Dunia haina usawa

Dunia haina usawa

SEHEMU YA 75

Matokeo ya darasa la saba yalipotoka, walifaulu vizuri na hivyo kutakiwa kujiunga katika shule za sekondari, Godwin alichaguliwa kujiunga na Shule ya Wavulana ya Azania huku dada yake, Irene alitakiwa kujiunga na Shule ya Wasichana ya Jangwani alipokuwa akifundisha mama yake.

Bado walikuwa na fedha, Rosemary hakuona kama shule hizo zilikuwa sahihi kwa watoto wake, kama alivyokubaliana na mumewe kwamba Godwin na Irene walitakiwa kupata elimu bora, akaamua kuwapeleka katika shule nyingine ya watoto wa matajiri na viongozi serikalini iliyoitwa Kingston iliyokuwa Mikocheni B jijini Dar es Salaam.

Huko, masomo yalianza, hawakubadilika, bado walikuwa na uwezo mkubwa darasani, walijua kuzungumza Kiingereza kizuri, walipendwa shuleni hapo, walifanana na hata uwezo wao darasani ulikuwa mkubwa kiasi kwamba hata walimu wa shule hiyo walitamani sana kuona watoto wale wakiwa watoto wao.
“Hawa ndiyo watoto wa Balozi Mapoto?” aliuliza mwalimu mmoja.

“Ndiyo!”
“Mmh! Hawa watoto wana uwezo wa ajabu sana. Ni magenius, wana akili kupita kawaida,” alisema mwalimu huyo huku akionekana kushangaa.
Huo ulikuwa mwaka wao wa kwanza katika shule hiyo, walisoma bila tatizo lolote lile na hata mwaka ulipokwisha, walifanya vizuri na kuongoza kwa wanafunzi wote wa kidato cha kwanza.

Kufaulu kwao vizuri ilikuwa ni kama zawadi kwa baba yao ambaye kila siku aliwaambia kuwa walitakiwa kusoma kwa bidii kwani kusingekuwa na kitu chochote ambacho kingewatoa pale walipokuwa mbali na elimu. Mwaka huo ukamalizika, ulipoingia mwaka wa pili na kuendelea na masomo yao ndipo matatizo yalipoanza rasmi.

“Mama! Kuna karatasi imetoka Benki ya Watu,” alisema mwanaume mmoja aliyekuwa amemfuata Rosemary shuleni alipokuwa akifundisha.

“Kutoka benki?”
“Ndiyo!”
“Inasemaje?”
“Sijajua!”
“Na wewe nani?”
“Mleta barua kutoka hapohapo benki!” alijibu kijana huyo, hakutaka kuendelea kubaki mahali hapo, akaondoka zake.
Rosemary akawa na hofu, hakujua ni kitu gani kilichokuwa kimetokea, hakujua sababu iliyomfanya kupokea barua hiyo, hakujua ilikuwa ni barua ya nini, akaifungua bahasha ile na kuanza kuisoma.
 
Hahahahhh yaan mule mule halafu yule aliyepanga mipango ya kumuwekea mwandishi madawa kafanana na naibu waziri
Jamani taratibu.....shunie tunakupenda hatutaki ukapimwe mkojo mama
 
Hutakiwi kumwamini mtu yeyote yule,jikaze kisabuni kwani usalama wamemwagwa kila kona"
Nimenukuu
 
Mkwe Mimi simuamini kabisa Bokasa hata alie machozi ya damu bado naamini anahusika na matatizo ya balozi na familia yake iliyobaki
 
Mkwe Mimi simuamini kabisa Bokasa hata alie machozi ya damu bado naamini anahusika na matatizo ya balozi na familia yake iliyobaki
Mkwe tutaona itakavyokuwa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom