Duru za siasa: Chama cha ACT-Wazalendo Mpini wa CCM kumaliza upinzani(?)

Adharusi

JF-Expert Member
Jan 22, 2012
13,891
2,000
Mtazamo wangu Mimi LOWASA kujiunga CDM itaisaidia CHADEMA ila lengo la Lowasa kwenda Ikulu halifanikiwi itabaki kuwa ndoto isiotimia,ataleta ushindani sana KATIKA Urais, kura zitoongezeka,wabunge pia,faida kwa upinzani,ila Lowasa haiwezi kushinda,sababu CCM ina mtu mwenye record KATIKA utendaji
 
Bavaria

JF-Expert Member
Jun 14, 2011
47,838

Do not underestimate majority vote. Utendaji sio tija, watu wamechoka mfumo.
 
MTAZAMO

JF-Expert Member
Feb 8, 2011
15,772
2,000
Wakuu siku zote naamini jinamizi linalotesa nchi hii ni CCM ...... kwa namna yoyote hatuwezi kwenda mbele bila kuanza upya .....huo upya hauwezi kuja bila CCM kufa ........ Unapotaka kuua adui huchagui silaha ..... binafsi sijali matokeo ya Lowasa kuwa Rais nje ya CCM ila ningeendelea kupinga hata kama yeye angepitishwa huko CCM .....

Kama uongozi wa CDM wamejiridhisha kupitia mgawanyiko huu wa CCM ndio mwarobaini pekee wa kuharakisha kifo cha CCM naomba iwe kweli.

Uwanja sawa wa siasa ndio dawa ya uwajibikaji uliokufa muda mrefu .......
 
JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
18,779
2,000
Hayo kayaongea baada ya kukatwa.

Lembeli, naye anasema alitakaa kuongwa milioni 200.

Ester, naye anasema aliahadiwa uwaziri akakataa.

Usihesabu siku zifanye siku ndiyo zihesabu
..Yes.p

..asingeweza kuyasema wakati bardo yuko ccm na anatafuta ridhaa ya chama.
 
Alinda

Platinum Member
Jun 26, 2008
1,690
2,000
Kitu ambacho najiuliza na sipati jibu ni kwanini Lowassa ana wafuasi wengi? Hivi ni pesa au ni ushawishi wake alionao kwa vijana au au?

Maana tukatae tukubali ndani ya CCM hakuna mtu mwenye wafuasi wengi kama Lowassa nasema hivyo kwa kuangalia mikutano yake mbali mbali (rejea mkutano wa Dar na vijana wa boda boda na mtu huyu hana record ya kusomba watu kwa mabasi) au wakati wa kutafuta wadhamini.

Hawa watu wanatafuta nini kwa Lowassa? ni kitu gani alichofanya ndani ya miaka 8 ambacho kinawavutia hawa watu?

Swala la pili, ni mgumu kumeza lakini ndizo siasa tunabadilika kutokana na wakati na kutona na watu wa jamii yako. Nafikiri watanzania uelewa wetu ni mdogo kuhusu swala zima la ufisadi na madhara yake.Hivyo basi watu walio wengi vijijini ukiwambia mambo ya ufisadi hawaelewi kabisa maana wao walishaona kuwa kuishi kwenye nyumba ya tope ni halali yao,kuna watu hata hawafahamu umeme ni nini au una umuhimu gani, kuna watu ambao hawaoni umuhimu kuwa na maji ya bomba wameridhika na maji ya visima ambayo utumia muda wa 1 mpk 6 kufuata maji. Visima vikakauka kwa ajili ya ukame wao hizo ni laana kutoka kwa mwenyezi Mungu. Na mtu wa jinsi hii kumpa elimu kuelewa kuwa umaskini wake unachangiwa na ufisadi au matumizi mabaya ya madaraka au rushwa ni ngumu. Na kwa bahati mbaya au nzuri hawa watu ndo wengi na ndo wanatuchagulia viongozi.

