Dunia haina usawa

SEHEMU YA 01 -Erick Shigongo

“Mume wangu! Naomba unisamehe!”
“Nikusamehe! Mara ngapi? Nahisi hunijui! Sasa subiri.”
“Mume wangu naomba unisamehe! Sitorudia tena!”
“Eti hutorudia! Unanifanya mimi mjinga! Leo nataka nikuonyeshee, utajua kwa nini Mungu alianza kumuumba Adamu kabla ya Hawa.”

Zilikuwa ni kelele kutoka katika nyumba moja chakavu iliyokuwa katika Mtaa wa Tandale kwa Tumbo jijini Dar es Salaam. Watu waliokuwa wakipita nje ya nyumba hiyo, walisimama na kusikiliza kile kilichokuwa kikiendelea.

Hiyo haikuwa mara ya kwanza, kila siku kulikuwa na fujo ndani ya nyumba hiyo waliyokuwa wakiishi watu wawili tu, Godwin Mapoto na mwanamke mrembo aliyewahi kutikisa kutokana na urembo wake, Winfrida Michael.

Kelele zile ziliendelea kuwakusanya watu wengi nje ya nyumba hiyo. Wale waliokuwa ndani ya nyumba zao, wakatoka na kwenda kusimama karibu kabisa na nyumba hiyo.

Hakukuwa na mtu aliyediriki kuingia ndani kugombelezea kwani walimfahamu Mapoto, japokuwa alionekana kuwa mwanaume dhaifu, mwenye mwili mwembamba lakini alivuma kutokana na ubabe wake mtaani hapo.

Alikuwa mwanaume wa fujo, aliyetikisa kuanzia Kwa Tumbo, Kwa Mtogole, Yemen mpaka Mwananyamala kwa Manjunju. Watu wengi walikuwa wakimuogopa, jina lake lilikuwa likivuma sehemu kubwa kuanzia Tandale, Mwananyamala mpaka Magomeni Kondoa.

Alikuwa mbabe wa mtaa kiasi kwamba watu walihisi kwamba asingekuja kuwa na mwanamke mrembo kutokana na ubabe wake, lakini kitu kilichowashangaza ni kwamba alifanikiwa kumnasa msichana aliyekuwa na sura nzuri, ya kipole, umbo matata, Winfrida Michael, msichana aliyekuwa akikubalika katika Chuo cha St. Joseph alipokuwa akisomea biashara.

Chuoni hapo, Winfrida alitingisha kwa uzuri, kila mwanaume alikuwa akimzungumzia yeye, alipokuwa akitembea, watu walimfananisha na twiga huku macho yake yakiwa na mvuto mithili ya mwanamke aliyekula kungu.
Hakuwa msichana mwepesi, alikuwa mgumu, wanaume walimfuata na kumtaka kimapenzi lakini Winfrida hakukubaliana nao hata kidogo.

Kila walipokuwa wakizungumza naye, alionyesha tabasamu kubwa kiasi kwamba liliwapa matumaini wanaume wengi lakini jibu lake halikufanana na tabasamu alilokuwa akilitoa usoni mwake.
“Nimekuelewa,” alisema Winfrida.

Mara nyingi sana wanaume Bad boys wanakuwaga na bahati ya kupendwa na wanawake wale walio wagumu sana wenye misimamo na wazuri kupindukia...

Kama hivyo Winfrida alivyozama kwa huyo jamaa tukutuku, pigaji na babe...

Cc: mahondaw
 
SEHEMU YA 34

Hilo ndilo waliloambiwa na daktari, hawakutakiwa kumuona Irene kipindi hicho kwa kuwa tu hali yake haikuwa nzuri na baada ya kutolewa kwenye chumba cha upasuaji, haraka sana akahamishwa na kupelekwa katika chumba cha wagonjwa mahututi.

Hilo lilimuuma sana Mapoto, hakujua ni kwa jinsi gani angeweza kukabiliana na hali hiyo ambayo ilikuwa ni yenye kuumiza sana, mbali na hayo yote, pia hakujua ni kwa jinsi gani angeweza kumwambia mke wake juu ya lile lililokuwa limetokea.

Alimfahamu Rosemary, aliwapenda sana watoto wake, kwake, hao walikuwa kila kitu katika maisha yake, alijua kwamba kama angempa taarifa moja kwa moja basi hali ingekuwa mbaya zaidi na angeweza kumsababishia matatizo.

“Nitamwambia tu, ila sitotaka kumpa taarifa akiwa nchini Tanzania, ni lazima aje huku,” alisema Mapoto.
Siku hiyo walikaa hospitalini hapo, hawakuruhusiwa kumuona mgonjwa mpaka ilipofika majira ya saa 2:00 usiku ndipo wakaruhusiwa na kwenda katika chumba maalum alicholazwa mtoto huyo.

Walipomuona kitandani, kila mmoja alionekana kuumia mno. Irene alikuwa kimya kitandani pale, mdomoni alikuwa na mashine ya oksijeni iliyokuwa ikimsaidia kupumulia huku pembeni kukiwa na mashine nyingine ambayo ilikuwa ikionyesha mapigo ya moyo kwa jinsi yalivyokuwa yakidunda.

Mapoto na Godwin wakamsogelea Irene pale kitandani alipokuwa, walipomfikia, wakasimama na kumwangalia. Alikuwa kimya kabisa kiasi kwamba ilikuwa ni rahisi kusema kuwa tayari aliaga dunia, walikuwa kama wakimwangalia mtu ambaye tayari alikuwa amekwishafariki dunia.

“Irene…We came for you, open your eyes and look at us,” (Irene…tumekuja kwa ajili yako, fumbua macho yako utuangalie) alisema Mapoto huku akimwangalia mtoto wake kitandani pale.
Walihuzunika, waliendelea kukaa ndani ya chumba kile kwa saa mbili ndipo wakaondoka na kurudi nyumbani.

Hakukuwa na mtu aliyelala, kila mmoja alikuwa kimya, walimkumbuka Irene, kitendo cha kutokuwa ndani ya nyumba ile kiliwapa mawazo mazito mno.

Inahuzuniasha sana...

Cc: mahondaw
 
SEHEMU YA 51

Hapo alipokaa kwenye ndege alikuwa na mwanaume mmoja, alikuwa mtu mzima kidogo, walianza kupiga stori na kuzungumza mambo mengi. Walichangamkiana na mzee yule aliposikia kwamba alikuwa mwandishi wa habari, alifurahi zaidi.

“Nitataka kuanzisha gazeti langu la siasa, nadhani nitafanya mawasiliano na wewe ili uje kunipa mawazo juu ya nini cha kufanya,” alisema mzee huyo huku akiwa kwenye tabasamu pana.
Wakakubaliana, walipofika Dar es Salaam, ndege ikaanza kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere. Iliposimama, wakainuka na kuanza kuelekeea nje.

“Nina mizigo mingi sana, unaweza kunibebea mmoja hadi nje?” aliuliza mzee huyo.
“Hakuna shida.”
Wakaelekea sehemu ya kuchunguzia mizigo yao, walipoichukua, mzee yule akampa begi lake Matamshi ili amsaidie mpaka nje ambapo angechukua teksi na kuelekea nyumbani.

Huku akiwa na begi lile na kupiga hatua nje, ghafla akashtuka akisimamishwa na polisi wawili waliokuja mbele yake. Mzee yule hakusimama, aliendelea kupiga hatua kwenda mbele, na hata alipoitwa, hakugeuka.

“Simama hapo,” alisema polisi mmoja.
“Kuna nini?”
“Tunahitaji kukuchunguza!”
“Ili?”
“Tunahisi umebeba madawa yya kulevya!”
“Nimebeba madawa ya kulevya?”
“Ndiyo! Twende kwenye chumba kile,” alisema polisi mmoja na polisi wengine watatu kuongezeka.

Matamshi hakuonekana kuwa na hofu, alijua kabisa kwamba hakuwa muuzaji wa madawa ya kulevya, hakuwahi kuyatumia, hakutaka kupinga, akaondoka nao na kwenda kwenye chumba kimoja na kukaa huko.

Polisi wale wakaanza kuangalia mizigo yake, hakukuwa na kitu. Hapo ndipo walipoanza kulipekua begi lile alilopewa na mzee yule. Muda wote Matamshi alikuwa akitabasamu, alijijua kwamba alikuwa mtu msafi na hakuhusika kabisa na biashara hiyo haramu.

“Umejitetea sana kwamba hujabeba madawa ya kulevya, na haya ni nini?” aliuliza polisi mmoja huku akitoa mfuko wa madawa ya kulevya, Matamshi akapigwa na mshtuko, hakuamini kuona mzigo wa madawa ya kulevya ukitolewa ndani ya begi.

“Hapana! Huo mzigo siyo wangu! Ni wa mzee aliyeniambia nimbebee,” alijitetea huku macho yakiwa yamemtoka.

Akiwa pale hospitalini si palikua na Balozi Mapoto mke wake, Rais na watu wengine...

Nahisi kuna mchezo hapo utakua amefanyika kumdhibiti huyu mwandishi wa habari...


Cc: mahondaw
 
SEHEMU YA 54

“Doctor…tell us what is going on…you freaking us out…” (daktari tuambie ni kitu gani kinaendelea…umetutisha…) alisikika Mapoto nje ya chumba kile huku akigongagonga mlango, alionekana kuwa na hofu kubwa kwani kitendo cha kumuona daktari yule akikimbia kuelekea ndani ya chumba kile, alihisi kulikuwa na tatizo.

“Welcome back to the world,” (karibu tena duniani) alisema Dk. Phillips huku uso wake ukiwa na furaha tele.
***
Rais Bokasa alichukia, kitendo cha kumuona mwandishi Matamshi akielekea chooni na Mapoto alihisi kabisa kulikuwa na kitu kilichokuwa kikiendelea. Moyo wake uliwaka kwa hasira na muda wote alikuwa akimwangalia mwandishi huyo huku akionekana kuwa na hasira kupita kawaida.

Hakukuwa na jambo jingine la kufanya zaidi ya kumuua mwandishi huyo kwani aliamini kwamba kama angemuacha akafika nchini Tanzania na kupelekea taarifa juu ya kile kilichokuwa kikiendelea basi hali ingekuwa ya hatari na watu wangeshinikiza mwanasiasa huyo kuandika barua ya kujiuzulu.

Ilikuwa ni lazima amuue, hakukuwa na jingine ambalo lingetakiwa kufanyika zaidi ya hilo. Akawapanga watu wake kwa ajili ya kummaliza kwa sababu tu alitaka kutetea kiti chake cha urais.
“Mkuu! Hatutakiwi kumuua! Nilikuwa na wazo moja,” alisema kijana wake aliyekuwa amempa kazi hiyo.

“Lipi?”
“Tumfunge. Tukifanikiwa katika hilo, basi tumemuweza. Kama tukimuua, kuna watu watahisi kwamba wewe ndiye umehusika, huyu ni lazima tumfanyie kitu ambacho kitawafanya watu kutokugundua kitu chochote kile,” alisema kijana huyo aliyeitwa kwa jina la Edson Pius.

“Sawa. Tutamfunga vipi?”
“Tumuwekee mzigo wa madawa ya kulevya, akifika uwanja wa ndege, akamatwe!” alishauri.
“Tutamuwekeaje?”
“Hapo ndiyo uniachie mimi!” alisema Edson.

“Sawa.”
Alimuamini kijana huyo, alikuwa miongoni mwa watu waliokuwa na uwezo mkubwa wa kufikiria, kazi hiyo akaiacha mikononi mwake kwa kuamini kwamba ingefanikiwa haraka iwezekanavyo.

Edson akamuandaa mwanaume mmoja ambaye alitakiwa kuondoka nchini Tanzania na kwenda Marekani haraka sana, huko alikuwa na kazi ya kurudi na mzigo mdogo wa madawa ya kulevya.

Sasa je... nilijua tu Rais lazima atafanya kitu...

Isingekua raisi kumuachilia yule muandishi wa habari kirahisi rahisi hivi... arudi na ukweli wote, wakati kwa kiasi fulani ameshaanza kufanikiwa...


Cc: mahondaw
 
SEHEMU YA 77

Ilikuwa ni barua fupi iliyompa taarifa kwamba alitakiwa kunyang’anywa nyumba aliyokuwa akiishi kwa kuwa mume wake aliiweka kama dhamana alipokwenda kuchukua mkopo wa shilingi milioni mia tano benki.

“Mkopo? Mume wangu alichukua mkopo? Lini?” alijiuliza swali hilo bila kupata jibu.
Alichanganyikiwa, hakuamini kama huo ulikuwa ukweli, alimfahamu mume wake, walipanga mipango pamoja, waliambiana kila kitu kilichokuwa kikiendelea, ilikuwa vigumu kwa mume wake kuchukua mkopo benki pasipo kumwambia, akahisi kwamba kulikuwa na kitu, alichokifanya ni kuwasiliana na mwanasheria wake.

“Umepokea barua kutoka Benki ya Watu?” aliuliza mwanasheria huyo aliyeitwa kwa jina la Emmanuel Makange.
“Ndiyo!”
“Inasema kwamba mumeo alichukua mkopo wa milioni mia tano kwa kuiweka dhamana nyumba yenu?” aliuliza Makange.

“Ndiyo!”
“Hebu niione!”
Akapewa barua hiyo na kuanza kuiangalia, ni kweli ilitoka katika benki hiyo, kulikuwa na sahini ya mkurugenzi wa benki hiyo na muhuri, ilionekana kuwa barua halisi iliyotoka katika benki hiyo.

Alichokifanya mwanasheria huyo ni kuondoka na kuelekea huko benki, alitaka kupata ukweli juu ya barua hiyo, alipofika, akaomba kuonana na mkurugenzi na kumwambia kile kilichokuwa kimetokea na mkurugenzi huyo kuthibitisha kwamba kweli Bwana Mapoto alichukua mkopo na aliahidi kurudisha mwezi huo.

“Hapana! Mzee asingeweza kufanya kitu pasipo kumshirikisha mama,” alisema Makange.
“Labda alifanya hivyo kwa ajili ya kimada wake, angemshirikishaje mama?” aliuliza mkurugenzi huyo.

“Hapana! Hakuwa mtu wa hivyo!”
“Wewe ni mwanaume! Hivi kweli inawezekana kuwa na mtu aliyekosa kimada? Usiusemee moyo,” alisema mkurugenzi huyo.

Hakuishia mahali hapo, ili kumuaminisha kwa kile alichokuwa amemwambia, akamtolea na nyaraka nyingine nyingi ambazo zilionyesha kwamba Bwana Mapoto alichukua mkopo huo ndani ya benki hiyo.

Hawakuishia katika nyaraka zilizokuwa kwenye makaratasi tu bali akamchukua na kumpeleka katika kompyuta na kumuonyeshea kila kitu ambacho alitakiwa kukiona.

Emmanuel alichanganyikiwa, aliangalia sahini, ilikuwa ni ya Bwana Mapoto. Akarudi nyumbani kwa Rosemary akiwa hana nguvu kabisa, alichoka, alichokiona kule benki kilimshtua sana.

Hapa kuna harufu ya utapeli... hili sakata litakua limetengenezwa...


Cc: mahondaw
 
SEHEMU YA 81

Alikuwa na mawazo tele, ubongo wake ulikuwa ukifikiria kupita kawaida. Alipewa muda wa mwezi mmoja kukamilisha deni alilokuwa akidaiwa, hakujua ni mahali gani ambapo angepata kiasi kikubwa namna hiyo na kukilipa.

Alijaribu kuwasiliana na ndugu zake wengine, wote walipogundua tatizo alilokuwa nalo, hata simu hawakuwa wakipokea. Hakuchoka, aliendelea kuwatafuta lakini majibu yalikuwa yaleyale.

Wakati zikiwa zimebaki siku kumi, akajaribu kumpigia simu Edward kwa ajili ya kumuomba msaada wa kisheria zaidi lakini kitu cha ajabu kabisa, mwanaume huyo hakuwa anapokea simu zake na hata alipokuwa akimtafuta ofisini kwake, mwanaume huyo alijifanya kuwa bize na kutokuwa na muda wa kuzungumza na mtu yeyote yule.

Hilo lilimuuma mno moyoni mwake. Edward, mwanaume ambaye kila siku alimwambia kwamba angepigana naye kwa moyo mmoja leo hii hakutaka kupokea simu zake na mbaya zaidi hata alipokwenda kumuona ofisini kwake, hakutaka kabisa kuonana naye.
Hakujua cha kufanya, akarudi nyumbani kwake na kutulia sebuleni. Kila alipokuwa akiwaona watoto wake, mawazo yake yalikuwa ni juu ya maisha ambayo wangeishi baada ya nyumba hiyo kupigwa mnada.

Alikitegemea kiasi cha shilingi milioni mia mbili kilichokuwa kwenye akaunti yake, akahisi kwamba hicho kingemsaidia kuyaendeleza maisha yake, angenunua nyumba ya kawaida kuendelea na maisha yake na watoto wake.
“Mama nimerudi tena!” alisema mwanaume mmoja aliyemfuata nyumbani kwake.

“Eeh! Jamani! Kuna nini tena?”
“Nimekuletea barua!”
“Nyingine?” aliuliza huku akionekana kushangaa.
“Ndiyo! Hii hapa!”

Mwanaume yule akampa barua hiyo. Rosemary alibaki akitetemeka, hakujua ni kitu gani ambacho angekutana nacho katika barua ile. Alipoifungua, maneno ya kwanza aliyokutana nayo ni kuhusu kufungwa kwa akaunti yake ya benki ya mume wake.

“Nini? Wanafunga akaunti?” alijiuliza huku akishtuka kupita kawaida.
Akasoma maelezo kwa kirefu. Benki hiyo iliyokuwa ikimdai mumewe ilieleza kwamba kwa kiasi cha shilingi milioni mia mbili kilichokuwa benki kilitakiwa kuchukuliwa chote na kisha nyumba hiyo kuuzwa kwa bei ya kawaida kwa ajili ya kupata hata nusu ya fedha walizokuwa wakimdai.

Inasikitisha sana...


Cc: mahondaw
 
SEHEMU YA 86

Hakuwa mtu wa siasa lakini hakuwa akiipenda serikali ya Chama cha Labour ambacho kilikuwa madarakani ambacho kazi yake kubwa kilikuwa ni kuwabana wafanyabiashara kwa kuwaongezea kodi.
Alikichukia chama hicho na hivyo kuwekeza nguvu zake kukisaidia chama pinzani cha Tanzania national Party kilichokuwa kimemuweka mwenyekiti wa chama hicho, Edward kuwa mgombea wa chama hicho.

Hawakushinda, walishindwa vibaya na hivyo Bokasa kuendelea kuiongoza Tanzania kwa miaka mingine mitano. Alikasrika, hakutaka kukiona chama hicho kikiendelea kuwa madarakani, aliawaandaa watu wake kwa ajili ya kufungua kesi ili kuyapinga matokeo hayo katika mahakama ya kimataifa lakini ilishindikana na hivyo kuamua kuachana na siasa na kufanya biashara zake.

Kila kitu kilichokuwa kikiendelea kwa Rosemary alikifahamu, moyo wake ulimuuma mno, alijua fika kwamba Mapoto hakuwa amekopa fedha hizo bali kulikuwa na mchezo ambao serikali ulitaka kuucheza, kumfilisi mwanamke huyo na kumuacha akiwa hana kitu kabisa.

Hakutaka kuona hilo likitokea, na hata nyumba ilipopigwa mnada, yeye ndiye aliyeinunua kwa kumtumia rafiki yake, Othman Ngolisho ili kusiwe na mtu yeyote ambaye angegundua kwamba yeye ndiye aliyeinunua nyumba hiyo.

Hakuishia hapo bali alichokifanya ni kupanga mikakati ya kumsaidia Rosemary kwa kila kitu. Alijua kwamba kama angemuweka ndani ya nyumba ileile ilikuwa ni lazima serikali kufahamu kilichotokea hivyo aliamua kuachana naye lakini mwisho wa siku amsaidie kumtunza na kumfanyia mambo mengine.

Wakati Rosemary hajui ni kitu gani kingeendeleakatika maisha yake, akamtuma kijana wake kwa ajili ya kumpa taarifa mwanamke huyo kwamba kulikuwa na nyumba iliyokuwa Kimara Stop Over ambayo alikuwa ameandaliwa kwa ajili ya kuishi na familia yake.
“Ni ya nani?” aliuliza Rosemary.
“Bosi wangu!”

“Nani?”
“Si lazima umfahamu! Ila ni yeye ndiye ameamua kukusaidia,” alisema kijana huyo aliyejitambulisha kwa jina la Juma Hassani.
“Sawa.”

Wakati Juma akizungumza na Rosemary, kulikuwa na wanaume watatu waliokuwa wakimfuatilia, walijua kwamba kulikuwa na kitu, walihisi hivyo kwa sababu kila walipomwangalia, kijana huyo alikuwa akiangalia huku na kule.

Nilijua tu serikali bado ipo kwenye harakati za kuipoteza hiyo familia...

Big up sana kwa huyo mfanyabiashara aliyeamua kumsaidia Rosemary mke wa marehemu Balozi Mapoto...


Cc: mahondaw
 
Kuna wanaume washenzi acha tu!
Anamwandama mwanamke mpaka siku anaregeza ujue keshapata mwelekeo wa kula vitu!
Wanawake wana magumu sana kwa kiumbe hawa!
Ila hata kuna wanawake makatili

Sema Rose hajafanyiwa poa
 

Hapa umetetea mwanamke kupitiliza
Wako makatili wa aina zote
Tena ogopa wana wake makatili wanakuwaga hawafai
Inawezekana.....
Lakini mfumo dume wa kujiona wanaume wako juu ya mwanamke unachangia sana...akitaka kitu akanywimwa hapo anageuka kabisa!
Ila......
Mi siongei ..dunia hii ...
 

Hapa umetetea mwanamke kupitiliza
Wako makatili wa aina zote
Tena ogopa wana wake makatili wanakuwaga hawafai
Mwanamke hata liwa kamili wa kutupa lakini ukipata mwanamme saivi kwa mda sahihi anatulia kabisa ....
Tatizo hakuna wanaume wa hivyo siku hizi....suruwali nyingi tu...mikanda urembo!
 
Mwanamke hata liwa kamili wa kutupa lakini ukipata mwanamme saivi kwa mda sahihi anatulia kabisa ....
Tatizo hakuna wanaume wa hivyo siku hizi....suruwali nyingi tu...mikanda urembo!
Hahahahah
Unaamini mwanaume akiwa katili anaweza tulizwa na mwanamke?
 
Back
Top Bottom