Dunia haina usawa

Dunia haina usawa

SEHEMU YA 99

“Mmejifunza wapi Kiingereza?” aliuliza mwanafunzi mmoja aliyejulikana kwa jina la Amina.
“Tulipotoka!” alijibu Godwin.
“Aisee mnaongea vizuri sana. Nifundishe na mimi!”

“Nitakufundishaje sasa Amina? Huwezi kufahamu lugha pasipo kuiongea, wewe tuongee na utaifahamu mbele ya safari,” alijibu Godwin ambaye kwa kumwangalia, alionekana kuwa kijana mpole kupita kawaida.

Maisha yalikuwa ni tofauti, walizoea kula chakula kizuri katika shule waliyotoka lakini ndani ya shule hiyo, maisha yalionekana kuwa magumu mno.

Hawakuviona vyakula walivyokuwa wakila walipotoka, kila chakula walichokitaka ilikuwa ni lazima kulipia tofauti na kule ambapo gharama zilijumuishwa katika ada yao ya mwaka.

Mbali na kufahamu Lugha ya Kiingereza, pia walikuwa hatari katika somo la Kiswahili na Hisabati. Walifanya vizuri, walifaulu katika majaribio waliyokuwa wakipewa kila wiki.

Wakawa maarufu shuleni hapo, watu waliwafahamu kutokana na uwezo wao mkubwa waliokuwa nao kwenye masomo. Wanafunzi wengi waliwafuata na kuhitaji kufundishwa, hawakujiona, walijiona kuwa sawa na wanafunzi wote waliokuwa shuleni hapo.

Wakati hayo yote yakiendelea, bado Rosemary alijiona kuwa kwenye wakati mgumu, hakujua ni kitu gani kilikuwa kikiendelea katika maisha yake. Moyo wake ulimuuma mno, kupoteza kila kitu lilikuwa pigo kubwa ambalo hakulitegemea kabisa.

Baada ya mwezi mmoja tangu ahamie Tandale hatimaye akapoka barua kutoka kwa mwalimu mkuu ambaye alipewa na serikali ambayo ilimfuta kazi ya ualimu shuleni hapo.

Alipoipokea na kuisoma, hakuamini kama kweli yeye ndiye aliyeandikiwa barua ile. Iliandikwa kwamba hakutakiwa kufundisha shuleni hapo, hakukuwa na sababu yoyote ya maana, ila kwa kifupi iliandikwa kwamba kulingana na matumizi makubwa, serikali iliamua kupunguza wafanyakazi wake.

“Nini? Nimefukuzwa kazi?” aliuliza huku akionekana kuchanganyikiwa.
Hakutaka kukubali, hapohapo akatoka ofisini na kwenda katika ofisi ya mwalimu mkuu, alipofika, akaambiwa asubiri kwenye benchi. Ndani ya dakika tano, akaambiwa aingie ndani.
 
SEHEMU YA 100

Alikuwa akilia, mashavu yake yalilowanishwa na machozi yaliyokuwa yakimtoka. Alimwangalia mwalimu mkuu, alikuwa akitia huruma mno, alishindwa kuzungumza, alikuwa kimya huku akiendelea kulia, kila alipotaka kuzungumza, alibanwa na kilio cha kwikwi.

Mwalimu mkuu akapata kazi ya kuanza kumbeleza, hakujua kilichokuwa kikimliza Rosemary kwani yeye alipelekewa barua na kumuagiza mwalimu ampe, hakujua ndani ya barua kuliandikwa nini na hata ishu ya kufukuzwa kazi, yeye kama mwalimu mkuu hakuambiwa lolote lile.

“Madam Rosemary, kuna nini?” aliuliza mwalimu mkuu, hapohapo Rosemary akaiweka barua hiyo mezani na mwalimu huyo kuanza kuisoma.

Alianzia juu mpaka mwisho. Yeye mwenyewe alishangaa, aliujua uwezo mkubwa aliokuwa nao Rosemary, miongoni mwa walimu waliokuwa wakipendwa kutokana na kufundisha vizuri basi alikuwa mwanamke huyo.

Hakujua sababu iliyowafanya watu wa ngazi ya juu kuamua jambo hilo. Alimwangalia Rosemary huku yeye mwenyewe akihisi maumivu makubwa moyoni mwake, aliyafahamu maisha ya mwanamke huyo, alifahamu hali aliyokuwa amepitia katika maisha ya shida na mateso, ilikuwaje leo afukuzwe kazi huku akiwa na watoto? Wangeishi vipi? Kila alichojiuliza, akakosa jibu.

“Rosemary! Haya ni maisha, hili ni jaribu kubwa sana kwako! Hutakiwi kuhuzunika sana, hutakiwi kulia kwa sababu kwenye kila jaribu Mungu anaweka mlango wa kutokea,” alisema mwalimu mkuu huku akimwangalia Rosemary.

“Inaniuma! Nimefanya nini? Kwa nini wamuamua hili? Kwa nini wamenifukuza kazi? Kweli hawajui maisha yangu niyoishi? Kweli hawajui jinsi ninavyohangaika na watoto wangu?” aliuliza Rosemary huku akilia kama mtoto.

Pamoja na kulia sana, pamoja na kuhuzunika sana ndani ya ofisi ya mwalimu mkuu haikuweza kubadilisha kitu, ukweli ukabaki palepale kwamba alifukuzwa kazi na alitakiwa kuacha kufundisha shuleni hapo mara moja.

Hakuridhika, mchana huohuo akaamua kwenda kumuona Waziri wa Elimu, Bwana Samson Massatu kwa ajili ya kumwambia kile kilichokuwa kimetokea.

Alipofika, akaanza kumuhadithia kila kitu, jinsi alivyokuwa akiishi kwa mateso, alivyokuwa na wakati mgumu wa kuihudumia familia yake.
“Umefukuzwa kazi? Inawezekana vipi?” aliuliza Bwana Massatu.
 
Hahhaha tater bana halafu jana mmu kuna mtu anatumia taiter nikajua wewe nisimshkuru kwa kubadili avatar atakuwa kanishangaa sana yule kaka

Hahahahahaha.. Kama ni muelewa atajua tuu umechanganya madesa..
 
SEHEMU YA 101

“Sijajua! Sijui chochote kile. Nimekuwa nikionewa, hakuna anayenionea huruma, sijajua ni kwa sababu gani mambo haya nafanyiwa mimi. Kila siku mimi tu,” alisema mwanamke huyo huku akiendelea kulia.
“Nitafuatilia mama! Nakuahidi kwamba nitafuatilia!” alisema Bwana Massatu.
“Nitashukuru!”

Rosemary akaondoka ofisini kwa waziri wa elimu huku akiwa na matumaini ya kusaidiwa. Njiani, hakuacha kulia, kila alipokuwa akiiangalia barua ile moyo wake ulikuwa na maumivu makali mpaka kuhisi kama kulikuwa na kitu chenye ncha kali kilichokuwa kikimchoma.

“Mungu! Mbona kila siku hivi? Ni nani yupo nyuma ya mambo haya yote? Na kwa nini kila siku ni mimi tu? Mungu! Kuna kitu nimekukosea? Kuna kitu nimekifanya hakipo sawa na umeamua kunipiga namna hii?

Mungu, hili jaribu limekuwa kubwa sana kwangu, siwezi kulibeba, nitie nguvu ya kusonga mbele, nionyeshe njia kwani bila nguvu zako, siwezi, nitashindwa kusimama na kusonga mbele,” alisema Rosemary huku akiwa ameinama chini ndani ya daladala, machozi yaliendelea kumtiririka mashavuni mwake kama maji.

Je, nini kitaendelea?
 
jaman kipenzi fupi
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom