wapinzani.

Hata siku 60 zilizoongezwa na JK ailikuwa ni kukamilisha tu wajibu.
Jibu ni kuwa CCM wanataka mchakato ushindwe kwa kuelewa kuwa ndani ya bunge wameshaonekana kushindwa mbinu zao, kuanzia mabaraza ya kata, kutoa mlungula kwa tume, kuwadhalilisha akina Warioba na kulazimisha sheria na hata kzuipinda.

Wanachokitaka ni kuendelea na katiba iliyopo. Mpango wao ni kuifanyia marekeisho katiba ya 1977 ili kuwafaraji wazanzibar kwa madai yao, wakitoa nafasi ya makamu wa Rais, misaada na mikopo kwa kiwango zaidi, na kuruhusu znz kuwa na uanachama na mashirika na taasisi za kimataifa.

Kwa ufupi CCM watakubaliana na matakwa ya wazanzibar hata kama ni kwa gharama za wananchi wa Tanganyika.

Hilo litamaliza nguvu ya CUF yenye karata kubwa sana ndani ya bunge la JMT na bunge la katiba. Marekebisho hayo yataambatana na kufarakana kwa UKAWA kupitia mbinu za CCM.

Ni katika wakati huo ACT itakuwa kwenye mtifuano na Chadema huku CUF wakiwaacha pembeni.
Hilo linaashiria jambo moja, kifo cha UKAWA na kuandikwa kwa katiba ya CCM bila matatizo.

Yote haya yanatokea kwasababu ACT itakuwa inagawa wanachama zaidi.
Hakuna arbitration kwasababu Chadema itakuwa mguu sawa kukabiliana na ACT na ACT ikijizatiti kuiangaush Chadema na si CCM.

Mtifuano utahamia katika majimbo ya uchaguzi na kugawa kura si za CCM bali wapinzani.
CCM taendelea kutawala daima.

Je, ACT wameangalia mwenendo( Political landscape) wa kisiasa na kubaini hayo?
Je, ile nia ya kuwa na upinzani thabiti wenye akili kubwa itatimia?
Je, Kitila kula matapishi yake akisaidiana na ZZK kunatueleza nini kuhusiana na wanasiasa wa Tanzania.

Chama kipya cha ACT, Je ni shoka la kukata au mpini wa shoka kuelekea mwisho wa upinzani?

Tusemezane.
 

Skype

JF-Expert Member
Nov 5, 2010
7,278
1,195
Mkuu Nguruvi3 baada ya kusoma mabandiko yako yote matano nimejikuta nashawishika kuamini kuwa ACT ni vitangulizi vya CCM ktk kuhujumu upinzani thabiti na kusimika mizizi ya kinyonyaji ya hicho chama tawala.

Ukiangalia kwa makini utagundua kua Zito na Kitila wameanza mipango yao muda mrefu kupitia makala kama ulivyoeleza huku wakishadidiwa na chama tawala kwa mlango wa nyuma. Ikumbukwe Zito kwa sasa anaonekana shujaa kwa wanaCCM kwa kua tu ameweza kupambana na chama chake ambacho ameshakihama kiutendaji ila yupo kwa masilahi yake na ya marafiki zake kwa lengo la kukivuruga kabisa na kukiua ikiwezekana.

Ukirudi nyuma miezi kadhaa utakumbuka lile sakata la pm7 na kilichotokea baada yake. Hapo ndipo taswira halisi ya vitangulizi vya mnyonyaji CCM vilipojidhiri.

Kiujumla niseme tu kwamba ACT ni tawi la CCM lenye lengo moja tu la kuua upinzani baada ya mbinu za kuisogeza karibu CUF kushindikana. Kama wapinzani wa kweli wasipokua makini kwa kweli ACT ndo b52 kwao ikirushwa toka CCM.
 
Last edited by a moderator:

Skype

JF-Expert Member
Nov 5, 2010
7,278
1,195
nasikitika tu, basi tu naomba watu wazidi kuelimika, ujinga wa voters dhidi ya politician upungue ndipo demokrasia ya kweli itakapoanzia.
Ulichokisema kiende sambamba na urekebishwaji wa daftari la wapiga kura kila baada ya miaka angalau miwili.
 

zumbemkuu

JF-Expert Member
Sep 11, 2010
10,104
2,000
Ulichokisema kiende sambamba na urekebishwaji wa daftari la wapiga kura kila baada ya miaka angalau miwili.
hata likirekebishwa kila mwezi kuzingatia wanaofikisha umri wa kupiga kura kila mwezi, bila kufuta ujinga kwa voters na elimu ya uraia kwa voters ni kazi bure, politicians hawawezi kuelimisha voters kamwe...,
 

Skype

JF-Expert Member
Nov 5, 2010
7,278
1,195
hata likirekebishwa kila mwezi kuzingatia wanaofikisha umri wa kupiga kura kila mwezi, bila kufuta ujinga kwa voters na elimu ya uraia kwa voters ni kazi bure, politicians hawawezi kuelimisha voters kamwe...,
Mkuu nimekuelewa vizuri ila nadhani wewe hujanielewa labda kwa bahati mbaya. Nilimanisha kuwa elimu ya uraia kwa wapiga kura itolewe na wakati huohuo daftari la wapiga kura likirekebishwa.