Sasa basi inapotokea watu wa jinsi hii wakataka mtu ambaye watu wengine wenye uelewa wa mambo wanaona huyu mtu hafai kwa sababu moja au nyingi, kuna kuwa hakuna ujanja tena bali kuwapa yule mtu ambaye wanaona anawafaa wao.
Na hiki ndicho kinachotokea Tanzania, na baadhi ya nchi za kiafrika.

Nachelea kusema uchaguzi wa mwaka huu kama Chadema wangemsimamisha DR,Slaa na CCM Magufuli, basi Mafuguli alikuwa anapata ushidi tena asubuhi ingawaje utendaji wa Dr. Slaa kwa hapa Tanzania hauna mfn. Record zake ziko safi kwa kila sehemu alipopita. na huu ndio ukweli na hii ndio gharama ya demokrasia,

Kwa maana hiyo watanzania hatupendi watu waadilifu tunapenda mafisadi, hivyo basi sisi sote ambao tunapingana na ufasidi na wale ambao hawana habari na ufisadi hatuna budi kuchagua kati ya fisadi mmoja (Lowassa) au mfumo wa kifisadi ambao ni CCM. Kwa bahati mbaya sana hata vyama vingine vya siasa vikaamua kumsimamisha malaika hakuna hatayempigia maana kama watu wangekuwa wanachukia ufisadi basi leo hii Kikwete hasingekuwa madarakani..

Wapeni watu mtu anayemtaka maana wao ndio wapiga kura husipowapa utashindwa katika sanduku la kura.

Kama watanzania wanamtaka Lowassa au la ngoja tuone huku mbeleni maana kwa ili sina uhakika kama ni mapenzi tu au ni nguvu ya pesa
 
Mkandara

Verified Member
Mar 3, 2006
15,478
2,000
Hapana Mkuu naona umechangaya dawa, aliyekubaliana na japo machache na kutilia mshaka 7, 8 na 9 ni Waberoya. Mimi sijatoa comment yoyote isipokuwa nimeomba tu comment kutoka kwa wadau niliowataja. Bado nayatafakari hayo madai yako na nikiwa tayari utanisikia loud and clear...hata hivyo kuna kitu kimoja kinanishangaza, unataka kuniambia kwamba hata baada ya kujiuzulu Lowassa aliendelea kuwa master mind muda wote wa ufisadi ccm? Kwamba aliendelea kuwachagua mawaziri? Kwamba aliendelea kuchukua 10% ya kila deal nchini? Aliendelea kuwa kinara wa miradi mingi ya kuuza ardhi na majumba?

Duh Mkandara, je katika muda huo tulikuwa na Raisi? Tulikuwa na serikali? Tulikuwa na cc ya kina Mkapa na Mwinyi na wazee wa kamati kuu na madili? Je kwa wakati huo tulikuwa na watu ambao walijua siri kubwa ya huyu mtu kuliko hata sisi wengine? Ila kwa sababu ya Lowassa wote wakakunja mikia, hakuna aliyethubutu kumgusa hata pale alipochaguliwa kuwa mwenyekiti wa kamati ya usalama bungeni au alijichagua!

Jamani tuache mambo ya kipuuzi kwenye issue kama hizi. Hizo nguvu Lowassa alizipata wapi! Kwa nini hazikuweza kuzuia asikatwe? Mwinyi aliwahi kujiuzulu akiwa waziri wa mambo ya ndani na hakuna aliyeuliza kwa nini alikubali kujiuzulu kama hakuhusika? Mwalimu Nyerere mwenyewe wakati anampiga biti Waziri Mkuu Malecela alionya, Waziri Mkuu anaweza kuchukuliwa hatua nchi ikabaki salama lakini si Raisi. Lowassa alikuwa kondoo wa kafara kwenye issue ya Richmond kama walivyokuwa Msabaha na wengine.

