Dunia ina mambo mengi ya kushangaza

Hivi zamani huko kabla ya sayansi wazee waliwezaje kujua mimea tiba na magonjwa yanayotibu?
Sio wazee tu hawa wanyama kama paka mbwa na wanyama pori wanajua kwa trial & error
 
Reactions: Lax
Kwa sababu unahisi nilichokuuliza ndio ulichojibu kumbe sivyo, ila acha nisikuchoshe.
 
Chai
 
Uchawi ungekuwepo kweli na ungekuwa unafanya kazi kweli, Africa ingekuwa bara tajiri sana.

Kila mwafrika angetajirika kupitia huo uchawi.

Uchawi siku zote una aminiwa na watu wajinga na watu duni maskini.
Una amini kuhusu Mungu?
 
Vp kuhusu bahati mbaya?
Ni kama vile
Sharif Majini alivyodunguliwa risasi akiwa barazani kwake wakati hakuwa katika maandamano, zaidi sana alikuwa timu October tunatiki,
Ni kama vile unavyoweza kuwa umesimama au unatembea kando ya barabara gari au pikipiki ikapoteza uelekeo ikaja kukuparamia ikabidi ukatwe mguu na uwe kilema wa kudumu,
Ni kama gari zinavyopata ajali wengine wanakufa au kuwa vilema huku wengine wakitoka wazima kabisa,
Ni kama vile unavyoweza kukamatwa na police ukawekwa mahabusu au ukahukumiwa kifungo magereza hata miaka 10 kwa kukutwa sehemu isiyo sahihi kwa wakati usio sahihi au hata kwa kusingiziwa tu kesi,
Ni kama vile anavyoweza kuja jiwe na sera ya kupambana na wafanyakazi hewa ukapoteza kazi yako kwa sababu tu majina kwenye cheti chako cha kuzaliwa yalitofautiana na cheti chako cha kidato cha nne,
 
Tukileta hayo makisio ya uchawi si ndio huwa mnasema ni mambo tu tusiyoyajua ila sio uchawi?
Kwa sababu ni makisio dhaifu sana , makisio ya historia na evolution watu wanayosoma wanayafanyia utafiti na bado wanaacha mlango wazi kwa mawazo mbadala ukosoaji na hata kurekebisha ikibidi, sio kama nyie wachawi ambao tayari mmeshafikia conclusion na ni experiences zenu binafsi tu.
 
Kwani wewe ulikubali aliposema Tanzania ipo vizuri kiuchumi kushinda Marekani?
nadhani alisema inafanya vizuri, sio ipo vizuri --- nchi tajir hizo kukua kiuchumi mara nyingi zinakua kwa asilimia ndogo ukilinganisha za kwetu kwa indicators zilizopo bongo ilikua na asilimia nyingi so ni sahihi
 
Vp kuhusu bahati mbaya?
zipo pia ni chances tu yani leo hii mtoto akizaliwa gaza hapo baada ya miaka mi5 kina netany wakipiga bomu, imagine kuna wadau wengi sana duniani wanafurahia, ila ukizaliwa hapa bongo probability ya kukumbana na bomu ni almost haipo
 
Shida ni kushindwa kuelewa kwamba kuna mchawi na kuna uchawi, hao ambao sijui wanaingia nyumba za watu kimazingara ni wachawi na ndio nasema sijawahi kuona mtu akijitambulisha mchawi akaeleza hayo mambo yao ya kichawi hata humu hutoona akija mtu aseme yeye ni mchawi na kuanza kujielezea.

Navyoelewa mie uchawi yeyote anaweza kuufanya maana ni ujuzi tu wa kujua ukifanya hivi na vile inapatikana athari gani, lakini mchawi kabisa tunakuwa tunazungumzia kitu chengine.

Halafu mkuu sijui kwanini umeshikilia sana hilo suala sijui wakoloni na kuiba bank, unachokifanya ni kukataa yale matukio yenye kuhusishwa na uchawi iwe wizi, kupata mali au kusababisha madhara kwa hoja ya kwamba ni story tu hazina ushahidi halafu unaenda kuchagua matukio ambayo hujawahi kusikia yakifanyika yakihusishwa na uchawi ndio unataka et hayo matukio kuwa ndio ushahidi wa kutokuwepo uchawi hii mie inanishangaza kwa kweli kwa sababu haueleweki unatafuta ukweli wa uchawi au ufanisi ama nguvu ya uchawi?

Kwa sababu hata sasa wapo watu wanaamini uchawi ila yapo mambo ambayo hawaamini kama huwezekana kwa njia ya uchawi.
 
Mtu kusema uchawi haupo pengine ni kutokana na taarifa alizonazo za masimulizi ya huo uchawi.

Mfano: Tukio la Mlandizi (2018) ambapo mwizi alidaiwa kushindwa kutua kiroba cha mahindi kwa sababu ya uchawi. Baadaye ilibainika kuwa ilikuwa ni maigizo yaliyopangwa, si uchawi.


Ikiwa tukio linaweza kupangwa na kuonekana kama uchawi, je, si inawezekana matukio mengine pia ni hadithi zilizopangwa au tafsiri zisizo sahihi?

Mtu anajiuliza, kwa nini matukio ya uchawi mara nyingi hayana ushahidi wa kisayansi au video halisi, bali simulizi za watu?

Mtu anayedaiwa kuwa mchawi huwa anatajwa kuwa na sifa hizi

  1. Uwezo wa kupotea bila kuonekana
  2. Ana uwezo wa kwenda mahali popote kwa sekunde tu.
  3. Ana uwezo wa kujua hatari inayokuja (machale)
  4. Ana uwezo wa kumdhuru mtu bila hata kumfikia (kumloga kwa kumnuia maneno)
  5. Ana uwezo wa kuiba pesa zako remotely bila kufanya robbery (chuma ulete)
  6. Ana uwezo wa kujibadilisha na kuwa kiumbe mwingine au hata kuwa jiwe (non living)
Kama kweli mtu ana uwezo wa kuiba pesa bila kuonekana, kwanini bado anaishi maisha ya umaskini? Kwa nini wachawi hawajulikani kama mabilionea?

Ikiwa wachawi wana uwezo wa kujua hatari kabla haijatokea, kwa nini mara nyingi wao ndio wanaoshukiwa na kufa kwa mateso au kunyanyaswa kijamii?

Kwanini wengi wanaoodaiwa kuwa wachawi ndio wanaoongoza kuishi maisha mabovu bila mali, bila elimu, bila afya bora nk.?

Kwa sifa wanazodaiwa kuwa nazo, wangepaswa kuwa na maisha bora kuliko watu wa kawaida. Ndio maana mdau anaona kama uchawi ungekuwa kweli, Afrika isingekuwa maskini. Wachawi wangeweza kutumia nguvu zao kuondoa umasikini na kujiendeleza.

Ushaajiuliza kwanini uchawi unadaiwa kuwepo zaidi katika jamii maskini kuliko katika jamii zilizoendelea?

Hapo ndio hoja ya mdau ilipo.
 
Kwa nini siku hizi baada ya smartphones kuwa nyingi na nyumba nyingi mjini kuwa na CCTV cameras hakuna tena zile habari za wachawi kuanguka kutoka angani kwa ungo, habari zilizokuwa zinatoka kila siku kwenye magazeti ya Shigongo??
 
Uchawi ungekuwepo kweli na ungekuwa unafanya kazi kweli, Africa ingekuwa bara tajiri sana.

Kila mwafrika angetajirika kupitia huo uchawi.

Uchawi siku zote una aminiwa na watu wajinga na watu duni maskini.

Hauna tofauti na dini yoyote ile
 
zipo pia ni chances tu yani leo hii mtoto akizaliwa gaza hapo baada ya miaka mi5 kina netany wakipiga bomu, imagine kuna wadau wengi sana duniani wanafurahia, ila ukizaliwa hapa bongo probability ya kukumbana na bomu ni almost haipo
Ni sahihi kusema kwamba neno bahati hutumika kumaanisha kukosa ujuzi wa kujua sababu za hayo matukio kutokea kwa namna yalivyotokea au yanavyotokea?
 
Reactions: Lax
hapo naweza kukubaliana na wewe kwa kiasi chake, kwa sababu wote tunataka kuwasikia hao wachawi ila inakua ngumu.

dhana ya ukoloni binafsi unaweza sema ndo kipimo changu cha juu sana kwa story za uchawi , kama tunaweza kukubaliana mtu anaweza tumia uchawi akamdhuru mtu mtu, akafanya aumwe, arukwe na akili, afe hapa afrika sidhani kama tungehitajika kubeba bunduki kupambana na mkoloni au wala tungehitaji kwenda UN kuomba uhuru wala kumuomba malkia uhuru --- magavana wa kikoloni wale na wanajeshi wao wangekua wanapigwa kipapai tu kweisha habari yao, sasa hapa hua kuna mgogoro kwa kua tunaambiwa haufanyi kazi katika namna hii --- na ukiuliza sasa unafanya kazi vipi , wanaoleta story za uchawi mara nyingi wanakimbia


mkuu story za uchawi tunazozisikia basi yawezekana hata wanaotupa hizo story na wao hawafahamu wanachosema --- kama tutakubaliana hapo litakua jambo jema.

bro uchawi mimi binafsi angekuja mtu akanipa huu apa atleast huu wa story tulizozisikia hapa bongo tusingekua tunailalamikia serikali jambo lolote
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…