Mbali na hapo kuna hoja nzuri umeipendekeza kuwa elimu ya uraia haiwezi kutolewa na wanasiasa, kweli hata mimi nakuunga mkono kwa hili maana wamezidi kuvaa ngozi ya kinyonga kila uchao, sasa tumebaki njia panda tunasubiri kusombwa na kimbunga kitakachotokea sijui nchi gani! Pamoja na hayo binafsi sijui na sijaona wa kutupa elimu ya uraia, kwa mantiki hiyo ndugu yangu naomba unisaidie maoni yako ktk hili, yani ni nani anaweza kutuokoa na janga hili la ujinga wa elimu ya uraia?

Kumradhi kwa mleta mada kwa kuchepuka kwenye maudhui lakini yote hii ni ktk kuelimishana.
 

zumbemkuu

JF-Expert Member
Sep 11, 2010
10,104
2,000
Mkuu nimekuelewa vizuri ila nadhani wewe hujanielewa labda kwa bahati mbaya. Nilimanisha kuwa elimu ya uraia kwa wapiga kura itolewe na wakati huohuo daftari la wapiga kura likirekebishwa.

Mbali na hapo kuna hoja nzuri umeipendekeza kuwa elimu ya uraia haiwezi kutolewa na wanasiasa, kweli hata mimi nakuunga mkono kwa hili maana wamezidi kuvaa ngozi ya kinyonga kila uchao, sasa tumebaki njia panda tunasubiri kusombwa na kimbunga kitakachotokea sijui nchi gani! Pamoja na hayo binafsi sijui na sijaona wa kutupa elimu ya uraia, kwa mantiki hiyo ndugu yangu naomba unisaidie maoni yako ktk hili, yani ni nani anaweza kutuokoa na janga hili la ujinga wa elimu ya uraia?
Kumradhi kwa mleta mada kwa kuchepuka kwenye maudhui lakini yote hii ni ktk kuelimishana.
mkuu Skype ni dhahiri kuwa wanasiasa wanacheza na akili za wapiga kura, mbaya zaidi wanajivika vivuli vya ujana kwa kujaribu kuwatumia vijana ambao kwa bahati mbaya wamepata elimu ndogo ya uraia japokuwa hawataki kujitambua, ukifuatilia uchambuzi makini wa mleta mada hapo juu, msomi kama dr.mkumbo anayepaswa kufundisha wanafunzi wake kujitambua yeye mwenyewe ama kwa bahati mbaya au kwa makusudi ameamua kujitoa ufahamu wa elimu iliyompa heshima kubwa na kuamua kuchagua kutumika badala ya kutumikia, amini tu kuwa siasa zina nguvu kubwa kuliko elimu iliyopo sasa, kama ingewezekana kuwahamisha wapiga kura wote wakae juu ya kilele cha mlima Kilimanjaro kisha waone namna wanasiasa wanavyocheza na akili zao huenda wangejitambua, wanaopaswa kutoa elimu ya uraia wameingia kwenye siasa na kuona utamu wa siasa, elimu ya uraia itatolewa na njaa kali na uonevu utakaompata mpiga kura na sivinginevyo,
 
Last edited by a moderator:

Skype

JF-Expert Member
Nov 5, 2010
7,278
1,195
zumbemkuu,
nimekusoma vizuri na majibu niliyoyapata ni kwamba anayepaswa kutupa elimu ya uraia ni taasisi za elimu ambazo nazo kwa bahati mbaya (nadhani) zimeamua kumezwa au kutekwa na siasa kama ulivyofafanua hapo juu.

Pia umesema kua kwa sasa mwalimu wetu pekee wa uraia aliyebaki ni madhila yatupatayo kutoka kwa watawala lakini napata shaka kwa nchi yetu na siamini kama huyu ndiye mwalimu sahihi. Kwa nini? Angalia majanga na mauaji yaliyowahi kutokea na yanayoendelea kutokea chini ya mkono wa chuma wa ccm, mfano kufukiwa wachimbaji wa madini kule Bulyankulu miaka ya 90 na Mererani hivi majuzi, ni nani aliyepata somo? Ukija mauaji ya Januari 27 mwaka 2000 kule Zanzibar, kuna yeyote aliyewajibishwa? Pia kuna mauaji ya Mwangosi kule Iringa, kama haitoshi ukaja mtindo wa kuwakamata na kuwasulubu wote walioonekana kuuamsha umma, anza na Saidi Kubenea kisha Absalom Kibanda akafuatiwa na Daktari Ulimboka kabla ya 'kutokea' kifo cha Sengondo Mvungi tukiwa bado tuna kumbukumbu ya Chacha Wangwe, Horace Kolimba, Imran Kombe na wengineo wengi bila kumsahau Moringe Sokoine. Je, matukio yote hayo hayatoshi kumwamsha raia achilia mbali PAYE, VAT, EPA, IPTL, RICHMOND na matakataka mengine?

Mimi nadhani bado hatujapata mwalimu mujarabu wa uraia tangu mwalimu wetu (ambaye ni taasisi za elimu) atutose na kutekwa na siasa. Kwa hayo madude hapo juu naamini tungeshakua tumepata elimu ya kutosha mpaka sasa.

Nikirejea kwenye mada, nadhani njia pekee iliyobaki kwa UKAWA ni kuweka nguvu zaidi ktk kuuendeleza na kuuimarisha muungano wao ili kuzitenza nguvu za ACT ktk kuvuruga upinzani kwa msaada wa mtawala.
 
