Shunie
JF-Expert Member
- Aug 14, 2016
- 157,054
- 463,974
- Thread starter
- #941
SEHEMU YA 95
Hakukuwa na siri tena, watu wa serikalini wakagundua kwamba mtu aliyenunua nyumba ya Mapoto hakuwa Othman kama ilivyojulikana bali alikuwa Bilionea Matiku ambaye hakutaka kujulikana.
Hilo lilionekana kuwa tatizo, watu ambao walitaka kumuona Rosemary akiteseka hawakutaka kubaki kimya, walichokifanya ni kumuita Othman kwa ajili ya kuzungumza naye.
Walitaka kufahamu utajiri wake mkubwa aliokuwa nao mpaka kununua nyumba hiyo. Biashara zake hazikuwa kubwa, hawakuamini kama angeweza kununua nyumba hiyo kwa bei kubwa. Alipofuatiliwa zaidi kuhusu biashara zake akagundulika kwamba hakuwa mnunuaji wa nyumba hiyo.
Akakamatwa na kuwekwa selo, huko, akalazimishwa kusema mtu aliyekuwa nyuma ya mpango wa kununua nyumba ile. Waliomuuliza ni kama hawakuwa wakifahamu lakini ukweli ni kwamba walifahamu kila kitu, walijua kwamba Bilionea Matiku ndiye aliyetoa kiasi cha fedha kununua nyumba hiyo.
Walikasirika, walitaka kumuonyesha Matiku kwamba walikuwa na nguvu hivyo walichokifanya ni kuanza kumsumbua katika biashara zake. Magari ya kampuni zake yalikuwa yakikamatwa hovyohovyo, alipandishiwa kodi kubwa bila sababu maalumu. Kila alipokuwa, alikuwa akifuatiliwa, kila alichokuwa akikifanya ripoti ilipelekwa katika kitengo cha juu.
Baada ya siku kadhaa, polisi wakatumwa kwenda kumkamata kwa kisingizio cha kufahamu kwamba alikuwa akifahamu kuhusu mauaji ya Juma yaliyokuwa yamefanyika Kawe.
“Hamuwezi kuja kunikamata kiholelaholela tu kama mmekuja kumkamata mbeba mizigo sokoni,” alisema Matiku huku akiwaangalia polisi waliofika nyumbani kwake.
“Unafikiri mabilionea wapo juu ya sheria?” aliuliza polisi mmoja.
“Arrest warrant yenu ipo wapi?” aliuliza Matiku.
“Hii hapa!’
Matiku akaichukua na kuanza kuangalia, akaisoma na kukubaliana nao kwamba alitakiwa kwenda nao kituo cha polisi.
Hata kabla hajafika mbali akawasiliana na mwanasheria wake kwa ajili ya kufika kituoni ili hata kama kingetokea kitu chochote kile, ajue nini cha kufanya.