SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 5,129
- 7,897
Pamoja na mapenzi kwa timu yangu, ila mara kwa mara sijasita kuja na malalamiko dhidi ya uongozi wa Simba na moja ya maeneo yanayokera wengi yanahusiana na treatment ya wachezaji wake kuanzia wale walio bora hadi wale ambao wanaonekana mchango wao umepungua mno na wanaigharimu timu. Imefika wakati unashangaa wachezaji walio bora wanapewa huduma mbovu ndani ya timu hadi kuachwa katika mazingira ya kutatanisha, halafu wale ambao viwango vyao vinatia mashaka ndiyo tunaaminishwa ndiyo tegemeo la timu.
Juzi nilikuwa naangalia video moja wakati Simba inakwenda Zanzibar, ukimsiklliza interview ya Aubin Kramo haupati picha kama ni mtu aliye na taarifa kuwa si tena sehemu ya kikosi cha Simba msimu huu. Ukimsikiliza Ahmed Ally anasema jina la Kramo liliondolewa ila anaendelea kulipwa stahiki zake zote. Kama kuna mtu anabisha, mtu ajitokeze amuulize swali hili moja kwa moja Kramo mwenyewe kama anajua kuwa jina lake limeondolewa. Kama anasema anajua natoa 100,000 kwa mwandishi yoyote atakayepewa jibu hilo. Kwa mtazamo wangu Kramo alishapona ila kuna watu wamemkazia ili kulinda wachezaji wao. Majeraha ya Kramo hayakuwa ya kumkalisha nje muda mrefu kiasi hiki.
Huyu ni mchezaji mwingine ambaye msimu ukiisha ataachwa katika mazingira ya kutatanisha halafu ukamkuta upande wa pili anakiwasha. Hii ni story inayojirudia ya Moses Phiri, tulikuwa tunaambiwa hajapona hajapona, mara amepona ila ni maamuzi ya mwalimu kumtumia, mwisho wa siku mchezaji mwenyewe anaona huu ni upuuzi anaonyesha dalili za kutojali maana hata juhudi zake bado hazimpi namba tena, mara anakuja kuachwa. Kuna tatizo kubwa sehemu pale Simba ila hatutaki kulisema.
Kwa kumalizia, kwenye dirisha dogo lililopita kuna mchezaji mwenye sifa ya kuikaba timu ambaye mkataba wake ulikuwa umeisha kulingana na taarifa walizokuwa wametupa hapo kabla ila dirisha dogo likafungwa hatukuambiwa kama ameongezewa mkataba na usishangae mwakani tena tukawa naye huku kina Kramo wakiachwa.