Dunia: Jela ya Wenye Ufahamu lakini Paradiso la Wajinga...

Dunia: Jela ya Wenye Ufahamu lakini Paradiso la Wajinga...

SankaraBoukaka

JF-Expert Member
Joined
Jul 2, 2019
Posts
3,564
Reaction score
5,645
Dunia imekuwa kama jela kwa wale wenye ufahamu wa kina. Wenye akili na macho ya ndani huona udanganyifu, uovu, na unafiki unaotawala jamii.

Kwao, maisha si mchezo wa furaha bali ni mzigo wa maswali yasiyo na majibu. Wanateseka kwa kuona ukweli ambao wengine wanaukwepa.

Ufahamu wao unawafanya washindwe kufurahia mambo madogo, kwa sababu wanatambua udhaifu wa mifumo ya kijamii, kisiasa na kiroho.

Kwa upande mwingine, wajinga huishi kana kwamba dunia ni paradiso. Wanafurahia bila kujali... na kusherehekea bila kuhoji wanachokiona hakipo sawa.

Wajinga hawana mzigo wa tafakuri nzito, hawajali kuhusu udanganyifu wa viongozi, au mateso ya wanyonge. Kwao, maisha ni rahisi: kula, kunywa, kucheka na kulala bila kujiuliza kesho kunakuaje....

Kutojua kwa wajinga
huwapa amani ya muda, kana kwamba wako peponi lakini uhalisia hawajui maumivu yatakayowapata wao au vizazi vyao vijavyo....
 
Hadi kulijua hilo maana yake yuko jela..

Nawe kushindwa kujua kama yuko jela maana yake wewe uko paradiso...
Mkuu humu ndani kuna watu hawana akili kwa kiwango ambacho hatukukidhania kabisa!
JF is no longer a home of great thinkers
 
Mfano mwepesi tu kwa atakayeshindwa kumuelewa jamaa anachomanisha muangalieni mtu kama Lissu!

Ana kila kitu pesa elimu kichwani kazi muda wowote zinamtafuta but anavyoona wanayoyafanya viongozi yanamkereketa kiasi anaona vyote alivyo navyo havina maana ila maskini wa nchi hii hawaelewi chochote wao ni simba vile yanga hivi diamond hivi zuchu vile.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom