Duru za siasa: Chama cha ACT-Wazalendo Mpini wa CCM kumaliza upinzani(?)

CHAMVIGA

JF-Expert Member
Oct 5, 2012
7,688
1,225
Tuliposimama kumtetea Lowassa asimamishwe kuiwakilisha CCM na tukasema Richmond ni skendo iliyotengenezwa kummaliza Lowassa tena kwa misingi ya makundi yakiimani tuliambiwa yy ni fisadi tena akaitwa Fisadi papa na Dr Slaa lakini leo fisadi papa atakuwa akiwakilisha CHADEMA/UKAWA Urais.

Siasa na umalaya hakuna tofauti.
Zitto alisema usimuamini mwanasiasa alikuwa sahihi 100%.
 
Kapwela

JF-Expert Member
Mar 11, 2015
2,013
2,000
K

Hawa walisutana hadi wakawa hawawezi kuangaliana, wiki kadhaa baadaye wakawa ofisini pamoja......

Mfano wa Mama Clinton na Obama hauendani kabisa na hili la kwetu.

Hawa tofauti zao zilikuwa juu ya sera tu na utekelezaji wake, hawa wakati wote walikiri kuwa kila mmoja wao anajali maslahi ya nchi yake japo kila mmoja alijiona angefanya vizuri zaidi kuliko mwenzake.

Lakini hii ya kwetu ni juu ya tuhuma juu za wizi na ufisadi, kufanya kazi na mtu uliyesema ni mwizi na fisadi, Clinton na Obama hawakuwa na mtihani huo.
 
Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
13,765
2,000
kama kuna watu wanadhani wataweza kumcontrol Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania(kwa katiba iliyopo) tena Rais mwenyewe ni Edward Ngoyai Lowassa basi watakuwa wanajidanganya

kinyume chake wabunge wengi wa Chadema watajenga ufuasi kwa Lowassa binafsi(Lowassa ana historia nzuri sana kwenye hili, iwe kwa vyeo au kwa favour zingine) na pia ataweza kushirikiana na wabunge wa vyama vyote ikiwepo CCM(anajua vizuri kuishi nao), hatimaye mwishowe badala ya Chadema kumsimamia ni Lowassa ndiye atakayeisimamia Chadema na kuipeleka atakavyo

Otherwise nampongeza sana Dr Slaa kwa kukubalia kuachia nafasi ya urais bila shida, sio watu wengi wanaweza kufanya hili kwenye siasa za Afrika, japo legacy yake juu ya ufisadi itaathiriwa sasa kwa kuanza kumpigia kampeni aliyemuita fisadi awe Rais lakini kwenye suala la kutokuwa na "uchu wa madaraka" atajijengea heshima kubwa.Hili litakumbukwa ata miaka mingi ijayo na kwa kweli anastahili pongezi.
Mtu anapokuwa mkubwa kuliko taasisi ni tatizo kubwa sana, agree!

Suala si mtu kuwa Rais, ni watu wa kusimamia mabadiliko. Huko mitaani wapo wanaosimamia mabadiliko katika vitongoji vyao. Wote hao hawana uchu bali uchungu.

Nchi hii haina upungufu wa viongozi, ina upungufu wa viongozi watakaoongoza kupata viongozi
 
Mag3

JF-Expert Member
May 31, 2008
11,146
2,000
Mag3: Najibu kwa kifupi sana:

1 mpaka 6 mkandara yuko sahihi

7 na 8, napingana na mkandara; si kweli kuwa CCM walijiandaa, kumekuwa na several unplanned meetings within CCM to discuss this matter

9, Well sijajua maana imekaa kihisia zaidi
Asante Waberoya, mpaka sasa ni wewe tu angalau umegusia mada kama nilivyoiwasilisha, wengine wote sina hakika kama kweli mmelielewa nililokusudia. Sijaongea habari za LOWASSA kujiunga UKAWA wala kuwa mgombea wa UKAWA, nimeuliza tu kuhusu tuhuma za Mkandara kwa Lowassa. Naomba nizirudie;
Mkandara anasema hivi;

