Duh, hii ni hatari! Kumbe wananchi walikusudia kumuua mkuu wa Wilaya

GAZETI

JF-Expert Member
Feb 24, 2011
5,277
6,673
Kwa taarifa nilizonazo kutoka Tandahimba ni kwamba wananchi walikusudia
kumuua mkuu wa wilaya hiyo Bi Hasna Mwilima kutokana na majibu mabovu
aliyowajibu wakulima hao walipotaka kujua kuhusu malipo ya korosho zao
walizokopwa.
Zoezi hilo lilifeli baada ya mashine ambayo walikuwa wanatumia kukatia miti
na kuziba barabara kushindwa kufanya kazi kutokana na kuharibika baada ya
kufanya kazi muda mrefu. Lengo lilikuwa ni kukata mwembe mkubwa na kuziba
barabara inayotoka kwa bosi huyo wa wilaya ili waweze kumshambulia vizuri.

Sijui tunaelekea wapi na KISIWA CHETU CHA AMANI.

Hii kali, nahisi ndo' tunakoelekea; watawala wanpojiona wao ni wafa;me na hivyo kutoa majibu ya kejeli na mauzi kwa wananchi wakijua aliyewateua hawezi kutengua uteuzi wao (Kwa sababu wazijuazo wao). Mwisho wananchi watachoka na ya-Tandahimba yatajirudia sehemu nyingine.

Wito wangu kwa serikali kushughulikia madai ya wanachi hawa haraka iwezekanavyo. Nawasilisha
 
haba na haba hujaza........................
Kama leo wakitaka kumpiga DC i hope kesho watampiga yula jamaa wa pale magogoni
 
Laiti Hawa Watu wangejua ungekuta wamemchagua Mbunge ambaye angewatetea Maslahi Yao!! Poa Mchelea Mwana Kulia Mwisho Hulia yeye!! Nawapa pole ila next Time wasifanye Makosa!!
 
Ujasiri wa usiotarajiwa toka kwa Matanzania huo ... "Everything has got its breaking point" ... Na fikiri hata kwa Mtanzania hilo sasa linaelekea kuwa kweli!!!
 
Jambo la kwanza kuhusu wananchi kutaka kumuua mkuu wa wilaya ni jambo la kusikitisha sana na ni la aibu kubwa,lazima tufahamu kwamba tuna nchi yenye katiba na sheria na mahakama na vyombo vya ulinzi na usalama ambavyo tunajivunia,kama mkuu huyo inavyodaiwa kuwa alijibu maneno ya kuudhi wananchi au kuwakejeli basi ingefaa wananchi hao wajitokeze kwa pamoja na kufanya kampeini kabambe ya kutaka mkuu huyo aondolewe katika wilaya hiyo au aombe radhi na baadae wasimamishe kesi na kama amekuwa mkuu kwa kuchaguliwa na wananchi basi kipindi chake kikimalizika wasimchaguwe tena,lakini sio kutafuta mbinu za kumuuwa,hiyo sio hatua ya kibusara na kidemokrasia, kama kila kiongozi akiwakosea wananchi anauliwa basi hapatakuwa na kiongozi tena nchini. Au mnasemaje wazee?
 
umeongea ukweli ila ukidadisi vizurh serikali yetu chini ya ccm utagundua kuwa hata raia ukiongea au ukiandamana unaweza usisikilizwe na matokeo yake huyo kiongozi m bovu anahamishwa kwa wananchi wengine na jiulize anachoenda kukifanya kule nini wakati ameacha varangati huku na ukisema mumfungulie kesi itakuwa unajisumbua manake kesi itapigwa danadana mpaka mwishoni wananchi mnachoka na kukata tamaa na mahakama .mimi nawaunga mkono hao raia
 
Jambo la kwanza kuhusu wananchi kutaka kumuua mkuu wa wilaya ni jambo la kusikitisha sana na ni la aibu kubwa,lazima tufahamu kwamba tuna nchi yenye katiba na sheria na mahakama na vyombo vya ulinzi na usalama ambavyo tunajivunia,kama mkuu huyo inavyodaiwa kuwa alijibu maneno ya kuudhi wananchi au kuwakejeli basi ingefaa wananchi hao wajitokeze kwa pamoja na kufanya kampeini kabambe ya kutaka mkuu huyo aondolewe katika wilaya hiyo au aombe radhi na baadae wasimamishe kesi na kama amekuwa mkuu kwa kuchaguliwa na wananchi basi kipindi chake kikimalizika wasimchaguwe tena,lakini sio kutafuta mbinu za kumuuwa,hiyo sio hatua ya kibusara na kidemokrasia, kama kila kiongozi akiwakosea wananchi anauliwa basi hapatakuwa na kiongozi tena nchini. Au mnasemaje wazee?
Mkuu Ulichosema ndicho hasa kilitakiwa kufanyika, but hao wananchi si vichaa wala wajinga. Unapokuwa na taifa ambalo limepoteza uwajibikaji then unatakiwa uyategemee haya na mengine mengi! si wameona OCD aliyekatwa kule Serengeti kwa wizi wa madini akibadilishiwa kituo cha kazi badala ya kushtakiwa?? au unadhani hawakuona Madaktari waliotaka waziri wa afya awajibishwe na kushindwa kutimiza wajibu wake akilindwa na wakubwa kwa nguvu zote. Haya ni baadhi ya mambo yanayowapa wananchi hasira na kuchukua sheria mikononi mwao kitu ambacho si sawa. ILI kuyakomesha haya Serikali ina wajibu wa kuamka na kutenda haki pia kurudisha ile dhana ya uwajibikaji.
 
kweli mkuu.
 
Wananchi hawaviamini tena vyombo vya ulinzi na usalama kwani havifanyi kazi ya kuwalinda, vimekuwa sehemu ya matatizo; wananchi wanakwenda kutoa taarifa za uhalifu polisi lakini polisi hao hao wanashirikiana na wahalifu sasa wananchi watakosa kuchukua sheria mkononi? Serikli ya ccm ni serikali ya watawala na sio serikali ya wananchi!
 
Ndo faida ya kuwasukuma watu mpaka mwisho. People have been pushed to the edge, and they have nothing to loose anymore! Tutaona mengi!
 
Huyu mama alikuwa dc wa Hai baadaye 'Mkulu' alimteua kuwa katibu mkuu wa UWT ccm kule wenzake walimtimua muda mfupi tu baada kufanya madudu kibao. Na JK hakumtupa mteule wake kwani siku chache tu 'alimrejeshea' u dc wake na kumpangia Tandahimba.

Kwa hiyo wananchi wasifikiri ataondolewa kirahisi hata akifanya utumbo wa aina yoyote kwa kuangalia 'trend' hapo juu. She is leaning on somebody (Mkulu)
 
Laiti Hawa Watu wangejua ungekuta wamemchagua Mbunge ambaye angewatetea Maslahi Yao!! Poa Mchelea Mwana Kulia Mwisho Hulia yeye!! Nawapa pole ila next Time wasifanye Makosa!!

ndo hao ukiwauliza mlimchagua nan watakwambia ccm haraf wanalalamika vp mbunge wao hajasema chochote
 
Kwa taarifa nilizonazo kutoka Tandahimba ni kwamba wananchi walikusudia
kumuua mkuu wa wilaya hiyo Bi Hasna Mwilima kutokana na majibu mabovu
aliyowajibu wakulima hao walipotaka kujua kuhusu malipo ya korosho zao
walizokopwa.
Zoezi hilo lilifeli baada ya mashine ambayo walikuwa wanatumia kukatia miti
na kuziba barabara kushindwa kufanya kazi kutokana na kuharibika baada ya
kufanya kazi muda mrefu. Lengo lilikuwa ni kukata mwembe mkubwa na kuziba
barabara inayotoka kwa bosi huyo wa wilaya ili waweze kumshambulia vizuri.

Sijui tunaelekea wapi na KISIWA CHETU CHA AMANI.

vp mbunge wao yupo au kasafir au yupo bize na kampen za ubunge wa east afrika
 
Ndo faida ya kuwasukuma watu mpaka mwisho. People have been pushed to the edge, and they have nothing to loose anymore! Tutaona mengi!
.
Wahenga walisema .... Ukimfukuza sana Mjusi mwishoni hugeuka nyoka

ndo hao ukiwauliza mlimchagua nan watakwambia ccm haraf wanalalamika vp mbunge wao hajasema chochote
wakati wa uchaguzi Tandahimba alishinda mbunge wa CUF,lakini kama mjuavyo "mambo ya kuchakachua"akatangazwa mbunge CCM.Tena kulitokea vurumai lisilo la kawaida,hadi polisi toka wilaya nyingine walipelekwa kusaidia kutuliza vurugu,na huyohuyo mkuu wa wlilaya ikabidi aende kujificha sehemu.
 
ndo hao ukiwauliza mlimchagua nan watakwambia ccm haraf wanalalamika vp mbunge wao hajasema chochote

nasikitika kwamba umechangia wakati huijui tandahimba! Acha nikujuvye kidogo, tandahimba ccm haikubaliki hata kidogo, huyo mkuu wa wilaya kapora ushindi wa mbunge aliyechaguliwa na wananchi kwa tiketi ya cuf akamtangaza wa ccm! Hata huyo wa ccm hakanyagi tandahimba akichelea maisha yake! Na kesi dhidi yake iko mahakamani, leo tena dc huyo huyo anawaletea upuuzi wananchi!!!
 
kwa kweli hili swala was in the pipeline, it was coming and i think the time is now! the masses are resorting to killing and assassinating leaders!!!! may seem extreme but it is a sign of how stretched the masses' patience has been!

it is always the case when the leaders forget their responsibilities and think that they are supreme over the masses. hata akiwa na beretta au 9mm, the masses always win! she now needs to be careful or at least she should humble herself.
 
Back
Top Bottom