Kesho CCM wameitisha mkutano, CCM ina nguvu, ina serikali, ina vyombo vya usalama ambavyo naviita vyombo vya kulida usalama wa genge lililoko kwenye utawala na kuwatesa wananchi...waangalie tu wasifungue pandora box!
Mkuu pengine huelewi jinsi gani Lowassa alikuwa na power ndani ya CCM hiyo ya Mtandao kiasi kwamba kujiuzuru kwake kulichukuliwa kama kujitoa mhanga. Na ndio maana alikuja kuwa bado mwenyekiti wa kamati ya usalama bungeni, mjumbe wa kamati kuu kitu ambacho hakuna waziri yeyote alokatwa na JK alirudi kuwa na madaraka.. Wako wapi kina Msabah na Karamagi! sii bungeni wala ndani ya chama wana sauti tena..

Hivi wewe kweli unashindwa kujiuliza kwa nini Chadema na UKAWA kwa ujumla wanafurahia na kumpokea kama Mungu mt huyu Lowassa ili kusimama kama mgombea wa UKAWA? Caham gani kingeweza mpichsha mtu mwingine zaidi ya Lowassa! na mbona hujiulizi kwa nguvu gani alizokuwa nazo hata akaachiwa yeye? tena Chadema wakamwamwaga mtu wao wa nguvu mtakatifu na msafi Dr.Slaa ambaye kaifikisha Chadema hapo ilipofika!.

Swala la Richmond ni KASHFA, hakuna aliyesema Lowassa alichukua fedha isipokuwa mradi ule ulikuwa wa Cartel yao ndio maana Dowans ilikuwa na address ya kampuni ya Rostam na ilidhihirishwa na tume ya Mwakyembe..Sii JK wala Lowassa wote hawakuchukua Rushwa (bribery) isipokuwa ilikuwa kashfa ya Kulipa fadhila (Napotism) kwa mfadhili wa kampeni za mwaka 2005. Kwa hiyo, hii ni scandal ya matumizi mabaya ya madaraka sio swala la kuchukua rushwa. Neno Corruption linabeba maana nyingi sana isipokuwa kutokujua kwa watu wengi wanadai ushahidi kama Lowassa alichukua rushwa, kwa sababu kwao Corruption ni kuchukua hongo!..

Na wala hatuhitaji ushahidi zaidi ikiwa Lowassa mwenye alikiri na kajisifia kuwa mtambo ya Richmond was state of the art..na hata rais wa Marekani Obama alimsifia! What more do we need. Na Lowassa aliendelea kuongoza mtandao hata uchaguzi wa mwaka 2010, kama unakumbuka Lowassa was on top ya kila mbunge alochaguliwa na mawaziri miaka minne baadaye. Waulize wana CCM wenyewe aliwezaje kuwa na asilimia 2/3 ya NEC katika uchaguzi huu kama angepita tano bora!

CCM walijua kwamba Lowaasa kama hatapitishwa atahamia Chadema na ndio maana wakaahirisha uchaguzi wao badala ya kuwa May wakaahirisha hadi July ili Lowassa aisipate muda wa kujipanga akiwa Chadema, lakini nao CDM wakashtuka wakabadilisha muda wa kutaja mgombea wao.. WALITEGEANA hadi ikabidi CCM wafanye maamuzi sahihi na ndio kumwaga Lowassa rasmi wakijua atakwenda Chadema namagmba wengine hivyo chama kujisafisha najisi bila la maji. Kifupi ilikuwa kama mwaka 2010 wakati Chadema wakitegemea Sitta kujiunga lakini akachomoa dakika za mwisho! ikabidi Dr.Slaa atangazwe (tulikuwa sote pamoja). Ila tofauti baina ya Sitta na Lowassa ni kwamba mmoja ni Jinn na mwingine Shetani japo wote waliumbwa kwa moto!