 1. Lowassa was the master mind muda wote wa ufisadi ccm
 2. (Lowassa)ndiye alokuwa akichagua baraza la mawaziri hata baada ya jk kubadilisha mara tatu.
 3. (Lowassa)ndiye alokuwa kinara wa miradi mingi ya kuuza ardhi na majumba.
 4. (Lowassa)ndiye alokuwa akichukua 10% ya kila deal nchini hata iwe tsh 500.
 5. (Lowassa)hili la jk kumgeuka ndilo limemuuma kuliko kila kitu na hasira zake zote ni kwa jk,
 6. (Lowassa)walomwaga haswa ni cc ya kina mkapa na mwinyi na wazee wa kamati kuu na madili ambao wanaijua siri kubwa ya huyu mtu kuliko nyie.
 7. hawa wote walijua lowassa atahamia cdm wakishamwaga na bado wakamwaga tena vibaya sana na kumuaibisha!
 8. hamuoni kama ccm imeshajiandaa kwa tukio hili na nani huko ccm atakubali lowassa awe rais wa nchi hii alipe kisasi kwao maana wanamjua kwa visasi!.
 9. yeye hataki kuwa rais kwa sababu ya mageuzi ila anataka kutimiza ndoto yake na kuwaonyesha watu kuwa yeye ni zaidi yao ni mungu
Tukiachana na hilo naomba mwenye kumbukumbu kwamba Dr. Slaa aliwahi kusema au kuonesha nia ya kugombea Uraisi kupitia UKAWA atufahamishe. Ninachokumbuka ni kauli moja aliyowahi kuitoa zamani kidogo kwamba hakuwa na mpango wa kugombea na ninavyojua hadi sasa hakuna mwana Chadema wala kiongozi amechukua fomu ya kugombea Uraisi hadi leo.
 
Last edited by a moderator:

JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
18,862
2,000
Kwa hiyo hamna tatizo Mbowe kumlilia Lowassa kujiunga na Chadema?

Hili hoja iwe na mashiko nani haiukubali wewe au Nguruvi3, Mag3, Mchambuzi Alinda au nani?

Chadema mtafanyaje sasa kwenye ile orodha ya mafisadi mliyoitoa pale Mwembe Yanga na kuwafahamisha watanzania kuwa Lowassa ni fisadi leo hoja ya ufisadi haina mashiko tena.
..lowassa kasema anayehusika na Richmond ni JK.

..Mwakyembe naye alisema kuna mambo tume haikuyaweka wazi ili kuepuka kuiabisha serikali.

..Waziri Ibrahim Msabaha alidai tume imemuonea, na akasema ametolewa kafara kuwalinda wakubwa.

cc Mkandara, Nguruvi3
 
Last edited by a moderator:

Mag3

JF-Expert Member
May 31, 2008
11,146
2,000
..lowassa kasema anayehusika na Richmond ni JK.

..Mwakyembe naye alisema kuna mambo tume haikuyaweka wazi ili kuepuka kuiabisha serikali.

..Waziri Ibrahim Msabaha alidai tume imemuonea, na akasema ametolewa kafara kuwalinda wakubwa.

cc Mkandara, Nguruvi3
Lowassa ni fisadi lakini kwa Richmond alipakaziwa...nilisema hivyo mwaka 2008 na thread iko humu humu JF.
 
Alinda

Platinum Member
Jun 26, 2008
1,690
2,000
Lowassa ni fisadi lakini kwa Richmond alipakaziwa...nilisema hivyo mwaka 2008 na thread iko humu humu JF.
Kaka yangu unaanza kumsafisha? lol (joke) baada ya ili pigo kwa wapenda mageuzi inabidi tujiliwaze liwaze tuzoe ndio siasa za upinzani ngoja tuangalie upepo unapoelekea.

Ila sijui kwanini watu wanamkimbilia vile maana jamaa kujieleza hawezi, kujenga hoja zenye mshiko hawezi, sasa sijui huu ushawishi unatoka wapi? sijui ni pesa lakini anaweza kuwapa pesa watu wote hawa? (rejea kutafuta wadhamini)

Tukatae tukubali jamaa ana team iliyojipanga...

Ngoja tuone haya maamuzi magumu kama yatakuwa na manufaa kwa chama au ndio tutaanza kujenga chama upya..
 
Alinda, naomba nikudokezee kidogo ambalo labda na wewe unapata shida kulipokea, amini usiamini ni katika kuipumzisha CCM tu mabadiliko yoyote yale yatapata nafasi ya kufanikiwa. Katika wakati huu tulio nao haitawezekana tena kwa mtu moja au chama kuwa na jeuri ya kuliongoza taifa kama ilivyo sasa chini ya serikali ya CCM.

Siku CCM ikiondoshwa madarakani itakuwa ni kama vile taifa limezaliwa upya na ole wako uende kinyume cha matarajio ya wananchi, sidhani kama utabaki salama. Lakini CCM ikibaki madarakani, sahau kabisa kuyaona hayo mabadiliko katika kipindi cha kizazi hiki (kumbuka wao wenyewe wameapa kubaki madarakani hata kwa miaka mia).

