Duni Haji: Ndani ya CHADEMA kila mtu ni Kambale

twahil

JF-Expert Member
May 31, 2011
4,100
2,795
Katika mahojiano yake na Azam TV Babu Duni ambaye juzi amerudi CUF amesema kuwa ndani ya CHADEMA kila mtu ni kambale.

Babu Duni amesema kwamba kuna bureaucracy kubwa sana ndani ya CHADEMA kiasi kwamba agizo linalotoka juu ngazi ya Taifa linaweza kukataliwa na ngazi ya jimbo kwakuwa kila mtu ana sharubu.

My Take: Babu Duni alikuwa akiwachora CHADEMA na ameona ni chama ambacho hakijawa tayari kuongoza nchi kwakuwa mfumo wake wa kiutendaji ndani ya chama ni 'chaos', je hawa watu tukiwapa nchi si haitatawalika kwakuwa kila mtu/kiongozi atakuwa ni kambale?. CHADEMA mrudisheni Dr Slaa aimarishe chama...

Source: Azam news ya saa 2 usiku.

===========================

Ukweli wa alichosema Babu Duni juu ya CHADEMA

Jana aliyekuwa mgombea mwenza wa UKAWA katika uchaguzi mkuu wa mwaka jana Haji Duni maarufu kama Babu Duni aliongea na chombo kimoja cha habari akiwa Zanzibar.Lengo la chombo hivho cha habari kumfuata Babu Duni ilikuwa ni kutaka kwanza kujuwa msimamo wake juu ya uchaguzi wa marudio uliofanyika Zanzibar,Uchaguzi mkuu uliopita na maisha yake ndani ya Chadema na pia kuelezea uamuzi wake wa kurudi chama chake cha CUF alichokitumikia kwa muda mrefu.

Kwanza Babu Duni kama walivyo wafuasi na wanachama wengine wa CUF hautambui wala kukubaliana na uchaguzi wa marudio wa Znz,na anaamini kuwa CUF na Maalim Seif walishinda ili wameapokonywa ushindi wao kwa nguvu ya dola.Babu Duni anasema takwimu ziliwapa kila kitu kuwa ushindi ni wao ili yakatokea kama yalivyotokea.

Akizungumzia maisha yake ndani ya Chadema kwa kofia ya UKAWA,Babu Duni anasema ilikuwa ni lazima yeye ajiunge na Chadema kama mgombea mwenza ili kukidhi matakwa ya kisheria na kikatiba,sababu kwa mujibu wa sheria za nchi asingeweza kugombea wakati bado ni mwanachama wa CUF.Hivyo walikubaliana yeye kwa maslahi ya UKAWA ajiunge na CHADEMA ili kuongoza harakati za kuingia madarakani kwa jina la UKAWA.Jambo hilo lilikuwa ni lazima ili kuhakikisha kuwa UKAWA haipati kizuizi kufikia malengo yake.

Babu Duni anasema alichoona changamoto wakati wa uchaguzi na maisha yake ndani ya Chadema ni ile hali ya yeye kutokuwa kiongozi na pia kutokujulikana na watu wengi ndani ya Chadema na hivyo kukosa watu alio na mazoea nao kama ilivyokuwa Chadema.Duni aliendelea kusema ugeni wake ndani ya Chadema ulimpa wakati mgumu sababu alikuwa hajui apite wapi pale ambapo alikuwa ana shida ya haraka sababu alikuwa bado hajawajuwa watu ndani ya chama tofauti na ilivyokuwa akiwa CUF.Babu Duni anasema CUF ilikuwa inampa wepesi sababu ni chama alichokijuwa na alishika madaraka makubwa kiasi cha kujuwa wapi apite na wapi atokee.

Changamoto nyingine aliyoiona ni ile hali ya Chadema kuwa na "beuracratic" ktk mfumo wakw wa kiungozi kiasi cha kuwa mambo mengi ama yanakwama au yanachelewesha maamuzi na hasa ktk kipindi kama kile cha kampeni.Ndani ya Chadema kuna uongozi wa Taifa,Kanda,Jimbo,Mkoa,Wilaya na Kata.Mtiririko huu wa uongozi na maamuzi unachelewesha sana mambo kwa mtazamo wake,sababu jambo linaweza kuamuliwa na Taifa lakini watu wa Kanda sababu ya mamlaka waliyopewa wanaweza kulizuia au kulikwamisha,au kitu kinaweza kutoka kwenye kanda lakini watu wa jimbo wakalikataa.Aina hii ya muundo wa kiutawala kwa maoni yake Babu Duni ni kama yanachelewesha hatua za maamuzi sababu kila mtu anakuwa kama "kambale mwenye sharubu" anaamua kile anachokiona kwake kinafaa.Hivyo kushauri kutazama upya aina hii ya muundo wa kiutawala.Amekipongeza CHADEMA kuwa ni chama kilichokuwa kwa kasi na amejifunza mambo mengi wakati akiwa Chadema kama mwanachama wa kukidhi matakwa ya kisheria na kikatiba.

Babu Duni anasema amejifunza kuwa kweli umoja ni ushindi,na wala hajutii kwa CUF kijiunga ndani ya UKAWA huku akiombea umoja huo uendelee kudumu ili kutimiza malengo yankukamata dola.Babu Duni anasema katika umoja huo CUF imefaidika sana sababu kwa mara ya kwanza imekuwa na idadi kubwa ya wabunge wa kuchaguliwa ndani ya Bunge la Tanzania toka kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi,hali hii imesababishwa na dhamira ya mshikamano ya UKAWA.Ametolea mfano wa CUF kupata halmashauri za kuziongoza Tanzania Bara kama ile ya Tandahimba na maeneo ya kusini,huku akisema na Tanga ilikuwa yao licha ya kupokonywa kwa nguvu ya dola.Duni amewataka viongozi wa vyama vinavyounda UKAWA kuyafanyia kazi mapungufu yaliyojitokeza mwaka jana ili yasijirudie tena 2020 na kusisitiza kuwa upinzani bila UKAWA ni sawa na debe tupu

Upotoshaji wa kusema Babu Duni ameikandia Chadema ni nia ya "uchonganishi" kati ya vyama hivi vya upinzani,ni hila na husuda dhidi ya umoja huu ulioleta matumaini na mabadiliko makubwa katika siasa za ushindani Tanzania kiasi cha chama dola kupoteza uongozi wa miji na majiji makubwa kama Iringa,Mbeya,Dsm na Tandhimba
 
Nimecheka sana nilivyomsikiliza Babu Duni. CHADEMA ni chama cha wapiga dili, yaani kama issue haiko na maslahi haipiti ktk tawi. CCM mbele kwa mbele, ndiyo maana mzee JK alisema atalala usingizi fofo fofo, kazi JPM achapa!
 
Kwani babu Duni ni nani nae ni binadamu tu kama wengine pia nae alikuwa kimaslahi zaidi mbona mwanzo hakusema chochote ?kakosa unaibu analeta maneno .Mtasema sana CHADEMA ina wanachama wengi sana ambao hawageuki nyuma .peopleeees .
 
Ujio wa fisadi Lowassa na Mzee Duni CHADEMA ni funzo kwetu,haiwezekeni MPITA njia akutembelee kwako siku moja then Umkalibishe chumbani na umpe siri zote za ndani kwako.
 
Huyu nae ni opportunist tu hana uzalendo wowote kwa cuf ni mtu wa kumwaangalia kwa umakini sana
 
WanaCCM waacheni Chadema Na mambo yao mbona CCM MNA misukosuko mingi ? Mngetumia muda mwingi kusema yenu , wabunge wenu wala Rushwa , majipu ni Wanaccm, ili mradi kila uozo wa nchi ni ccm
Duni Hajji sio CCM tafadhali...
 
Duni haji kama namwoooona vile!!!! Hahahha ndembendembe kifo cha mende kimegeukia chadema
 
Haya Duni naye sijui watamuita msaliti au? Maana kila mtu anajua kuwa Duni ni mpinzani
 
Katika mahojiano yake na Azam TV Babu Duni ambaye juzi amerudi CUF amesema kuwa ndani ya CHADEMA kila mtu ni kambale.

Babu Duni amesema kwamba kuna bureaucracy kubwa sana ndani ya CHADEMA kiasi kwamba agizo linalotoka juu ngazi ya Taifa linaweza kukataliwa na ngazi ya jimbo kwakuwa kila mtu ana sharubu.

My Take: Babu Duni alikuwa akiwachora CHADEMA na ameona ni chama ambacho hakijawa tayari kuongoza nchi kwakuwa mfumo wake wa kiutendaji ndani ya chama ni 'chaos', je hawa watu tukiwapa nchi si haitatawalika kwakuwa kila mtu/kiongozi atakuwa ni kambale?. CHADEMA mrudisheni Dr Slaa aimarishe chama...

Source: Azam news ya saa 2 usiku.
Kichwa cha habari kama hakijakaa vizuri; kingekuwa hivi: Aliyekuwa Mgombea Mwenza wa Urais CHADEMA asema kila mtu ni Kambale ndani ya CHADEMA
 
Back
Top Bottom