Kwa hiyo usiseme haya ni mambo ya kipuuzi laa sivyo msingekuwa mnashangilia kiasi hiki tena mkitegemea Ushindi sijui wa nini halafu unasema Lowassa ana nguvu gani? Wewe nambie kama unaona Lowassa hana nguvu imekuwaje Chadema waache mbachao kwa msali huu upitao! maskini Dr.Slaa tena kwa matusi na aibu kama aloipata Lowassa huko CCM leo watu muone sawa tu kazeeka, ni mzoga kisiasa lakini huyu huyu Lowassa alipomwagwa CCM mnasema kaonewa, Lowassa sii fisadi bali alikuwa kondoo wa kafara!

Jamani kondoo wa kafara ni Dr.Slaa ambaye kusema kweli sielewi kama Lowassa ana ushawishi wa kura za wananchi kuliko Dr.Slaa! Ila nachoweza kusema Lowassa ana mifeza na wafadhili na anaweza kabisa kununua chama na ndicho alichokifanya! kusema kweli hapo mmeniacha hoi na sijui kama Dr. Slaa naye akiamua kufanya kama alivyofanya Lowassa na kuhamia chama kingine mtasemaje? Mtamwita MSALITI? Mimi siungani nanyi kwa mara nyingine tena kwa sababu nakumbuka hotuba ya hayati mwalimu Nyerere juu ya kiongozi anayetaka kununua kura za watu ama kufadhiliwa!.
 
Zakumi

JF-Expert Member
Sep 24, 2008
4,858
2,000
Kitu ambacho najiuliza na sipati jibu ni kwanini Lowassa ana wafuasi wengi? Hivi ni pesa au ni ushawishi wake alionao kwa vijana au au?

Maana tukatae tukubali ndani ya CCM hakuna mtu mwenye wafuasi wengi kama Lowassa nasema hivyo kwa kuangalia mikutano yake mbali mbali (rejea mkutano wa Dar na vijana wa boda boda na mtu huyu hana record ya kusomba watu kwa mabasi) au wakati wa kutafuta wadhamini.

Hawa watu wanatafuta nini kwa Lowassa? ni kitu gani alichofanya ndani ya miaka 8 ambacho kinawavutia hawa watu?

Swala la pili, ni mgumu kumeza lakini ndizo siasa tunabadilika kutokana na wakati na kutona na watu wa jamii yako. Nafikiri watanzania uelewa wetu ni mdogo kuhusu swala zima la ufisadi na madhara yake.Hivyo basi watu walio wengi vijijini ukiwambia mambo ya ufisadi hawaelewi kabisa maana wao walishaona kuwa kuishi kwenye nyumba ya tope ni halali yao,kuna watu hata hawafahamu umeme ni nini au una umuhimu gani, kuna watu ambao hawaoni umuhimu kuwa na maji ya bomba wameridhika na maji ya visima ambayo utumia muda wa 1 mpk 6 kufuata maji. Visima vikakauka kwa ajili ya ukame wao hizo ni laana kutoka kwa mwenyezi Mungu. Na mtu wa jinsi hii kumpa elimu kuelewa kuwa umaskini wake unachangiwa na ufisadi au matumizi mabaya ya madaraka au rushwa ni ngumu. Na kwa bahati mbaya au nzuri hawa watu ndo wengi na ndo wanatuchagulia viongozi.

Sasa basi inapotokea watu wa jinsi hii wakataka mtu ambaye watu wengine wenye uelewa wa mambo wanaona huyu mtu hafai kwa sababu moja au nyingi, kuna kuwa hakuna ujanja tena bali kuwapa yule mtu ambaye wanaona anawafaa wao.
Na hiki ndicho kinachotokea Tanzania, na baadhi ya nchi za kiafrika.

Nachelea kusema uchaguzi wa mwaka huu kama Chadema wangemsimamisha DR,Slaa na CCM Magufuli, basi Mafuguli alikuwa anapata ushidi tena asubuhi ingawaje utendaji wa Dr. Slaa kwa hapa Tanzania hauna mfn. Record zake ziko safi kwa kila sehemu alipopita. na huu ndio ukweli na hii ndio gharama ya demokrasia,

Kwa maana hiyo watanzania hatupendi watu waadilifu tunapenda mafisadi, hivyo basi sisi sote ambao tunapingana na ufasidi na wale ambao hawana habari na ufisadi hatuna budi kuchagua kati ya fisadi mmoja (Lowassa) au mfumo wa kifisadi ambao ni CCM. Kwa bahati mbaya sana hata vyama vingine vya siasa vikaamua kumsimamisha malaika hakuna hatayempigia maana kama watu wangekuwa wanachukia ufisadi basi leo hii Kikwete hasingekuwa madarakani..

Wapeni watu mtu anayemtaka maana wao ndio wapiga kura husipowapa utashindwa katika sanduku la kura.

Kama watanzania wanamtaka Lowassa au la ngoja tuone huku mbeleni maana kwa ili sina uhakika kama ni mapenzi tu au ni nguvu ya pesa

Nilipata bahati ya kuhudhuria semina iliyotolewa na kitengo deliberative democracy. Moja ya hoja wanazotoa watu wa kitengo hicho ni kuwa katika jamii kuna watu wachache wanao-influence maamuzi ya kijamii.

Lowassa hakukaa kimya katika kipindi cha miaka 8. Alikuwa na kikundi cha Friend of Lowassa kilichoshiriki katika kampeni nyingi za chini kwa chini. Kama hawa watu walifanya kazi nzuri kwanini basi Lowassa asiwe na mvuto kwa jamii?

Sumaye alikuwa waziri mkuu kwa miaka 10. Baada ya hapo alikwenda Havard na kuchukua Masters. Lakini hakufanya kampeni yoyote ya kumfanya awe na mvuto katika jamii. Kuchukua Masters hakumsaidii mtu kuwa na mvuto. Na matokeo yake amebaki kama waziri mkuu wa zamani.

Mvuto wa Lowassa hauna tofauti na mvuto wa babu wa Loliondo.
 
TUJITEGEMEE

JF-Expert Member
Nov 6, 2010
15,417
2,000
Naona kaliamsha dude tena (Zitto). Mpaka sasa siungi mkono kauli za kutugawa watanzania
------------
Ukienda mkoa wa Kilimanjaro wana barabara mpaka vijijini ndani.

Kuna mwaka nilienda Kilimanjaro kuna mzee alisema kuna shule 50 za sekondari,lakini sisi Kigoma tulikuwa nayo moja tu.

Wale wenzetu wako mbali kimaendeleo...
Kwenye link hii hapa chini kuna clip yake akisema maneno hayo ni kuanzia dakika 23.40
Zitto Kabwe: Kuna kachama kana mdomo mdomo maana K/njaro wana maendeleo. Hamkuchagua mbunge zwazwa
 
MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
12,098
2,000
Ningependa kupata maoni ya Nguruvi3 kwa sasa katika muktadha wa bandiko lake hili kuhusiana na Zitto na ACT-Wazalendo katika dhana ya mpini wa CCM kumaliza upinzani nchini.
 
Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
13,752
2,000
Nguruvi3. Can you tell us now who's killing the opposition? Is that ACT or an invisible hand >
Yeah, nimeuona uzi, naomba yoyote mwenye comment, swali au chochote aeleze kwanza. Nipo na nitazungumzia suala na hoja zote kwa undani, kina na uyakinifu
 
MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
12,098
2,000
Nguruvi3. Can you tell us now who's killing the opposition? Is that ACT or an invisible hand >
Mkuu,
Swali lako ni fupi lakkni limebeba mjadala mpana sana.

"Mtaalam" wetu wa masuala ya kisiasa Nguruvi3 nadhani anaogopa urefu wa kina cha swali lako!

Tuendelee kusubiri labda anakusanya vielelezo!

Wahenga walisema "ukimya una mshindo"

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
13,752
2,000
Mkuu,
Swali lako ni fupi lakkni limebeba mjadala mpana sana.

"Mtaalam" wetu wa masuala ya kisiasa Nguruvi3 nadhani anaogopa urefu wa kina cha swali lako!Tuendelee kusubiri labda anakusanya vielelezo!Wahenga walisema "ukimya una mshindo"
Naam una mshindo! Nilichokisema nasimama nacho kwa ushahidi bila shaka.

Nilikuwa nasubiri kama kuna hoja nyingine nizipitie zote kwa ujumla

Kuanzishwa kwa ACT ilikuwa ni matokeo ya mtafaruku ndani ya Chadema.
Mtafaruku ulioanza kidogo kidogo kabla ya siri kufichuliwa na Mghamba baada ya kubainika anakiuza chama

Mtafaruku ulipelekea kufukuzwa kwa Zitto, Mghamba na Mkumbo Kitila na kuanzisha ACT-Wazalendo

Kabla ya hapo, tukiwa jamvini na siasa za nchi zikiwa huru tulimshauri Zitto kuwa na subira kwani muda ungetoa matokeo makubwa kuliko haraka alizokuwa nazo.
Watu walidhani ni 'ujana' wa Zitto bila kujua nini nyuma yake

Kile kilichoitwa 'waraka' kilifunua waliokuwa nyuma ya mpango huo akiwemo Mghamba na Prof Kitila

Walipounda ACT-Wazalendo, Mghamba, Kitila na Mwenyekiti Anna Mghwirwa walikuwa viongozi

Leo Kitila ni mwanachama mtiifu wa CCM. Mghamba ni mwanachama mtifu wa CCM
Anna Mghwirwa ni mwanachama na kada mtiifu wa CCM. Albert Msando ni kada kindaki ndaki wa Lumumba

Wote hao walikuwa ni nguzo ya ACT Wazalendo ambao leo tunajua haikuwa ACT ilikuwa ni 'mpini' wa kumaliza upinzani ulioanzia ndani ya Chadema, ukahamia ACT.

Baada ya kushindikana, wakarudi ''nyumbani'' kuendelea na majukumu ya kawaida wakimwacha Zitto

Ukimtazama Zitto na historia yake utabaini alikuwa anatumiwa bila kujijua na makada wa Lumumba kama 'mpini' wa kumaliza upinzani.

Kumbuka shoka lenyewe ni Lumumba walipo akina Mghamba, Msando, Kitila na Mghwirwa

Mara baada ya kuondoka ACT-Wazalendo picha halisi ya Zitto imeonekana.

Akiwa katika chama kidogo, bado amekubali kushirikiana na wenzake aliokorofishana nao siku za nyuma, akiendeleza harakati za upinzani. Hii ni maturity ya hali ya juu sana na nampa big up

Kuna mahali hapa JF niliandika ' ACT inafanya kazi ya upinzani' kuliko chama kikuu cha upinzani Chadema
Hoja yangu ilijikita namna ACT inavyo react katika masuala ya kitaifa na kimataifa

Baada ya makada kurudi nyumbani na kupewa nafasi zao, nampa Zitto ''benefit of doubt'' , kwamba, kuna mahali alipotezwa hasa baada ya kubaini nyuma yake alizingirwa na team Lumumba iliyokuwa kazini kikamilifu

Kwangu mimi simuangalii Zitto kama ACT, namuangalia kwa hoja zake na mantiki.
Nakubaliana naye 100% akiwa sahihi na natofautiana naye 100% inapobidi kwa mantiki na hoja

Nikiangalia nyuma, ushauri wangu kwa Zitto ulikuwa sahihi kabisa, nilichoshindwa kuelewa ni nguvu kubwa iliyokuwa nyuma yake ikiwa imebeba agenda za mtaa mkubwa wa Lumumba.

Kuna wakati namuona kama 'victim of circumstances'

Sasa nasimama wapi na ACT? ACT hii ya 'one man show' Zitto ni bora sana kuliko ile ya 'Mpini' wa Lumumba
Imeonyesha kukua na kuimarika licha ya udogo wake. Imejidhihiri katika kauli na matendo

Naiangalia kama future opposition party endapo hakutakuwa na 'remnant' kutoka mtaa wa Lumumba
 
Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
13,752
2,000
Hakika siasa za Tanzania ni ngumu..

Miaka minne baadaye yametokwa mambo ambayo hakuna mtu yeyote angeweza kufiiria kama yanaweza kutokea..Siasa imekuwa ni uhasama. Watanzania tumepoteana..
Kama kuna eneo tulilorudi nyuma kama Taifa ni kushindwa kutumia siasa kwenda pamoja na uelekeo mmoja. Siasa imekuwa uhasama, chuki na hata kufikia kuondoa utu.
 
JingalaFalsafa

JF-Expert Member
Apr 13, 2012
761
250
Kama kuna eneo tulilorudi nyuma kama Taifa ni kushindwa kutumia siasa kwenda pamoja na uelekeo mmoja. Siasa imekuwa uhasama, chuki na hata kufikia kuondoa utu.
Kuondoa UTU. Na hilo ndilo kusudio Kuu la aina yoyote ya Umagharibi pale unaposhadadiwa kwa pupa. Ni kututoa katika UKUU WETU ili tubaki kuwa wanyonge tutawalike. Haya si Mapya ni Matokeo tarajiwa.

Mungu wetu yu vitani tayari!
 
Alinda

Platinum Member
Jun 26, 2008
1,690
2,000
Kabla Mwenyezi Mungu hajanichukua nilitamani kuona tunazalisha taifa la vijana wa kuhoji, vijana ambao si wa ndio mzee, vijana ambao si wapiga goti kwa watawala bali vijana ambao wanaheshima, busara na hekima lakini hapo hapo vijana ambao wanaweza kuhoji, kujenga hoja za msingi kwa manufaa ya taifa lao.

Matokeo yake tunarudi nyuma tunajenga taifa la ndio mzee, Taifa ambalo si la hoja tena bali vitisho, Taifa ambalo mawazo kinzani yanapewa tafsiri ya uadui, Taifa ambalo mtu kutoa maoni yake anafikiria mara mbili mbili.Taifa ambalo maongezi ya kawaida kabisa yanarekodiwa na kusambazwa, Taifa ambalo viongozi wanategemea mtu mmoja ndo awe.muamuzi wa kila kitu kwa kuogopa/kudhubutu kuchukua maamuzi ambayo hata mbeleni wakiulizwa basi wanaweza kusimama na kuyatetea. Kumbe yalikuwa matumaini hewa.

2020 katika uchaguzi mkuu tukibahatika kupata hata wabunge 5 wa vyama vya upinzani basi itakuwa ni bahati ya mtende.

Hayo ndo matokeo ya taifa la ndio mzee'

..
 
Alinda

Platinum Member
Jun 26, 2008
1,690
2,000
Kabla Mwenyezi Mungu hajanichukua nilitamani kuona tunazalisha taifa la vijana wa kuhoji, vijana ambao si wa ndio mzee, vijana ambao si wapiga goti kwa watawala bali vijana ambao wanaheshima, busara na hekima lakini hapo hapo vijana ambao wanaweza kuhoji, kujenga hoja za msingi kwa manufaa ya taifa lao.

Matokeo yake tunarudi nyuma tunajenga taifa la ndio mzee, Taifa ambalo si la hoja tena bali vitisho, Taifa ambalo mawazo kinzani yanapewa tafsiri ya uadui, Taifa ambalo mtu kutoa maoni yake anafikiria mara mbili mbili.Taifa ambalo maongezi ya kawaida kabisa yanarekodiwa na kusambazwa, Taifa ambalo viongozi wanategemea mtu mmoja ndo awe.muamuzi wa kila kitu kwa kuogopa/kudhubutu kuchukua maamuzi ambayo hata mbeleni wakiulizwa basi wanaweza kusimama na kuyatetea. Kumbe yalikuwamatumaini hewa.

2020 katika uchaguzi mkuu tukibahatika kupata hata wabunge 5 wa vyama vya upinzani basi itakuwa ni bahati ya mtende.

Hayo ndo matokeo ya taifa la ndio mzee'

..
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom