Duru za biashara za mtandao: Kuna dalili za watu kulizwa huko kwenye soko la forex, wajuzi wa haya masuala njooni huku

Cannabis

JF-Expert Member
Jan 20, 2014
8,943
25,284
Wakuu hii nawaletea baada ya dogo fulani kunitafuta huku amefura analalamika ameingia kwenye biashara ya kudownload pesa na kampuni fulani inaitwa 360 Capital na kushindwa kutoa pesa zake. Nikazama kwenye mitandao ya kijamii na kuitafuta kiundani maana jina lake ni kama niliwahi kulisikia.

Katika pita pita zangu nikaiona ni Kampuni iliyoanzishwa na kijana wa kitanzania mpambanaji na mtafutaji almaarufu kama jina fulani la mji fulani huko Canada, wakongwe wa humu mtakuwa mmeshamjua.

Sasa nikazama zaidi kwenye page zao za instagram na twitter na kukuta malalamiko ya wa wadau wengine kuwa wanashindwa kutoa hela (withdrawal) kwa uelewa wangu mdogo wa forex ni kama wameingiza hela na kufanya trading sasa faida waliyoipata haitoki...na wengine wanasema akaunti zao zilizokuwa verified zimeondolewa hiyo status.

Hapo nikaishia kucheka tu na kumwambia dogo hiyo hela yake afanye kuachana nayo, labda kama kuna technical issues tu za kiungwana baadaye anaweza kuipata, ila kwa historia ya huyu mtafutaji kuna uwezekano mkubwa imeshaondoka.

Nimeweka baadhi ya screenshot za wadau hapo chini , natoa tu angalizo hii si kwa ajili ya kuchafua biashara ya mdau yoyote bali ni kutoa tahadhari, huyu dogo nilimuonya kuhusu kufanya hizo biashara kama hana uelewa wa kutosha akanivimbia nikamuacha afanye kitu roho inataka, pia natoa angalizo kwa wabongo kama mnaanzisha biashara mtandaoni basi jitahidini kuweka technical issues sawa, kama mambo yakienda vibaya hakuna mfumo utakaofanya kazi at 100% siku zote basi mijitahidi kutoa mawasiliano na kujibu wateja wenu kwa haraka, kukaa kimya huku watu wanashindwa kupata huduma kunatengeneza picha kwamba wamepiga, bado naendelea kufuatilia maendeleo ya hii kitu, kama kuna wadau mnajua kinachoendelea njooni huku mtujulishe, mjini kuna mambo mengi na muda ni mchache
IMG-2021-11-11 11-40-04.png

IMG-2021-11-11 11-40-16.png

IMG-2021-11-11 11-40-39.png

IMG-2021-11-11 11-40-57.png

IMG-2021-11-11 11-41-02.png

IMG-2021-11-11 11-41-19.png

IMG-2021-11-11 11-41-27.png

IMG-2021-11-11 11-41-38.png

IMG-2021-11-11 11-43-43.png

IMG-2021-11-11 11-44-18.png

IMG-2021-11-11 11-45-15.png

IMG-2021-11-11 11-46-32.png

IMG-2021-11-11 11-40-47.png

IMG-2021-11-11 11-44-29.png
 
Hype imekuwa kubwa sana hasa huko Twitter,mambo ni magumu sana huko kwenye hizo forex ands their likes.
Wapo wachache sanaaa waliootea na kutoboa ila wengi wampigwa na vitu vizito na kuishia kuwa broke.
Kaa kitaalam hakuna mtu anauchungu na pesa yako hata kama ni kidogo
 
Huwa nashangaa sana watu wanaomkejeli sana huyo kijana, kiukweli simtetei lakini namuunga mkono katika suala la uthubutu, pia kama anafanya utapeli kwa nini vyombo vya Dola havimshugulikii au na wao nisehem ya dili zake, pia mkuu naona umescreen shot ujumbe wa wiki MOJA/mbili zilizopita, vipi ujumbe waleo.

Kitu cha ziada kama kijana anafata taratibu zote nakutapeli watu kwa mujibu wa sheria basi nampongeza maana serikali haimchukulii hatua .
 
naona mahasimu wa Jeff mmnaendeleza pale mlipo ishia wazee wa infinoxx

mna ng'ata na kupuliza wawekezaji wa machimbo ya dhahabu chunya
 
kuna dogo alinijia na mahesabu ya excel jinsi atakavyokuwa ana "danlodi" hela na ku "akumuleti" faida mpaka mwisho wa mwaka atakuwa dolari laki kadhaa za kimarekani..nikajaribu kumkumbusha msemo wa lugha ya malikia if it is too good to be true it probably... hakunielewa kabisa akachukulia kama namuonea wivu mafanikio yake....sijamsikia tena kitambo kuhusu kudanlodi hela...
 
Huwa nashangaa sana watu wanaomkejeli sana huyo kijana, kiukweli simtetei lakini namuunga mkono katika suala la uthubutu, pia kama anafanya utapeli kwa nini vyombo vya Dola havimshugulikii au na wao nisehem ya dili zake, pia mkuu naona umescreen shot ujumbe wa wiki MOJA/mbili zilizopita, vipi ujumbe waleo.

Kitu cha ziada kama kijana anafata taratibu zote nakutapeli watu kwa mujibu wa sheria basi nampongeza maana serikali haimchukulii hatua .
Humlaumu kijana wakati unaona vijana wenzio wamesuuzwa toka mwaka 2017 na ngonjera za ku download pesa humu😂!!!

Kijana amehamia kwenye ghorofa mkabala na Mlimani City baada ya kuwanyoosha kwa usajili wa TMT au “The Money Team” wale magwiji wa JF akiwemo Maxence Melo mwenyewe 😂 kipindi kile yupo pale Jangid Plaza na kuendesha campaign zake za Forex kwamba msome vitabu sana ila mlipie training na huduma ya signals!

Sasa baada ya kukinukisha Jangid plaza na wana usalama kuanza kumjazia nzi amehamishia goli sam nujoma road mkabala na mataa ya kuelekea sinza makaburini😅 na kubadilisha jina toka TMT na kujiita 360” Capital!

Kijana anapush Jaguar matata sana huku akiendelea kuwanyenga vijana wazembe wazembe kwa matumaini kuwa crypto currency itawatoa kimaso maso! Review nyingi za mtandaoni insta ni kwamba kijana anawa inspire sana yani na lifestyle yake ya ki motivesheno speaker! Anaonekana katoboa sana yani 😂😂😂

Ushauri wangu ni kwamba hakuna pesa rahisi jamani😅 pesa ni ngumu sana! Forex wala cryptocurrency zitakufilisi tu ni mavitu yanayotaka uwe na mapesa ya mchezo ni kama kamari tu za kiuchumi zile😅
 
Mimi nilichukua changu mapema nikaishia tangu mwezi wa 9 baada ya kuona brokerage haiishi matatizo 😂😂nimemuachia hiyo usd 1.11

EA6A4271-CAB2-46FA-95B1-30C79B91D95B.png
 
Hivi bado hamjui tu kwamba hakuna hela rahisi, hela lazima uparangane kuipata....Sasa vijana mnataka hela za kudownload tu..
 
Back
Top Bottom