Kama njia pekee ya kulisambaratisha hili zimwi ni kwa kupitia kwa mtu moja anayeitwa Edward Ngoyai Lowassa mimi Mag3 nasema, so be it! Naunga mkono. Times have changed comrades.
 
Last edited by a moderator:

Ritz

JF-Expert Member
Jan 1, 2011
42,278
2,000
..lowassa kasema anayehusika na Richmond ni JK.

..Mwakyembe naye alisema kuna mambo tume haikuyaweka wazi ili kuepuka kuiabisha serikali.

..Waziri Ibrahim Msabaha alidai tume imemuonea, na akasema ametolewa kafara kuwalinda wakubwa.

cc Mkandara, Nguruvi3
Hayo kayaongea baada ya kukatwa.

Lembeli, naye anasema alitakaa kuongwa milioni 200.

Ester, naye anasema aliahadiwa uwaziri akakataa.

Usihesabu siku zifanye siku ndiyo zihesabu
 
Last edited by a moderator:

zumbemkuu

JF-Expert Member
Sep 11, 2010
10,106
2,000
Alinda, naomba nikudokezee kidogo ambalo labda na wewe unapata shida kulipokea, amini usiamini ni katika kuipumzisha CCM tu mabadiliko yoyote yale yatapata nafasi ya kufanikiwa. Katika wakati huu tulio nao haitawezekana tena kwa mtu moja au chama kuwa na jeuri ya kuliongoza taifa kama ilivyo sasa chini ya serikali ya CCM.

Siku CCM ikiondoshwa madarakani itakuwa ni kama vile taifa limezaliwa upya na ole wako uende kinyume cha matarajio ya wananchi, sidhani kama utabaki salama. Lakini CCM ikibaki madarakani, sahau kabisa kuyaona hayo mabadiliko katika kipindi cha kizazi hiki (kumbuka wao wenyewe wameapa kubaki madarakani hata kwa miaka mia).

Kama njia pekee ya kulisambaratisha hili zimwi ni kwa kupitia kwa mtu moja anayeitwa Edward Ngoyai Lowassa mimi Mag3 nasema, so be it! Naunga mkono. Times have changed comrades.
Naunga mkono hoja
 
Mag3,

Nadhani labda ndiyo maana Dr. Slaa hakuhudhuria kwenye mkutano labda alifahamu kitakachoulizwa na kujibiwa!

Yaani viongozi wa CHADEMA wanaambiwa kimantiki to shut up kwa kumuida Lowassa ni fisadi halafu wanashangilia!

Yaani viongozi wa CHADEMA kwa sasa wamegeuka kuwa wana CCM. Wanawaomba wanaCCM ushahidi wa ufisadi wa Lowassa wakati waanzilishi wa shutuma ni CHADEMA.

Huu ni unafiki wa kiwangio cha juu!

Siasa za Tanzania niza ajabu kweli.

Mnasahau kuwa shutuma za ufisadi wa Lowassa zilikuwa zinatolewa na Dr.Slaa, Lema, Mnyika, sasa Lowassa anamuomba ushahidi nani.
 
Last edited by a moderator:

zumbemkuu

JF-Expert Member
Sep 11, 2010
10,106
2,000
Naona unaongelea kwenye matapishi yako bila dodoki.

Jana tu umetoa viapo vingi na kusema unaachana na Chadema baada ya ujio wa Lowassa na kusema bora uwe mwanaharakati.

Teh teh teh
Siasa ni mchezo unaobadilika, teh teh teh
 
Mkandara

Verified Member
Mar 3, 2006
15,478
2,000
Asante Waberoya, mpaka sasa ni wewe tu angalau umegusia mada kama nilivyoiwasilisha, wengine wote sina hakika kama kweli mmelielewa nililokusudia. Sijaongea habari za LOWASSA kujiunga UKAWA wala kuwa mgombea wa UKAWA, nimeuliza tu kuhusu tuhuma za Mkandara kwa Lowassa. Naomba nizirudie;
Mkandara anasema hivi;