Last edited by a moderator:

Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
13,752
2,000
mkuu Skype ni dhahiri kuwa wanasiasa wanacheza na akili za wapiga kura, mbaya zaidi wanajivika vivuli vya ujana kwa kujaribu kuwatumia vijana ambao kwa bahati mbaya wamepata elimu ndogo ya uraia japokuwa hawataki kujitambua, ukifuatilia uchambuzi makini wa mleta mada hapo juu, msomi kama dr.mkumbo anayepaswa kufundisha wanafunzi wake kujitambua yeye mwenyewe ama kwa bahati mbaya au kwa makusudi ameamua kujitoa ufahamu wa elimu iliyompa heshima kubwa na kuamua kuchagua kutumika badala ya kutumikia, amini tu kuwa siasa zina nguvu kubwa kuliko elimu iliyopo sasa, kama ingewezekana kuwahamisha wapiga kura wote wakae juu ya kilele cha mlima Kilimanjaro kisha waone namna wanasiasa wanavyocheza na akili zao huenda wangejitambua, wanaopaswa kutoa elimu ya uraia wameingia kwenye siasa na kuona utamu wa siasa, elimu ya uraia itatolewa na njaa kali na uonevu utakaompata mpiga kura na sivinginevyo,
Hapa umegusia kitu kimoja kuhusu Kitila. Hawa ndio walioaminisha umma kuwa demokrasia lazima ifanyike kwa kuchukua mkondo wake. Kwamba, chaguzi ndani ya vyama zifuate taratibu.

Kitila pamoja na mengine amekuwa akilaani mfumo wa NEC ya CCM huko nyuma kuwa kama genge la 'wahalifu' walio na nia ya kumaliza demokrasia nchini. Yeye na swahiba yake kwa maono ya kisiasa Zitto walionekana kutoridhika na kile wanchoikiita Ukanda au ukasakazini. In fact Zitto alishawahi kutoa kauli juu ya hilo kwa mfano wa EAC.

Leo wale wale wanaohubiri na kukemea uchafu, wanarudi kufundisha kile walichokemea jana.
Zitto anaweza kuwa mwanachama wa ACT na ni haki yake. Anaweza kugombea nafasi na ni haki yake.
Kitendo cha Kitila ambaye ndiye 'brain' ya ACT kumpigia debe hata katiba haijapatikana wala Zitto kujiunga ni kukiuka misingi ya demokrasia kwa kiasi kikubwa sana.

Sina uhakika baada ya mfumo wa CCM wa ufisadi, Wa CDM wa ukanda waliousema, akina kitila wanataka kuanzisha mfumo wao wa 'Uswahiba'. Kitila hana haki ya kuwachagulia ACT mwenyekiti! hiyo si demokrasi ni kile kile walichoaminisha umma hakipo sawa. Nani kampa Kitila nguvu za kumteua Zitto akiwa nje ya chama kuwa mwenyekiti?
 

Skype

JF-Expert Member
Nov 5, 2010
7,278
1,195
Mkuu Nguruvi3, maelezo yako hapo juu kuhusu Zitto, Kitila na madudu ya ccm na madudu ya chadema kwa mujibu wao hao maswahiba kisha mazuri ya act inaonyesha wazi hawa jamaa wanafagilia hili dude liitwalo "DOUBLE STANDARDS".
 
Last edited by a moderator:

Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
13,752
2,000
Mkuu Nguruvi3, maelezo yako hapo juu kuhusu Zitto, Kitila na madudu ya ccm na madudu ya chadema kwa mujibu wao hao maswahiba kisha mazuri ya act inaonyesha wazi hawa jamaa wanafagilia hili dude liitwalo "DOUBLE STANDARDS".
Ndiyo maana tunamuuliza Dr Kitila kama ameamua kumeza 'matapishi yake'

Huwezi kulaani mfumo wa kidikteta Chadema halafu ukatenda hayo hayo ACT nasi tukupe pass tu.
Kitila aliandaa nyaraka na taratibu nyingi za Chadema. Ghafla anaamka na kutueleza kunahitajika mbadala wa CCM na Chadema.

Ukweli ni kuwa alilenga Chadema, akimaanisha mbadala wa Chadema.
Sote tunajua tunahitaji mbadala wa CCM kutoka mahali popote penye watu wenye akili. Hivyo kauli yake ilikuwa kudanganya watu.

Hapa ndipo tunajiuliza, hivi siasa zile walizokataa iweje leo zionekane ni nzuri?
Kitila anawezaje kumtangaza ZZK agombee Uenyekiti hata kabla ya kuchukua kadi. Ni kitu gani hicho jamani.

Kwa kutambua yeye yupo behind ACT kauli yake haiwezi kuwa na uzito mwepesi.
Ni kwamba atafanya aliwezalo ili ZZK awe mwenyekiti akitokea 'Ughaibuni' asikojua sera za chama anachokabdhiwa na Kitila.

Kitila ameamua kuwachagulia ACT mwenyekiti hata kabla ya katiba au ZZK kujiunga.
Hichoni kituko tukizingatia waraka wao ulisema' lengo ni kuandaa mkakati wa ushindi'
Akiwa ACT hana mkakati bali kubambikizia watu mwenyekiti anayemtaka yeye kwasababu wana maono sawa ya kisiasa.
Huu mfumo wa uswahiba sijui umelenga nini hasa.

Ndio maana tunasema, wait a minute, kuna tatizo kubwa kuliko tatizo la utitiri wa vyama.
Siasa zetu si za sera ni za nani mwenyekiti! Kuna tatizo kubwa!
 

Mchambuzi

JF-Expert Member
Aug 24, 2007
4,826
2,000
Kama alivyojadili Nguruvi3, Dr. Kitila Mkumbo amewaacha wananchi na maswali mengi kuliko majibu. Haikutegemewa kwamba Kitila na kundi lake wangeenda kutenda yale yale ambayo walidai hayakutendea haki demokrasia ndani ya Chadema. Kwa maana nyingine na rahisi ni kwamba zile shutuma zote ambazo kina Kitila walipewa ndani ya chadema na kufanikiwa kuokota baadhi ya sympathizers, shutuma zile zimeanza kunenepa na ukweli, lakini sio kutokana na uongozi wa sasa wa chadema kuendelea kuonyesha umma kina Kitila walikosea wapi, bali kwa maneno na matendo ya kina Kitila wenyewe.

Moja ya matatizo makubwa yanayovikabili vyama vyetu vya siasa ni pamoja na vyama hivi kutoheshimuu demokrasia, sio tu nje ya chama bali hata ndani ya chama. Sasa iwapo sakata la kina Kitila lilichangiwa na wao kutoridhika na mwenendo wa demokrasia ndani ya chadema, kama alivyohoji Nguruvi3, nini wanachofanya kina Kitila sasa hivi ambacho tunaweza sema ni mbadala wa ccm na chadema linapokuja suala la demokrasia ndani ya vyama?

Nguruvi3 amejadili jinsi gani Dr. Kitila amekuwa akila matapishi yake. Binafsi ningependa kwenda mbali na kuchukua nukuu za Dr. Kitila kutoka kwenye makala zake za "Tunahitaji Mbadala wa CCM na Chadema". Nukuu hizi zitathibitisha jinsi gani hoja ya msingi ya nguruvi3 inasimama.

Katika makala zake juu ya "Tunahitaji Mbadala wa CCM na Chadema", Dr. Kitila anasema hivi:

["ITACHUKUA muda kuelewa nini hasa kilichokikumba Chama Kikuu cha Upinzani nchini (CHADEMA) hadi kikashindwa kutatua mgogoro wa uongozi na hatimaye kuingiza nchi katika kizungumkuti cha kisiasa tunachokishuhudia leo."]

Ni kweli ilituchukua muda lakini hatimaye tumeelewa nini kiliikumba chadema. Majibu yapo kwenye hoja ya msingi ya nguruvi3 hapo juu lakini pia kwenye uzi wake mwingine wa: duru za siasa - mgogoro kambi ya upinzani chadema, hivyo nisingependa kuyarudia.

Kitila anaendelea kusema kwamba:

["Walionipa lawama ni wale waliokubaliana mia kwa mia na viongozi wa CHADEMA waliotujengea taswira ya usaliti na uhaini kwa chama kwa uamuzi wetu wa kuandaa mkakati wa kushinda uchaguzi ndani ya CHADEMA; mkakati ambao ulikuja kutafsiriwa kama mkakati wa mapinduzi ya uongozi halali ndani ya chama."]

Ni kwa mantiki hii, nguruvi3 anahoji - je, uongozi ambao Dr. Kitila anataka usimika ACT utakuwa na uhalali gani?

Kitila anaendelea:

["Na kwa kuwa viongozi waliongea sana na kulirudia jambo hili mara kwa mara, na kwa kuwa jamii yetu imejengwa katika kuamini uongozi zaidi kuliko mtu mwingine yeyote, wapo watu wengi ambao wameafikiana na tafsiri ya uongozi kwamba waraka ule ulikuwa ni mkakati wa mapinduzi na haukuwa na nia njema."]

Hapa wanachama wa ACT watakuwa na haki ya kumhoji Kitila, je haoni kwamba tayari anamuamini Zitto kama kiongozi wa ACT kuliko mtu yoyote mwingine ndani ya chama hicho? Je Kitila haoni kwamba anachofanya ni kupindua kanuni, taratibu na itifaki za chama chake kipya cha ACT za kupata viongozi wa chama? Ipo wapi nia njema kwa ACT na wanachama wake katika hili?

Kitila anaendelea kujadili kama vile ACT offers a new platform ya kurekebisha mapungufu ya kidemokrasia ndani ya vyama vikuu vya siasa nchini pale anaposema:

["Nieleze tu kwamba mgogoro huu unatukumbusha kuwa, pamoja na kwamba tupo katika mfumo wa vyama vingi, bado tumeendelea kuukumbatia utamaduni wa chama kimoja. Kwa hiyo tuna vyama vingi vya siasa, lakini vyama hivi bado vinakumbatia utamaduni wa chama kimoja. Utamaduni wa chama kimoja ni utamaduni hodhi na wa kiimla"]

Hapa anakula matapishi yake mchana kweupe kwani kitendo cha kuamulia wanachama wa ACT viongozi wanaowafaa ni ujenzi wa utamaduni "hodhii na wa kiimla".

Kitila anazidi kula matapishi yake pale anaposisitiza kwamba:

["Uongozi katika utamaduni wa chama kimoja unapatikana kwa njia za uteule, ukiwahusisha watu wachache wateule. Utamaduni wa chama kimoja unakataa ushindani wa wazi. Katika utamaduni wa chama kimoja kutamani cheo fulani ndani ya chama na katika serikali ni ulafi na uroho wa madaraka. Ndio maana vyama vyetu vyote vikubwa hapa nchini vinakataza na kukemea wanachama wao kutamani na kutangaza nia ya kuwania madaraka makubwa kama vile urais au uenyeviti wa vyama"]

Hapa Dr. Kitila ametuacha hoi bin taaban kwani anayopingana ni ndiyo yale yale anayoyajenga ACT. Kwa mfano, Zitto ni mteule wa mtu mmoja ACT. Kitila hataki ushindani wa wazi ukipatie act mwenyekiti wake. Na kwa maana hii, mwanachama yoyote atakayajitokeza kupambana na zitto ACT atapingwa vikali na Kitila.

Kitila anaongeza kwamba:

["Makosa yaliyofanywa na uongozi na wanachama wa CHADEMA unafanana sana na makosa yaliyofanywa na viongozi na wanachama wa NCCR Mageuzi miaka ya tisini. Kama inavyotokea kwa CHADEMA leo, wanachama wa NCCR Mageuzi waligeuka kuwa mashabiki wa viongozi, kundi moja likimshabikia Mrema na kundi jingine likiwashabikia akina Marando. Kwa kudhani kwamba chama kilikuwa imara sana, kundi la akina Marando likaamua kumfukuza Mrema likiamini kwamba alikuwa hana madhara yoyote kwa sababu chama kilishaimarika mno, wakisahau kwamba msingi wa ufuasi ulijengwa kwa viongozi na sio kwa chama. Mrema alipotimka, akatimka na mashabiki wake. Hicho ndicho kinachoendelea ndani ya CHADEMA. Kuna watu wenye mtazamo finyu wanaamini kwamba chama hiki ni imara sana kwa sasa kiasi kwamba hata wakimfukuza Zitto kitaendelea kubaki imara. Wamesahau kwamba wamejenga ufuasi kwa viongozi, na hivyo watakapomfukuza Zitto atatimka na wafuasi wake na chama kitayumba."]

Hapa Kitila anatuchanganya kidogo. Je, yeye na wenzake waliamua kutumia uzoefu wa NCCR ya kina mrema kama njia ya kuiboma chadema? Au uzoefu wa NCCR uliwapa funzo yeye na wenzake kuzuia ya NCCR yasijirudie tena chadema kwa faida ya chama?

Na ni nani aliyejenga ufuasi kwa viongozi kuliko chama kama si Kitila kiasi cha kufikia hatua ya kutumia umaarufu wa chaguo lao "zitto" kukisambaratisha chama? Waraka wa Kitila and company ulijaa ushabiki wa personality moja dhidi ya nyingine, kuliko masuala ya sera, itikadi au chadema kama taasisi.

Kitila anashauri kwamba:

["Wangekuwa na mtazamo mpana wa kimantiki, na kama wangekuwa ni watu wa kujifunza, viongozi wa CHADEMA wangelimaliza sakata la Zitto ambalo sasa lipo mahakamani kwa njia ya usuluhishi kimya kimya kama walivyofanya NCCR kwa Kafulila."]

Hapa analeta hisia kwamba kafulila ni sehemu ya mpango wao kwani alichofanya kafulila NCCR hakikuwa tofauti sana na cha kina kitila "kimkakati".

Sakata la Zitto analojadili kwamba lilitakiwa limalizwe kimya kimya ni lipi hasa, lile la waraka? Wao waliandaa waraka ule kimya kimya na kimakosa, na dawa yake kwa manufaa ya chama haiuhitaji ukimya kwani waraka ule ulikuwa ni sumu iliyohatarisha uhai wa chama.

Pamoja na hayo, mara ngapi uongozi wa chadema ulimvumilia ZZK na kujaribu kumaliza migogoro ya zzk kimya kimya? Zipo rekodi kwamba wajumbe wa baraza kuu, sio mara moja katika vikao walitaka ZZK ashughulikiwe huku yeye (zzk) akiwa meza kuu akilindwa na Mwenyekiti.

Kitila anasema:

["Lakini kwa sababu ya upofu unaoendelea unaotokana na kugubikwa na ulevi wa utamaduni wa chama kimoja kwa upande mmoja, na ulevi wa umaarufu kwa upande mwingine, hawatakubali yaishe nje ya Mahakama, na hatimaye watamfukuza Zitto."]

Hili nguruvi3 kalijadili vyema. Suala la mahakama lilikuwa ni la kimkakati zaidi kununua muda ili kuona Watawezaje kulitumia BLK, kuangalia chadema itapambana vipi na sakata la kina zitto lakini muhimu zaidi, kutoa muda kwa ACT kusajiliwa na kujipanga kumpokea mwenyekiti wake in a "top down" fashion.

Nguruvi3 kajadili kwamba ACT ina nia ya kupambana na Chadema, sio CCM, hatua ambayo itazidi imarisha CCM. Hili linadhihirika wazi na kauli ya Kitila kwamba:

["Wakishakumfukuza Zitto atatimka na mashabiki wake, chama kitayumba na kutoa unafuu kwa CCM. Katika mazingira haya tunahitaji sana mbadala wa CCM na CHADEMA"]

Kitila alitakiwa asijadili kabisa chadema bali CCM kwani pamoja na mapungufu ya chadema, matatizo yanayowakabili wananchi yanatokana na mapungufu ya CCM kuliko Chadema. Mapungufu ya chadema yanasaidia ccm iendelee kutawala nchi itakavyo, na hali hii haitabadilishwa na ujio wa ACT, badala yake, ACT will endorse this predicament facing the majority of Tanzanians.


Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:

Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
13,752
2,000
Mchambuzi;9515040]Moja ya matatizo makubwa yanayovikabili vyama vyetu vya siasa ni pamoja na vyama hivi kutoheshimuu demokrasia, sio tu nje ya chama bali hata ndani ya chama. Sasa iwapo sakata la kina Kitila lilichangiwa na wao kutoridhika na mwenendo wa demokrasia ndani ya chadema, kama alivyohoji Nguruvi3, nini wanachofanya kina Kitila sasa hivi ambacho tunaweza sema ni mbadala wa ccm na chadema linapokuja suala la demokrasia ndani ya vyama?
Na ikumbukwe akina Kitila walisema wanataka siasa za kisayansi zikiongozwa na akili kubwa na si ndogo.
Tulitegemea kuona mambo tofauti kwa njia za sera za chama kuwavuta wanachama kutoka pande zote.

Mbadala wa akina Kitila ni kutafuta njia za kuondoka na wanachama wa Chadema. Hiyo ni mbinu inayokinzana na waraka wao uliosema chama chao kilikuwa kinalega lega kutokana na kutokuwa na mipango endelevu na sera.

Kwa mwendo wa kutangaza habari za mtu kuhama na wanachama wake watiifu na wala si sera za ACT kuvuta watu, hakika si mbadala wa CCM au Chadema.
 

Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
13,752
2,000
Mchambuzi;9515040]je, uongozi ambao Dr. Kitila anataka usimika ACT utakuwa na uhalali gani?

Hapa wanachama wa ACT watakuwa na haki ya kumhoji Kitila, je haoni kwamba tayari anamuamini Zitto kama kiongozi wa ACT kuliko mtu yoyote mwingine ndani ya chama hicho?

Je Kitila haoni kwamba anachofanya ni kupindua kanuni, taratibu na itifaki za chama chake kipya cha ACT za kupata viongozi wa chama? Ipo wapi nia njema kwa ACT na wanachama wake katika hili?

Hapa anakula matapishi yake mchana kweupe kwani kitendo cha kuamulia wanachama wa ACT viongozi wanaowafaa ni ujenzi wa utamaduni "hodhii na wa kiimla".

Hapa Dr. Kitila ametuacha hoi bin taaban kwani anayopingana ni ndiyo yale yale anayoyajenga ACT.
Kwa mfano, Zitto ni mteule wa mtu mmoja ACT. Kitila hataki ushindani wa wazi ukipatie act mwenyekiti wake. Na kwa maana hii, mwanachama yoyote atakayajitokeza kupambana na zitto ACT atapingwa vikali na Kitila.


Hapa Kitila anatuchanganya kidogo. Je, yeye na wenzake waliamua kutumia uzoefu wa NCCR ya kina mrema kama njia ya kuiboma chadema? Au uzoefu wa NCCR uliwapa funzo yeye na wenzake kuzuia ya NCCR yasijirudie tena chadema kwa faida ya chama?

Na ni nani aliyejenga ufuasi kwa viongozi kuliko chama kama si Kitila kiasi cha kufikia hatua ya kutumia umaarufu wa chaguo lao "zitto" kukisambaratisha chama? Waraka wa Kitila and company ulijaa ushabiki wa personality moja dhidi ya nyingine, kuliko masuala ya sera, itikadi au chadema kama taasisi.


Kitila naleta hisia kwamba kafulila ni sehemu ya mpango wao kwani alichofanya kafulila NCCR hakikuwa tofauti sana na cha kina kitila "kimkakati".

Sakata la Zitto analojadili kwamba lilitakiwa limalizwe kimya kimya ni lipi hasa, lile la waraka? Wao waliandaa waraka ule kimya kimya na kimakosa, na dawa yake kwa manufaa ya chama haiuhitaji ukimya kwani waraka ule ulikuwa ni sumu iliyohatarisha uhai wa chama.

Pamoja na hayo, mara ngapi uongozi wa chadema ulimvumilia ZZK na kujaribu kumaliza migogoro ya zzk kimya kimya? Zipo rekodi kwamba wajumbe wa baraza kuu, sio mara moja katika vikao walitaka ZZK ashughulikiwe huku yeye (zzk) akiwa meza kuu akilindwa na Mwenyekiti.


Kitila alitakiwa asijadili kabisa chadema bali CCM kwani pamoja na mapungufu ya chadema, matatizo yanayowakabili wananchi yanatokana na mapungufu ya CCM kuliko Chadema.

Mapungufu ya chadema yanasaidia ccm iendelee kutawala nchi itakavyo, na hali hii haitabadilishwa na ujio wa ACT, badala yake, ACT will endorse this predicament facing the majority of Tanzanians
Mchambuzi, huo uongozi wa Kitila unaotaka kumsimika ZZK uenyekiti siyo tu hauna uhalali, bali pia unatia shaka kama kweli mbadala unaohitaji ndio huu.

ZZK ni mwanachama wa CDM hadi mahakama itakapoamua vinginevyo.
Kwa maoni ya Kitila, anachotaka ni kumshauri ZZK ajiunge na ACT.

Kitila anakubaliana na sera za chama hicho na hivyo kumshawishi rafiki yake azisome kwani zinavutia. Rafiki hajasoma sera iweje apigiwe upatu wa uenyekiti akiwa mwana CDM na asiyejua sera za ACT? Hapo kina kitila wanataka kujenga chama gani.

Hadi sasa kuna uongozi wa ACT unaofanya kazi usiku mchana.
Hatuamini kama Kitila ni mmojawapo kwasababu yeye amejitambulisha juzi baada ya usajili wa kudumu.

Hivi inakuwaje Kitila anafikia mahali pa kudharau uongozi uliopo hadi kutafuta mwenyekiti nje kwa njia za ajira kwa maana hajui sera wala malengo ya chama.

Kitila anaamini ZZK ni mtaamau aliyebobea katika kazi ya uenyekiti au CEO anayeweza kumudu nafasi ya uenyekiti hata kama ni CCM.

Ndivyo ilivyo kwasababu ZZK ni mwanachama wa CDM, leo anaalikwaje kuwa mwenyekiti na si mwanachama wa ACT. Jibu ni rahisi, Kitila anaamini kwa kupitia Waraka na kupitia uanachama wa ACT kuwa ZZK ni CEO katika vyama vya siasa.Ndio mbadala unaohitjaika huo?

Mkuu, hadi sasa ACT haina katiba wala kanuni za kueleweka.
Anachokifanya Kitila ni kutunga kanuni zake kabla ya wanachama wa ACT hawajaamua muundo na mwelekeo wa chama chao.

Ni huyu ndiye aliyeandika waraka wa chama cha ukanda, sijui yeye itakuwaje maana yake watakaposema ni chama cha Uswahiba, kitila hana jibu.Atulie na akae kimyaa!

Katika waraka Kitila amedai Viongozi wa CDM hawakutaka kufanya chaguzi ni madikteta ukilinganisha na watangulizi wawili akimaanisha Mzee Mtei na Marehemu Makani.

Hivi kitendo cha kujitokeza wazi wazi na kutafuta mwenyekiti kwa njia ya CV na si sanduku la kura la ACT hicho si udikteta ule ule alioukimbia CDM na kuulani. Ndio mbadala kweli!!!

Kitila anadai sakata la ZZK limalizwe kimya kimya.
Hii sijui inaitwaje kwa kiswahili fasaha nitajaribu kufafanua.

Zitto aliitwa Bagamoyo na kupewa onyo huku viongozi wenzake wakitaka aadhibiwe.
Kakingiwa kifua na Mbowe

Akaitwa Diamond na kuambiwa hadharani aadhibiwe, kaikingiwa kifua.
Sakata la masalia M7 mshiriki alikuwa Zitto
Sakata la akina Juliana ZZK alikuwa na mkono

Hakuna sakata lolote lililoisumbua CDM ambalo ZZK hana mkono, si kuanzia Arusha hadi Mwanza.Leo Kitila anasema matatizo yamalizwe kimya kimya.

Endapo alitaka yamalizwe kimya kimya, Kitila alipaswa amshauri ZZK kujiunga na ACT kimya kimya.Kitendo cha kwenda kumtangaza mwenyekiti wa ACT wa kuteuliwa na Kitila si cha kimya, leo ana morala authority gani ya kutamka neno kimya kimya.

Kitila alikuwa mshauri mwanadamizi wa CDM. Kushindwa kwa CDM ni sehemu ya mikakati yake aliyoiandaa akiwa kiongozi wake. Leo hawezi kusema failure za CDM zipo mbali na mikono yake.

Muhimu ni kuwa kama angetaka mwenyekiti CEO ZZK akubali uteuzi huo, Kitila asingekwenda magazetini kutangaza.

Angemshauri aondoe suala mahakamani ajiunge na ACT halafu waendelee na mkakati wa waraka hadi CEO mwenyekiti atakapopatikana. Huo ndio mkakati.

Kitila hakufanya hivyo, alijua kuwa nia ya ZZK ni masilahi yake katika bunge la katiba.
Kwasasa anaona ni muda muafaka aanze kuandaa wanachama wa kutimka na ZZK.


Je, hilo litakisaidia ACT kukua? Kipi bora wafuasi wa ZZK au wafuasi wa sera za chama cha ACT.
Na Kitila ajiulize, hiyo ndio mikakati mikubwa ya kisayansi anayotaka kufanya?

Kuna sayansi gani wakati mbogo anapigana na nyumbu na wala si mbogo na nyumbu kuungana ili kukabliana na Simba anyewamaliza wote.

Je, tatizo la ACT ni kuangamiza upinzani au kukabiliana na nyangumi CCM?

Kwa mwendo wa uteuzi wa mwenyekiti kutoka CDM kuwa mwenyekiti wa ACT kuna mbadala hapo?

Kitila anajaribu kuonyesha siasa gani ambazo ni mbadala na zile tunazoona CCM na CDM?
 

Mkandara

Verified Member
Mar 3, 2006
15,478
2,000
Mimi nashindwa sana kuwaelewa Watanganyika. Hivi kwa nini watu tusitazame Itikadi za chama hiki ACT badala yake tunatazama unaminifu wa mtu kwa chama kisha kesho wanaCCM wakiwa waaminifu kwa chama chao mtasema Maslahi ya Taifa kwanza. Kwa nini tunapenda malumbano yasokuwa na tija kwa Taifa hili nila kuongeza chuki na Uadui.

Sasa naomba nyie wataalam wenye taaluma ya Siasa za Upinzani, Huyu Kitila anawawakwaza kipi haswa ikiwa yeye kaamua kujitoa na kuunda chama chake? Hivi Mzee Mtei si alikuwa CCM na akaamua kujitoa na kuanzisha chama chake, Mrema, Maalim Seif na Kina Lipumba mbona hwa leo wanaitwa mashujaa ilihali walipingana na Uongozi wa CCM miaka hiyo na wengine wakaitwa hawana nidhamu kwa viongozi!. Ni kosa gani kubwa alofanya Mze Mtei kutokubaliana na Mwalimu na hata kuanzisha chama! Ni unafiki upi alokuwa nao?

Sisi kama wananchi tunachotakiwa ni kusikiliza sera, kujifunza ktk kila wanalosema hawa wananchi badala ya kuweka maslahi ya Chadema mbele ya Taifa kwa sababu chochote annachoweza kuchangia Dr.Kitila kwa manufaa ya Taifa iwe ndani au nje ya Chadema ni muhimu sisi wananchi tukipokee. Hata ikiwa kiongozi huyo anatoka CCM.

Leo mnamzungumzia Zitto na Kitila kama vile ni wahaini wakati maamuzi ya kuwafukuza yamefanywa na chama na sii kwa hiari yao. Nijuavyo mimi mtu anaye kihama chama wakati anahitajiwa zaidi ndiye mtu wa kupigiwa vuvuzela lakini tulomfukuza wenyewe? Hii mnazidisha kuonyesha jinsi gani chama cha Chadema kinahaha kwa maamuzi yake maana hata wacheza mpira wa kulipwa akiuzwa inatakiwa huyu ndiye alalamike kuliko yule aloihama timu ndiye huzomewa. Ikiwa mnawahofia kiasi hiki kwa nini mliwafukuza au mlitaka wakae pembenio kabisa nje ya siasa ilihali Kitila alikuwa sii kiongozi tu bali mshauri wa chama!

Na swala la Nidhamu tumewaona wangapi wakikiuka nidhamu, wapo walokashifu hadi waasisi wa Muungano wetu, walodai kuwa hati ya Muungano ni fake kama vile wao walikuwepo na wanajua hati halali inafafanaje! Haya ni nmambo yasokubaliaka ikiwa mtajali mustakabali wa taifa letu. Ni kwa akili hii ya UMIMI, Uchadema ambayo siku zote tunawakemea CCM na wafuasi wake leo imekuwa mchezo wa Chadema na ndio maana mnadai Tanganyika kwa Watanganyika na itafikia wakati yule asokubaliana na Utanganyika akawakosoa na kuanzisha upinzani. Jamani tangnzania ni nchi ya Demokrasia tukubali kutokubaliana na tusiweke nyodo kwa sababu hatukubaliani.

Kila kukicha Zitto Hivi Zitto vile mbona mnaonyesha kiu kali kama cha yule Sungura alokosa zabibu akidai mbichi. Sisi wengine sii wajinga hivyo, na tunapowasoma ktk mabandiko kama haya tunaziona hadi roho zenu zilivyojaa chuki, Ubinafsi na kutaka kila mtu akubaliane nanyi na kuwasujudia. Sisi wengine tupo Chadema kwa sababu ya Kiitikadi tu tena nilivutiwa baada ya kusikia sera na ahadi za Chadema ambazo walijaribu sana Kumuenzi Mwalimu, leo wanatukana fikra za mwalimu wazi waizi. Chadema yangu ili ahidi kuchukua mazuri ya Utawla ule na kuacha yalokuwa mabaya ama yamepitwa na wakati.

Chadema ilokuwa ikidai miiko na maadili kwa viongozi dhidi ya Ufisadi, Chadema ilokuwa ikidai responsibility na Accountability kwa viongozi wote, Chadema iloweka ahadi ya Kutoa huduma za Elimu na Afya BURE kwa Taifa zima na sii Bara au Zanzibar pekee. Ilifikia hadi Kingunge Ngambale Mwitu achukie na kusema Mbowe hawezi kufuata nyayo za Mwalimu, hajui kuhusu Ukoloni japo alibanwa kabali la roho kwa hoja nzito za Mh. Mbowe wakati ule. Yule Mbowe yuko wapi? yule Slaa wa List ya Mafisadi yuko wapi? Hee jamani Chadema imepigwa kipapai?

Leo Chadema imekuwa chama cha nipashe kila siku kuzungumzia hadith za CCM na watu kama vile tumeishiwa sera? Kama Kitila ameamua kuunda chama mbadala dhidi ya CCM na Chadema kwa maana yakwamba CCM na Chadema wamejifutika ktk Udaku na habari za mipasho, ninampongeza sana kwa kuliona hilo na hunichukiza shsana kila naposoma habari za Chadema wakilumbana juu ya vyama na kuyaweka maslahi ya vyama vyao mbele ya Taifa.

Ikiwa Kitila amekuja na Itikadi ya kuchekesha, sera zisizowezekana na ahadi (ilani) ya kufikirika hapo ningewaunga mkono na kuanza kuchambua sera zao lakini hii habari ya kumsema mtu ama watu hakika ni SIMPLE MIND people tu ndio hucheza karata hizi kisiasa.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom