Duni Haji: Ndani ya CHADEMA kila mtu ni Kambale

Duni Haji: Ndani ya CHADEMA kila mtu ni Kambale

Hana lolote wangeshinda UKAWA makamu angesema hayo? Sana sana angezidi kutuimbia ngojera zake
 
Wenye macho waliliona hili mapema, chadema wana kazi nguvu kufanya org kuwa strong kama mwanzo.
 
Babu duni aende zake hayo matamko akayatolee zanzibar kwa shein..
 
Katika mahojiano yake na Azam TV Babu Duni ambaye juzi amerudi CUF amesema kuwa ndani ya CHADEMA kila mtu ni kambale.

Babu Duni amesema kwamba kuna bureaucracy kubwa sana ndani ya CHADEMA kiasi kwamba agizo linalotoka juu ngazi ya Taifa linaweza kukataliwa na ngazi ya jimbo kwakuwa kila mtu ana sharubu.

My Take: Babu Duni alikuwa akiwachora CHADEMA na ameona ni chama ambacho hakijawa tayari kuongoza nchi kwakuwa mfumo wake wa kiutendaji ndani ya chama ni 'chaos', je hawa watu tukiwapa nchi si haitatawalika kwakuwa kila mtu/kiongozi atakuwa ni kambale?. CHADEMA mrudisheni Dr Slaa aimarishe chama...

Source: Azam news ya saa 2 usiku.
Vipi ndani ya CUF kambale ni mmoja tu eeh.....
 
Kama chama hakiwezi kuwa Na mtu mmoja tuu wa kusikilizwa kama mfalme, Kama cuf walivoweka utawala wa chama chao. Mzee Juma duni Ni mtu amezowea Hewallah.

Chama Kama Chadema chenye wasomi wengi Ni lazima kiwe Na changamoto nyingi, vijana kwenye Chadema wanapata fursa ya Kutoa michango Yao Ni tofauti Na Cuf ambayo kila kitu anakifanya mtu mmoja tuu. Mhasibu yeye, msemaji yeye,katibu yeye, Rais wa mioyo yeye nk sehem nyingi amekamata Mwenyewe. Huu Ni udhaifu mkubwa kwa chama.

Kuna mwenzangu mmoja alipokua chama x alikuwa Na Nyota kali sana alitoka akaingia Cuf, Kama Cuf wangeweza kuiboresha Nyota ile Leo tungehesabu habari nyengine. Lakini cha ajabu Tokeo aingie Cuf Ndio haitoi hata muangaza.
Kwa maneno yako CUF haiwezi kuleta mabadiliko ya kidemokrasia kwa kuwa ni chama cha wafalme na wasio kubali fursa ya mawazo kutoka kwa vijana na watu wengine. Hii ni tatari saana kwa ustawi wa demokrasia katika nchi kama zetu.
 
Watu wa chama cha majizi mnapenda kushadadia mambo yasiyowahusu sio yeye tu hata awe nani akitaka kutoka atoke tu sisi raia tutabaki na chama chetu cha chadema
 
CHADEMA hatutaki mfumo wa ndio mzee kutoka ngazi ya juu,ndio maana kuna ugatuaji wa madaraka kutoka makao makuu kwenda ofisi za kanda.Juzi katibu mkuu amesema chama kinataka kushusha madaraka chini zaidi,yaende ngazi ya kata na vijiji ili watu wajiamulie mambo yao kutokana na mazingira yao.Makao makuu ibaki na sera na miongozo.Hicho ndo chama tunachotaka...yeye kama anaona hiyo haifai arudi CUF ambako katibu mkuu ana nguvu kuliko mwenyekiti na hata chama,labda yeye anaona hiyo ndio sahihi Zaidi.
 
We unafikiri tunaposema mfumo wa majimbo tunamaanisha nini kila jimbo liwe na utawala wake
 
Kwa maneno yako CUF haiwezi kuleta mabadiliko ya kidemokrasia kwa kuwa ni chama cha wafalme na wasio kubali fursa ya mawazo kutoka kwa vijana na watu wengine. Hii ni tatari saana kwa ustawi wa demokrasia katika nchi kama zetu.
Yani kwakuwa Duni kawaponda CHADEMA mmeungana na CCM kuwaponda CUF...

Kweli wazanzibar wana akili kuinyima kura CUF.
 
CUF wanawaamini Prof Lipumba tu, je hakuna mtu mwingine? Kwa Zanzibar Maalimu Seif ndio maana hakina wateja kwa huku Bara!
 
We unafikiri tunaposema mfumo wa majimbo tunamaanisha nini kila jimbo liwe na utawala wake
Unamaanisha kila jimbo lijitangazie uhuru...maana halitakubali kupokea maelezo au kutekeleza sera kutoka ngazi ya taifa. Kila jimbo kama halitakubali kuingiliwa nchi haitakuwepo tena....
 
Ni muda muafaka kwa CDM kuangalia upya na kuipa msukumo mpya sera yake ya majimbo/ukanda. Lazima tuwe na ushindani wa serikali za majibo/kanda katika kuendesha nchi. Sio lazima mawazo yote yatokee Dar. Li nchi likubwa kuna watu wanasema wamechoka kuwa wa pembezoni.
 