 1. Lowassa was the master mind muda wote wa ufisadi ccm
 2. (Lowassa)ndiye alokuwa akichagua baraza la mawaziri hata baada ya jk kubadilisha mara tatu.
 3. (Lowassa)ndiye alokuwa kinara wa miradi mingi ya kuuza ardhi na majumba.
 4. (Lowassa)ndiye alokuwa akichukua 10% ya kila deal nchini hata iwe tsh 500.
 5. (Lowassa)hili la jk kumgeuka ndilo limemuuma kuliko kila kitu na hasira zake zote ni kwa jk,
 6. (Lowassa)walomwaga haswa ni cc ya kina mkapa na mwinyi na wazee wa kamati kuu na madili ambao wanaijua siri kubwa ya huyu mtu kuliko nyie.
 7. hawa wote walijua lowassa atahamia cdm wakishamwaga na bado wakamwaga tena vibaya sana na kumuaibisha!
 8. hamuoni kama ccm imeshajiandaa kwa tukio hili na nani huko ccm atakubali lowassa awe rais wa nchi hii alipe kisasi kwao maana wanamjua kwa visasi!.
 9. yeye hataki kuwa rais kwa sababu ya mageuzi ila anataka kutimiza ndoto yake na kuwaonyesha watu kuwa yeye ni zaidi yao ni mungu
Tukiachana na hilo naomba mwenye kumbukumbu kwamba Dr. Slaa aliwahi kusema au kuonesha nia ya kugombea Uraisi kupitia UKAWA atufahamishe. Ninachokumbuka ni kauli moja aliyowahi kuitoa zamani kidogo kwamba hakuwa na mpango wa kugombea na ninavyojua hadi sasa hakuna mwana Chadema wala kiongozi amechukua fomu ya kugombea Uraisi hadi leo.
Kwanza shukran leo tumekubaliana japo machache sasa nikurudishe kwenye hilo la 7,8 na 9 ambalo wewe unadhani ni hisia. Hapana mkuu sio hisia kwa sababu Lowassa alishajijenga kugombea Urais mapema sana na wapambe wake wote walikuwa wakisema ovyo ndani ya CCM na nje. Na maandalizi haya yalikuwa wazi kabisa hata kabla ya kutia nia ilieleweka kuwa akikatwa atahamia CDM isipokuwa kuna watu walitaka kuipotezea CCM wadhani sio mpango wake. Yale maneno ya hatatwi mtu ni hadaa ya JK mwenyewe aliwaahidi hakatwi mtu...

Elewa CCM ni chama kubwa kuliko mnavyokidhania, Ndani ya UKAWA wamo watu wa CCM hadi kesho na ndani ya makundi ya CCM wapo waliokuwa wanafiki wakila pande zote, hivyo haikuwa habari ngeni kwa CCM hata kidogo. Sasa ujue kama huyu mtu EL hafai kabisa ni jinsi anavyofanya maamuzi MAGUMU maamuzi ambayo mtu yeyote mwenye akili timamu asingeyafanya. CCM kufanya vikao ni lazima wakati huu wa Uchaguzi hata kama angechaguliwa Dr.Slaa au Lipumba kwa sababu muda wa kampeni ndio umeshafika na hata UKAWA watakuwa na vikao karibu kila siku.

Kwa nini nawashangaa UKAWA ni kutokana na ukweli kwamba wametumia MAFISADI walokuwa wakiogopwa na pande zote mbili yaani CCM na wananchi wakija chukua madaraka. Yasemekana hawa watu ndio walopiga hata hela za Escrow kwa ajili ya maandali ya uchaguzi huu bado mnataka kusema haramu imehalalishwa maadam anayeondolewa madarakani ni CCM...

Kenya wenzetu walichukua kundi la wasafi kina Odinga, Rutu na Kibaki dhidi ya Mafisadi kia Moi na Kenyatta na wakashinda, Leo kweli mnategemea Ushindi kwa kutumia kundi la Mafisadi mkimtangaza Lowassa wakati anakuja na genge lake kina Rostam, Karamagi, na Chenge? Piga ua hawa watu lazima wawepo kweli ndio kupigana na mfumo tawala huu ama kuuokelza! au kwa sababu mengi naye kajivuta akitegemea vitalu vya gas?...
 
Bavaria

JF-Expert Member
Jun 14, 2011
47,882
2,000
Hayo kayaongea baada ya kukatwa.

Lembeli, naye anasema alitakaa kuongwa milioni 200.

Ester, naye anasema aliahadiwa uwaziri akakataa.

Usihesabu siku zifanye siku ndiyo zihesabu
Kama JK amechafuliwa kwa makosa ambayo sio yake basi atumie rungu la urais kujisafisha. Ila akikaa kimya hili ni doa kwake. Lowassa ameshajisafisha, the ball is in the JK's court.
 
Mag3

JF-Expert Member
May 31, 2008
11,146
2,000
Kwanza shukran leo tumekubaliana japo machache sasa nikurudishe kwenye hilo la 7,8 na 9 ambalo wewe unadhani ni hisia.
Hapana Mkuu naona umechangaya dawa, aliyekubaliana na japo machache na kutilia mshaka 7, 8 na 9 ni Waberoya. Mimi sijatoa comment yoyote isipokuwa nimeomba tu comment kutoka kwa wadau niliowataja. Bado nayatafakari hayo madai yako na nikiwa tayari utanisikia loud and clear...hata hivyo kuna kitu kimoja kinanishangaza, unataka kuniambia kwamba hata baada ya kujiuzulu Lowassa aliendelea kuwa master mind muda wote wa ufisadi ccm? Kwamba aliendelea kuwachagua mawaziri? Kwamba aliendelea kuchukua 10% ya kila deal nchini? Aliendelea kuwa kinara wa miradi mingi ya kuuza ardhi na majumba?

Duh Mkandara, je katika muda huo tulikuwa na Raisi? Tulikuwa na serikali? Tulikuwa na cc ya kina Mkapa na Mwinyi na wazee wa kamati kuu na madili? Je kwa wakati huo tulikuwa na watu ambao walijua siri kubwa ya huyu mtu kuliko hata sisi wengine? Ila kwa sababu ya Lowassa wote wakakunja mikia, hakuna aliyethubutu kumgusa hata pale alipochaguliwa kuwa mwenyekiti wa kamati ya usalama bungeni au alijichagua!

Jamani tuache mambo ya kipuuzi kwenye issue kama hizi. Hizo nguvu Lowassa alizipata wapi! Kwa nini hazikuweza kuzuia asikatwe? Mwinyi aliwahi kujiuzulu akiwa waziri wa mambo ya ndani na hakuna aliyeuliza kwa nini alikubali kujiuzulu kama hakuhusika? Mwalimu Nyerere mwenyewe wakati anampiga biti Waziri Mkuu Malecela alionya, Waziri Mkuu anaweza kuchukuliwa hatua nchi ikabaki salama lakini si Raisi. Lowassa alikuwa kondoo wa kafara kwenye issue ya Richmond kama walivyokuwa Msabaha na wengine.

Kesho CCM wameitisha mkutano, CCM ina nguvu, ina serikali, ina vyombo vya usalama ambavyo naviita vyombo vya kulida usalama wa genge lililoko kwenye utawala na kuwatesa wananchi...waangalie tu wasifungue pandora box!
 
Last edited by a moderator:

Zakumi

JF-Expert Member
Sep 24, 2008
4,858
2,000
Kabla sijatia neno ningpenda kujua wachangiaji wengine wanayachukuliaje haya madai yako mkuu;

cc: Waberoya, Nguruvi3, Alinda, JokaKuu, Zakumi, Ritz, Mchambuzi, ZeMarcopolo, zumbemkuu, Mzee Mwanakijiji, gfsonwin, Sikonge, MTAZAMO, suleiman, Mwalimu, Pasco, TUJITEGEMEE, Adharusi, Barubaru, Pipiro,

Mkuu mag3:

Sio tetesi tena. Lowassa ni CDM/Ukawa. Nadhani katika ukumbi huu ilitakia thread rasmi. Naona kama hatutendiki kuendelea kuchagia hapa.
Nguruvi3:

Tuwekee thread mpya.

cc: Nguruvi3
 
Last edited by a moderator:

Zakumi

JF-Expert Member
Sep 24, 2008
4,858
2,000
Kwa ndugu Nguruvi3:

Pokea salaam nyingi kutoka kwangu. Hama baada ya salaam ningependa unifahamishe mambo mawili au matatu kuhusiana na matukio yanayoendelea hivi sasa ya uchaguzi.

Kwanza ningependa msimamo wako kuhusiana na tetesi za Lowassa kujiunga na CDM. Je kuna ukweli ndani yake? Au ni tetesi tu?

Pili kama kuna ukweli, je uoni kuwa inabidi uanzishe thread mpya. Kichwa cha thread hiyo LOWASSA ni mpini wa CDM wa kuiua CCM.

Tatu kama Zitto alikuwa mchu wa madaraka ndani ya CDM, je Lowassa atakuwa katika ngazi gani?

Wako katika kusukuma gurudumu la maendeleo,

Z10.

Komredi Nguruvi3:

Tumekee thread ya Lowassa kujiunga na CDM/Ukawa. Hii ya Zitto/ACT is too prehistoric now.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom