Mine eyes
JF-Expert Member
- Apr 11, 2016
- 6,581
- 7,231
10%Hahahahah
Unaamini mwanaume akiwa katili anaweza tulizwa na mwanamke?
10%Hahahahah
Unaamini mwanaume akiwa katili anaweza tulizwa na mwanamke?
Wanawake sku hizi hawapo wa kufanya hvo
Wameteseka sana sasa wamekuwa sugu...Wanawake sku hizi hawapo wa kufanya hvo
Wengi wazinguaji ndio maana unaona kila mtu roho mkononi mwake
SEHEMU YA 103
Moyo wake ukawaka kwa hasira, alijua dhahiri kwamba kulikuwa na mtu aliyesababisha hayo yote. Roho ya kichungaji aliyokuwa nayo, ikatoka, akagubikwa na hasira nzito, hasira ya kisasi ambayo aliamini kwamba ni lazima ahakikishe wale waliowafanya kuwa katika hali ile wanakufa mara moja.
Hakutaka kuwa na huruma tena, aliikumbuka mistari kadhaa ya Biblia iliyohusu ghadhabu kali ya Mungu kwa mtu atakayelipiza kisasi, alijua fika kwamba kisasi chochote kile kilitakiwa kuachwa kwa Mungu aliye hai.
Hakutaka kukubali, aliona kama Mungu akichelewa kulipa kisasi, iwe isiwe ilikuwa ni lazima kulipa kisasi kwa mikono yake mwenyewe.
“Mungu! Nimekutumikia tangu nikiwa mdogo, nilitamani sana niwe mchungaji kama Bonke, ila siwezi, sitaki kuwa mchungaji tena, ni lazima niwe muuaji kwa kila mtu aliyemfanya mama yangu kuwa katika hali hii,” alisema Godwin kwa hasira huku machozi yakimtoka.
Walipaswa kumsaidia mama yao kazi ya kuuza genge. Kila walipokuwa wakitoka shuleni, walifikia kuuza genge. Mwanzoni walijisikia aibu lakini kadiri siku zilivyozidi kwenda mbele, walizoea na hatimaye kukubaliana na hali halisi kwamba yale yalikuwa maisha yao.
“Amina! Natakiwa kurudi nyumbani haraka sana,” alisema Godwin, alikuwa akimwambia rafiki wake wa kike aliyeitwa Amina.
“Ila si mara moja tu! Tunakwenda halafu tutawahi kurudi!” alisema msichana huyo.
“Hapana! Tufanye siku nyingine. Siwezi kumuacha mama akiuza genge peke yake,” alisema Godwin.
“Lakini Irene si yupo?”
“Haijalishi! Na yeye pia anatakiwa kupumzika Amina,” alisema Godwin.
“Please!” (tafadhali)
“Am I understood?” (nimeeleweka?)
“A little bit,” (kidogo tu)
Amina alisimama akimwangalia Godwin, alimpenda mvulana huyo lakini alishindwa kumwambia ukweli. Alikuwa kijana mpole ambaye hakuonekana kuzungumza jambo lolote kuhusu mahusiano ya kimapenzi.
Alijaribu kumuonyeshea ishara zote kwamba alikuwa akimpenda lakini Godwin hakuonekana kabisa kuelewa. Alikuwa bize na masomo, maisha ya nyumbani kwao yalikichanganya mno kichwa chake.
SEHEMU YA 102
Hakukuwa na maisha ya raha wala furaha, majonzi ambayo alikuwa nayo tangu mumewe afariki dunia ndiyo yaliendelea kila siku. Umasikini ukaanza kumnyemelea Rosemary na familia yake.
Alijaribu kuwafuata ndugu zake na ndugu wa mume kwa ajili ya kuwaomba msaada lakini wakati huo kila mmoja alimkimbia, hakutaka kumsaidia, hawakukumbuka wema waliokuwa wakifanyiwa na familia ya Mzee Mapoto, kwao, chuki na majivuno yalitawala moyo yao.
Hilo lilikuwa pigo kubwa kwa Rosemary, hakuwa na pesa ya kutosha na ilikuwa ni lazima ailee familia yake, watoto wake waliokuwa kidato cha tatu waendelee kusoma lakini hakujua angepata vipi pesa.
Alipokwenda benki kuchukua pesa zilizobaki, akakuta akaunti yake ikiwa imefugwa na alipouliza, hakupewa majibu ya kuridhisha hata kidogo. Mkononi hakuwa na kitu, alikuwa mweupe kabisa, shilingi elfu ishirini aliyokuwa nayo ndiyo fedha pekee iliyobaki ambayo ilitakiwa kuyaendesha maisha yake na familia yake.
Alilia, hakujua ni kitu gani alitakiwa kufanya. Kwa kuwa alikuwa uswahilini, akaanzisha genge siku hiyohiyo. Ulikuwa ni uamuzi wa haraka, watu walimshangaa, waliomfahamu, walimuonea huruma kwani alishuka chini kabisa na kuanza maisha ambayo hakuwahi kufikiria hata siku moja kwamba angeyaishi.
Godwin na Irene waliporudi nyumbani, walishangaa, mama yao alibadilika zaidi, walijua kwamba alikuwa na mawazo tele, moyo wake uliumia lakini siku hiyo alionekana kuwa tofauti kabisa.
Godwin akamfuata mama yake na kumuuliza kilichofanya kuwa katika hali hiyo lakini mwanamke huyo hakumjibu chochote zaidi ya kutoka nje na kwenda gengeni.
“Hili genge ni letu?” aliuliza Godwin huku akionekana kushangaa.
“Ndiyo!”
“Umelijenga leo?”
“Ndiyo!”
Godwin aliumia mno, hakuongea tena, akaelekea ndani na kulala kitandani. Moyo wake ulimuuma mno, aliyakumbuka maisha ya raha waliyokuwa wakiishi zamani, aliyakumbuka maisha ya nchini Marekani baba yake alipokuwa hai, kitendo cha kutoka katika maisha yale na kuwa na maisha waliyokuwa nayo yalikuwa ni mabadiliko ya haraka ambayo hakuamini kama kungekuwa na mtu mwingine duniani ambaye angekuwa na mabadiliko ya maisha kwa haraka kama waliyokuwa nayo
Rais wao ni kama jiwe tuuRose mpaka huruma jamani maisha haya mtu alikuwa tajiri ghafla tu kaporomoka sababu ya binadamu