Ni muda muafaka kwa CDM kuangalia upya na kuipa msukumo mpya sera yake ya majimbo/ukanda. Lazima tuwe na ushindani wa serikali za majibo/kanda katika kuendesha nchi. Sio lazima mawazo yote yatokee Dar. Li nchi likubwa kuna watu wanasema wamechoka kuwa wa pembezoni.
Sio mara zote majimbo yatakua yanafanya maamuzi bila kuingiliwa hasa pale maamuzi yanapokuwa not for interests of the majority. Sasa hapo ngazi ya taifa ikiingilia katu nyie jimbo mkakataa huoni huo ni ukambale?
 
image.jpeg



Jana aliyekuwa mgombea mwenza wa UKAWA katika uchaguzi mkuu wa mwaka jana Haji Duni maarufu kama Babu Duni aliongea na chombo kimoja cha habari akiwa Zanzibar.Lengo la chombo hivho cha habari kumfuata Babu Duni ilikuwa ni kutaka kwanza kujuwa msimamo wake juu ya uchaguzi wa marudio uliofanyika Zanzibar,Uchaguzi mkuu uliopita na maisha yake ndani ya Chadema na pia kuelezea uamuzi wake wa kurudi chama chake cha CUF alichokitumikia kwa muda mrefu.

Kwanza Babu Duni kama walivyo wafuasi na wanachama wengine wa CUF hautambui wala kukubaliana na uchaguzi wa marudio wa Znz,na anaamini kuwa CUF na Maalim Seif walishinda ili wameapokonywa ushindi wao kwa nguvu ya dola.Babu Duni anasema takwimu ziliwapa kila kitu kuwa ushindi ni wao ili yakatokea kama yalivyotokea.

Akizungumzia maisha yake ndani ya Chadema kwa kofia ya UKAWA,Babu Duni anasema ilikuwa ni lazima yeye ajiunge na Chadema kama mgombea mwenza ili kukidhi matakwa ya kisheria na kikatiba,sababu kwa mujibu wa sheria za nchi asingeweza kugombea wakati bado ni mwanachama wa CUF.Hivyo walikubaliana yeye kwa maslahi ya UKAWA ajiunge na CHADEMA ili kuongoza harakati za kuingia madarakani kwa jina la UKAWA.Jambo hilo lilikuwa ni lazima ili kuhakikisha kuwa UKAWA haipati kizuizi kufikia malengo yake.

Babu Duni anasema alichoona changamoto wakati wa uchaguzi na maisha yake ndani ya Chadema ni ile hali ya yeye kutokuwa kiongozi na pia kutokujulikana na watu wengi ndani ya Chadema na hivyo kukosa watu alio na mazoea nao kama ilivyokuwa Chadema.Duni aliendelea kusema ugeni wake ndani ya Chadema ulimpa wakati mgumu sababu alikuwa hajui apite wapi pale ambapo alikuwa ana shida ya haraka sababu alikuwa bado hajawajuwa watu ndani ya chama tofauti na ilivyokuwa akiwa CUF.Babu Duni anasema CUF ilikuwa inampa wepesi sababu ni chama alichokijuwa na alishika madaraka makubwa kiasi cha kujuwa wapi apite na wapi atokee.

Changamoto nyingine aliyoiona ni ile hali ya Chadema kuwa na "beuracratic" ktk mfumo wakw wa kiungozi kiasi cha kuwa mambo mengi ama yanakwama au yanachelewesha maamuzi na hasa ktk kipindi kama kile cha kampeni.Ndani ya Chadema kuna uongozi wa Taifa,Kanda,Jimbo,Mkoa,Wilaya na Kata.Mtiririko huu wa uongozi na maamuzi unachelewesha sana mambo kwa mtazamo wake,sababu jambo linaweza kuamuliwa na Taifa lakini watu wa Kanda sababu ya mamlaka waliyopewa wanaweza kulizuia au kulikwamisha,au kitu kinaweza kutoka kwenye kanda lakini watu wa jimbo wakalikataa.Aina hii ya muundo wa kiutawala kwa maoni yake Babu Duni ni kama yanachelewesha hatua za maamuzi sababu kila mtu anakuwa kama "kambale mwenye sharubu" anaamua kile anachokiona kwake kinafaa.Hivyo kushauri kutazama upya aina hii ya muundo wa kiutawala.Amekipongeza CHADEMA kuwa ni chama kilichokuwa kwa kasi na amejifunza mambo mengi wakati akiwa Chadema kama mwanachama wa kukidhi matakwa ya kisheria na kikatiba.

Babu Duni anasema amejifunza kuwa kweli umoja ni ushindi,na wala hajutii kwa CUF kijiunga ndani ya UKAWA huku akiombea umoja huo uendelee kudumu ili kutimiza malengo yankukamata dola.Babu Duni anasema katika umoja huo CUF imefaidika sana sababu kwa mara ya kwanza imekuwa na idadi kubwa ya wabunge wa kuchaguliwa ndani ya Bunge la Tanzania toka kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi,hali hii imesababishwa na dhamira ya mshikamano ya UKAWA.Ametolea mfano wa CUF kupata halmashauri za kuziongoza Tanzania Bara kama ile ya Tandahimba na maeneo ya kusini,huku akisema na Tanga ilikuwa yao licha ya kupokonywa kwa nguvu ya dola.Duni amewataka viongozi wa vyama vinavyounda UKAWA kuyafanyia kazi mapungufu yaliyojitokeza mwaka jana ili yasijirudie tena 2020 na kusisitiza kuwa upinzani bila UKAWA ni sawa na debe tupu

Upotoshaji wa kusema Babu Duni ameikandia Chadema ni nia ya "uchonganishi" kati ya vyama hivi vya upinzani,ni hila na husuda dhidi ya umoja huu ulioleta matumaini na mabadiliko makubwa katika siasa za ushindani Tanzania kiasi cha chama dola kupoteza uongozi wa miji na majiji makubwa kama Iringa,Mbeya,Dsm na Tandhimba
 
Back
Top Bottom