Dunia ya giza nyuma ya kuta za mochwari

Dunia ya giza nyuma ya kuta za mochwari

GT tuonee huruma hali ngumu ya maisha inatupiga halafu tena hii dah?
ef41daea-fd38-43cb-b7b0-77dadd1d5964.jpeg
 
Babu yangu alifariki, nikapata taarifa saa saba usiku nikafika hospital ilikuwa tayari wamemhifadhi mochwari nikaingia kuhakikisha Kiukweli sikuwa na uwoga wowote kuingia mochwari ingawaje kulikuwa na maiti wengi sikuogopa kitu na nilirudi nyumbani nikalala vizuri tu bila hofu/shida yoyote.

Kesho yake asubuhi nikaamkia pia hospital kwa ajili ya kukamilisha taratibu zingine, mhudumu aliyekuwepo zamu asubuhi ni mdada mmoja mrembo ila kazi yake ni mochwari, ebana eeeeh hii asubuhi ndo sikutaka hata kuingia mochwari(nilikwepa). Huyu dada nili mrespect sana japo alinipa namba tukawasaliana kwa mengineyo lakini kiukweli huwa namuangalia kwa namna ya utofauti kidogo.
 
bad98342-6e9e-40fe-b635-efdf8c0dbef4.jpeg
 
Vu bin vu katika moja na mbili nikawa na ushikaji na kizee kimoja kichawi hatari kinachoaminika kuwa ndo kinashikilia kiti cha ukuu wa walozi wa huku kanda ya ****. Siku moja kulikuwa na mfanyabiashara mmoja mkubwa sana wa madini alikuwa amekuja na bonge la V8 mpyaaa. Baada ya kupata alichokifuata tukaendelea na stori zetu.

Kizee kile (ni cha kiume - 80yrs+) kikaniambia huyu dogo wa madini kafuata kakitu fulani na kaacha milioni 6 cash. Nilishangaa sana. Kitu gani cha hela nyingi hivyo? Ndiyo nikagundua kuhusu ishu za mochwari.

Kilisema dawa zingine zinakuwa ghali sababu ya vitu ghali vya kuchanganya. Kikasema kuwa dawa aliyofuata dogo wa madini siku ile eti ilikuwa inahitaji kisimi cha kichanga kilichofia tumboni. Na upatikanaji wake ni mgumu balaa. Wanachofanya waganga wengi ni kuwahonga wahudumu wa mochwari ili wapatiwe viungo wanavyovihitaji. Kipande cha ulimi wa kichaa, damu ya mwanamke aliyefariki akiwa kwenye hedhi, vidole vidogo vya maiti mapacha na mengine mengi ya kutisha. Kikasema chenyewe huwa kina watu wake mochwari moja katika hospitali kubwa huko kanda ya **** na kwamba huwa kinawauzia waganga wengine baadhi ya viungo hasa vile vya nadra sana. Watu mashuhuri, wachawi na waganga wakubwa, mamanju, vichaa, watu wenye vipaji, watoto wadogo...viungo vyao mbalimbali hutafutwa sana katika ulimwengu wa giza na vingi huibwa huko huko mochwari - na vingine huchukuliwa kichawi. Ndiyo nilijua kuwa kuna ulimwengu wa kutisha sana ambao hatuuoni na kuna watu wanafanya mambo ya ajabu sana hapa duniani.

Hii ilikuwa miaka ya nyuma kidogo na yule dogo wa madini kwa sasa ni tajiri mkubwa ana mahoteli (siyo lodge), mabasi na malori ya mizigo kibao japo ndo anaitafuta 40s. Tunafahamiana na nilipomkumbusha kuwa nilimwona siku ile kule kwa kile kizee alicheka sana. Mwaka jana aligombea ubunge lakini bahati mbaya alianguka kwenye kura za maoni.

Kuna dunia nyingine kabisa watu wanaishi aisee na mochwari huko nilipaogopa sana tangu siku ile japo siku moja hata mimi nitaingia huko maana katika hali ya kawaida hakukwepeki! 😭😭😭

View attachment 3599874
Kuna dunia nyingine kabisa watu wanaishi aisee na mochwari huko nilipaogopa sana tangu siku ile japo siku moja hata mimi nitaingia huko maana katika hali ya kawaida hakukwepeki!✍🏿
 
Back
Top Bottom